Ijumaa, 27 Machi 2020

Mwalimu Mwakasege Atoa Wito wa Kushiriki Maombi Dhidi ya Ugonjwa wa Korona

Anaandika katika mtandao wa kijamii ;
Bwana Yesu asifiwe.
Hili ni ombi kwa kila aliyewahi kuhudhuria kongamano letu,la maombi la kitaifa, tunalofanyia Dodoma kila mwaka. Lakini,hata kama hujawahi kuhudhuria kongamano hilo-ombi hili linakuhusu pia.Tunajua umekuwa ukiombea tatizo la ugonjwa wa 'Corona'. Pamoja
na maombi hayo ufanyayo, tunakuomba utenge muda utakaoona unafaa kwako,(kufuatana na mazingira uliyonayo),siku ya jumamosi tarehe 28 machi 2020,uombee kwa angalau muda usiopungua saa moja-mambo yafuatayo:
1).Toba kwa lolote ambalo halikumfurahisha Mungu,na likafungua mlango wa ugonjwa wa 'Corona' kutokea na kuenea nchi mbalimbali,pamoja na Tanzania;
2). Uponyaji kwa waliougua ugonjwa wa 'Corona';
3). Uponyaji wa uchumi  katika maeneo yalioathirika kutokana na ugonjwa wa 'Corona';
4)Ugonjwa wa 'Corona' usiendelee kuenea.

MUHIMU:
i) Simamia mistari hii ya biblia: Ezekieli 22:30,31 na 2 Mambo ya Nyakati 7:13,14,15

ii) FUATA TAHADHARI YA SERIKALI JUU YA MAKUSANYIKO. OMBA UKIWA PEKE YAKO AU WATU WAWILI AU WATATU SAWA NA MATHAYO 18:19,20

Toka kwa Christopher na Diana Mwakasege Arusha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni