Jumatatu, 12 Juni 2017

NGUVU YA AGANO . Sehemu ya 2.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Kwa furaha na tabasamu mwanana ninachukua muda huu kukukaribisha katika sehemu hii ya pili ya makala yetu ikiwa pia ni masomo yaliyopo kwenye kitabu changu cha NGUVU YA AGANO KIROHO.
Jana tuliishia katika kipengele cha pili cha Agano la Mungu na Ibrahimu lilolenga kumbariki kiuzao, Kiroho na hata kiuchumi. Kipengele cha kwanza tuligusia Baraka za uzao na kusema kuwa Mungu alimpa Isaka japo umri wake ulipita na sababu kubwa ikiwa ni Ahadi iliyokwepo kwenye lile Agano, Na ya Pili ilizungumzia Baraka za kiuchumi ambazo pia tutaziangazia hapo mbeleni zaidi. Sasa tuangaziye ya leo.
(c) Mungu alimjuza kuhusu maswala yajayo, Unapokuwa ni Mtu wa Agano, Mungu hawezi kukaa kimya bila kukujuza maswala muhimu katika hilo Agano. Fungua nami maandkyo yafawatayo:
Ni Mwanzo 15: 13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.

14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.
15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.
16 Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado.


Tunaona hapo Uzao unatajwa, na tuliokuwa wote katika darasa hili wanakumbuka kuwa Uzao ni sehemu ya hili Agano, pia anataja watarudi hapa, Hapa panapotajwa ndipo mahali ambapo Mungu aliwapa yaani KANANI ama Nchi ya Ahadi, na Ahadi hiyo ipo kiagano.
Mambo hayo yote Ibrahimu anajuzwa ikiwa ni Faida ipatikanayo katika Nguvu ya Agano.

(d) Mungu analinda maisha na kila kilicho chako, Wakati Ibrahimu ameelekea kwenye nchi ya Gerari chini ya Utawala wa mfalume Abimeleki, Ibrahmu kwa hofu ya kuuwawa alimnenea mkewe kuwa ni ndugu yake. Na mfalume wa ile nchi alimtwaa ili awe mkewe.
Na Mungu hakukubali  lile, kwa hiyo aliipiga nyumba ya Abimeleki kwa kuwafunga matumbo wasizae, na kisha kumuonya mfalume kwa kumtaka asimguse huyo Mwanamke huku akitoa maelekezo ya kumrudisha kwa mumewe haraka na kisha mumewe amuombee ili awe salama.

Ni Mwanzo 20: 3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.
10 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili?
11 Ibrahimu akasema, Kwa sababu naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu.
 17 Ibrahimu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana.
18 Maana Bwana alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Ibrahimu.

Sasa ni SIKILIZE, Mungu anatumia gharama kubwa Sana kumlinda Mtumishi huyu hadi kufikia hatua ya kufunga matumbo ya Nyumba nzima, Ndiposa ninakutaka kuwaheshimu sana watumishi wa Mungu maana kila Mtumishi ni sehemu ya Agano hili na lile la  la Chumvi, ambalo nitakujuza hapo mbeleni.
Katika Kipengele hiki tunamuona Mungu akimlinda Sara, na sababu kubwa ni kwamba huyu ni mali ya Agano, rohoni Mungu anasema, “Hii ni Property ya Agano, kwa hiyo Mfalume huyu hawezi kumgusa.”
Si unafahamu kuwa bila Sara hakuna Isaka, na bila Isaka hakuna Yakobo na bila Yakobo hakuna Iziraeli? Kwa hiyo wote hao ni mali ya Agano. Ndio maana katika kuoa kwao Isaka anaelekezwa mahali pa kwenda kuoa, na Yakobo pia nae analekezwa m ahali na babaye, huku Isaka akiletewa mke na Mtumishi wa baba yake aliyepewa maelekezo yote.

Kwa nini? Jibu ni kwamba Agano hili lilihusisha Uzao, kwa hiyo kila anayehusika kweye Uzao ni Mali ya Agano. Si unakumbuka kuwa aliaidiwa kuwa na Uzao  kama Nyota, ama Mavumbi au Mchanga wa Baharini ama Ufukweni. Kwa hiyo chochote kilicho najisi kingepita hapo ni fika kingeharibu Uzao huo ama kingetia dosari hili Agano.
Baada ya kulitazama Agano hili kwa Sura ya Ibrahimu, hivi sasa tulitazame kwa Sura ya Isaka akiwa ni mwana wa Ibrahimu.
Kwa Isaka Agano hili lilikuwa na Baraka kubwa sana kwake kwani wakati wengine wakijiuliza pakwenda kuoa ama namna ya kulipa mahari na kuwapata watu wakwenda naye ukweni, kwake mambo yalikuwa mepesi. Tujionee kwa mapana zaidi.
Na jua unatamani kuyaona mambo hayo ila muda kwangu ni kama Wavu wa umme nikishindana nao hakika utanirusha mbali ama kuninasa, nami nalihofu hilo, natumai hata nawe kwani nikinaswa hutampata Mwalimu tena na kwako usingalipenda litimiye hilo kwa maana Mwalimu amekuwa wa Baraka sana kwako. Nikutake kuwa tukutane Kesho na ni yangu ahadi kuwa nitaendelea na hapo pa Isaka.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                      
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple    Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni