Jumatano, 22 Septemba 2021

MUOMBE BWANA AYAFUNGUE MACHO YAKO

 Zaburi 119:18 Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako.

Muombe Mungu Akufunulie Njia zake ili uweze kumuelewa..ukiona unalalamika..umechoka kiroho..umeishiwa nguvu za kusoma neno na hata kuomba..umepoteza hamu ya kwenda ibadani...

..umevunjika moyo

kiasi cha kutamani hata Yesu angerudi leo..uwe na hakika kuwa Macho yako hayaoni ktk sura ya Mungu..ndio maana humuoni Mungu ktk magumu hayo badala yake unaona wingi wa adui zako..au mateso..Gehazi alipofumbuliwa macho..aliona ukuu wa Mungu..Hajiri alipofumbuliwa macho ndipo alipokiona kisima..

Kumbe kisima kilikwepo ila tatizo macho hayaoni..Mungu yupo kama kwa Elisha na Gehazi ila macho ya Gehazi hayakuwa yakimuona..Watu wa kijiji cha Emau walipoumega mkate na kufumbuliwa macho ndipo walipomuona na kumtambua Yesu..

Stori za maumivu na masimulizi ya kinyonge kuwa tumaini lao limeuawa na kufifia zilikoma mara baada ya kufumbuliwa macho..

Waliokuwa wakieneza habari za kushindwa kwa Yesu kuwa ndie waliomtarajia kuwa mwokozi wa kisiasa wa Wayahudi ameuawa..walijikuta wakikimbia mbio mjini na kueneza habari mpya za Ufufuo wake..

Tazama hapa!
Stori zimebadilika sio kwamba uhalisia haukwepo ulikwepo ila macho yalikuwa yamefumbwa..

Na wewe umejawa na manung'uniko sio kwamba Yesu hayupo..la yupo ila macho yamefumbwa..huoni mbele sio kwamba hakuna njia la!! Ni macho yamefumbwa..

Muombe akufungue  macho leo...

Na Mwalimu Oscar Samba

Tafadhali *Share* au Shirikisha wengine ili kuwatia Moyo nao pia..bariki wengine kama ulivyobarikiwa..

Ukiwa hujaokoka nakusihi kufanya hivyo ili macho yako ya weze kifumbuka.. Ni Wokovu pekee ndio uwezao kukupatia nuru..Yesu ni Nuru km Yohana 1 ifunzavyo..akiingia ndani yako giza lote la dhambi na mateso na vifungo vya mapepo hukimbia.

Kama u tayari tafadhali fuatisha sala hii ya toba

..sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NISAMEHE DHAMBI, NIOKOE, WEWE NI MUNGU WANGU NA BWANA, Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo..amen.

Endelea kutembelea
www.ukombozigospel.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni