Jumatatu, 10 Juni 2019

Upako ni Kulipa Gharama

Nimeandika hivi, katika kitabu chetu cha NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA !
Najifunza kitu kisichochepesi kwa Elisha ! Natumai unajiuliza ni kipi tena hicho Mwalimu ! Ni hiki ! Elisha alikuwa na msimamo sana, maana Elia licha ya kumpa upinzani mzito ili kuuhakikisha moyo wake kama kweli umekusudia, kuna mthihani mwingine alimpa mara baada ya kuomba ombi lile !
2 Wafalme 2:10 Akasema, Umeomba neno gumu; lakini, ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona, hulipati.
Ni baada ya kuomba upako mara dufu, sasa Elia anampa shariti, kuwa akimuona saa anaondoka, atapokea, la hakumuona, hatapokea !
Huu ulikuwa ni mtihani muhimu sana, na kwa
umuhimu huo ulimbidi Elisha kuhakikisha anaushinda !
Kuna mambo mengine yanatokea maishani mwetu tukiwa tunaomba, kama mitihani, sasa sijui huwa unashinda, au unasema kama ni hivyo basi, maadamu nikifa nitaenda mbinguni, yatosha hata nisipokuwa na gari, nisipokuwa na nyumba, Mungu anajua nampenda !
Huku nako ni kukosa ufahamu na bidii ya kukaza katika kuupata mujiza wako ! Ni kweli wote wapo mahali pema peponi, Ibrahimu Tajiri na Lazao Maskini, ila huyu aliacha alama kutokana na maisha yake, na huyu hatuoni alama ya mwilini njema nje ya sifa duni ya umaskini !
( Kama kweli umedhamiria kuendelea kuishi maisha duni kwa sababu za kushindwa kukaza sawa, ila usije ukahuburi kuwa Mungu ndivyo alivyo, ila kiri wewe ndivyo ulivyo ! Elisha angekwama bado Elia asingelaumiwa, ukitaka kufanya kazi ya Mungu chini ya kiwangi sawa ila usije kusema Mungu wa siku hizi sio wa Matendo ya Mitume, wa wakina Elia, na Elisha waliotenda miujiza, la ! Sema wewe wa siku hizi au nyie wa siku hizi, au wale wa siku hizi sio kama wale wa zama hizo, maana kupokea kutoka kwa Bwana kuna gharama zake !)
Wengine hata kufunga na kuomba kwao kumesalia kuwa historia, ni wazito hata kwa maombi ya nusu saa ! Sasa unatarajia nini ? Elia aliomba kwa bidii, wewe unaomba kwa ulegevu, kisha unataka mfanane ! Kweli ! Basi huyu Mungu atakuwa amebadilika ! Ila kama ni yule, jana leo na hata milele, uwe na uhakika na kanuni walizozipitia wakina Petro, Paulo Mtume, Elia, na Musa, ni lazima nasi tuzipitie ! Japo kizazi cha leo kina neema zaidi, maana wapo kwenye Agano lililo bora zaidi, (na kuna wepesi wa kuhubiri zaidi) kwani Damu yake imelifanya vivyo, lakini ndicho kilichogeuka na kuwa duni, na dhaifu zaidi, maana adui amewatwika uvivu na uzito zaidi, malalamiko ni mengi, kuliko kuchukuwa hatu, wanataka miujiza na ishara ila hawapo tayari kulipa gharama !) ( Naye Shetani akaaa pembeni na kujiinulia nguvu "feki" na ishara "feki," na wengi wamemlaki.
Mpendwa , kama hujaokoka na unataka kufanya hivyo sasa tafadhli kwa imani kubwa nakuu kabisa fuatisha pamoja nami maneno haya, au sala hii ya toba ili uweze kuokoka, Sema;

BWANA YESU, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NATUBU MBELE ZAKO LEO, NISAMEHE NA NINAKUOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, TAFADHALI LIANDDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NINAKUKIRII NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, HAKIKA WEWE NI MUNGU NA ULIFUFUKA KATIKA WAFU, Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombi, sadaka kwa njia ya M-Pesa, kupiga simu au Wasats App, ni +25559859287. Tupo Arusha Tanzania.

Kwa undani wa Mafundisho au Habari zetu tembelea; www.ukombozigospel.blogspot.com .
#MwalimuOscarSamba #UgMinistry #UkomboziGospel #MwalimuOscarVitabu #Neno #Biblia #Zaburi #Pic #Picha #Tanzania #Afrika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni