Jumanne, 18 Julai 2017

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 13.

Na Mwalimu Oscar Sama wa Ug Ministry.
Asante Yesu Kristo kwa majira haya mazuri uliyonikutanisha na msomaji wangu huyu, Leo mpendwa ni sehemu ya kumi na tatu ya makala hii na tunaendelea kuitanzama Nguvu ya Agano kwa kabila la Yuda.
Tutaanze na ule Mstari wa kumi,
10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Nisikilize, Baraka hizi zilinenwa miaka mingi ila zilibeba hatima nzima ya kiutawala na kifalume katika Iziraeli na Ulimwengu mzima.

Fimbo maana yake ni Mamlaka, tuna fahamu kuhusu habari za fimbo ya Haruni na Musa, kwa hiyo swala la Utawala katika Izireli lilikuwa chini ya kabila hili, ndio maana tunamuona Mfalume Daudi, Sulemani, na wengineo ambao walitoka katika hili kabila na kuwa watawala wenye historia kubwa.
Kisha anatajwa  Mwenye Miliki ambaye mataifa watamtii huyu sio mwingine bali ni YESU. Hii ni Nguvu ya Agano ya ajabu sana, ya kwamba usipo ifahamu unaweza ukaona mambo yanatokea kwenye maisha ukadhani yanakuja bahati mbaya ama kwa kubahatisha kumbe tayari mpangilio upo.
Jambo hili halikuishia hapo bali hata Nabii Isaya alilinena katika kulithibitisha kisha likaja jithiirisha katika Agano Jipya.
Ni Isaya 9: 6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele, Mfalme wa amani.
7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.



Tuangaziye ule msari wa kumi na moja,
11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
Nataka kukuonyesha jambo hili lilivyonenwa ama lilivyokuja kutiwa mihuri na manabii wengine kisha jinsi lilivyotimia kwenye ulimwengu wa Mwili kisha nitakujuza maana yake kiroho. Tuanze na Zekaria 9: 9 Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.
10 Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
11 Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo na maji.
12 Irudieni ngome, enyi wafungwa wa tumaini; hata hivi leo nasema ya kwamba nitakurudishia maradufu.
13 Maana nimejipindia Yuda, nimeujaza upinde wangu Efraimu; nami nitawaondokesha wana wako, Ee Sayuni, wapigane na wana wako, Ee Uyunani, nami nitakufanya wewe kuwa kama upanga wa shujaa.
14 Naye Bwana ataonekana juu yao, Na mshale wake utatoka kama umeme; Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta, Naye atakwenda kwa pepo za kisulisuli za kusini.
15 Bwana wa majeshi atawalinda; Nao watakula na kuyakanyaga mawe ya teo; Nao watakunywa na kufanya kelele kama kwa divai; Nao watajazwa kama mabakuli, kama pembe za madhabahu.
16 Na Bwana, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimeta-meta juu ya nchi yake.
17 Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.
Nilitaka kukupa Mstari ule mmoja tu wa tisa maana umejishibisha kimauthui ila inayofwata inasadifu jambo hili kimuundo na kimantiki pia, nataka uone maneno Agano la Damu, kumbuka katika mwanzo tuliona maji ya zabibu, na katika Zekaria  hapo mstari wa 11 anaitaja Damu ya Agano, pia divai inatajwa mara kwa mara na divai ni maji ya zabibu . Wakati Yesu alipo kuwa kwenye karamu ile ya kwenye Luka 22 alitwaa maji ya mzabibu na kusema kuwa kikombe kile ni Agano Jipya na ni Damu yake imwagikayo.
Tu hakiki ndiposa tuendelee. Luka 22: 20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
Kwa mantiki rahisi ni kwamba Nguvu ya Agano la Ibrahimu ilizaa Agano Jipya, katika hili tutakutana zaidi kwenye mada ya Agano Jipya. Tuchambuwe na Isaya.
Kabla sijakupa hili andiko nataka ushike mambo muhimu kwenye mstari wetu wa msingi hapo juu, Nguo, Zabibu na damu ya zabibu.
Isaya 63: 1 Ni nani huyu atokaye Edomu, Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake?
2 Kwani mavazi yako kuwa mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu?
3 Nalikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote.
4 Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu, Na mwaka wao niliowakomboa umewadia.
5 Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.
6 Nikazikanyaga kabila za watu kwa hasira yangu, Nikawalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nikaimwaga damu yao chini.

Kumbuka Mstari wetu wa msingi wa Mwanzo 49:11na mingineyo inanena habari za Yesu, Ufunuo 19: 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Nataka tuone tukio hili kisha nitakujuza maana ya tafsiri ya Punda, Mathayo 21: 21.7 wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake.
21.8 Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani.
21.9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
21.10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?
Katika andiko la Mwanzo kuna maneno kama vile Punda na Nguo na hapa tunamuona Yesu akipanda Punda na kisha wakimtandikioa Nguo.
Mwishoni mwa mstari niliokupa kuna swali wana uliza pia katika Isaya alianza na hilo Swali.
Katika maelezo yao hapo kwenye Mathayo wanamtaja Yesu kama mtu wa Ukoo wa Daudi na fahamu Ukoo wa Daudi ni katika Kabila la Yuda.
Sasa tafsiri ya Punda ni hii, Punda anawakilish Utumishi, tena ulio tukuka, Zabibu ama maji ya Zabibu ni Agano Jipya kama tulivyoona kwenye Luka 22:20. Kwa hiyo andiko linaposema atafunga punda wake katika mzabibu maana yake atafanya Agano la Kitumishi na Yuda ambapo ndilo alilokuja kufunga na Daudi na Agano hilo ndilo lililomzaa ama kutupatia Yesu, na Linaitwa Agano Jipya.

Anaposema atamfunga Mwana Punda kwenye Mzabibu Mzuri maana yake: 1. Mwana Punda Ni Yesu, ambaye ni Mwana wa Daudi ama Yuda,2. Na kumfunga katika Mzabibu Mzuri maana yake Yesu atafungwa katika Agano Jipya ambalo ni zuri zaidi au ni Bora zaidi kama maandiko ya Waebrania yanavyonena kuwa ni Agano bora zaidi.
Tu hakiki Mchango wa Daudi ambaye ni Yuda katika swala hili la kiagano;
Hakikisha hapa, Yeremia 31: 31 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.
33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
35 Bwana asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; Bwana wa majeshi, ndilo jina lake;

Yamkini unaniuliza Daudi anaingiaje hapo? Yeremia 33: 14 Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapolitimiza neno lile jema nililolinena, katika habari za nyumba ya Israeli, na katika habari za nyumba ya Yuda.
15 Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii.
16 Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.
17 Maana Bwana asema hivi, Daudi hatakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli;
18 wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo, na kufanya dhabihu daima.
19 Neno la Bwana likamjia Yeremia, kusema,
20 Bwana asema hivi, Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana, na agano langu la usiku, hata usiwepo tena mchana na usiku kwa wakati wake,
21 ndipo agano langu nililolifanya na Daudi, mtumishi wangu, laweza kuvunjika, hata asiwe na mwana wa kumiliki katika kiti chake cha enzi; tena agano langu nililofanya na Walawi makuhani, wahudumu wangu, laweza kuvunjika.
22 Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari kupimwa; ndivyo nitakavyoongeza wazao wa Daudi, mtumishi wangu, na Walawi wanaonihudumia.


Kuhusu hili tukutane kwenye mada ya kitabu hiki itwayo Agano la Daudi na ile ya Agano Jipya.

Upo Mstari wa Mwisho ambao ni ule wa kumi na mbili ambapo nitaumalizia kesho panapo majaliwa yake Maulana, na nitaufafanua pia kupitia maandiko ya Ufunuo na yale ya kikombe cha Ghadhabu, sina la ziada ni wako katika kuujenga mwili wa Kristo tukutane kesho mie ni Mwalimu Wako Oscar Samba wa Ug Ministry, tafadhali kwa maswali na maoni tuwasiliane kwa namba hizo hapo chini.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGospel  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel 
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa

 Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA  https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA  (Ukombozi Gospel)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni