Jumanne, 5 Oktoba 2021

KUPENDA MAFUNDISHO au NENO

 Na Mwalimu Oscar Samba

Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu cha NGUVU YA NENO LA MUNGU KWENYE MAISHA YA MWANADAMU, pwenti ya; . PENDA MAFUNDISHO. Kiu ya Mafundisho imepotea kwenye kanisa leo; kuna kiu ya mambo mengine! Hata kwa wale wenye kiu ya Kiungu, wamejikuta wakitekwa na misisimko wa wahubiri wenye mbwembwe na kujisifia mali, na vitu vya dunia hii sanjari na ujanja wa maneno kuliko neno la kweli na yale yenye maarifa ya kiungu ndani yake. Itisha semina ya VIKOBA au ujasiriamali kanisani, utashangaa hata mwenye wiki tatu ambaye hajaja kanisani atakavyowahi, siku hiyo hakuna mchelewaji! Tuendelee;

Mahubiri, mawaitha ya Yesu,

nasaha za kiroho zenye mrengo wa maadili safi, mafundisho ya neno la Mungu. Utafutaji wa maarifa kwa njia mbalimbali ni sehemu muhimu sana itakayokuwezesha kupata kunufaika na neno la Mungu. 

Ila ukikwama hapa ni umekwama katika ujumla wa jambo hili la kunufaika na neno la Mungu. Nayanena haya kwa mana leo tuna watu na sio vijana tu bali kanisa kwa ujumla wake, (watumsihi kwa washirika,) wapo ambao hawapendi maarifa.

Yupo tayari kutumia muda mwingi kuangalia na kufuatilia vitu visivyo na faida au tija kwenye maisha yake ya kimwili wala kiroho.

Mfano kutazama tamthilia, filamu, ama maigizo mbalimbali, na video nyingine hata maadili hazina. Kusoma magazeti ya udaku, ushabiki usio na tija wa kimichezo. (Maana wengine siku timu yao inacheza ibadani hawaendi, kama kuna ratiba ya maombi atajifanya haioni kisa mechi.)

Unamuunganisha mtu kwenye kundi la mtando wa kijamii wa “internet” ili apate mafundisho ya neno la Mungu, na bila sababu ya msingi anajitoa au anatoka. Lakini hakuna sababu yoyote ya kimsingi, ila jibu ni kwamba injili kwake “niboadi, anaboeka” ila utamkuta kwenye vikundi vya kishenzi kama vile vya, Cheka Unenepe, Vunja Mbavu, na kadhalika. 

Yupo tayari kuangaika na vichekesho kuliko neno la Mungu. “Post” au “Stutas” zake nyingi zimejawa na vichekesho, na vituko au vioja. Hakuna hata kitu cha kuujenga ufalme wa Mungu. Ili akujibu “sms” ni pale ulipomtumia kichekesho, sio andiko la Biblia.

Huyu naye ameokoka na amekata tiketi ya kwenda mbinguni. Hili ni tatizo na msiba mkubwa sana! Na huku Shetani na makundi yake ikiwemo ya “Freemason” wamewekeza sana.

(Huwa nasema; Simu yangu kama haihubiri injili, haina faida kwangu. Ninatamani kuhubiri injili sio na “komputa” au simu yangu tu, bali ingewezekana hata pumzi ninayovuta na kutoa, au nywele zangu, nguo zangu, ama hata kutembea kwangu kungehubiri injili.)

Data zake nyingi za “Mb” huishia kwenye kuperuzi mambo yasiyo na tija. Atakutajia tovuti au blogu makumi kwa makumi za michezo, za urembo na picha zisizo na mrengo mwema, ila hata mbili au tau za mafundisho hazijui.

 (Anajua wasanii kumi bora wa muziki duniani na nchini kwake, anaweza kukutajia kikosi kizima cha timu yake ya nchini na ile ya bara Uropa ama Ulaya, ila hajui wahubiri watatu, ukimbana atakutajia mchungaji wake, askofu mkuu, na yule wa jirani; ‘anayemuombeaga’. Ila mtake akutajie wahubiri watano wa kimataifa hajui. Ila mrembo wa dunia na nchini kwake anamjua, na hata shindandano la sasa anajua nani mshindi.) Huu sio msiba ni nini! Huyu ni mpendwa sio mmataifa..ukibisha chukua simu yako mpigie nanilii, alafu mulize haya maswali..au uliyekaa naye jirani muda huu…

Kama hujaokoka na unataka kuokoka tafathali fuatisha Sala hii ya Toba kwa imani, na pia kama umejikuta una kiu ya mambo ya kipuzi, na unataka kuachana nayo, ifuatishe pia, ni ishara ya kuingia kwa jambo jipya ndani yako, ukiyanywa haya maji, kiu ya kidunia itatoweka kabisa, haijalishai umeokoka muda gani wewe ifuatishe na tumaini jipya litaingia ndani yako, najua unanena kwa lugha, ila wewe fuatisha, kutii ni kupona, usibishe kama Naamani..

Sema; MUNGU BABA, NINAKUPENDA, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NISAMEHE, FUTA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, LIAnDIKE SASA KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE, NIPE MWANZO NA MWENENDO MPYA KUANZIA SASA, NIPE KIO KATIKA WEWE, Ameni.

Mawasiliano; Simu: +255 759859287 Barua Pepe: ukombozigospel@gmail.com

Tembelea www.ukombozigospel.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni