Mwalimu Oscar Samba |
Tatizo lako
halipo tena kaburini bali limefufuka na Bwana YESU, Wakati watu wakikuona
wanakuona kama mtu aliyepoteza matumaini ama wengine wakikumbuka jinsi
ulivyokuwa mfanikiwa ila kwa sasa maisha ni kama yamekupiga wewe tambua ya
kwamba matatizo hayo ni kweli yalikwepo
ila kwa sasa yamekwisha kufufuka na YESU WALA HAYUPO TENA KABURINI.
Mtazamo wa
wengine usikutishe kwani hadi leo huko Uyaudi zipo dini zinazongonja masiya
wakiamini kuwa hajaja na wapo wachache wanaoamini ya kwamba YESU hakufufuka
kama viongozi wa mafarisayo na wakuu wa makuhani walivyowahonga wale walinzi na
kuwataka kusema ya kwamba watangaze eti wanafunzi wamemuiba na haja fufuka. Hakiki hilo jambo hapa, Matahyo 28:11-15.
Naguswa
kukudokezea walau kidogo, 13 wakisema, “Semeni, ya kwamba wanafunzi
wake walikuja usiku, wakamuiba, sisi tulipokuwa tumelala.” 15….Na neno hilo
likaenea kati ya Wayahudi hadi leo.
Kwa hiyo
wapo watu ambao hawataamini mujiza wako ulikwisha kuumbika rohoni milele na
wengine ni wakina Tomaso hadi wa guse, pia usisahau kundi jingine lile la wale
watu waliokuwa wakielekea Emau, walikuwa na Yesu ila hawakumtambua maana macho
yao yalipofushwa kwa hiyo wengine wamepofushwa na subira punde Yesu akiumega
mkate watafumbuliwa macho wala usiwabaguwe.
Na wewe
achana na hiyo mitazamo bali amini hicho kilichokuwa kimekufa hivi sasa
kimefufuka na Yesu kristo. Na wakikugasi wewe waambie ya kwamba wasimtafute
aliye hai miongoni mwa wafu kwani amefufuka kama alivyosema.
Tumsikilize
Malaika alivyotangaza Ushindi huu bila kipaza sauti wala spika ama chombo cha
habari ila ulienea ulimwenguni mwote.
Mathayo 28:5 Malaika
akajibu, akawaambia wale wanawake, “Msiogope ninyi! Kwa maana ninajua
mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. 6 Hayupo hapa: Kwani amefufuka kama
alivyosema, njooni mpatazame mahali
alipolazwa.
Na kusihi
endelea kusoma makala nyingine na hongera kwa Imani iliyokwisha jengeka ndani
yako na kwa kupokea mujiza wako, Tafadhali utunze vyema.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi
nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha
nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI
MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI
YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple, PAGE:
https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni