Jumatatu, 10 Juni 2019

Endelea Kumkumbusha Mungu, Kamwe Usiwe Kimya, Kaza Kuomba Bila Kukoma !

Kukaa kwako kimya kutamfanya Mungu nae kunyamaza, ila kuendelea kumzongazonga kwa maombi yako na sadaka ndiko kutakakomfanya kutokutulia, na kisha kukupatia majibu yako upesi !

Amejiaidia mwenye hapa ! Isaya 62:1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
:2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.

Daudi anatuambia kuwa katika taabu yake alimlilia Bwana, kisha naye akasikia kilio chake ! Sijui wewe katika taabu yako huwa unafanyaje ?


Mimi naimizwa kukwambia tu kuwa Mungu ni mwaminifu, naye atakupatia haki yako upesi, ama haraka !
Najua umeliombea hitaji hilo kwa muda mrefu sasa, ila nikutie tu moyo kuwa Mungu amekusikia, wala hajaenda likizo au kukusahau kama wewe uzanivyo !

Na sauti,au mawazo yanayokujilia yanayonuia kukufanya uache kuomba, au uliweke kando hilo hitaji sio sahihi hata kidogo ! Sio ya Kiungu ! Bali yananuia kukuzuilia mujiza wako ! Yanataka kufanyika kizuizi cha majibu yako ! Ni kikwazo cha wewe kufikilia hatima yako !

Usiwe na Kimya ehwe mwenye kumkumbusha Bwana !
Maana Yeye aliyekuadia ni mwaminifu kwako ! ( Amini tu mpendwa na uinuke sasa usonge mbele !)

Naomba uniruhusu nimalizie na swali hili muhimo maishani mwako ! ( Asante) Je umeokoka ?
Kama bado nakuimiza kufanya hivyo sasa maana mujiza wa kwanza ni wewe kuupokea wokovu, kisha mengine ni ziada, pili wokovu hukufanya kuitwa mwana yaani mtoto wa Mungu, na baba huwa mwepesi kumjibu nwanae, kwa hiyo wokovu utarahisisha majibu yako !
Kwa hiyo hujaokoka na unataka kufanya hivyo sasa tafadhli kwa imani kubwa nakuu kabisa fuatisha pamoja nami maneno haya, au sala hii ya toba ili uweze kuokoka, Sema;

BWANA YESU, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NATUBU MBELE ZAKO LEO, NISAMEHE NA NINAKUOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, TAFADHALI LIANDDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NINAKUKIRII NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, HAKIKA WEWE NI MUNGU NA ULIFUFUKA KATIKA WAFU, Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombi, sadaka kwa njia ya M-Pesa, kupiga simu au Wasats App, ni +25559859287. Tupo Arusha Tanzania.

Kwa undani wa Mafundisho au Habari zetu tembelea; www.ukombozigospel.blogspot.com .
#MwalimuOscarSamba #UgMinistry #UkomboziGospel #MwalimuOscarVitabu #Neno #Biblia #Zaburi #Pic #Picha #Tanzania #Afrika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni