Mwalimu Oscar Samba wa huduma ya Ukombozi Gosple |
Najua
umekuwa na wakati mgumu sana maishani mwako, na umelia vyakutosha, ila sasa
ninakwambia usiliye tena maana Yesu amekusikia na kukuhurumia.
Kitabu kile
cha Luka 7:11-17, Kinaeleza kisa cha
mwanamke mjane aliyefiwa na kijana wake wa pekee, na Yesu alipoukaribia huo mji
wa Naini alimuona na kisha kumuhurumia na hakuishia kumuhurumia tu, bali
alimwambia; “USILIYE.”
Mara baada
ya maneno hayo alitenda mujiza wa kumfufua mwanaye. Bila iyana nakufunulia
maandiko hayo ili ujidhibitishiye mwenyewe.
13 Bwana alipomuona
alimuonea huruma, akamwambia, “Usiliye.” 14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale
waliokuwa wakilichukuwa wakasimama. Akasema, “Kijana nakuamuru: Inuka.” 15 Yule
maiti akainuka, akaketi, akaana kusema. Akampa mama yake.
MAOMBI: Mpendwa na kwa upako niliopewa na YESU KRISTO
kama mtumishi wake ninakiamuru hicho kitu kilichokufa maishani mwako kiinuke
sasa na kwa kinywa hiki ninaligusa jeneza kwa
JINA LA YESU KRISTO MNAZARETI.
Amini sasa
ya kwamba muujiza wako umekwisha kupatikana. Langu jina ni Mwalimu Oscar Samba
mtumishi wa Huyu Mwanaume wa ajabu aitwaye YESU KRISTO. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com, ama ukurasa wetu wa facebook na
kundi: Ug Ukombozi Gosple. #Like hiyo page na #Share
ujumbe huu.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoa ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KAUMINI KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA
KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO,
AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Kwa Maswali
au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com Simu: +255 759
859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni