Aliinuka Sauli mfalme enzi za Biblia na kujaribu kupigana na shauri la Bwana akimuwinda Daudi aliyekuwa mfalme mtarajiwa kila kona lakini mwisho wake alijikuta akiishilia kwa mganga wa kienyeji na hatimae shauri la Bwana kushinda ndani ya Daudi !
Yamkini huyo anayepigana nawe hana hata cheo cha ubalozi wa nyumba kumi, na uwenda hakuwahi kuwa hata kiranja alipokuwa shule !
Sasa kwa nini uogope ! Ni kwa nini ukubali kutishwa na mwenye mwili wakati yupo awezae kuuzima kwa dakika ama sekunde moja na hata nusu sekunde !
Enzi za wakina Petro ama kanisa la kwanza aliinuka mtu mkoja aliyeitwa Herode, na kujipiga kifua mbele za Mungu wetu ila mwisho wake aliishilia kutafunwa na mdudu hadi kufa !
Farao alijifanya kupigana na taifa teule na mwisho wak
e majeshi yake, na farasi zake wakawa maiti, maandiko husema waliona miili za maiti zikiwa kando ya pwani; Kutoka 14:30 Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa.
Wakati adui anapambana na wewe kuna kitu kimoja kikubwa sana huwa kinatokea ! Nacho ni hiki hapa !
Wewe unazidi kuchanua kwa yeye anadidimia, na ndivyo ilivyokuwa kati ya Daudi kijana wa Mungu na yumba ya Sauli aliyemuasi ama kumkataa Mungu; 2 Samweli 3:1 Basi kulikuwa na vita siku nyingi kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi; Daudi akaendelea akasitawi, lakini nyumba ya Sauli ikaendelea kudhoofika.
La umuhimu ni wewe kuhakikisha tu unatenda kwa akili au kwa busara, na hii ni kanuni muhimu sana itakayokusaidia kuepuka kumpa adui au Ibilisi nafasi, na kadri utakavyokuwa ukifanya kwa busara ndivyo utakavyokuwa ukistawi, maana adui huweza kukutegea mitego akinuia akuangushe au akunase, aje aseme siniliwambia kuwa huyu kijana ana kiburi, si niliwahi kusema hamkuniamini kuwa huyu ananidharau kumbe la ama wala ! Kijana wa watu alizidiwa na kujikuta uchungu unamfanya kufanya maamuzi magumu, ama kama mwanadamu alilemewa na kuamua kuondoka, lakini kwako wewe isiwe hivyo, msikilize Bwana daima na ijapo kuondoka utajua tu huu ni wakati wa Bwana kama Daudi alivyofanya maana hata Yonathani alishuhudia kuwa ulikuwa ni wakati wa kuondoka.
Sasa wewe majira haya,amua au tenda kwa akili, sio kwa hasira wala kwa kujilipizia kisasi, la ! Bali ni kwa akili,ili uweze kutegua mitego yao;1 Samweli 18:9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.
14 Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye Bwana alikuwa pamoja naye. 15 Sauli alipoona ya kwamba alitenda kwa busara sana, yeye alimwogopa.
Ukiwaona wanakuandama sana, uwe na hakika kuna wivu umeinuka ndani, maana kuna namna neema ya Bwana i juu yako ya ziada sasa matumbo yao yamepata joto wakizania utawanyanganya kazi hapo mjini, lakini hawajui kuwa kila mtu na fungu au shamba lake, maana hatujaitiwa kunyanyana kazi, labla kama amevurunda kama Sauli, na hapo anapaswa kumkasirikia muajiri ambaye ni Mungu na sio wewe !
Fahamu sana kila utakapokuwa ukitenda kwa busara ama hekima kwao ni kama fimbo ! Hapo Sauli alimuogopa kwa kutenda kwake vyema ! Ni kama Yesu kwa mafarisayo !
Alipokuja aliwakuta wameshatangulia mjini, wao ndio waliopewa kukaa katika kiti cha Musa kama Matahyo 3 isemavyo, ila hawakutenda kwa akili, walijibinafsishia huduma, walilifanya hekalu kuwa pango la wanyanganyi, sasa kaja mwenye kazi wakasema huyu ni mrithi na tumuuwe, lakini kila walipokuwa wakijaribu kumtega kwa maneno, na vitendo Yesu aliwajibu kwa mafumbo na akili kuu, hapo walizidi kuchanganyikiwa na kutafutana.
Utendaji wa akili, utakuongezea sifa katika utumishi, au eneo lako la kazi; 1 Samweli 18:21 Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa mkwe wangu.
29 Naye Sauli akazidi kumwogopa Daudi; Sauli akawa adui yake Daudi sikuzote. 30 Wakati huo wakuu wa Wafilisti wakatoka; kisha ikawa, kila mara walipotoka, Daudi akatenda kwa busara zaidi ya watumishi wote wa Sauli hivyo jina lake likawa na sifa kuu.
Ukitaka heshima, wewe tenda kwa akili, ukitaka adui zako wathoofike na kusalia magofu, wewe tenda kwa akili ! Wakikununia wewe cheka, wakiwa na njaa wapelekee kipande cha makate, wakiambizana wasikusalimu wewe wasalimu mara mbili mbili, maana kwa kutenda hivyo unawapalia mkaa ama makaa ya moto katika vichwa vyao, na hayo makaa hakika hayataacha bali yatawateketeza, na baada ya muda kidogo usishangae wanageukiana wao kwa wao, ona upaliaji huo unavyokuwa;
Warumi 12:19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. 20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. 21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Yamkini adui zako wanaringia vyeo vyao, wanajivunia fedha zao, wanajikinga na nafasi walizo nazo ! Hilo lisikusumbuwe wewe jivunie jina la Bwana, (hili nimeliweka kwenye matendo na limenivusha mahali, kwa hiyo nakufunza zana na silaha ya kivita niliyoifanyia majaribio na kuona matokeo yake chanya maishani ,) mtu mmoja akaniambia lakini siunajua huyu ni mtu fulani kiwathifa, mimi nikampa andiko ambalo siku hizo nalipewa na Bwana kuwa wao wanataja ... ila mimi nina ..
(Zaburi 20:6 Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu.
7 Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.
8 Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.)
Mpendwa mtazame Yesu ! Hakuna aliyewahi kushinda na haki akashinda ! Ninachojua maandiko husema mwenye haki akaa milele naye hataondoshwa !
Na kama hujaokoka na unataka kufanya hivyo sasa tafadhli kwa imani kubwa nakuu kabisa fuatisha pamoja nami maneno haya, au sala hii ya toba ili uweze kuokoka, Sema;
BWANA YESU, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NATUBU MBELE ZAKO LEO, NISAMEHE NA NINAKUOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, TAFADHALI LIANDDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NINAKUKIRII NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, HAKIKA WEWE NI MUNGU NA ULIFUFUKA KATIKA WAFU, Amen.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombi, sadaka kwa njia ya M-Pesa, kupiga simu au Wasats App, ni +25559859287. Tupo Arusha Tanzania.
Kwa undani wa Mafundisho au Habari zetu tembelea; www.ukombozigospel.blogspot.com .
#MwalimuOscarSamba #UgMinistry #UkomboziGospel #MwalimuOscarVitabu #Neno #Biblia #Zaburi #Pic #Picha #Tanzania #Afrika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni