Ijumaa, 9 Juni 2017

MSAADA WA KIROHO KWA WANAOOTA NDOTO WANAKULA VYAKULA, NYAMA, DAMU ,IKIWA NI SEHEMU YA MAAGANO YA KIPEPO. Sehemu ya 2.

 Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Kwa furaha isiyopikama kwa Uzani wala Mizani ninakukaribisha tena katika sehemu hii ya pili na ya mwisho ya makala yetu, na ni rai yangu kama jana hukufanikiwa kusoma sehemu iliyotangulia basi yakupasa kuitafuta ili tuweze kweda sanjari.
NAMNA WATU WANAVYOINGI MAAGANO HAYA YA KIPEPO. Unapokwenda kwa mganga, na mganga kukupa mashariti, ya kufanya fahamu mashariti hayo ni sehemu ya agano la kipepo, kwa bahati mbaya wengine hulazimika kuingia ama kufanya kiapo cha uaminifu ama chakuto kuvunja au kukiuka mashariti hayo. Sio kwa waganga tu bali hata wa lewatu wa Fremason, Ilumineta na kadhalika.
Na agano hilo huwa na nguvu sana pale atakapokuhitaji kumwaga damu, mfano wapo wanaoambiwa walete kuku, mbuzi ama kondoo na hata ng’ombe. Na mganga humchinja. Pale anatafuta kulitia nguvu ama kulikamilisha lile agano. Kumbua Agano jipya maandiko husema kuwa lina nguvu kwa sababu ya mauti ya Yesu. Andiko tulilolisoma hapo juu la Luka tunamuona Yesu anasema  damu hiyo iliyo ndani ya kikombe ni Agano Jipya, ile imwagikayo. Maana yake damu ile ya kuku na mbuzi ama wengine hutoa kafara ndugu zao, kipepo ni agano pia.


Mambo haya ni magumu na ni yakificho mno, wapo wanaodai yakwamba sababu za mganga kudai kuku ama wanyama ni ili ale, haya ni mafundisho mapotofu, na husema ni kwa nini asidai mboga za majani. Labla kama mganga huyo ni wauongo ila kama kweli ameitwa na Shetani fahamu anakuingiza kwenye kitazi kibaya mno.

Damu inapo mwagika aridhini huifanya aridhi kuambatana na jambo ama maneno yaliyonenwa na agano hilo kwa bahati mbaya sana hukaa katika aridhi na huwa na nguvu maana aridhi ni lango kwenye ulimwengu wa roho. Ndio maana Yesu anatamka fika ya kwamba damu yake imwagikayo kwa ajili yenu. Maana yake kipepo ile ni damu imwagikayo kwa ajili ya jambo lililokupeleka kwa mganga.

Ikisoma kitabu kile cha mwanzo utaona swala hili la damu kukaa katika aridhi. Tufunguwe, Mwanzo 4: 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
Inapolia maana yake inahitaji jambo fulani, na kwa Kaini ilihitaji ulipizwaji wa kisasi. Fahamu maandiko yanasema kuwa Damu ya Yesu inanena mema kuliko ile ya Habili, ikiwa na maana kuwa hata damu ya kiagano maana damu ya Yesu ni yakiagano nayo pia hunena mneno ama hulia.
HATARI YA AGANO HILI LA DAMU, unapolifanya hataka kama Shetani akiwa amebanwa na shuli nyingi na kutokutilia maani, ni fika ile aridhi inamkumbusha na kumwmabia yamkini mika mia ama mia mbili kuna babu wa fulani alifanya agano na kusema watoto wa nyuma hii ama ukoo huu au kabila hili fulani halitaolewa hadi watakapo toa sadaka kwa miungu ya mahali fulani. Haiishi hapo bali hujenga na hoja; Sasa mbona huyu mtu anataka kuoa nje ya makubaliano haya, au huyu fulani ametukiuka na kuoa nje ya mpango huu, ninataka ndoa hii ivunjike.

Ndiposa unashangaa katika ndoa kunatoke magonvi yasiyo na mwisho, alikadhalika katika uchumi mambo hayo hutokea. Unakuta kuliwepo na maagano kama hayo ndio maana wenzangu wakabila moja nami kila ikifika mwezi fulani ni lazima akaweke mambo yake sawa kwa njia ya kimizimu, na anapokaa mjini na kukumbwa na matatizo, hukimbilia kufanya mambo fulani nitakayo yagusia hapo mbeleni. (Kwa  kifupi ni matambiko)

Na hata kama umeokoka mambo hayo hutokea, na Mungu atakapo jaribu kukutetea maana maswala ya rohoni huenda kwa haki usifikiri kwa kuwa ni Mungu basi atatumia nguvu ama fujo kukusaidia. Maana fahamu Mungu na Shetani kuna wakati wanakaa kikao na kujadili na Shetani fahamu nimshitaki wetu, kama yupomshitaki basi yupo hakimu na kama yupo hakimu yupo mstitakiwa ama mdaiwa, mashahidi ambaye hapa ni ardhi, ushahidi, ambao hapa ni kiapo, cha umaninifu na sadaka ile ya damu uliyompatia mganga, au fedha. Kwani mwilini havipo ila rohoni vimeifadhiwa kwenye masijala ama stoo au kwenye mafaili ya kumbukumbu, kuzimu na aridhini.
Ila wakili wetu ni Roho Mtakatifu huku Yesu akisimama kama Hakimu na katika hili aridhi inaleta ushahidi wake kama ilivyokuwa kwa Kaini na hatimaye Mungu kumuhukumu kaini. Ni dhairi pale ukisoma kwa jicho la tatu kuna jambo la ajabu sana utaliona, nalo ni hili, kwa fikra zangu pevu naliona kwamba Mungu ni kama vile hakutaka kumuadhibu kaini kwa adhabu ile na alihitaji kutulia zaidi lakini Sauti ya damu ya Marehemu kutoka aridhini ilimsukuma ama ilimfanya ashindwe kustaimili.

Ndio maana gadhabu ya Mungu ilielekea kwenye aridhi, na Mungu hakuwa na shida ama haja ya kulaani kitu kingine bali ni hiyo aridhi. Mwanzo 4: 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Tarama hapo mahali laana ilielekea, Kitu cha ajabu hapa Mungu anasema haya; “umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;” Nataka uone kwamba kwenye aridhi kuna kinywa, na ilifungua na ikanywa hiyo damu.
Sasa chakunishangza hapa ni kwamba aridhi hii ilikuwa na maamuzi ya kukubali ama kukataa kuhusu kufa kwa Habili ikiwa na maana ingeliweza kufunga kinywa chake na kugoma kuinywa hiyo damu. (Mpendwa hili sio somo la aridhi tukutane kwenye somo hilo). Tuendelee;
Sasa Nataka kukutoa hofu kabla ya kuendele na mwendo huu wa pole, Katika yote hayo ipo damu iwezayo kukukomboa ambayo ni Damu ya Yesu inayonena uzima kwako. Na hapo mbeleni nitakupa matumizi yake katika kipengele cha kanuni za kukusaidia.
Maagano haya huwa na namna ambavyo yanahitaji kutiwa nguvu ama kurepewa, ndio maana kwa wanaofanya biashara za kichawi ama za kishirikina, hutakiwa kutoa sadaka za umwagaji wa damu ama nyinginezo ikiwemo za vyakula kwa kufanya sherehe nakuwalisha watu kwa gaharama kubwa bila sababu ya msingi  angali mtu huyo akiombwa msaada yamkini asiwe ni muungwana wakutoa.Ufanyaji huo ni kulipejea agano hilo. Na wanaoshiriki hicho chakula huwa katika hatari ya kuingizwa kwenye hilo agano.

Alikadhalika kwa wanaofanya mila, ukiona watu wanafanya mila jua wanalipa agano la kipepo nguvu na kama mila hiyo ni yakikabila ama tambiko hilo ni lakikabila jua aliyeaingi agano hilo alikuwa ni muasisi ama adamu wa kwanza wa hilo kabila. Alikahalika kama ni la ukoo, fahamu aliyeingia agano hilo ni mwanzilishi ama muasisi wa huo ukoo na pia yaweza kuwa ni kiongozi aliyekuwa na nguvu mno.

Siku kadhaa zilizopita niliota ndoto fulani nikiwa nyumbani kwetu, na kuna jambo lilikuwa likifanyika, katika ile ndoto nikamuona mtu akiwa ameshika kwenye chombo ambacho hupenda kuitwa; “kikontena” nadhani ni kwa sababu ya muundo wake, kwa wasio kijua ; ni kama kibakuli cha pembe nne ama kipo kama kiboksi ila ni cha plastki.

Alikuwa akiongea maneno fulani na kile chakula kilikuwa kikibadilika rangi, kisha nikamkazia macho na yeye kujikuta akiropoka ya kwamba anaonge na adamu na hawa.

Punde niliamka na kuanza kutafakari ndoto ile. Roho wa Bwana akanipa tafsiri ifwatayo. Chakula ni mapatano katika agano, na kubadilka kwake rangi huko ni kwamba mapatono hayo hubadilika badilika kulingana na nyakati ama pia agano hilo limeundwa na maagano mengi kiasi chakuwa na mpatano tofauti tofauti.
Wasomaji wa bibilia hususani kitabu cha Mwanzo wanafahamu kuwa Agano la Ibrahimu na lile la Nuhu ndani yake yana maagano mengi madogo madogo. Kwani karibia kila mahali Mungu alipoona jambo fulani aliongeza nyama katika hilo agano na pia liliongezwa kwa Isaka na hatimaye kuwa dhairi kwa Yakobo.

Alikadhalika ndiyo ilivyokuwa kwangu, kisha adamu na hawa waliwakilisha mababu wa asisi wa agano husika. Waweza kuwa katika ngazi ya kitaifa, nchi, bara, kabila, ukoo na hata familia. Kumbuka pia ndoa ni Agano.

Ndio maana kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaotaka kuingia madarakani ni vigmu kwao kama katika nchi hiyo muasisi wake; Fikra, Falisafa na chama chake bado kingali kinatawala na hakuna chama kingine kilichowai kuingi katika nafasi hiyo. Na hili kufanikiwa yawapasa kutambua agano husika alilofunga na kiti hicho kisha waanze kulishuhulikia. Pia fahamu na ishara za hilo agano.
Kwa wengine ishara huwa ni Mwenge, ama Sanamu fulani, ndio maana ukienda katika mataifa mbali mbali duniani utakuta sanamu za waasisi wa mataifa hayo katika maeneo fulani muhimu au miungu yao.Usipoikuta katika njia panda, basi ni katika lango la mjia, ufukweni mwa bahari au eneo muhimu katika mji husika. Na wakati mwingine kwa bahati mbaya sana mambo haya huwekwa hadi kwenye nembo ya taifa.

Ni ruhusu nitoke huko kwenye sura yakiutawala wa serikali, pia katika kabila ambalo unataka kulifanyia ukombozi yakupata kufahamu mambo hayo kiundani zaidi. Nashindwa kwenda mbele zaidi katika mukutadha huo maana somo hili sio la kimaagano moja kwa moja bali ni la chakula katika maagano.

Ila fahamu kuwa maagano hao ndiyo yanyowapa nguvu wa asisi hawa, ndiposa kila mwanzilishi wa taifa ama wa jambo fulani huwa na heshima kubwa na hata kama alifanya mambo ya kawaida ama ana mapungufu mengi watu hawawezi kuona hayo mapungufu badala yake huishia kumtukuza na anayejaribu kuyafumbua au kuyasemeya , huonekana kama ni msaliti ama muasi angali ukichimba kwa kina kirefu kupitia  fikra yakinifu huwezi kuliona hilo hilo kosa analothumiwa nalo.

Ni kweli nimenena mengi ila niruhusu kwa wakati huu nikujuze mbinu zitakazo kusaidia kukutoa hapa, na ninamumba Mungu anipe kibali cha kuandika kitabu cha NGUVU YA AGANO KIROHO, Ashukuruwe Mungu wakati huu ananiambia kipo. Nami moja kwa moja nimsha tengeneza Folder na hatimaye Faili kwa ajili ya kuanza kuchangamkia tenda hi. Katika hicho kitabu nitakujuza kiundani maagano ya kimungu na namna ya kuomba kiagano na siri ya watu wanaoomba kwa jina la Mungu kama Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ila kwa kifupi maombi hao ni yakiagano na matumizi ya Damuya Yesu na Jina la Yesu kiagano.
MBINU ZA KUKUNASUA NA ADHA HIYO YA KUOTA UNAKULA CHAKULA CHA KIPEPO.
Awali ya yote yakupasa kufahamu ya kwamba, jambo hili lina nguvu kwako hata kama wewe hukuhusika katika kulifanya hilo agano, na yamkini liliingiwa wewe ukiwa haupo duniani nikiwa na maana kabla hata ya kuzaliwa kwako. Kumbuka Mungu katika kitabu kile cha Ezekieli ananena na wana wa Iziraeli kuhusu matatizo yanayowakumba na kuwaeleza chanzo chake kilitokea kabla hata wao hawajawa taifa kama ilivyo kwa wakatati ule.

Ezekieli 16: 3 useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti.
4 Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.
5 Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa.
Wasomaji wa bibilia wanafahamu fika ya kwamba, Asili ya Iziraeli sio makabila hayo kwa upande wa kimbari ama kindugu, bali ni Ibrahimu, Isaka na Yakobo na hakuna aliyeoa katika makabila hayo maana tuna ona kuoa kwa Ibrahimu naye alichukizwa an makabila hayo na kisha kumtaka mtumishi wake kumtafutia mke mwanaye Isaka kwa watu wa mbara ya kwao kwa wakina Labani na hatimaye Isaka kumrithisha hilo kwa Yakobo ambaye pia alienda kuoa binti za Labani mjomba ake.

Sasa nisikilize ili kuipata mantiki ya kimungu kiusahihi anapowataja watu wa makabila hayo kama sehemu ya uovu unao wakabili na ukisoma msatari wa pili wa sura hiyo anamtaka Ezekieli kujuza uovu wao na ndipo anataja asili ya makabila hayo ambayo kiukweli yalijawa na matendo maovu.

Sasa maana ya Yesu ni hii, Mantiki ya Mungu hapo ipo kwenye aridhi waliyokuwa wakiikalia wana hawa wa Iziraeli ambayo kiasili ilikwua ikimilikiwa na hayo makabila, ya Wahiti, Wakaanani, na hata Waamori na kadhalika. Kwa hiyo maagano waliyoyafanya na miungu yao yalisalia katika ile aridhi na wana Waiziraeli walipofika au walipoamua kuishi hapo hawakukikata kile kitovu ama kiunganishi kati ya aridhi na watakapo ikalia hiyo nchi.
Ni kweli waliwafurumusha baadhi ya adui kimwili, ila kiroho hawakufurumusha miungu yao ama maagano yao. Ndio maana baada ya muda walijikuta na wao wanaanza kufwata tabia za asili za lile eneo. Na usipotazama mambo haya kiundani unaweza kujiuliza chanzo cha mzabibu mwema kubadilika kuwa mbaya.

Ila ashukurwe Mungu anayemtumia Nabii Ezekieli ili kuwanasua hapo na nina shaka kama hawa watu walimuelewa vyema huyu Mtumishi, na wewe jitaidi unielewe vyema. Mungu alishaanda mpango wakuikomboa hile aridhi ndiposa toka katika jangwa aliwapa mikakati ya kuangusha maashera yao, sanamu na hata miungu yao kazi ambazo hawakuiamalizia ama kuifanya kiufanisi.

Ni kweli hata kwako Damu ya Yesu ilishamwagika ila usipoitumia kuikombo aridhi unayoishi hutaweza kuwa huru na utakuta mbona ukiishi eneo fulani unakuwa tofauti na eneo jingine. Kwani wapo watu wakilala sehemu fulani huota hizo ndoto na wakiwa eno jingine huota nyingine ama hawaoti kabisa. Siku chache zilizopita nilikutana na kijana mmoja aliyeniambia kuwa akiwa nyumbani haoti ila kuna mahali akilala huota ndoto anafanya mapenzi ama anazini ndotoni na wanawake ama na wapenzi wa zamani kabla hajaokoka.Nilijua namna ya kumsaidia nami nilimnasua hapo. Na leo ni ukombozi wako.
1. KOMBOA ARIDHI UNAYOISHI, Katika kitabu changu cha Ndoto na kile cha Malango kwenye ulimwengu wa roho nimelifafanua jambo hili kwa kina kipana zaidi na hapa sitazama kama humo. Katika aridhi unayoishi hakikisha ya kwamba, unaiombea rehema. Kuombea rehema ni kutubu ama kuomba maombi ya toba kwa ajili ya maovu yaliyowai kufanyika katika hiyo arihi, ikiwemo maagano ambayo yaliingiwa kwa njia mbali mbali ikiwemo ile ya kumwaga damu za kafara za wanyama, ndege na hata zile za wanadamu. Ya kupasa kuomba kwa muda mrefu hadi upate amani ya Bwana.
2. TAKASA MAVAZI, NA MALAZI, Usikubali kulala kitanda kigeni, (ama hata hapo nyumbani kwako,) na kulalia malazi yake bila kuombea rehema mahali hapo kwani hujii kilichowai kufanyika hapo na uwenda ikawa aliwai kulala mtu aliyegombana na mwenzake na usiku kucha alikuwa akitafakari hayo na kuazimia mabaya na uwenda walilala watu waliopatana ama kuazimia kumhuru mtu fulana. Ombea rehema kwa kina na fanya hivyo, hata unapokuwa  hotelini au kwa rafki yako, na yamkini ni kwao ulitoka kwa muda mrefu na umerudi safarini. Pia ombea rehema nguo mpya utakayo inunua na ile uliyoiazimisha kwa mtu. Usipende sana kuazimisha nguo kwani nguo hubeba roho na ukilazimika kufanya hivyo basi ibadike mikono, alikadhalika kwa nyumba mpya utakayo iamia ama chumba, milango na madirisha na kuta zibandike mikono.
Baada ya kumea rehea vitu hivyo yani mavazi na malazi, anza maombi ya kuvitakasa kwa adamu ya Yesu kisha mfukuze Shetani hapo. Fanya maombi haya ya utakaso hata kwa njia ile ya kwanz aya Aridhi, na maombi ya kumfukuza Shetani ni yale ya vita.

3. SHUHULIKIA MAAGANO KITOBA, Ingia katika maombi ya Rehema kwa kuombea toba au rehema kwa kitendo wewe kujiingiza kenye  maagano kwa kujua ama bila kujua au cha wazazi waasisi wa kitu husika ama mababu na mabibi kuingi maagano hayo na jina ama nafsi yako kuingizwa huko. Tubia uovu wao kwa maombi ya kumaanisha kwani fahamu kuwa dhambi zao ama maagano yao huweza kukudhuru na wewe pia. Katika kitabu kile cha Maombolezo tunaona ya kwamba makosa ya wazazi wao yaliwaingiza hatiani wana wa Iziraeli. (Maombolezo 5:7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao.)
Maana yake ni kwamba maagano ya waliokutangulia hukudhuri nawe pia. Tubia dhambi zao kama alivyofanya Danieli, Kitabu kile cha Danieli; Danieli 93 Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.
4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;
5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako;
6 wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.
Danieli angeweza kujifanya wa kiroho sana kwa kutokuona haja ya kutubia uovu wa marehemu, ila alijua ya kwamba wamechukua matokeo ya uovu huo. Kumbuka na fahamu kuwa kusudi la kuomba kwako sio kuwaombea waliokufa wasamehewe bali ni kumtaka Mungu akutowe wewe katika hiyoo hatia kwa yeye kusahau ama kufuta kilichotokea maana rehema hufanya dhambi iliyokuwa nyekundu kama bendera ama damu kuwa nyeupe kama dheluji na mara baada ya ukombozi huo ndipo Shetani na Aridhi hukosa uhalali na hatimaye kukuwezesha kufwata hatua inayokujia hapa mbeleni.
Ila kabla sijakujuza njia hiyo Murwa na Mubashara kiukombozi nataka kukuonyesha msisitizo wa hoja hii ya kutubia maovu ya walihusika na maagano hayo. Maombi ya Danieli kenye huwo mstari wa 6 sura ya tisa anataja wahusika hawa hapa, “1. wafalme wetu,  na 2.  wakuu wetu, na 3.  baba zetu.” Maana yake ni kwamba hao ndio waliohusika katika hilo tatizo.

Na wewe yakupasa kutambua kiundani wa husika wa maagano unayoyashuhulikia na kama huwajui usiwe na Shaka wewe muombe Yesu na kwa mkono wa Roho Mtakatifu atakujuza aidha kwa ndoto ama kwa sauti ama kukupa msisitizo wa kuombea sehemu au mtu fulani na anaweza kukuongoza katika maombi ya kunena kwa lugha ambayo ni mazuri sana katika maswala haya ya ukombozi maana Yeye anayekuongoza hutuombea vyema tena kusiko tamkika na hufahamu mbinu za kufanya zaidi, kwa hiyo ukinena usifanye haraka kuchomoka hapo.

4. FUTA HAYO MAAGANO, (njia hii ya 4 na ijayao ya 5, unaweza kutanguliza moja wapo kama jinsi roho atakavyokuongoza ingawaje wapo wanaoshauri kuwa ni vyema zaidi kutanguliza ya 5. Ila sikiliza Muongozo wa ROHO na kama uwezo wako wa kuomba na nguvu zako sio mkubwa basi ni wangu ushauri kutanguliza ya 5).

Tumia Damu ya Mwanaume Yesu ambay ina uwezo wa hali ya juu wa kufuta hayo maagano yote na tayari aridhi kama shahidi na Shetani kama Mshitaki wetu na wa ndugu zetu hataweza kusimama mahakamani ili kupinga jambo hili maana tayari maombi ya rehema yameshafuta hatia zote na maovu yote na kuondoa ule ushahidi wa sadaka na viapo vya kimaagano. Na punde Shetani atakapohitaji kukata rufaa na kuchungulia kabla ya mafaili ama Msijala,(Eneo la kutunzia kumbukumbu). Akiingia hapo hatakuta chochote na aridhi itamwambia kuna mtu aliomba rehema na naliona Damu ya Yesu kama Mafuriko ya mto yakipita hapa na kufuta kumbukumbu zote na kuodoa usadidi wote.
Kumbu kama tulianza pamoja vyema kuna mahali nimekujuza kuwa aridhi ni kitu hai na kina kinywa, ndio maana ilifunguka na kuwameza wakina Kora na Dathani na  Abiramu na kundi lao kipindi kile cha Musa kwenye Hesabu kumi 16 hicho ni kitabu kilichopo kwenye Agano la Kale.

Pia ilifungua kinywa na kunywa damu ya Habili, Tuendelee: Pia inamasikio ya kusikia, Tulihakiki hili hapa, Yeremia 22: 29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana.
Nchi inayotajwa hapa ni Aridhi.
Pia inauwezo wa kuandika, hii inamaana kuwa wakati maagano yananenwa aridhi hii huchukuwa kalamu na kufanyika dafutari ama faili kwa ajili ya kutunza makubaliano yaliyopo kwenye agano husika na tuhakiki jambo hili kwenye mstari unaofwata.
Ni Yeremia 22:30 Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.

Ndio maana wapo watu wanaoapa ama wanaoapizana na kutema mate angani na kisha aridhini au kukikitia kidole mate, kisha kulamba udongo wa aridhi na hatimaye kuweka ishara ya kiapo. Jambo hilo ni hatarishi sana.
Tumia Damu ya Yesu kufuta hayo maagano na ni rahisi sana omba maombi haya kwa muda mrefu hadi uone mpenyo na ni mazuri ama huwa na nguvu zaidi kama yatakuwa ni yakufunga na kuomba.
NAMNA YA KUOMBA KWA KUTUMIA DAMU YA MWANAUME YESU; (Kwa jina la Yesu Kristo na kwa mamlaka aliyonipa, ninajitakasa na kuomba rehema, ninatumia Damu ya Yesu ile iliomwagika kwa ajili yangu, na ninaifanya kuwa futio, “Dasta”, Dekio na mafuriko ya Damu isafishayo; Ninafuta maagano yote, [kama unayafahamu unayataja]. niliyoingia na yale niliyongizwa kwa kujua ama kwa kutokujua, kwa Damu ya Yesu, futika, kwa Damu ya Mwana kondoo ninafuta na kukushinda wewe Pepo unayesimamia hayo maagano.)
Yaombe kwa muda wakutosha na tumia silaha hiyo ya Damu ya huyu Kidume Yesu aliyeshinda kifo pamoja na Mauti.Mungu anawezakukuonyesha kama alivyowai kunionyesha mimi jambo hili na ni hakika niliona Damu ikifanya kazi yake.
5. TUO JINA AU NAFASI YAKO KWENYE HAYO MAAGANO, Kilichofanyika kilikuingiza kwenye hayo maagano hata kabla hauja zaliwa. Fahamu Yesu aliingizwa kwenye Agano ambalo Mungu alifunga na Dudi kwenye Zaburi ile ya 89 kabla hata haja zaliwa. (Zaburi 89: 3 Nimefanya agano na mteule wangu, Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu.
4 Wazao wako nitawafanya imara milele, Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.
)
Tulifwatiliye hadi kwenye kitabu kile cha Yeremia,Yeremia 31: 31 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.  Kumbuka Agano Jipya ni Yesu mwenyewe kwa wale tulikuwa nao pamoja, tumepita katka darasa hilo na ni pale anapotaja Damu yake na Chakula chake, kwa hiyo ukitajaka Agano Jipya fahamu ndani ya mabano unagusa vitu hivyo ambavyo ni Yesu mwenyewe.

Tusonge mbele na Ufwatiliaji huo, Yeremia 33: 15 Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii. 
Tuhakikishe kama kweli Chipukizi linalotajwa hapa ni Yesu au La! Fungua bila woga kitabu kile cha Ufunuo wa Yohana kitabu ambacho ukinikuta nakifundisha hutatamani kutoka kwenye hilo darasa.
Ufunuo wa Yohana 5: 5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.

Umeona hiyo?, “Shina la Daudi,” Pia ukifwatilia katika andiko hilo la Yeremia katika pia sura hizo zote unaona hilo la Simba wa Yuda ama Yerusalemu yakigusiwa humo pia.

Hapo Yesu hajazaliwa ila tayari ameshaingizwa kwenye Agano na kupewa majukumu. Kama tulivyoona kwenye kitabu kile cha Yeremia ambacho ni cha Agano la Kale, na Yesu anazaliwa Agano Jipya.
Na maagano hayo yakipepo ndivyo yalivyo, kabla ya wewe kuzaliwa walisha sema, hutaolewa na mtu wakabila jingine, ukiolewa naye hutazaa, ama hamtadumu kwenye ndoa, hutafanikiwa nje ya mila zao. Au ukiacha mila ama kuoka uchumi unakuwa mgumu mno. Ndiposa unajuzwa kwa njia ya ndoto kwamba wewe ni wa kwetu, huwezi kujenga bila sisi, huwezi kudumu kwenye ndoa bila sisi, huwezi kuacha kufanya uganga ikiwa ni mrihi wa mikoba ya bibi. Katika hayo yote fahamu ya kwamba ni maagano ndiyo yanayokutaabisha, ila leo kama Ezekieli alivyotumwa kwa Wana wa Iziraeli nami nimetumwa kwako nikiwa nimembeba huyu Yesu aliyeshina la Dadu na chipukizi la katika hilo shina kukuletea ukombozi.
Kwa hiyo hakikisha unaitoa nafsi yako kwenye hayo maagano ama jina lako na maombi hayo omba hivi:
(Katika jina la Yesu Kristo na kwa kutumia Damu yake, najitakasa na kujiombea rehema kwa hatia yoyote iliyopo juu yangu, nami nakaa katika nafasi ya kikuhani kama maandiko yasemavyo kwenye Agano Jipya ya kwamba kila aliyekuamini we amefanyika kuwa kuhani. Natumia Damu yako na jina lako la Yesu Kristo lenye Nguvu ya Msalana kulitoa jina langu kwenye maagano yaliyofanywa na mababu, viongozi, mmi mwenyewe na yale yaliyopo kwenye aridhi. Kwa Jina la Yesu Krsisto ninafuta kumbukumbu zangu huko, na itoa nafsi yangu huko.)
Endelea kuomba hadi uone ukombozi na maombi hayao yafanye kwa kumanaisha na imani ilyokuu.
6. FANYA MAREJESHO. Hii ni hatua ya mwisho kabisa na hulenga kukusaidi kufanya marejsho kwa vile vitu vilivyoaribiwa ama kuibiwa wakati uhai wa hilo agano. Na maombi haya yafanye kwa njia ya kuamuru yaani tumia mamlaka ya kimungu kuita kila kilichopotea, kufichwa ama kufungiwa magerezani. Pia kila kilichokufa wewe fufua kwa jina la Yesu Kristo.
Tuanze kutazama namna ya kutumia mamla ambayo tunaipata kimaandiko kwenye Bibilia. Kitabu kile cha Isaya, andiko hili litakusaidia kufungua kila kilichofungwa, kama ni kwenye ndoa yako, uchumi na hata kwenye huduma, litakupa uwezo wakuitisha kibali kilichoibiwa ama kufichwa.
Ni Isaya 42: 22 Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.
Kwa iyo ingia kwenye maombi muda huu na useme RUDISHA KWA JINA LA YESU.
Lipo andiko la Ayubu 20 ambalo hukutaka kumtapisha adui aliyemeza baraka zako, nalo pia litumiye kumtapisha.
Ni Ayubu 20: 15 Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.
Ingia kazini na hilo andiko sasa, omba kwa kumaanisha na tafuta mahali utakapo kuwa huru zaidi.
Usisite kutumia andiko hili pia, Ambalo hufanya fidia kwa vilivyoharibiwa, kufa, ama kupotea. Kumbuka kile ulichowai kukipoteza ama kilichokuponyoka kipindi cha uhai wa hayo maagano na kisha ingia kazini kwa hasira ya Roho Mtakatifu.

Ni Yoeli 2: 25 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. Tumia maandiko yote hayo ili kufanya marejesho.
Kufikia hapa katika safu hii sina la ziada ila ninakutaka kuendelea kufwatilia makala zetu ili kupa mwanga zaidi katika maswala haya na pia lipo somo nimeliandaa la namna ya kujinasua kutoka kwenye matatizo ya kuridhi. Pia somo hili nitaliweka kwenye kitabu hicho cha Nguvu ya Agano Kiroho.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                       PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple                                              
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni