Jumatatu, 3 Januari 2022

BAADA YA MAFUTA, CHUMVI, STIKA, MAFUTA, JALENDA NA MAJI YA UPAKO, SASA WAJA NA NGUO ZA NDANI, Hizi ni Imani Potofu

Imani Potofu, sasa ya zalisha na Chupi au Nguo za ndani za Upako, ni baada ya mafuta, maji na Chumvi za upako

SIPENDI SANA KUSHAMBULIA IMANI NYINGINE..ila tunapaswa kuwa Makini sana na Wahuni walioivamia kazi ya MUNGU wakifanya vituko kwa vigezo vya Ufunuo... Wewe Mshirika usiweke akili mfukoni na kukubali kukubaliana na kila kitu kisa kimetoka kwa mtumishi anayejiita wa Mungu kwa kisingizio cha Ufunuo..

Ndio maana watu wananyweshwa hadi Jick ya kuondolea madoa kwenye nguo, waDada wanatomaswa viungo vyao na kupakwa mafuta sehemu nyeti..ukiuliza unaambiwa alifunuliwa!

Maji na Mafuta vimegeuka kuwa uganga wa Kilokole siku hizi..Yesu hapewi heshima bali ni maji yaliniponya, mafuta ya upako yalinisaidia sana..Imani kwa Yesu hakuna tena.

Akiombewa bila kupewa maji na chumvi ya upako anaona kama hajaombewa vile! 

Tuna kizazi ambacho hakimtaki Yesu kama alivyo bali kinataka aina fulani ya mbwembwe na mazingaumbwe na sarakasi za kiroho..mimi sishangai sana maana ilishanenwa hivi; 

2 Petro 2:1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.

2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.

3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.

4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu.

Jina la Yesu linatukanwa kwa ajili yao..hizo chupi za Upako, na Kalenda za upako, na Stika za upako, nasikia kuna na Keki za upako, kule Afrika Kusini kuna na Nyoka wa Upako, huku tanzania tuna maji na Mafuta ya upako..vyote hivyo vinauzwa..

Hawa washirika wengi wao hata ukiwaambia na kuwaonya ni wabishi kama nini!! Na ukikaza kuwakemea mnagombana milele!! 

Ukiona hivyo wala usiumize kichwa na kutafuta nani kawaloga, au wamemezeshwa nini huko!! Maana wapo tayari kumtetea mtumishi wao kwa nguvu zote kuliko hata kumtetea Yesu! 

Ukitaka ugomvi mguse huyo mtumishi!! 

Kweli kuna ambao wanavishwa mapepo au maroho, ambapo huwa vipofu na hawaoni, Paulo hutuambia akili zao zimekamatwa! Au fahamu ama fikra zao zimepofishwa!

Lakini wengine ni matokeo ya nia zao kuwa mbovu! Ama moyo mbovu..!

Wewe hata ukifundisha kweli hawatakuja au kukusikiliza, maana kizazi hiki kilishatabiriwa, na ni wao wenyewe kwa akili na mashauri yao hutafuta watu kama hao!! Soma hapa ili upate jibu kama ulikuwa ukijiuliza sana ni nani aliyewaloga na ujuwe sasa leo kuwa..

2 Timotheo 4:3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;

:4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.

5 Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.

Na Mwalimu Oscar Samba

0759859287

Endelea Kutembelea

www.ukombozigospel.blogspot.com



 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni