Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Ayubu 13:13a Nyamazeni, niacheni, ili nipate kunena.) Hayo ni maneno ya
Shujaa Ayubu aliyoyanena mbele ya adui zake. Na wewe leo ujumbe huu ni wa kwako
kwani ninakutaka kutokutishwa ama kubabaishwa na maneno au mtazamo mbovu wa
adui dhidi yako bali wewe mtazame Yesu aliyebingwa wakuwafunga vinywa kwa
Utukufu atakao kutendea.
Adui zako walinena
kila lilobaya vinywani mwao, huku wakimtuhumu ya kwamba ametenda dhambi.Ndio
maana mabaya yanampata, tutizame sehemu ya maneno ya Elifazi.
Ayubu 4: 7 “Kumbuka, tafadhali:
ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali
wapi? 8Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, na kupanda mathara, huvuna yayo
hayo. 9 Kwa pumzi ya Mungu huangamia, na kwa kuvuma kwa hasira yake humalizika.
”
Ona tena kebei hii
katika mstari wa 11; “Simba mzee
huangamia kwa kukosa mawindo, nao watoto wa simba mke wametawanyika
mbalimbali.”
Rafiki na ndugu yangu
katika Bwana huenda upo katika majira ama nyakati au wakati kama huu ila yangu
kauli ni hii; “Usitishwe na manongono hayo bali wewe waambiye ama watake
wafumbe vinywa ili uvuke.”
Wakigoma wewe waache
maana hata kwa Ayubu alifanya hivyo ila walikataa. Ukiweza kujitetea ni sawa
ila usitumie muda mwingi kufanya hivyo bali wewe muache Bwana ajitukuze ndani
yako na Falisafa yako iwe ni kuwataka wanyamaze ili uvuke. Ikiwa na maana ya
kwamba majibu kamili watayapata mara baada ya wewe kuvuka na hapo ndipo
watakapojua ya kwamba ulitenda dhambi ama ilikuwa ni Mungu anajivunia wewe.
Na hata kama umetenda
dhambi kazi yao sio kukushutumu ama kukuteta bali ni kukuombea rehema kwani
wanatakiwa kukumbuka ya kwamba mwenye haki wa Mungu huanguka mara saba na
kuinuka tena.
Njia yakujisafisha sio
njema kama ile ya kusafishwa na Mungu, Jionee jitiada za Ayubu zakujitakasa
mbele yao;
Ayubu 21:7 “Mbona waovu wanaishi, na kuwa na wazee, naam, nakuongezeka
kuwa na nguvu? 8 Kizazi chao
kinadhibitika nao machani pao, na wazao wao mbele ya macho yao”
Hapo Ayubu anajaribu
kujibu hoja zinazomshutumu kuwa ametenda dhambi ndio maana anapatwa na mabaya
ila yeye anadhirisha kwamba wapo wasiomjua Mungu na bado mabaya hayawapati hapa
ulimwenguni, na ukiendelea kusoma hiyo mistari utapata taswira halisia.
Lakini ashukuriwe na
atukuwe Mungu Baba juu mbinguni na Duniani atendaye mambo makubwa kuliko hata
yale tuyawazayo kwani ilifika majira ya Mungu yakuwafumba vinywa hawa adui
zake. Tena kwa kitisho na kuwataka wakamuombe msamaha ama kupiga magoti mbele
yake.
Ayubu 42:7.. Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, “Hasira yangu
inawaka juu yangu, na hao rafiki zako wawili, kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo katika
habari zangu, kama alivyo nena mtumishi wangu Ayubu.”
Hivyo ndivyo Bwana
alivyo jidhiirisha kwa hao waliopaswa kunyamaza kimya ili Ayubu avuke salama.
Na wewe yakupasa kuishika hii Falisafa ili kuwataka wanyamaze kimya na wakigoma
wewe endelea kuwa mpole kwani majira ya wakina Elifazi yanakuja na Mungu
atawataka kurejea kwako kama hao na hayo utayaona zaidi katika misitari
inayoendelea.
Bwana wangu akupiganiye
salama nami sina la ziada hadi wasaa huu ila ninakukumbusha kuwa somo la kesho
linaitwa, BONDE LA KUKATA MANENO. Tafadhali usilikose kwani limesheheni ujumbe
marithawa kuhusu mathara ya maneno na namna ya kupambana nayo. Mie ni Mwalimu
wako Oscar Samba wa UG Ministry.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni