Jumanne, 18 Julai 2017

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 12.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Furaha ya leo iliyopo Moyoni Mwangu ni zaidi ya ile ya Jana, yamkini nimatokeo ya kuvushwa kwako kiroho kwa maudhui ya ujumbe wa jana. Leo ninakuletea matokeo ya baraka kwa makabila kumi na wawili ya Mzee Yakobo na uwenda nikapata kibali cha kudodosa machache ila ninaanza na kabila la Yuda. Tutaona siri ya Yesu kuitwa Simba wa kabila la Yuda ikiwa ni Jina la Kiagano huku wengine wakisalia bila kulijua hilo.

Katika kuwabariki wanaye ambao ndiyo makabila ya Iziraeli Mzee Yakobo aliwatamkia maneno ya baraka yaliyoambatana nao hadi kwenye hatima ya Maisha yao yote.
Tuone, Mwanzo 49: 1 Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.
2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.
 

YUDA: Mwanzo 49: 8 Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.
Jambo hili limekuwa halisi, kwani Mfalume Daudi, Yesu, Mfalume Sulemani, Ni miongoni Mwa watu waliosifiwa sana katika historia ya Bibilia kwani wao wote ni watu wa Yuda.

Pia katika Wosia wa Musa alilinena hili katika kumtaka kuwa msaada juu ya adui wa nduguze yaani Iziraeli.
Kumbukumbu la Torati 33: 7 Na baraka ya Yuda ni hii; akasema, Isikize, Ee Bwana, sauti ya Yuda, Umlete ndani kwa watu wake; Alijitetea kwa mikono yake; Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake.
Si unakumbuka kilichotokea kwa Goliati? Ambaye alikuwa ni tishio kwa Usalama wa Iziraeli yote, Ila aliibuka Mtu wa kabila la Yuda aitwaye Daudi na kumpiga. Halikuwa jambo la kubahatisha bali ni siri ama ni Nguvu iliyopo kwenye hili Agano. Kwa Nguvu ya Agano aliwalinda Ndugu zake, sio siku hiyo tu bali katika utawala wake hakuna aliyemwaga Damu kama yeye nyakati zote, likaja kuwa halisi zaidi kwa Yesu aliyekuja kuwa Shujaa wa Ulinzi kwa njia ya Agano lililo bora zaidi lililotiwa Nguvu kwa Damu ya Msalaba.
Katika huo mstari wa 8, kuna maneno kama vile ndugu zako watakusifu na watakuinamia pia wanatajwa adui zake, katika mstari nitakaokuonyesha, adui ni mataifa, kukuinamia ni kukusujudia na kukusifu ni matokeo ya uwe bwana wa ndugu zako.
Mstari huo ni ule uoonyeshao baraka za Isaka wakati anambariki Yakobo aliye baba yake na Yuda kwa hiyo sehemu kubwa ya Baraka za baba yao zimewaendea Yuda na jambo hili linajidhiirisha katika ugawaji huu na matokeo yake kibibilia.
Ni Mwanzo 27: 29 Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.

Jambo hili lilikuwa na Nguvu hadi kwenye urithi, Ndiposa ukifwatilia wakati wa kugaiwa urithi wana hawa wa Yuda walipewa Eneo kubwa na pia lililojawa na sifa kedekede kama Yerusalemu, na Milima ya Hebroni ambapo jamaa ya Kalebu ilipewa. Ujuwe jinsi walivyo majasiri hata mpelelezi waliyemtuma aliambatana na nguvu hiyo ya Simba kama mstari unaofwata usemavyo, Alikuwa ni Kalebu; Wakati wenzake wanawaona Wana wa Anaki na Wanefili kuwa ni Majitu yeye aliwoana kuwa ni Chakula chake kama alivyo Simba. Kitu kilichomfanya Musa kumuongezea ama kumpa Urithi wa ziada katika milima hiyo ya Hebroni. Ila chanzo cha yote hayo ni Nguvu ya Kiagano.
Tuendelee;
9 Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?
Anamtaja Yuda kama Mwana Simba, kumbuka hapa ni Mwanzo kabisa na hakuna aliyekuwa anajua hatima ya Watoto hawa nje ya macho ya kiimani. Baraka hizi ndizo zinazokuja kuzaa ujasiri kwa watu wakabila hili, na hatimaye Yesu kuja kuitwa Simba wa kabila la Yuda.
Usipoijua siri hii ni hakika utalitumia jina la Simba wa kabila la Yuda kimazoea katika maombi ama kupambana na adui zako, ila kuanzia leo natumai kuna kitu kikubwa ama “Kiduve” kama wasemavyo wachaga wa Rombo, kimejengeka ndani yako.

Kumbuka kuwa kabila hili lilipewa dhima ya ulinzi ama jukumu la kuwalinda nduguze dhidi ya adui zake, ikiwa na maana kiagano hawa ni walinzi, na ili kujilinda kwao wana wa Iziraeli kutimiye yawapasa kuwatumia ama kutumia miongoni mwa kauli ama vifungu vya ulinzi vilivyopo humu kiagano.
Wakati wanasafiri wana hawa wa Mzee Yakobo wakiwa Jangwani kwa shabaha ya kuelekea Kanani njiani walikutana na maaguzi ama uchawi wa Balaamu ukiwa nyuma ya Balaki, na walitumia maneno hayo ama vifungu hivyo vya ulinzi kiagano vilivyomo juu ya Yuda. Na kumbuka Sifa kubwa ya Simba mke ni Mawindo na Ulinzi na Yuda ni Mfano wa huyo.
Hesabu 23: 23 Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
24 Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba mke, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hata atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa.

Ona pia hapa,Ni Hesabu 24, ukisoma sura yote utajionea taswira ya ajabu sana na itakujuza kuwa swala la ulinzi ni jambo kiagano, ndio maana Mungu aligeuza laana kuwa baraka. Nitakuonyessha kwa kiduchu na nitakupa picha ya kiagano hapo ambapo nitarudi hadi kipindi kile cha Isaka anambariki Yakobo katika baraka zilizo za kiagano.
 Hesabu 24: 9 Aliinama, akalala mfano wa simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha? Na abarikiwe kila akubarikiye, Na alaaniwe kila akulaaniye.
Umeliona hilo jambo? La Simba limo kwa Yuda dhidi ya Yakobo na lililosalia tulione kwa Yakobo dhidi ya Isaka.
Mwanzo 27: 29 Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.
Tuhitimishe hili la Simba ya kwamba Ndiye Yesu, Ufunuo wa Yohana 5:5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.
Hongera kwa kuwa mtulivu kwenye darasa hili siku ya leo ambapo tumegundua kitu kilicho jificha mno, kesho panapo majaliwa tutaendelea na habari za Yuda na nitakujuza kuhusu siri ya kiti cha Enzi cha Daudi ama Utawala wa kifalume wa Daudi kuelekea ule wa Yesu huku mtaji wetu ukiwa ni huo Mstari wa 10 katika Mwanzo 49.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com   #UkomboziGospel  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel 
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa

 Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA  https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA  (Ukombozi Gospel)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni