Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Nina
wasalimu katika jina lenye Uweza na Furaha ya hali ya juu la Bwana wetu Yesu
Kisto, Leo nimeandaa ujumbe mahususi kwa ajili ya wanafunzi waliokoka katika
ngazi zote za Elimu hususani vyuoni ila wazazi walimu, walezi na watumishi pia
ni wahusika wa ujumbe huu ili kutimiza adhima hii.
Kusudi kuu
la ujumbe huu, Ni kuwataka wanafunzi kutokuacha utayari wao wakumtumikia Mungu
pindi waendapo ama wamalizapo vyuo.
Kuna tatizo
kubwa sana linawakumba wanafunzi hawa nalo ni hili, Kabla ya kwenda vyuoni
katika makanisa walipotokea walikuwa ni watumishi wa zuri sana ila baada ya
kwenda wanaacha kumtumikia MUNGU.
Wengine
wanajitaidi pindi wa wapo chuoni ila wakimaliza na kupata kazi huacha kabisa
kufanya utumishi na baya zaidi wengine wana WITO na kusudi la Mungu kuwapeleka
vyuoni ni ili wamtumikiye.
Kama
watafanya utumishi baada ya kuhitimu, wengi ni wakati wanasubiria majibu aidha
ya chuo, vyeti ama yale ya Kazi.
Inamsikitisha
sana Mungu kuona jambo hili linatokea, kwani Utumishi wake haukusudiwi kufanywa
tu na watu ambao hawajafika kiwango hicho cha Elimu bali hata wasomi wana Nafasi
kubwa kwake kwani Paulo Mtume alikuwa Msomi na aliifanya kazi yake kwa umakini na
weledi mkubwa .
Kinachotokea
ni hiki, Wanapokuwapo chuoni uwanapoteza utayari wakumtumikia MUNGU, ambao
huwakilishwa na viatu kwenye ulimwengu wa roho.
Tuone kwenye
kitabu kile cha Wefeso; WAEFESO 6: 15 NA KUFUNGIWA MIGUU UTAYARI TUUPATAO KWA INJILI YA
AMANI.
Na sababu inayopelekea hayo ni kuweka kando Fikra za kutumia elimu yao
ili kuujenga ufalume wa mbinguni badala yake huzijaza nafsi zao na fikra za kufanikiwa
kimwili kwa elimu yao.
Jambo hili maandiko yamelizungumzia kwenye mfano wa Mpanzi na
yanalifananisha na mbegu iliyodondoka kwenye miiba na kusongwa nayo, ambapo
tafsiri yake ni mtu aliyesongwa na shuhuli nyingi na udanganyifu wa mali. Kwenye
shuhuli nyingi ni hizo fikra na udanganyifu wa mali ni huo udanganyifu wa
mafanikio ya kielimu.
Ukiwahitaji kumtumikia MUNGU huwa na kisingizio cha “ubize” ama ratiba
ni nyingi, kumbuka jibu la huo mfano wa Mpanzi linasadifu majibu yao. Tuhakiki
hilo jambo.
Mathayo 13:22 Naye aliyepandwa penye
miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shuhuli za dunia na udanganyifu wa
mali hulisonga hilo neno, likawa halizai.
Rai yangu kwao ni kuwakumbusha jinsi MUNGU alivyowatoa mbali kipindi
ambacho ada ilikuwa ikisumbua walivyomlilia kwa magoti, walipofukuzwa shule kwa
kukosa karo za shule walivyoombolezana kuwaendea watumishi ila wakati huu
imefika hatua ya kuwakwepa na wakipigiwa simu kuhusu changizo za huduma huzima
hata simu ama huona wanasumbuliwa.
Kumbuka ulipokosa msaada YESU
alikupigania, kabla hujasoma ulivyokuwa na nia ya kuifanya kazi ya MUNGU tena
kwa mzigo. Kumbuka siku ile ulipokuwa kwenye taabu kubwa kimaisha ulivyomuaidia
Mungu kama atakutoa hapo kwa kumuwekea nadhiri ya jambo utakalolifanya kwenye
utumishi wake.
Fanya hima sasa kumrejea yeye.
Ni kweli sio kila mtu ameitwa kuwa Mchungaji ama Mwalimu ila wapo walio
waimbaji, wapiga vyombo, wanaodeki kanisani na cha ajabu wanaofanya usafi siku
hizi sio wale wasomi wa chuo tena bali wasomi wameweka Elimu yao mpaka kwa
MUNGU. Paulo alisoma ila alijishusha na Mungu kumuinua.
Mshahara wako utumiye kuifanya kazi yake, masomo ama kazi ikichukuwa
muda mwingi ama kukupa ubize epeleke msalabani kwa maombi na sadaka maalumu
ukimsihi MUNGU akupe hekima ya namna ya kumtumikia pia kukupa muda katika hiyo
shuhuli.
Rudia enzi zile za maombi yako ya kufunga na kuomba, usiombe tu siku
ukiwa na jaribu ama uliyokosa amani. Mungu akutiye nguvu pia #Share ujumbe huu
na uweneze kwa wengine ikiwemo kwenye vikundi vya wanafunzi ili waliokoka
wapone kiroho.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni