Jumanne, 28 Septemba 2021

Mtazame Yesu Sio Wimbi

 

MTAZAME YESU NA SIO WIMBI

Mathayo 14:29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

Sijui umekwamia wapi..? Nina chojua ni kwamba ulianza au ulipokea wazo hilo la biashara katika imani kubwa, na moyoni mwako ulisema huyu ni Mungu ndie aliyenipatia wazo hili, kazi hii, mke au mume huyu..ila mara baada ya kuanza kumeanza kuinuka vikwazo naq ghafula ukajikuta unaanza kukata tamaa kiasi cha kuyumbisha imani yako sio katika hilo jambo tu bali hata kwa Mungu kama kweli ulimsikia sawasawa ama kama kweli bado yu pamoja nawe..


Leo nikutake kutokuendelea kutazama wimbi, au jaribu ulilonalo bali mtazame Yesu, narudia tena kuwa mtazame Yesu na sio wingi wa adui zako..siku chache zilizopita nilikujuza kuwa unatakiwa kuomba macho yako yafumbuliwe ili uweze kuona wingi na ukuu wa Mungu kwako..

Huku awali yake nikikutaka kutokuogopa..

Petro alipohitaji kutembea juu ya maji alianza kwa imani kubwa sana, alimuamini Mungu katika viwango vikumbwa mno yamkini kama wewe ulivyoanza...

Ila bahati mbaya ni kwamba wimbi lilipotokea alijikuta anaingiza shaka! Kwa nini?

Ni kwa sababu alitazama wimbi, macho yake hayakumkazia ama hakukaza kutazama alipo Yesu bali alitazama 🌊 wimbi na kilichofuta ni kuzama..

Yesu alikwepo, naye alijua kuwa yupo ila mashaka yakamuondolea kumtegemea Yesu...

Nawe sio kwamba Yesu amekuacha la! Ila ni kwa sababu umeingiza shaka! Sii kwamba Yesu yu mbali nawe ni! Ni kwa sababu umeingiza shaka!

Na sababu ni kwamba umelegeza katika kumtazama YESU..

Kama kwa Wana wa Israel walivyopaswa kumtazama Nyoka wa Shaba aliyeangikwa mtini nao kupona, nawe huna budi kumtazama Yeye!

Hapo ndipo msaada wako utatoka..
Mtunga Zaburi alijaribu kutazama milima, akageuka huku na kule, ila hakuona msaada, alipokuja kutuliza akili na fahamu aligundua kuwa msaada wake utatoka kwa Bwana ama Mungu aliyeziumba mbingu na nchi ambaye hataacha mguu wake usogezwe!!

Sijui wewe, ila Mtunga Zaburi alijua fika kuwa msaada pekee watoka kwa Bwana!!
Acha kulaumu ndugu zako, wazazi wako, mchungaji na wapendwa kuwa hajakusaidia  angali waliweza au kupaswa kufanya hivyo..!

Inua macho yako mtazame Yesu maana msaada wako hauwezi kutoka milimani na popote bali hutoka kwa BWANA...

Kama umeshaanza kuzama, yaani umefikia hatua ya kukata tamaa kabisa, uwe na hakika hata sasa Bwana aweza kukusaidia..muite kama Petro na unyoshe mkono wako naye atakushika...

31 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

Na Mwalimu Oscar Samba, Tanzania

Kama hujaokoka na upo tayari kufanya hivyo nikutie moyo sasa kuwa unapaswa kuokoka, na Hongera kwa maamuzi hayo...

Sema; MUNGU BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NINAKUJA KWAKO, NISAMEHE NA UNIOKOWE SASA, WEWE NI MUNGU NA MWOKOZI WANGU, NINAKUAMINI NA KUKUPOKEA SASA: Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Mawasiliano: Simu, 0759859287 Emaul: ukombozigospel@gmail.com
Tembelea pia www.ukombozigospel.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni