Jumatatu, 13 Desemba 2021

SULUHU KWA JAMIII AU ENEO LENYE KUKABILIWÀ NA TATIZO LA WATU KUJIUA

Na Mwalimu Oscar Samba

Mithali 28:17 Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie.

Andiko hilo hapo la Mithali linatupa kufahamu kuwa watu wanaojiua au kukimbilia mauti (ambao hapo imetumika au yametumika maneno kukimbilia shimo) ni matokeo ya kulemewa au kuwa na deni au mzigo wa damu iliyowahi kumwagika.

Sasa inawezekani aliimwaga yeye, au imemwaga kwenye eneo anaoloishi ama i juu ya uzao au jamii yake. Kwa ujumla ni kwamba kuna deni juu yake.

Damu huweza kukaa kwenye uzao nasi twajua hivyo, maana hata wale waliomsulibisha Yesu walikiri kuwa iwe juu yao na uzao wao. Pia eneo laweza kubeba damu maana hata aridhi iliyonunuliwa na fedha za usaliti wa Yuda ilitwa konde la damu.

Lakini pia damu ya Habili ililia kutoka aridhini. Kuna somo au kipengele cha kwenye kitabu fulani nichowahi kukiandika kinaitwa, ARIDHI KAMA KIUMBE HAI. Hapo nafunza vyema namna ya kushughulika na mambo kama haya.

Inawezekana pia damu hiyo ilimwagwa kwa mtu kupigwa hadi kufa, au ni kafara na kadhalika. Na ina wezekana pia alijiua mwenyewe ama ni ajali fulani au uvamizi wa watu wabaya.

Deni hili au damu hii huweza kumlemea yeyote nikiwa na maana kwamba inawezekana alihusika au la! Anafahamu kilichotekea au afahamu, alikwepo ama hakwepo, alikuwa ameshazaliwa au kuhamia hapo au bado.

*Lakufanya* :

*1. Omba Rehema* , Kwenye  eno ndilo lenye shida, yaani watu wa eneo hilo mara kwa mara hujinyonga, hujiua kwa kunywa sumu au jamii fulani, ama kwao kuwa na misiba ya mara kwa mara.

Uchagani kuna uchawi wa asili unaitwao "Sesu" au kupiga "Mmanga" ambapo watu wa jamii husika kila baada ya kipindi fulani hufariki, ambapo aliyeupiga ni matokeo ya kufanyiwa jambo fulani ambapo huamua kujibu mapigo kwa njia hiyo. (Maarifa haya pia yatasaidia)

Itumie Damu ya Yesu kutubia uhalali wa damu hiyo au deni hilo la mauti juu ya eneo au jamii ama familia husika. Mathayo 26:28 na Luka 22:20 pamoja na 1 Yohana 5:7, hubeba thima ya Damu hii katika kuondoa hatia au dhambi. Maana kilichopo hapa ni agano la damu lenye kulipwa na uhai wa mtu.

Kuna wengine agano hili la damu hulipwa na watu kuwa na tatizo la kutokwa damu puani, au damu za hethi, ambapo hutoka nyingi kupita kiasi au hethi zisizokoma ama mara kwa mara. Huku muhusika akiona baathi ya dalili rohoni, ikiwemo ndoto zenye kuhusisha jambo hilo, au huja kipindi cha msimu fulani.

Maandiko moja wapo tajwa hapo juu husema kuwa hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya ondoleo la dhambi, ilimwagika wapi  ? Aridhini. Ikipambana na nini? Dhambi au hatia, tena za kizazi na kizazi na zile za wakati ule na hata za wakati huu, na hata zijazo bado ina huo uwezo!

Kwa hiyo, unaposema ninaimwaga Damu ya yesu kwenye eneo hili au familia hii nikitubia damu iliyomwagwa au sababu iliyopelekea tatizo hili, uwe na hakika kuwa moja kwa moja Damu ya Yesu inaenda kushughulika na uhalali huo. Waweza omba pia ukisema ninaomba rehema kwa Damu ya Yesu ya kunyunyiza, na kadhalika.
Zaidi tuna kitabu cha SABABU YA DAMU YA YESU KUWA NA NGUVU ILIYONAYO. kitaimarisha ufahamu wako zaidi, na kuna kipengele cha mauti pale pia.

*2. Fanya Ondoleo la Hiyo Roho ya Mauti au Lipa Hilo Deni kwa Damu ya Yesu* . Rehema ilikupa uhalali wa kufanya ondoleo, ama iliondoa haki na uhalali wa damu hiyo kuwa juu ya eneo ama famliaa husika.

Kitabu kile cha Ufunuo wa Yohana kinatuambia kuwa Yesu alitununua kwa Damu yake,..ikiwa na maana kwamba kama alitununua basi kuna malipo alifanya. Kumbe Damu yake yaweza kutulipia madeni ikiwemo madeni ya damu! ( Kuna siku nilimuombea mtu mwenye roho za madeni na nikaitumia kumlipia huyo mtu, baada ya muda alijikuta anasamehewa ama mtu ambaye ni kiongozi wa kijiji ambako alishitakiwa aliamua kumlipia deni hilo, alimwambia mama mimi nimekulipia wewe nenda! ) Sasa sikupi ujanja wa kukopa kisha utake Yesu alipe la! fahamu waswahi husema Dawa ya deni ni kulipa...

Unapotangaza kuilipa hivyo moja kwa moja nguvu ya adui kuidai jamii au eneo hilo kudaiwa inao doka! Hii inayokupa uhalali wa hatua ya tatu ya kufukuza hayo Mapepo ya mauti kwa kuyakemea.

Katika hatua hii ya pili pia unapaswa kuinyamazisha hiyo damu. Kumbuka damu ina tabia ya kuongea, au kudai malipizi ya damu.
Hata kama walipoenda kwa mganga walitoa damu za mbuzi au kuku na kuifanya kuwa na uhalali wa kudai mauti kwa jamii au eno husika, uwe na hakika nayo inahitaji kushighulikiwa. Agizo la Mungu dhidi ya wana wa Israel kuhusu matumizi ya damu kwamba wasiinywe na jinsi Mungu alivyoagiza itumike kikuhani ni ushahidi kuwa damu za wanyama zikitumika rohoni huwa na matokeo fulani.

Tumia andiko hili hapa: Waebrania 12:24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.

Damu ya marehebu Habili ililia kisasi, malipizi na mapigo, ndio maana Mungu aliamua kuachilia adhabu kwa muhusika. Ila Damu ya Yesu ilinena uzima, uponyaji, utakaso na kuwekwa kwetu huruhu ikiwimo vifungo vya mauti kama Waebrania 2 ifunzavyo.

Kwa hiyo, tamka kwa jina la Yesu ninaimwaga au ninainyunyiza hii Damu ya Yesu ni kinyamzisha damu zote za wanyama, na ndege au kuku, au mbuzi na watu zilizomwagwa, (kama unamjua muhusika aliyeuawa unamtaja) ambapo inalia mabaya ikiwemo malipizi na adui huitumia. Sasa ninaitaka Damu ya Yesu Kristo ile ya kiagano ikanene mema sasa.

Unapoitaka inene mema kumbuka itaanza kuongea kuwa kwanzia leo, hata kufa tena mtu hapa, kwaanzia leo, hakuna mauti tena, uzima utatawala.

Waweza pia kutamka kwa jina la Yesu ninainyamzisha hiyo damu na madai yake.

*3. Fukuza hayo Mapepo na Roho za Mauti* . Kemea ukiyafukuza, yaambie wazi kuwa uhalali wenu umeshatanguka ama kuondolewa, ile damu imeshanyamazishwa, haipo tena. Sasa  kwa amri ni moja na kwa jina la Yesu Kristo, kwa ile amri niliyopewa ya kufukuza mapepo, ninawaamuru muondoke juu ya jamii au eneo hili, kijiji hiki, au kwenye kona hii ya barabara ambapo mnasabisha sana ajali, kwanzia leo ni mwisho... Na kadhalika..

*4* . Mshukuru Mungu, funga roho za kisasi na mashambulilizi, kwako na jamii husika, pia ifunike kwa Damu ya Yesu, nawe pia jifunike.

Pi wakati unaomba ukisikia msukumo wa kuachilia sadaka fanya hivyo, maana kama kuna kifungo cha kisadaka kuna wakati Roho huweza kukusukuma kufanya hivyo.

(Maaria haya pia yatumie kwa wanaoota ndoto za mauti, ikiwemo kuwa msibani, kwenye mazishi, ndoto za majeneza, makaburi na kadhalika.)

Kama hujaokoka ninakimiza kufanya hivyo, wokovu utakupa uhalali wa kuomba maombi haya na kunasuka..na itakuweka huru pia kutoka kwenye mateso kama haya.

Fanya sala hii ya toba sasa pamoja nami kwa imani..

Sema; MUNGU BABA, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NINAKIRI HIVYO, NINAKUAMNI KUWA WEWE YESU NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA, TAFADHALI FUTA JINA LANGU SASA KWENYE KITABU CHA HUKUMU, NA ULIANDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA: Amen.

Hongera kwa kuokoka, na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Kwa mawasiliano; Simu: +255 759859287

Baruapepe: ukombozigospel@gmail.com

Zaidi, pata mafundisho yetu hapa: www.ukombozigospel.blogspot.com

Tafadhali #Shate au Shiriki Ujumbe huu kwenye makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii, ili kuifikia jamii kubwa. 


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni