Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug
Ministry.
Haijalishi
umeachwa ama kukataliwa kwenye Ndoa, Mwenzako amekuacha ama ni Mchumba amekusaliti,
Umekataliwa kazini na hatimaye kufukuzwa.
Ama umekosa kibali mbele ya wapendwa kanisani kwako au viongozi wako wa kiroho
wamekukataa na kukutelekeza na imefika hatua ya wewe kujiona kama mtu
aliyeachwa.
NISIKILIZE,
Leo nimekuletea TUMAINI na TUMAINI hili ni YESU KRISTO aliye Bingwa wakuwakumbatia
waliokataliwa na kuachwa. Ni kweli jambo ama mambo hayo yanaumiza na mimi
katika uzoefu wangu wa miaka isiyofika Theladhini hapa Duniani kwani umri
wanguni ni miaka 28 na siku tatu, nimebaini kwamba kama kuna mambo ambayo
huujerui moyo; Kukataliwa ni miongoni mwayo.
Ukitaka kuamini, jaribu kumwambia mtoto mdogo
asiyejua hata kunena ya kwamba unampenda atatabasamu na hata kuachia kicheko,
ila punde umamwambiapo kwamba haumpendi, ama unamchukia tabasamu lile hugeuka
kuwa simanzi. Ndio maana mtu anapokuwa kwenye tatizo ama uhitaji na kisha kuwaona
watu hawaguswi na tatizo lake ni rahisi sana kuumia zaidi.
Ndiposa
kwenye misiba wafiwa mara nyingi huzungukwa na watu, huku wakiwafariji na
wengine huacha shuhuli zao na kuamua hata kulala kwao ama kujumuika nao kwa
muda mrefu. Hiyo yote ni kuwaondolea upweke.
Jambo hili
liliwai kumsumbua Mfalume Daudi, Zaburi 69: 20 Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa
kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
Nifika kwamba alitamani mtu wakumfariji ila alimkosa. Na wewe kama umefika hapo Usijali wala usiumize Kichwa maana Yesu yupo tayari kufanyika Faraja yako leo.
Kitabu kile
cha Zaburi kina chambua jambo hili na tunapata TUMAINI la ajabu sana hapa,
kwani unapopapitia pia Mtumishi huyu
aliwai kupapitia na alitambu haya kwamba ni Mungu mwenyewe pekee ndiye awezaye
kumpa Faraja hiyo. Fungua nami kitabu hicho;
Zaburi 27:10 Baba
yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake.
Umeona
Mukutadha wa hilo andiko? Anasema kuwa wazazi wake wamemuacha ila Mungu
atamkaribisha kwake. Kwa hiyo kwako wewe kilicho cha Msingi ni kuhakikisha ya
kwamba unasimama katika mstari wa Mungu majira kama haya ili Mungu akukaribishe
kwake.
Tatizo kubwa
kwa watu wengi leo wanapojikuta wamekwaruzana ama kuachwa au kukataliwa hujikuta
wanatupa maneno, kujibu hoja kwa njia za “mipasho,” kukasirika ama kuweka
kinyongo au kushindwa kusamehe walio wa udhi.
Shetani
akifanikiwa kukuumbia vitu hivyo basi jua hali yako itakuwa ngumu maana MUNGU
hata kukaribisha kwake, maana tayari umeshajitengenezea Mazingira ya wewe kujitetea ama kujipigania.
Kuna kisa
kimoja kilichozaa chanzo cha wimbo wa Baba na Mama wakiniacha sitarudi kwamwe,
sitarudi;
Kisa hicho
ni hiki hapa. Ilikuwa ni nchini India, ambapo kulikuwa na binti mmoja aliyeamua
kuokoka na wazazi wake wakamuonya ila alikataa kumuacha Yesu, kisha wakampeleka
ufukweni mwa bahari kwa ajili ya adhabu ama kumuacha au kumtenga kabisa na
familia yao maana wao waliamini miungu ila binti bado aliendelea na msimamo
wake.
Wakiwa
ufukweni tayari kwa ajli ya jambo hilo, Ndipo walipoanza kujitenga, Upako wa
Mungu ulitiririka na kisha mtoto huyu kujikuta akijawa na nguvu za Mungu na
kuimba huo wimbo. Kwa upako huo wazazi wake walishindwa kuvumilia na kuhairisha
jambo lile. Leo hii wimbo huo umekuwa ni wabaraka kwa watu wengi mno.
Ilitokea India
na hata leo inatokea kwa wengi wanaoamua kuokoka katika familia zenye mazingira
magumu kama hayo, wewe ikikutokea fahamu kama mtunga Zaburi anavyo Nena “Baba
yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake. Zaburi 27:10 .”
Kila la heri;
Cha msingi hapa usikubali kumuacha Yesu kwa sababu ya kuachwa ama kukataliwa na
wanadamu maana kwa ndiko liliko TUMAINI la kweli; kwani ukimkimbilia Yeye
hutaaibika.
Yule mama
aliyetokwa na Damu kwa muda ule wa miaka 12, alitengwa na kukataliwa na jamii
yake kwa kuonekana kuwa ni najisi na hali ile ilikuwa ni kama msiba kwake ila
alitambua ya kwamba msaada na TUMAINI lake ni kwa YESU pekee.
Alipomkimbilia
tu, Punde misiba yake ikakoma hapo hapo, aliyeitwa najisi, akapata kibali na
kuwa maarufu mbele ya maelufi ya watu katika makutano na hadi leo tanasoma
habari zake.
Huyo Binti wa
India alimkimbilia Yesu akijua kuwa ndiye TUMAINI lake na amekuwa maarufu hadi
leo, mimi na wewe tunaimba wimbo huo. Na wewe hakikisha unamkimbilia Yesu ili
siku moja vizazi vijavyo vikukumbuke kwa tendo hilo la Ujasiri huku maelufu kwa
mabilioni na hata matrilioni ya watu wakitiwa moyo na jambo hilo.
Ninakutakia
maisha mema ya ushindi katika Kristo Yesu huku nikikusihi kuendelea kufanya
maombi ya vita ili kuoma kibali kwa wanaokupinga na pia kumuomba MUNGU akutiye
nguvu katika majira hayo huku nawe ukijilinda ili usijibize neno kwa neno wala
usitende lililobaya ama kujiwekea kisasi au kukasirika, vitu ambavyo vinaweza
kukutenga na YESU na kumfanya asikukaribishe kwake.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata
habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Pia kwenye
mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni