Jumamosi, 29 Juni 2019

MNGOJE BWANA KAMA MKULIMA ANGOJAVYO MAVUNO


Na Mwalimu Oscar Samba:
Kwenye pwenti ya kumngoja Bwana kwa Saburi; Mpendwa Mwenzangu katika Bwana ! Mwenye kungoja kwa Saburi huwa na taraja, ndani yake mna imani dhabiti, hana mashaka wala manongono, ni kama vile mkulima angojavyo mazao !
     📜Hana haraka, ana hakika yaja majira ya mavuno, kwanza hulikwatua ama huliandaa shamba hata kabla ya mvua kunyesha, hutia mbegu chini majira ya mvua ya kupandia, wakati wa palizi hana haraka ya kuvuna bali hufanya palizi, huwekea mbolea na kuyalinda dhidi ya wadudu, kisha huja wakati wa kuchanua, napo hana haraka, anajua kuna majira ya ngano au suke, ama mahindi yake kukomaa; Marko 4:26 Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi;

27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye.
28 Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.
29 Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.
Aina hii ya uvumilivu, ndio tunaotakiwa kuwa nao, ili kutuwezesha kuyafikilia mema yetu, mwisho wa maandiko nikupayo kuna onyo kuhusu manongono ! Hii ikupe kuwa makini na mwenendo huu, wenye ishara ya kukosa au kupungukiwa saburi, (Zakaria alimngoja Bwana kweli, ila kuna namna Saburi ilipungua ! Ni kweli ilikwepo
ila ni dhairi ilipungua ! Kwa hiyo akapewa majibu na adhabu juu ! Kwako isiwe vivyo ! Ni kweli sio jambo jepesi kungoja kama alivyongoja yeye maana ni hitajio lake la miaka mingi, ila ninachofahamu ni kwamba majira yake yalikwepo, sasa saburi itakupa tumaini na kisha udhabiti au uimara wa moyo.) Tuyaone hayo maandiko yakikulima;

Yakobo 5:7 Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.
8 Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. 9 Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.

Lakini pia katika kumngoja Bwana hakikisha taa yako ina mafuta, taa yako inawaka, nikimaanisha kuwa uhusiano wako na Mungu unapaswa kusalia kuwa dhabiti, usije ukawa umevunjika moyo, umeacha utumishi, maana ni heri yule mtumishi ambaye Kristo akija atamkuta akiendelea kutenda kazi kama Zakaria, ili ampatie majibu yake, hakikisha unaendelea na uombaji, hakikisha unaendelea na kusoma neno, wala furaha ya wokovu isipunguke ndani yako, maana maandiko yanena hivi;

Luka 12:35 Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; 36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Ni muhimu kujua kuwa Roho Mtakatifu ni wa thamani sana lifikapo swala la kungoja, maana huachilia saburi ndani yetu, ikiwa na maana kwamba atakuwezesha kungoja kwa kukupa uwezo wa kustaimili, maana Yeye ni muombezi wetu, (a) hukuombea kuwa na saburi, lakini pia (b) kwa kupitia kungoja kwako, au saburi yako, huwa na uwanda mpana wa kuombea hitaji lako unalolitarajia kwa imani, kwa hiyo, a na b ni muhimu na hutegemeana;

Warumi 8:24 Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?
25 Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.(Shika hii sana.)
26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

Mpendwa , kama hujaokoka na unataka kufanya hivyo sasa tafadhli kwa imani kubwa nakuu kabisa fuatisha pamoja nami maneno haya, au sala hii ya toba ili uweze kuokoka, Sema;

BWANA YESU, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NATUBU MBELE ZAKO LEO, NISAMEHE NA NINAKUOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, TAFADHALI LIANDDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NINAKUKIRII NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, HAKIKA WEWE NI MUNGU NA ULIFUFUKA KATIKA WAFU, Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombi, sadaka kwa njia ya M-Pesa, kupiga simu au Wasats App, ni +25559859287. Tupo Arusha Tanzania.

Kwa undani wa Mafundisho au Habari zetu tembelea; www.ukombozigospel.blogspot.com .
#MwalimuOscarSamba #UgMinistry #UkomboziGospel #MwalimuOscarVitabu #Neno #Biblia #Zaburi #Pic #Picha #Tanzania #Afrika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni