Alhamisi, 6 Juni 2019

Muhesabu Mungu kuwa ni Mwaminifu, ni katika kitabu cha NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA.

Muhesabu Mungu kuwa ni Mwaminifu, ni katika kitabu cha NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA.
Kwa hiyo, Mungu akikuaidia ni hakika atalifanya hilo kuwa jema, jambo muhimu kwako ni kumuhesabu kuwa ni mwaminifu, ukijuwa vyema kazi aliyoianza ni lazima ataimaliza tu ! Wafilipi 1:6 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.Kama amekupa mke au mume, uwe na hakika na mwana atakupa ! Kama ameweza kukupatia biashara, uwe na hakika na swala la wateja atalimaliza. Kama ameweza kukuleta ulimwenguni, basi na uponyaji ni haki yako.

Yamkini umeliombea jambo hilo kwa muda sasa, na imefika mahali limegeuka na kuwa jaribu ! Nikimaanisha sio hitaji la kawaida, maana limeanza kukuweka njia panda na kukufanya uanze kufikiri kwa upya kuhusu uhusiano wako na Mungu, au kuhusu uendelee kumngoja Bwana kwa saburi au umngoje katika hali ambayo akitenda sawa na asipotenda pia ni sawa, ili mradi wewe unachojua ukitwaliwa leo ni mbinguni mengine hutaki tena kuyajua !


( Kuna kipindi nilipitia mahali pagumu kuhusu chakula kiasi cha kuishi kwa kula miwa, kula mboga za majani, na hata kwa wiki kupika mara mbili, kuna muda nilikuwa napika chapati na ninamega kipande asubuhi, kipande mchana na kipande usiku, maana bajeti ni muhimu, sasa ninachotaka kukwambia ni hiki, siku moja nikala na kugundua kuwa sijashiba, moja kwa moja niliiambia nafsi yangu kuwa utashiba mbinguni ! Nilisikia sauti ikiniambia hapana utashiba hapa hapa duniani mana mbinguni hakuna kunywa wala kula. Na kukumbushwa maandiko ya Torati, ile kuanzia sura ya saba na nane kuwa huko tutakula na kushiba, ikimaanisha kuwa ni kweli leo nipo jangwani ila kuna majira yanakuja ya kunishibisha.)

Sasa kuna watu wamefika hatua ya kuona hiyo hali ni sehemu ya maisha yao, wana uvumilivu lakini sio wenye tumaini, nikimaanisha hawana saburi, maana penye tumaini pana imani pia, wasomaji wa Yakobo moja, na Warumi tano hufahamu kwa kina kuhusu saburi, uvumilivu na tumini pia.

Sasa andiko nikupalo linabeba dhima muhimu sana kuhusu uaminifu wa Mungu katika jaribu, au pito lako; 1 Wakorintho 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Pwenti ya neema itakupa kunielewa kwa kile ambacho nilitaka kukipachika hapa, ila tuendelee na uaminifu maana nalitaka kukwambia kuwa usiichezee neema ambayo Mungu huiachilia katika jaribu hilo nikitaka kuanzana sentensi isemayo kuwa huwa "nawaambiga" watu wasiichezee au wasiisukumie mbali neema inayoachiliwa ili kuwavusha wanapopitia kwani kila jaribu lina neema yake, pia ninawashauri kuomba kuona mlango wa jaribu, maana kila jaribu lina mlango wa kutokea kama hilo andiko lisemavyo, kwa mujibu wa kitabu kile cha NAMNA YA KUISHI WAKATI WA MAJARIBU AU MAPITO, nimeeleza kuwa milango mingine ni uvumilivu kama ilivyokuwa kwa Ayubu na Ibrahimu na mkewe !
( Maana jaribu ambalo, au hitaji ambalo majibu yake Mungu amenuia kuyaachilia kwa wakati wake, lina hitaji sana saburi,sasa sina maana usiliombee; omba, maana katika kuomba yamkini muda ukafupishwa kwani maandiko husema katika Ufunuo kwamba kipindi kile kimefupishwa kwa ajili ya wateule, uwe na hakika hata kwako chaweza fupishwa, lakini maombi pia huishikilia imani yako, hukupa pia kuendelea kumngoja kwa saburi, hukusaidia au hukuzuilia kuanguka au kuingia majaribuni, ikiwa na maana kwamba utapitia jaribu sawa ila hutamezwa nalo, na pia hukuwezesha kuzitambua na kuzipinga hila za adui kiwepesi.)

Nikutie Moyo tu kuwa Mungu aliyekuadia ni Mwaminifu naye atafanya au atatenda tu, na nafsi yako ianze kumuhesabu vivyo; 1 Wathesalonike 5:24 Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya
Na kama hujaokoka na unataka kufanya hivyo sasa tafadhli kwa imani kubwa nakuu kabisa fuatisha pamoja nami maneno haya, au sala hii ya toba ili uweze kuokoka, Sema;

BWANA YESU, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NATUBU MBELE ZAKO LEO, NISAMEHE NA NINAKUOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, TAFADHALI LIANDDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NINAKUKIRII NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, HAKIKA WEWE NI MUNGU NA ULIFUFUKA KATIKA WAFU, Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombi, sadaka kwa njia ya M-Pesa, kupiga simu au Wasats App, ni +25559859287. Tupo Arusha Tanzania.

Kwa undani wa Mafundisho au Habari zetu tembelea; www.ukombozigospel.blogspot.com .
#MwalimuOscarSamba #UgMinistry #UkomboziGospel #MwalimuOscarVitabu #Neno #Biblia #Zaburi #Pic #Picha #Tanzania #Afrika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni