Jumanne, 13 Juni 2017

Mwalimu Oscar Samba, MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA. 2

Na Mwandishi wetu wa Ug Ministry
Nina Kusalimu katika jina la Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha Yetu, ni yangu taraja kuu ya kwamba huu mzima tena buheri wa afya. Ninakukaribisha katika makala hii fupi inayolenga kukujuza mafundisho ya Neno la Mungu yaliyofundishwa jana na Mwalimu Oscar Samba katika viwanja vya skolo la Morombo hapa mkoani Arusha.
Kama alivyoaidi kuanza na pwenti ya kuutafuta kwanza ufalume wa mbinguni na haki yake ndivyo ilivyokuwa jana. Mwalimu aliwataka watu waliokoka kuwekeza nguvu nyingi katika kumtafuta Mungu kwenye nyaja zote na kisha kumuomba maarifa, Moyo wa Akili na wa Hekima katika swala la uchumi na maisha kwa ujumla kama ilivyokuwa kwa Mfalume Sulemani na kisha Mungu kumpatia Utajiri.
Alisema kuwa wapendwa wengi hupenda kuomba fedha lakini hawaombi kufahamu kanuni za kupata fedha, alitoa mfano na kuwafananisha na mtu anayependa kupewa samaki badala ya kupenda kufundishwa namna ya kuvua samaki huku akibainisha kuwa Mungu akimfundisha kuvua basi ni lazima ampatiye na Ndoano.

Ninamnukuu, "Tatizo kubwa la watu waliokoka siku za leo, wamekuwa wepesi wa kupenda kuomba kupewa fedha, jambo ambalo ni zuri ila sio sahihi sana, ni kama mtu anayependa kupewa samaki badala ya kupenda kufundishwa kuvua samaki. Na Mungu akikufundisha kuvua ni lazima akupe na Ndoano."
Mantiki yake kubwa hapo ilikuwa ni kuwataka wakristo kuwa na Akii ya kufundishwa kufanya biashara na Mungu kisha kumtakaYeye awape Maarifa, Hekima, Akili, ili waweze kuimili hiyo biashara vyema.
Kumbuka Mpendwa kuwa Hekima hiyo ndiyo itakayokusaidia kuimili hiyo biasha vyema maana bila Hekima ya Kimunguu biashara ikichanua inaweza kukutoa kwa Yesu, Ndiposa Mwalimu akasema;
"Kuna watu waliokuwa wakifanya usafi kanisani, kudeki na hata kufuta viti, ila mara baada ya kuanza biashara na kufanikiwa jambo hilo wameacha na hapo awali walikuwa ni waaminifu kuudhuria ibadani kila siku ila mara baada ya biashara kuwa kubwa wamejikuta wakishindwa kuudhuria tena ibadani kama ilivyo ada"
Kwa mujibu wa Mwalimu, haya ni matokeo ya kukosa Hekima ya kumiliki Mali, ndiposa Mfalume Sulemani alipopewa Hekima alipewa na Mali maana Mungu aliamini kuwa hataangamia, na kwetu sisi kama hatutapata Hekima hii mali itatuangamiza. Alitoa mfano uliosadifu jambo hili.
Ninamnukuu tena hapa; "Ukisoma ule Mfano wa Mpazi, unaelezea ya kwamba kulikuwa na mbegu zilizoanguka kwenye miiba na kusongwa, tafsiri yake inasema kuwa ni kusongwa na shuhuli nyingi na udanganyifu wa mali. Maana yake ni kwamba mali hudanganya na ukikosa Hekima ya kuimilki ndipo utapotea. Utamkuta mtu anashindwa kwenda ibadani kwa sababu mali imemwambia twende leo kazini ili umaliziye lile deni ama ile oda, pia huweza kumwambia kuwa kumbuka kesho ni marejesho."
Pia Mwalimu alitoa pwenti ama Mbinu nyingine ikiwemo ya AKIBA, Alibainisha ya kwamba mfumo wa kuweka akiba kwenye benki ama vibubu kama waswahili wanavyo viita; (ikiwa na maana ya kibosi cha nyumbani cha kuifadhi fedha), Ni mfumo ambao Mungu amempa Mwanadamu ili aweze kufanikiwa kiuchumi.
Alitoa mafano wa kipindi kile cha Utawala wa Mfalume wa Misiri yaani Farao kulikuwa na taarifa za uwepo wa njaa na Farao aliposikia lile jambo aliogofia sana ila Yusufu alipewa na Mungu Akili na Hekia iliyolenga kumpatia Farao mtu atakayemsaidia kuweka akiba.
Mwanzo 41:33 Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri.
34 Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba.
35 Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji.
 36 Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa.
37 Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote.
Sanjari na hayo pia alisoma maandiko ya kitabu kile cha Mithali yanayomja Chungu yaani Sisimizi ambaye ni mdudu mdogo ila amejaliwa kuwa na akili ambayo inamsaidia yeye kujiwekea AKIBA.
Mithali 6:6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7 Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu,
8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
Akiba hiyo anaiweka kipindi cha chakula, ama shibe ila baada ya kipindi hicho kuisha huja kipindi cha mvua ambacho asingeweza kujipatia riziki na huitumia ile akiba aliyoiweka.
Alikadhalika kwa wana wa nuru jambo hilo latupasa kulifanya, aliongeza kuwa inampasa mpendwa kujiwekea akiba maana kuna vipindi tofauti tofauti vya kimaisha ikiwemo kile cha Hari ama Ukame pia Uchache wa Mvua kama maandiko yanavyovitaka kwenye kitabu kile cha Yeremia 17.
Yeremia 17:8b....Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.
Kama ndivyo hatuna budi kulifahamu hili, alisistiza Mwalimu. Hakuishia hapo bali alitanabaisha ya kwamba kuna kipindi hapa nchini sukari iliadimika na watu wengi walihaha kuitafuta, ila waliokuwa na akiba waliishi salama.
Pia alisema kuna aina mbili za akiba ambazo alizichambua jana, ya kwanza ni hiyo aliyoanza nayo ya maswala ya mali na ya pili ni hii ya Kujiwekea Hazina Mbinguni, alisema maana yake ni kutoa sadaka na utoaji huo unaweza kuufanya kwa kuwapa yatima, wajane ama masikini kama alivyofanya Korinerio. Na kisha kuitwa Mchaji Mungu.
"Usikubali jirani yako akalala njaa wakati wewe una chakula, akikuomba chumvi mpe na kiberiti, hujui kesho kwako yatakuwaje, ama hatima ya watoto wako, kwani leo yamkini una nyumba, una magari, una feha ila nyumba ya weza kuungua moto, na magari kupata ajali. Lakini kama utawekeza kwa kutoa sadaka ni fika kwamba sadaka hizo zitakaa kama akiba na siku ya uhitaji zitakusaidia, wewe ama wanao."Alibainisha Mwalimu
Alisema pia, ni jambo jema kuwatembelea wagonjwa magerezani na kuwalisha, maana Yesu anasema kuwa atatuambia nalikuwa gerezani ila hamkuja, nalikuwa uchu hamkunivika, nalikuwa na njaa ila hamkunilisha. Maana yake ni kwamba kuwatendea watu kama hao ni kumtendea YESU.
Aligusia kwa kifupi pia aina nyingine ya akiba ikiwa ni kutenda wema, kulia na wanao lina ikiwemo kwenda misibani na kushiriki matukio mbali mbali ya kijamaa, alisema kwamba hata kama utakayemtendea hayo hata kuja kwako basi fahamu kuwa siku ukipatwa na wewe akiba ile itakuinulia mtu atakaye kusidia.
Mungu akubariki sana kwa kuwa pamoja nami, ila Mwalimu alihitimisha kwa wito kwa watu ambao hawajaokoka kumjua YEYE maana hakuna ajuaye muda anaoweza kufa maana wapo walioanguka na kufa, waliofia usingizini na hatujui ujio wa MWANA wa ADAMU Maana atakuja kama mwivi.
Watu walikubali kumjua Yesu nami pia ninakutaka na wewe kukubali ili ukifa sasa uwe na uwakika wa kwenda mbinguni na jambo hili tulilolinena la kufanikiwa kiuchumi linakuwa halisi kwako maana mbinu hizi ni halisi zaidi kwa waliokoka.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple#MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple, PAGE:https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni