Jumanne, 18 Julai 2017

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 14.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ninakukaribisha ndugu msomaji wangu katika safu  hii ya mafundisho ya Neno la Mungu kupitia makala zetu, leo tunamalizia kulitazama kabila la Yuda.
Mstari unaofwata una mantiki ya aina yake katika hii Nguvu ya Kiagano,
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
Wekundu wa macho unawakilisha Ghadhabu na Mvinyo kulevia, weupe wa meno ni umaridadi wa maneno yake ama hotuba zake. Tukimtazama Yesu alikuwa ni mwenye hekima kinywani mwake na aliyekubalika kwa maneno yake.
Kwa uapnde wa Mvinyo ama kulevia na Ghadhabu wasomaji wa maandiko wanafahamu fika ya kwamba ipo silaha ya ajabu sana ya kupigania vita kwenye ulimwengu wa roho itwayo kikombe cha ghadhabu, kikombe hiki hulevia kisha huaribu na kuangamiza. Mimi binafsi hukitumia sana kikombe hiki ninapokuwa nikipigana vita vya kimaagano na mizimu. Maana hutambua silaha hii ina nguvu ya ziada katika hivyo vita.

Ona hili katika Yeremia 25:15-18, Upo uhusiano mkubwa wa kikombe hiki na jambo ninalolizungumzia hapa na nikipata nafasi nitalifafanua kwenye sehemu ya kupambana ama kufuta maagano ya kipepo, yaani yale ya mizimu na mababu ama kwa waganga na wachawi na walozi, na yakimatambiko na mila ovu. Katika hiyo mada pia nitakuonyesha matumizi ya damu ya Yesu kama silaha ya kiagano katika kupambana na hayo maagano, na namna ya kumtumia Yesu  kama Mwanakondoo aliyechinjwa kama Ufunuo wa Yohana unavyomuelezea na Ibrahimu alivyomtoa Sadaka, ambapo Sadaka ile iliweka Alama ya kiagano katika Agano Jipya lililokuwa na dhima ya Ukombozi. Tutayaona haya katika kitabu hiki kwa mapana zaidi pindi tufikapo katika hiyo mada na itatanguliwa na ile ya Agano Jipya.

Natumai hizi nazo zitakuwa habari njema kwako; Leo ndio mwisho wa mfululizo wetu wa jumbe hizi za Nguvu ya Agano kwenye safu hii, ila usikose kununua kitabu punde kikitoka maana kimesheheni maagano zaidi ya sita ama matano yaliyomo humu kwenye Bibilia, na hapa tumedodosa tu Agano moja hili la Ibrahimu nalo hatujalimalizia maana kwa upande wa ufwatiliaji wa baraka hizi tuliona tu za watoto wa Yusufu na hizi za Yuda. Ila wapaswa kufahamu watoto wa Mzee Yakobo ni wengi, na katika kitabu uchambuzi wake ni mpana zaidi.  Mungu akujaze baraka tele hizi za kiagano na endelea kutufwatilia ili kujua masomo tutakayoendelea nayo tena.


Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGospel  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel 
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
 Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA  https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA  (Ukombozi Gospel)




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni