Watu wengi hawaijui hii siri...ndio maana sio wepesi wa kuzidai baraka hizi iwe ni kutoka Madhabahuni, (kwa watumishi wa Mungu) Wazazi na Kadhalika...
Hata wao wanaopaswa kuzitoa wengi wao hawana weledi wa kutosha kuwahusu au kuzihusu....
Nikiwa katika mkoa ambao hivi sasa nipo, nimejikuta nashangaa kuona sherehe za SendOff hata za watu walio okoka zisizokuwa na ibada ndani yake.
Sherehe hizo unakuta nyingine zinaudhuriwa hata na wachungaji na zinafanyikia kanisani ama mazingira hayo...lakini hata muda wa neno la Mungu haupo...(Hawajui kilichotokea kwa Rebeka saa anaagwa).
Wakati wa Ndoa pia baraka kama hizi hazizingatiwi, hii ni kutokuwa na weledi wa kutosha kuhusu swala hili la kibaraka kindoa na kiuzao..
Wakati Mungu anaifungisha ndoa ya kwanza Duniani yaani ya Adamu na Hawa; aliwabariki....leo tuna mawaidha mengi kuliko baraka...sipingi mawaidha ila nahimiza sana kuhusu baraka hizi.
Tazama : Mwanzo 1:22 Mungu akavibarikia , akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
And God blessed them, saying, Be fruitful, and multiply, and fill the waters in the seas, and let fowl multiply in the earth.
Najua mnaweza mkazaa hata bila kuwa na baraka...maana swala la kuzaa limefungwa pia katika kanuni za kibaolojia, sanjari na kuoana...lakini uzao uliobarikiwa ni swala jingine kabisa..
Watu wengi hawajaelewa nafasi na thamani ya baraka katika maisha ....ndio maana hawawi wepesi wa kuzitafuta au kuzihitaji..
Baraka na laana vimebeba hatima ya maisha ya mtu !
Kwa hiyo, baraka katika uzao na ndoa; vitabeba hatima yenu kama wanandoa pamoja na watoto wenu!
Tazama au kasome katika Mwanzo 49 kuhusu zile Baraka za Yakobo kwa wana wake, ndipo utakapoelewa...utakuta zimewafuatilia hadi sasa...kwa Yuda utaiona fimbo ya Enzi, ambayo inakuja kutimia kwa YESU...na Daudi akiwemo... Benjamin anatajwa hapo....tazama hatima yake ilivyokuja kujaa ushujaa!
Alikadhalika kwa walioambatanishiwa na laana, utakuja kukuta kuna mahali imewakwamisha...mfano Musa ni uzao wa Lawi, Lawi alilaaniwa kutokana na kosa lile walilolifanya kwa wenyeji ..na hasira ile ile ilikuja kumkwamisha Musa asiingie Kanani!
Hii ikupe Sana kujihoji na kuwa makini punde unapokaribia kuozesha au kuoa ama kuozeshwa na kadhalika....maana muda huo ni lango la hatima ya maisha yako! Na ni aidha uondoke na Baraka ama Laana!
Unaniuliza Mwalimu Unataka Kunidokezea Nini?
Wakina Simoni na Lawi, kama wangeijua hii siri wasingekubali kuondokewa na baba yao bila matengenezo! (Muda wa kufa kwa mzazi ni lango, aidha la Baraka au Laana).
Ni muda ambao katika ulimwengu wa roho anasukumwa kucheua hatima ya watoto wao. Rubeni mtoto wa Yakobo, yamkini alifikiria kosa lile limeshapuuzwa: vijana husema "limepotezewa". Alikadhalika Simeoni na Lawi. Hawakujua limeifadhiwa pahala na muda kama lango utalicheua..ndipo laana akaachiliwa...
Wanaowauguza vizuri wazazi wao huwa na hatima kubwa sana na ya ajabu...hukuwahi kujiuliza kwa nini wanapokaribia kufa wanasema niitieni na fulani? Mwambieni na fulani moja, 2, tatu!
Muda huo ni lango...kwa hiyo..
Mosi, kama ulikorofishana na mzazi wako, unapoukaribia muda kama huu, uwe ni wa kuolewa, kumaliza masomo (ukitarajia kazi) ama unapoagana naye na kwenda kutafuta maisha au pia ukiona muda wa kuishi kwake unakaribia ukingoni (utaujua tu kwa ushuhuda moyoni/na wazazi wengine au wakina bibi na babu huwa wanasema...kwamba siku zangu zinakaribia...hakikisha unatengeneza...narudia tena tengeneza...ili kuepukana na kucheuliwa adhabu kama ilivyokuwa kwa wakina Ruben, Lawi na Simeoni...katika Mwanzo 49...
Hata sasa unaweza kujiuliza, je; kuna machozi gani kutoka kwa Baba, Mama, au bibi na babu na hata walezi wako juu yako?
Akiwa alishakufa pole...angali hai tengeneza...tafuta kazawadi kaombe Msamaha...
Wakati Rebeka anaagwa...kuna maneno yakibaraka yalitamkwa....na yalielekezwa moja kwa moja kwa uzao wake...(Uchaggani zamani ilikuwa ukizalia mjini, unaenda na Watoto wako kijijini waze wanawatamkia maneno ya baraka...kwetu unatemewa mate na unapakwa usoni...)
Kama hii ni mila basi ni mila nzuri...hakikisha una muda wa kubariki watoto na wajukuu zako...kila mzazi kapewa baraka kwa ajili ya watoto na wajukuu...Yakobo alibariki Watoto wa Yusufu yaani Manase na Efraim; na akawaingiza katika baraka za Kiagano moja kwa moja...mamlaka hiyo ilikwemo ndani yake...
La kuepuka tu ni mila na tamaduni za matambiko...ila hizi za wazazi kuwabariki ni kiroho kabisa... fikra za kuwa baraka zinatoka kwa wachungaji tu sio za Kibiblia...Yakobo hakuwa mchungaji...baraka za kichungaji kwa uzao wa Israel utaziona kwa Musa mwishoni mwa Kumbukumbu la Torati, (hapo pia tunajifunza kifo cha mkubwa ni lango...muda wa kufa kwa Musa ulifanyika lango kwa Yoshua na Makabila 12 ya Israel).
Wazazi wana hatima kubwa sana katika hatima yako na uzao wako...
Tumtazame Rebeka : Mwanzo 24:60 Wakambarikia Rebeka, wakamwambia, Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu , mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Chunguza Baraka hizo...kwanza fahamu zinatoka kwa wazazi ama walezi...maana Labani ambaye ni kaka anatajwa hapo....ndio maana ni muhimu kujiuliza unapotoka au unapoondoka unaondokaje?
Nyuma ya kaka, dada, na wajomba au shangazi zako kuna maneno na machozi ya aina gani?
Furaha saa wanakuaga isikufanye kuona mpo pamoja...maana tukio hilo hufurahiwa na yeyote!
Baraka hizo kama umezichunguza utagundua ya kuwa, anataja .."ndugu yetu uwe wewe mama wa kumi elfu"...maana yake uzao utakaoongezeka... Leo tuna Israel ya mwilini na ya rohoni ambayo ni mimi na wewe tulio okoka...na hakika tu wengi....
Pili akaumiliki mlango wa adui zake, Baraka ambazo zipo pia katika Mwanzo 22 ambapo Ibrahim alitamkiwa na Mungu...huo mlango sehemu moja wapo ni Kanani, ambapo katika Laana ya mtoto wa Nuhu mara baada ya baba yake kuutazama uchi wa babu yake....ambapo mbaraka huo ulielekea moja kwa moja kwa wale wana wawili...ambapo pia ni kwa uzao ambao Ibrahim alikuja kupita kwa kumpitia Tera...
Hata sisi leo ili kumiliki, lazima tujifunze kuumiliki uzao wa adui zetu...katika Edeni Shetani 😈 alikabidhiwa dunia... kanisa likihitaji kumiliki, linalazimika kufanya vita vya namna hii...na vita hivi huwa vyepesi pale unapofanikiwa kuwa na hizi baraka....
Naomba sasa niishie hapo...ila kwa zaidi endelea kutembelea na KuFolo Channel Yetu hii ya Wasapu ya Baraka Za Mungu... Àsante
Follow the Baraka Za Mungu Juu Yako (Wewe Ni Mbarikiwa) channel on WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VbBZGFZ1CYoaefQvAa12
Lakini Mkini pia Hujaokoka, na Nikuomize Kufanya hivyo ili uwe sehemu ya Baraka hizi za Kiagano....
Sema; MUNGU BABA, NIMEKUJA MBELE ZAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUOMBA UNISAMEHE SASA: Amen.
Tafuta Kanisa la Watu Waliokoka Ukasali Hapo..
By Mwalimu Oscar Samba (Mwanza Tanzania).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni