Ijumaa, 26 Mei 2017

NYAMAZA KIMYA MUNGU AKUTETEE.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry
Ayubu akawaambia  adui zake; Laiti mnge nyamaza kabisa, hilo lingekuwa hekima kwenu. Ayubu 13:5.
Kumbe Ukimya ni Hekima? Na wewe fanya hima kuipata Hekima hii. Yaamkini adui zako wamekusonga na maneno kila kona, ukigeuka kulia unasikia, Eti Umefilisika, Kushoto wanasema; Huna tena Upako, Ukitaka kusonga mbele masikio yako husikia haya, “Alijiona kapata kumbe kapatikana.” Unafika mahali unataka kukata tamaa kwa kurudi nyuma, Looh! Kumbe Nyuma nako hakurudiki kwani yapo manongono haya; “Mwaka huu lazima atembee na viraka.”

Basi unajilazimisha kubaki hapo ulipo, napo hapakaliki kwani kila uchwao wanakuwinda kwa ndimi zao ili wakumalize, tena cha ajabu ni watu wako wa karibu na yamkini ni viongozi wako kanisani.


#Sasa ni sikilize, wewe nyamza kimya kwani hukutega kwa maneno yao ili urushe ngumi ama ujibizane nao, na hapo wajipatiye sababu maana maneno yao ni kama mshale, upanga.( Zaburi 57:4…Wanadamu maneno yao ni mikuki na mishale, na ndimi zao ni upanga mkali, Tena kwenye Zaburi 64:3 Waliouona ulimi wao kama upanga, wameelekeza mishale yao, maneno ya uchungu.)
Na pia ni mtego wa mwindaji. Cha kufanya wewe kaa KIMYA ILI BWANA APIGANE NAO.

Katika kitabu changu kile cha NAMNA YA KUISHI WAKATI WA MAJARIBU AU MAPITO nimelielezea hili jambo katika kipengele cha Namna ya kuishi na adui wa mwilini. Kwenywe Pwenti ya NYAMAZA HADI BWANA ATAKAPOKUPA KIBALI CHA KUONGEA.

Nami bila hiyana ya Moyo nakupakulia kama kilivyo;
Kunyamaza ni hekima, Ayubu 13:5.Laiti mnge nyamaza kabisa, hilo lingekuwa hekima kwenu.
Unapokuwa kwenye jaribu zito ni vyema kunyamaza kwa upole na kunena kwa kibali cha Mungu. Kwani usipofanya hivyo utajisababishia matatizo, hali itakayokufanya kujiingiza katika mtego wa Ibilisi. Unaweza kujikuta unanena maneno ya hasira na uchungu yatakayokupa majuto baadae. Na sio kunena tu bali hata kutenda. Usiwaze watu watakuonaje bali jilinde wewe kwanza. Fahamu ya kwamba kuna wakati utanena. Na wakati huo umekaa kimya sio kwamba unafurahishwa na linalotokea bali kinachokufanya uwe kimya ni ulinzi wa Moyo wako na kuepuka kumpa Ibilisi nafasi.


Kuna kipindi nilipatwa na tukio la ajabu sana ambalo lilinifanya kuchukuliwa kwa vitu vyangu vya ndani na mtu niliyempa dhana kwa kuwa karibu nami. Wala hakwenda kuishi mbali na vitu hivyo bali ni jirani huku akijipitiza karibu yangu kwa kuja maeneo ninayoishi.

Halikuwa jambo dogo ila kanuni hii ilinisaidia. Kwa muda wa miezi mingi nilikaa kimia bila kulinenea lile jambo. Na ni kwambiye siri hii ya kwamba ukimya ni fimbo kali kwa adui. Ukitaka adui akushinde wewe jibizana naye ila ukitaka kumtandika wewe nyamaza kimya.


Ila ilifika wakati wakujibu tuhuma na kuweka bayana udhalimu wake. Nika mwambia mtumishi mmoja kuwa wakati wangu wa kunena umefika. (Mhubiri 3:7b kuna.. wakati wa kunyamza na wakati wa kunena. Ayubu 13:13a Nyamazeni, niacheni, ili nipate kunena.)

Nikamwambia huu ni wakati wa bonde la kukata maneno. Alihitaji kujua sababu za mimi kuwa kimya nami nikamwambia kuwa wakati ule ningeongea ningali nena yasiyofaa kwani moyo wangu ulikuwa na majeraha pili ningeweza kulaani badala ya kubariki kwani kinywa chenye uchungu hutoa uchungu. Na penye ukali wa maneno hapana hekima.

Kutulia kwangu kulinifanya kugundua mengi, na mengine sikuona busara kuyanena machoni na masikio mwa watu ye yote yule”

Mungu akubariki sana na ni yangu Imani ya kwamba utakuwa makini na watesi wanaokuzunguka. Na Usikose ujumbe wa Kesho uitwao NYAMAZENI NI VUKE na wa Kesho kutwa uitwao BONDE LA KUKATA MANENO, hapo nitakuelekeza namna ya kushuhulikia maneno ya adui zako ikiwemo mbinu ile ya Isaya 54:17.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                       PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple                                              



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni