Alhamisi, 18 Novemba 2021

Maelekezo Muhimu kwa Watumishi na Wapendwa

 Kuna wakati tunampa adui nafasi sisi wenyewe, wanapata nafasi ya kutushitaki kutokana na makosa ya ulimi na mwenendo.


Ila tukijifunza kutenda vyema, kwa akili kama Daudi alivyokuwa akitegewa mitego na mfalme Sauli kisha naye kutenda kwa maarifa, hakika adui hatapata uhalali wa kututia hatiani.


Hata akipambana itakuwa ni kwa hila tu, na hila zinamwisho wake.


1 Samweli 18:21 Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa mkwe wangu.


:29 Naye Sauli akazidi kumwogopa Daudi; Sauli akawa adui yake Daudi sikuzote.


Mbinu pekee ya kumshinda adui wa namna hii ni kutenda kwa akili, hususani adui anapokuwa ni mwenye nafasi fulani ikiwemo kubwa kukuzidi kama ya mchungaji wako, mwangalizi, askofu na kadhalika, na hata mkuu wako wa idara au kiongozi fulani.


Ama akiwa ni mwanandoa mwenzako. Busara inahitajika siku zote, maana kwa nafasi yake anaweza kukushitaki na kukuhesabia hatia japo nia yake sio kosa alilokushitakia bali ni ile chuki iliyopo moyoni, na wewe ili kumdhibiti ni kuhakikisha unamnyima nafasi.



:30 Wakati huo wakuu wa Wafilisti wakatoka; kisha ikawa, kila mara walipotoka, Daudi akatenda kwa busara zaidi ya watumishi wote wa Sauli hivyo jina lake likawa na sifa kuu.


Zaidi tembelea:

www.ukombozigospel.blogspot.com


Zaburi 119:110 Watendao uovu wamenitegea mtego, Lakini sikuikosa njia ya mausia yako.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni