Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry |
Maziwa na
Asali, hayapatikani Misiri wala jangwani hakuna malisho yawezeshayo ng’ombe
kutoa Maziwa ama maua ya mimea ili nyuki wazalishe Asali. Bali ukiyataka
yakupasa Kufika Kanani kwani ndiko kwenye mizabibu na tini na zaituni zenye
maua mazuri ya wezeshayo nyuki kutanda hapo na kisha kufwonza na hatimaye kuunda
Asali.
Maziwa ama
majani yatoayo maziwa hustawi kando ya mito na karibu na chemichemi za maji, na
vitu hivyo hupatika kanani ambapo ndipo paitwapo; “NG’AMBO YA YORIDANI.”
Huku
hawaingi, Waoga, Wasioamini ahadi za Mungu, yaani wasiochanganya ahadi za Mungu
na imani, Wanung’unikaji, kwani hao hufa kwa nyama za kware kuwatokea puani;
Hesabu 11. Ama kwa nyoka wa Moto; Hesabu 21.
Bali
Mashujaa kama wakina Yoshua na Kalebu hao ndio waingiao, katika jiji hili la
maraha. Hata leo ndivyo ilivyo kwetu siye kwani kama unataka kutimiza maono
yako yakupaa kushinda vikwazo kama Yusufu ili kuishi maisha ya raha na
mustarehe katika Kanani yako. Usifuraiye tu ahadi ya Maziwa na Asali bali
tazama pia vikwazo ambavyo huna budi kuvishinda.
Embu
tuangaliye walionshindwa na walioshinda katika safari hii ya kufika ng’ambo ya
Yoridani. Manung,uniko yalifanyika kikwazo kikubwa sana kwa wana wa Waebrania. Na
sababu ikiwa ni Chakula, chunga na wewe kulala njaa ama kula mlo mmoja mwaka
mzima kusifanyike kikwazo kama hawa ndugu.
Hesabu, 11:5 Twakumbuka samaki
tuliokula huko misiri bure,na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu,
na vitunguu saumu 6 Lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu
chochote, hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu.
Hesabu 11: 1-35, 33
Kisha hiyo nyama ilipokuwa ingali kati ya meno yao, hawajaitafuna bado, hasira
za Bwana ziliwaka juu ya watu, Bwana akawapiga watu kwa pigo kuu mno. Umeona hicho kikwazo kilivyo
waangamiza?
Tutizame mfano mwingine, Hesabu
21: -4 Wakasafiri kutoka mlima wa Hori
kwa njia ya Bahari ya Shamu, ili kuizunguka nchi ya Edomu ;watu wakafa Moyo kwa sababu ya ile Njia. 5 Watu wakamnung’unkia Mungu na Musa, “Mbona
mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misiri? Maana hapa hapana chakula wala hapana
maji, na roho zetu zinakinai chakula
hiki dhaifu.
Tuone matokeo yake, Mstari wa 6 Bwana
akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa.
Lakini katikati ya hayo matatizo bado Mungu
alitoa Rehema zake ambazo zilimuitaji aliye Hodari wa kushinda vikwazo ili
aweze kupona. Ona tukio hili lililo na uajabu wenye ajabu.
“Musa
akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti: hata ikiwa nyoka amemuuma mtu, alipoitazama
ile nyoka ya sahaba, akishi”.Hesabu 21:9.
Ni
walioshinda kikwazo hicho pekee ndio waliokutana na Bwana katika ng’ambo ya Mto
Yordani. Na tuangaziwe mfano wa wakina Yoshua na Kelebu walivyo shinda kikwazo
cha hofu dhidi ya majitu na kisha kufika ng’ambo ya Yordani salama.
Kumbuka hiki
ni kisa cha wale wapelelezi kumi na wawili walioleta habari za nchi waliotumwa
kuipeleleza ila kumi walileta mbaya huku wawili wakileta njema. Kwa kuwa watu
wengi walikuwa waoga wakushinda vikwazo; walilazimika kuzipokea zile mbaya na
hatimaye kukwama ila wajanja wanao ujua uzuri wa Ng’ambo ya Yordani ya kwamba
ndimo mlimo Maziwa na Asali, walihakikisha wanashinda kikwazo hicho. Bila
kukupotezea muda, pata Stori kamili kimaandiko.
Hesabu 13:31 Bali wale watu waliopanda naye
wakasema,Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa, kwa maana wana nguvu kuliko sisi. 32Wakawaletea wana
wa Iziraei habari mbaya za ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, “Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanayoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu
warefu mno 33 Kisha humo tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka
kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kama mapanzi , nao
ndivyo walivyo tuona sisi”
Kilichofwata
ni hiki: Hesabu 14:4 "Na tuweke
mtu mmoja awe akida , aturudishe Misiri.
Mbele
yake katika sura ya 14 wanataka kuwapiga kwa mawe wakina Musa. Na Bwana
anagadhabika na kuwaangamiza kwa hasira yake. Kuwa makini na tatizo kama hili
la hofu lisikukwamishe kufika hatua ya kutaka kuacha wokovu. Kwani kutamani
kurudi Misiri ni kutaka kuacha Wokovu, pia Usitake kumpiga Musa wako na mawe,
kwani huku ni kulisengenya kanisa ama kumsema vibaya Mchungaji wako au wazee wa
kanisa.Ukitenda hayo utakwama.
(“Hesabu 14:10
Lakini Mkutano wote wakaamuru watu wote wapigwe kwa mawe”)
Tuwaangaliye
walioshinda kikwazo hiki kama nilivyokujuza hapo awali: Kelebu pasina hofu wala woga alinena haya:
Hesabu 13:30. Natupande mara, tukaitamalaki
;maana twaweza kushinda bila shaka”
Wakati
walioshindwa kuvuka vikwazo wanaona ni nchi ilayo watu walioshinda wanatamani
kuiendea kwa haraka ili kuitamalaki.
Kwani
ndani yao hawakuona majitu bali waliliona kusudi la Bwana likiwa hapo ng’ambo
ya Yordani.
Hesabu 14:7 “Ni nchi njema mno ya
ajabu.. 8 Ikiwa Bwana anatufuraia,atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu,
nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. ” (
Ona maziwa na Asali katika ng’ambo ya
Yordani Mpendwa usione majitu)
Hayo
ni maneno Mubashara yeye kutia moyo kutoka katika vinywa vya mashujaa Yoshua
mwana wa Nuni na Kalebu mtoto wa Mzee Yefune.
Kwa
Ujasiri Yoshua alisimama na kusema hili.
14:9 “Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi,maana
wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa
juu yao umeondolewa, Naye Bwana yu
pamoja nasi;msiwaogope”
Kumbe
Yoshua hapa anatufundisha jambo ya kwamba mtazamo ndio kikwazo, kwani
walioshindwa walijiona kama mapanzi, na mithali husema aonavyo mtu nafsi mwake
ndivyo alivyo. Ila hawa walioshinda kikazo waliwaona ni chakula wala wao sio
kitoweo chao kwani hawakuwa na taswira ya kuliwa kama walivyonena walioshndwa
ya kwamba ni nchi ilayo watu. Na walioshindwa wanaiona kama ni nchi watakayoila.
Kisha mtazamo huo unapata nguvu kiimani kwa kubainisha kwamba MUNGU YU PAMOJA
NAO. Kumbe anayeshindwa huona kama Mungu
hayupo pamoja naye. Ndio maana anakuwa mwepesi wa kulaumu mara michango mingi
kanisani, Sadaka zimezidi, Mchungaji hana upako, mara Oh! Sikuizi hata uwepo
haupo.
Yamkini
Mpendwa mwenzangu kikwazo kikubwa ulicho nacho ni huyo mume/mkeo kugeuka teso
kwako, tafadhali usiikimbiye ndoa kwani kufanya hivyo ni kuyaogopa majitu bali
wewe Muombe Mungu naye atakuongoza chakufanya au kubadilisha kabisa na jambo
hilo kubakia kuwa historia iliyosaulika.
Usikubali
kuchelewa kwako kuolewa ama kupata mwenzi kufanyike kikwazo, badala yake mngoje
Bwana kwa Saburi naye atakujibu, huyu Mungu aliyempa Ibrahimu Isaka akiwa na
miaka mia moja na kumpa Hana mwana Samweli aliyedharauliwa na Penina
atakukumbuka na wewe.
Haijalishi
ugumu wa mazingira uliyo nayo, yamkini unaupata ujumbe huu ukiwa jela,
mahabusu, ama wewe ni mfanyakazi wa ndani au maisha uliyo nayo ni magumu kiasi
cha kukosa chakula ama kukosa kodi ya nyumba. Watoto huenda wamerudishwa ada,
umesoma lakini huna kazi, au umefukuzwa kazi na uwenda biashara imekudodea; Kwani
kila ukiuzacho hakitoki ama unauza ila hela au faida hauioni.
Skia
Neno la Bwana: Mungu wetu hashindwe na jambo, wala mazingira hayo yasifanyike
kikwazo kwako, aliyemtoa Yusufu gerezani na kumpa mujiza wa ajabu na wewe
inawezekana hii leo. Hakika Mungu wetu sio mwanadamu hata ashindwe kufanya
jambo ama aseme yaliyo ya uongo. Wewe hakikisha unasonga mbele na kuyatazama majitu
kama chakula yaaani hizo changamoto kama mtaji wako huku ukiamini bila hizo
hakuna kuinuliwa.
Ngoja
ni kupe kisa hiki, Kijana mmoja aitwaye Daudi kijana wa mbari ya Mzee Yese
alikuwa akienda siku moja kutembelea nduguze mjini na alikutana na kikwazo
kikubwa sana maishani mwake ila hakukitazama hicho.
Unataka
kukijua? Alikuwa ni mtu mkubwa na mzoefu kivita, Shujaa na pande la mtu, kwa
kiluga cha leo tungali mwita; “Jitu la miraba minne.” Ila alilitazama kama
ngazi ya kuinuliwa ama daraja la kufika ng’ambo ya Yoridani kwani bila Goliati
Asingali pata alichokipata.
Alijitoa
sadaka kama Shujaa asiyejulikana anayetafuta kujulikana, alipambana na kuhakikisha
anampiga tena kwa jiwe la mkono, mara baada ya hapo kijana alipata ushindi
mkubwa na kuuvuka mto Yordani huku akiiacha ng’ambo ya kunuka kinyesi cha Mbuzi
ama kondoo, ya kupambana na simba na dubu na kunukia pafyumu ama marashi ya
mazizini.
Unaonaje
kama kijana huyu angemuogopa Goliati? Hakika asingefika ng’ambo hiyo ya
heshima. Muhubiri mmoj akasema kuwa, “Usimuogope Goliati wako kwani ni
Promosheni ya kuinuliwa.”
Bila shaka wala takshishi ninakubaliana naye
kwani mara baada ya ushindi huo wa mama walipita mji mzima wakimuimbia ya
kwamba ameua makumi elufu huku aliyeogopa kuvuka ng’ambo hiyo akipewa elufu
zake.
( Ona maziwa na Asali katika ng’ambo ya Yordani
Mpendwa usione majitu yaani Wanefili na wana wa Anaki.)
Hongera
kwa kuanza kuchukua hatua ya kukutana na Bwana katika ng’ambo ya Yordani kwani
ni yangu imani kwamba hutatazama tena vikwazo kama vizuizi bali vitafanyika kuwa daraja kwako.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoa ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni