Na Mwalimu Oscar Samba
Ni kweli ngoja ngoja huumiza matumbo, au fahamu pia simba mwendapole ndie mla nyama! Maana mtaka yote kwapupa hukosa yote! Hawakuwahi kukosea waliosema kuwa subra yavuta heri!
Narudia tena
na tena kuwa kawia ufike, pole pole ndio mwendo! Unaonaje mkulima akapanda
mbegu leo na kutaka kuvuna siku hiyo hiyo! Kama kwa mkulima haiwezekani uwe na uwakika
kuwa na katika safari ya mafanikio ndivyo ilivyo.
Embu tujionee jinsi maandiko
mtakatifu ya Biblia yanavyotufunza katika kitabu kile cha Yakobo: 5:5 Kwa hiyo
ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi
yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na
ya mwisho.
8 Nanyi vumilieni, mthibitishe
mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.9 Ndugu, msinung'unikiane,
msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
Unaonaje mtoto ama mwanafunzi
wa darasa la kwanza akatamani kwenda hosipitalini na kuanza kufanyia watu
upasuaji akiulizwa ajisemee kuwa mimi ni daktari!
Kuwa na ndoto ama kipawa cha
udakitari haikufanyi kuwa dakitari! Kama inavyompasa kuingia darasani na amalize
shule ya msingi, kisha sekondari, na hatimae chuo tena akae huko muda wa
kutosha, basi na ndivyo ilivyo kwa mtu mwenye ndoto ya mafanikio!
Maisha hayaitaji njia ya mkato!
Yanahitaji kanuni! Unaonaje mpishi akitaka kupika ugali achukue maji ya baridi
na kuchanganya na unga na kuanza kusonga akiwa na nia ya kupata ugali! Hakika atapata
kituko, maana kitakachotoka hapo hakitakuwa hata na sifa ya kuitwa uji!
Ukitaka ugali, ama wali, kuna
kanuni zake! Alikadhalika mafanikio ya kiroho, ama kimaisha ndivyo yalivyo! Haraka
ya mafanikio kwenye huduma, utajiri wa haraka na kadhalika! Kitabu cha Mithali
chenyewe kina onyo katika hili!
Mithali 20: 21 Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka,
Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.
Pupa ni
hatari, fanya kazi kwa malengo, panga mpango, nenda hatua kwa hatua, acha
kurukia ngazi,usitake kuiona kesho kutwa ungali leo! Maandiko katika Mithali
yanatupa mambo muhimu hapa, ama kuna taadhari kama sio onyo toka hapa! Jionee;
Mithali 21:5 Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.
Mali iliyopatikana
kwa haraka au utajiri hauwezi kudumu, maana muhuska hakupitia shule ya Mungu
ambayo ni mapito, kibiblia hii ipo ili ikujengee nidhamu ya fedha ili
kukuwezesha kuwa na uwezo wa kutambua nafasi ya Mungu katika mafanikio yako, 1
Thimotheo 6, inakupa mambo muhimu ya kuzingatia kwa anayetaka kuwa tajiri!
Hayo hujifunza katika shule ya Mungu! Haipatikani
ukiwa na fedha, hupatikana ukiwa huna! Ile sura ya tano inaeleza jinsi ambavyo
fedha huweza kuwa ni shina la mabaya yote!
Fedha
ikikosa nidhamu ni hatari na adui! Maana mafanikio ya mpumbavu ni kwa
uharibifwa nafs yake! Acha Pupa, Kawia
Ufike!
Nikuhitimishie
na andiko hii la Ayubu inalonena kuhusu mwanzo mdogo ambao ungeongeeka tu kama
muhusika angalikaa kwenye kanuni! …..
Tena
ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka
sana. Ayubu 8:7 SRUV.
Kama hujaokoka
na umesoma ujumbe huu na unataka kuokoka, (maana ni fika huwezi kunufaika na
msaada wa Kiungu maishani mwako kama hujaamua kumruhusu Yesu aingie kwenye
maisha yako.) kwa hiyo fuatisha Sala hii ya Toba kwa Imani.
Sema; MUNGU
BABA, NINAKUJA KWAKO, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, TAFATHALI FUTA
JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, LIANDIKE SASA KWENYE KITABU CHA UZIMA WA
MIELE: Ameni.
Hongera kwa kuokoka,
tafathali tafuta kanisa la watu waliokoka, usisite kuwasiliana nasi kwa maombi,
ushauri, na hata kwa msaada wa kitabu cha Kuukulia wokovu.
Simu,
WhatsApp au Telegram: +255759859287, Baruapeoep: ukombozigospel@gmail.com, Web: www.ukombozigospel.blogspot.com,
Facebook page: @mafundishoyanenolamungunamwalimuoscarsamba, (Mafundisho ya Neno
la Mungu na Mwalimu Oscar Samba)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni