Jumatano, 29 Septemba 2021

KWETU NI MBINGUNI



Waebrania 13:14 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.

Sijui wewe! Ila nijualo ni kwamba Sisi Tuliokoka, ama Tuliomuamini Bwana Yesu kwetu ni Mbinguni hapa Duniani sio kwetu!

Ni sawa na kituo cha Mabasi cha Ubungo ama kile cha Mbezi, ni sawa na stendi ya Daladala au Matatu! 

Hapa Duniani ni sawa na Njiani..mimi sijafika wala wewe hujafika, bali tunapaswa kukaza mwendo, huku tukiwa na taraja ama shabaha yetu ikiwa ni kuvikwa taji ama kupata Thawabu ile isiyoharibuka..

Kwa hiyo huna haja ya kujitaabisha na mateso na shida ama manyanyaso ya dunia hii..

Wewe fahamu neno moja tu kuwa huku duniani tunasafiri, na tunakoelekea ni Mbinguni..

Huko hakuna manyanyaso ya ndoa, hakuna masimango ya mama au baba mkwe..hakuna midomo ya mawigu wala mashangazi..

Hakuna masimanggo ya wapendwa waliokengeuka.. bali huko ni faraja na furaha..huko kuna kufutwa machozi na kupongezwa kwa ushindi mkubwa..

Usiyatazame mateso kana kwamba ndio hatima yako..yageukie na uyaambie kuwa wewe siku zako ni chache, hapa sina mji udumuo, najiandaa kushuka kwenye hili gari la misiba, uchungu, umaskini na kila adha punde ijayo...

 *Tazama Wosia Huu* : 1 Petro 2:11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.

Usikubali Tamaa ya na Hanasa za Dunia hii Kukukwamisha...kaza mwendo, usiuze tiketi yako kwa rushwa ama kwa ngono ya dakika chache, kama Esau alivyouza kwa chakula cha siku moja..linda tiketi kwa Utakatifu...

Sina Mengi..ila fahamu tu kuwa..hapa Duniani tunasafiri...linda tiketi...taabu na mateso yaone kama kero ndogondogo za konda, ambapo huwa unajipa moyo "kwani naenda naye nyumbani..mimi sinashuka hapo tu..nitamuacha kwenye gari.." 

Mpendwa.."Linda Tiketi"..

Na Mwalimu Oscar Samba

Endelea Kutembelea blogu yetu ya:
www.ukombozigospel.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni