Alhamisi, 13 Juni 2019

Jifunze Kuongeza au Ombea Imani yako ya Kupokelea Majibu

Aina za Imani katika Kuomba, na Mwalimu Oscar Samba
 ( Unapohisi imepungua, au itapungua, ingia kwenye maombi maalumu, ) awali ya yote nikufunze kuhusi imani ya kuomba, au aina ya imani ambayo hukusukuma au hukuwezesha kufanya maombi; Marko 11:23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Wakati unaomba, unatakiwa kutokuwa na shaka, na uamini kile unachokihitaji, au kukiamrisha kiwe, kitakuwa, ama itakuwa kama vile ulivyokusudia au kunuia moyoni mwako. Ukisema ugonjwa huu toka, pona, uwe na hakika unachokihitaji kitakuwa, na ugonjwa utatoka. ( Hii ni imani inayotumika muda wa kuomba.)

Sasa ukishaomba, inakuja imani au inatakiwa iwepo imani ya kupokelea majibu, nikiwa na maana kwamba yale uyaombayo, au uliyokwisha kuyaomba, unatakiwa kuamini kuwa yamekwisha kuwa yako, pia imani hii itakusaidia kuendelea kushikilia wingu la maombi, na kukusaidia mara kwa mara kurejea katika imani ya kuomba, na kukuwezesha kuomba bila kukoma, ikiwa ni sehemu ya uhusiano uliopo kati ya aina ya kwanza na ya pili, na fahamu ya pili haiwezi kuja bila ya kwanza kufanya kazi yake.

Na sababu kubwa
ikuwezeshayo kudumu au kupokea nguvu ama kusaliwa na nguvu za kuomba bila kukoma ni hii, ni kwamba hii ya pili, imebeba saburi, ama ni yenye uvumilivu na matumaini katika Kristo Yesu.

Tuione; Marko 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

Unaambiwa ukishasali, amini ya kwamba unayapokea ! Alafu ndipo yawe yako !

Sasa ukiwa mwanafunzi uliyenielewa sasa natumai utaweza kujibu hili swali langu sasa ! Petro alipoanza kutembea juu ya maji, na kisha kuzama, na Yesu kumwambia mbona uliona shaka, ewe wa imani haba, alikuwa akimaanisha kuwa alipungukiwa na aina ipi ya imani ?

Natumai umeshaanza au umekwisha nijibu wala haujatupia macho kwa hara aya iliyofuta ukitarajia kuchungulia jibu hapo ! Pia jibu ni lazima liwe na maelezo au sababu za kutosha, maana hili sio swali la " multiple choice" ama la kuchagua jibu sahihi.

Nami nasahihisha jibu lako ! Ni kwamba alipungukiwa na imani ya pili, maana ya kwanza inaonekana dhairi alikuwa nayo, yaani ile ya kuombea, ndiposa aliweza kuomba akisema Bwana ikiwa ni wewe niamuru nije juu ya maji, naye kuamriwa.

Baada ya hapo yakupokea majibu ilianza kutenda kazi, na kisha kuanza kutembea, sasa adui akaijaribu kwa kuleta wimbi, kwa bahati mbaya hofu iliingia ndani, na kuzaa shaka, hali iliyo adui mkubwa sana wa imani, (na wasomaji wa kitabu chetu cha Imani wananielewa,) ndipo imani ilipopungua, na kujikuta akishindwa kudumu katika mujiza wake.

Kisa hiki ni muhimu sana kwetu maana wapendwa wengi hujawa na imani hii kwa mara ya kwanza waombapo, huwa na imani kubwa sana, ila wanashindwa kudumu katika kungoja, kuwa na uvumilivu au taraja au kushindwa kumuhesabu Mungu kama mwaminifu kwao, na kisha hujikuta wakipoteza nguvu za kutembea juu ya maji na kuanza kuzama !

Kipimo au mtihani mkubwa sana wa hii imani katika maombi lengwa huku kitabuni ni muda ! Kwamba, kama Mungu angejibu mwaka jana, au juzi, au wiki iliyopita kuna watu wasingekata tamaa kabisa, na wasingehesabiwa kuwa walipungukiwa, ni sawa na kwa Petro, sijui alipiga hatua ngapi, lakini kama angefanikiwa kumfikia Yesu akiwa katika hatua za awali, hakika asingeitwa na Yesu mwenye imani ndogo, au shaka na woga tusingeviona, ila kuna mwendo aliutembea, na ikawa kabla ya kumfikia, mjaribu akaja, na wengi wamekwama kutokana na umbali wa safari yao, utaliona sana kwa wana wa Israeli, kwamba kama safari yao ingekuwa ya siku moja, au walipoivuka bahari wangekuwa ndo wamefika, basi wengi wao wasingefia njiani, ila umbali, uliwafanya wengi kutindikiwa na imani.

Ndiposa aina hii ya imani ninaihusisha kama yenye saburi, uvumili, na tumaini, ambapo huja udhabiti au uimara wa moyo, kama Warumi 5 ifunzavyo, bila kuisahau ile Yakobo moja.

Ukimuona mtu aliyevunjika moyo katika hitaji lake la muda mrefu, na ukimwambia kuwa Mungu anaweza hana shida, ama ana imani katika mambo mengine, lakini katika hitaji lake amepoteza matumaini, uwe na hakika ni aina ya pili ya imani imeyayuka, au kupungua.

Ukimwambia Yesu anaweza kuponya, ataamini ila kwa wengine au mengine, mfano, hitaji lake la muda mrefu ni mke au mume, na hapo alipo anahitaji fedha, ukimwambia Mungu anaweza kukupa fedha, na atakwambia naamu hakika anaweza kabisa, au kama kuombea wengine katika mahitaji mengine yu aweza,  uwe na hakika amepungukiwa na imani hii kwenye hitaji alilomngoja nalo Bwana, maana imani ya kuomba, na kuombea mengine tayari anayo, ila ukitaja hitaji husika liloonekana gumu kwake, huachi kupokea mrejesho wa utofauti.

Kabla ya kukuleta kwa Zakaria, ngoja tuendelee na Petro, alikuwa akizama kwa kupungukiwa na imani kama Yesu anavyotujuza, ila bado alikuwa akimuamini Yesu, ndiposa alimuita au alipiga yowe akimtaka amsaidie asizame, hapa najifunza kuwa alimuamini Yesu kuhusu kumsaidia kuzama, ila alipoteza imani katika kumuamini Yesu kuhusu kumsaidia kuendelea kutembea juu ya maji, japo awali haikuwa hivyo !

Yowe yake ilinuia kupeleka ujumbe kwa Yesu kuwa nisaidie nisizame, na sio nisaidie niendelee kutembea juu ya maji ! Yaani aina ya imani yake ilibeba taraja la kuwezeshwa kuokolewa, na sio la kuwezeshwa kuendelea na kutembea juu ya maji !

Na leo tuna maombi mengi mbele za Mungu tena ya yowe, sio ya Mungu nisaidie niinuke tena na kuendelea kutembea juu ya maji, bali ni ya Mungu niokowe nisizame, ( yakinuia kushikwa mkono,  badala ya Mungu niwezeshe nitembee mwenyewe, ni kweli nazama, ila nisaidie, nitembee kwa imani, ila wengi, Yesu, niokowe, niingie kwenye boti !

Lakini lengo la awali lilikuwa ni kutembea juu ya maji, limegeuka sasa, na wengi hawajui kuwa hili ni tatizo la kiimani ! Unaweza kupokea mujiza kweli, ila ni wakukatisha safari ya kutembea juu ya maji, na kuingia potini, na unaweza kupokea mujiza kwa kufanikiwa kutembea juu ya maji, na kuzama sio dhambi, japo Yesu hukukemea, ila hoja yangu, unapoomba msaada unajawa na fikra zipi, za kuhitaji kuimarishwa ili uzidi kutembea juu ya maji, au za kuhitaji kuokolewa, na kuingia kwenye boti, ni ushikwe mkono na Yesu na kubebwa, au ni ushikwe mkono na kuimarishwa miguu na kutembea !

Waliowahi kumuinua mtoto mdogo anayejifunza kutembea watakubaliana nami, kwamba kuna unayemuinua, na kumsimamisha na kumuacha atembee mwenyewe, na kuna unayemuinua, na akitaka kumuacha tu, ataanguka tena, au atalia, na kutaka abebwe !

Jipime, na ikupe kuwa na fikra mpya kama kweli umenuia kuhakikisha unaipindua dunia kwa kuwa jitu la imani, au unaupendeza moyo wa Mungu kwa uhusiano wenu kuimarika.

Tuje kwa Zakaria sasa, alikuwa na imani kwa Mungu, ila sio kwa swala lake, au hitajio lake la mtoto, yamkini ilikwepo ila ilisalia ndogo sana, inawezekana unajiuliza unajuaje hayo ?

Tazama alipokuwa akifanya shuhuli za kikuhani, ikiwa na maana kwamba alikuwa akiombea wengine, kwa hiyo, alijawa na imani kuwa Mungu atajibu maombi ya wengine, lakini sasa alipokuwa akijuzwa kuhusu majibu yake na malaika, tunaiona shaka, na malaika kutumia sentesi kwa kuwa hukusadiki au hukuamini, ikiwa na maana kuwa, kuna namna imani ya kupokea majibu yake ilitindika. ( Tafadhali kitabu kikitoka kitafute.)

Ila nakuomba uniruhusu kuhitimisha ujumbe huu kwa kusihi kumpokea ikiwa ni baada ya kumuamini Yesu Kristo moyoni mwako kama Bwana na mwokozi wa maisha yako, ili upate uhakika wa kwenda mbinguni kama ukitwaliwa leo, lakini pia au kubwa zaidi ni ili uyaishi maisha ya kumpendeza Bwana, uwe na maisha aliyoyakusudia Mungu hapa duniani na kisha kule mbinguni, na hii ndiyo itakayokuwekea mazingira makubwa zaidi ya wewe kujawa na imani zote mbili, maana imani hubebwa na neema, na neema imo ndani ya Kristo kama Yohana moja isemavyo kuwa alimuona akiwa amejaa Kweli na Neema, sasa ukimpata Yesu ni umepapa vyoye! Karibu sasa kwenye wokovu.

Mpendwa , kama hujaokoka na unataka kufanya hivyo sasa tafadhli kwa imani kubwa nakuu kabisa fuatisha pamoja nami maneno haya, au sala hii ya toba ili uweze kuokoka, Sema;

BWANA YESU, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NATUBU MBELE ZAKO LEO, NISAMEHE NA NINAKUOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, TAFADHALI LIANDDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NINAKUKIRII NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, HAKIKA WEWE NI MUNGU NA ULIFUFUKA KATIKA WAFU, Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombi, sadaka kwa njia ya M-Pesa, kupiga simu au Wasats App, ni +25559859287. Tupo Arusha Tanzania.

Kwa undani wa Mafundisho au Habari zetu tembelea; www.ukombozigospel.blogspot.com .
#MwalimuOscarSamba #UgMinistry #UkomboziGospel #MwalimuOscarVitabu #Neno #Biblia #Zaburi #Pic #Picha #Tanzania #Afrika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni