Na Mwl. Oscar Samba
5. Omba Mpenzi ya Mungu Yatimie.* Unajua maana yake ni nini?
Ni kwamba, umefikia mahali ambapo kwa akili na fahamu zako,
hujui mpango wa Mungu, ama unajua lakini huna ujasiri na uwezo
wakuukukabili! Sasa mwambie Mungu sio kama mimi nitakavyo bali
mapenzi au mpango wako, ama njia yako ndiyo niiendee, sio njia
nyingine. Yaombe haya kwa mzigo mkubwa sana, na kwa kumaanisha
kwa viwango vikubwa mno.
22:41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,
42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki;
walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Tunaona baada ya kuomba au kuyataka mapenzi ya Mungu, ndipo
malaika wa Bwana anamtokea na kumtia nguvu! Wakati mwingine
nguvu zinakuja pale unapokuwa tayari, kutoka ndani ya moyo wako
kuya kubali mapenzi yake! Maana anajua akikupa nguvu za maombi
kiholela; unaweza jikuta unazitumia kinyume: kwa kuombea mipango
ambayo siyo yake.
Kuna kisa cha mtu mmoja aliyekuwa na njaa sana, naye alikaribia kufa.
Akaja mtu akamletea biskuti, alipoiona alicheka kwa furaha; na ghafula
akadondoka na kufa! Kwa nini? Alikuwa na nguvu ndogo, alisalia na
nguvu kidogo sana. Ambazo alitakiwa kuzitumia kwenye kula chakula,
ila akazitumia kwenye kucheka!
Unapaswa kuwa makini sana unaposalia na nguvu ndogo za maombi!
Usizitumie kumlaumu, au kumlalamikia Mungu, ama kuombea
mipango mingine. Bali zielekeze moja kwa moja kwenye kumtukuza Mungu. Kuonyesha uku wake, kumuonyesha kuwa bila Yeye wewe
huwezi lolote. Kumuonyesha kwa hata hapo ulipofika sio kwa uweza au
nguvu zako; bali kuna mkono wake Mungu nyuma yake. Na hata unako
kwenda Yeye bado anakujua. Onyesha kuwa Yeye anakuwazia mema,
maana anayajua mawazo anayokuwazi; kwani ni ya mema siku zote.
Baada ya hapo sasa penyeza wazo la kumtaka akupiganie. Akupe
kutembea kwenye mapenzi yake, mueleze ukweli kuwa mwili na fikra
na nafsi yako ni dhaifu. Ila akutie nguvu na uyakubali na kuyatimiza
mapenzi yake. Kama huyajua anza na wewe kuyajua, kisha uyakubali
na hatimaye kuyatimiza.
Kumbuka sana hili; kuwa Mungu ni Mungu na atabaki
kuwa Mungu hata kama hujamuelewa. Hata kama unaona
amekupitisha mahali pa gumu sana; haimbadilishi kuwa Mungu:
kwa kuwa wewe umekwama au unataka kukwama!
Ukibisha kawaulize wakina Meshaki, Shedraka na Abernego
watakusimulia. Haikumbadilisha kuwa Mungu kwa waokuwa kwenye tanuru la moto!
Wakati hao wanaokolewa wengine walikufa kwa kuawa. Stefano, na
Agripa Shaihidi wake na msashujaa wa Agano la Kale waliifia imnai.
Na hiyo haikumbadilisha hata kidogo; kuwa Mungu: kwa sababu tu hakuwaokoa!
Mungu ni Mungu hata kama humuelewi, atabaki kuwa Mungu! Hawi
Mungu kwa sababu amekujibu, wala haibadilishi Uungu wake kwa
kuwa unamuona amekaa kimya! Ukifa kwa kuungua moto, bado ni
Mungu, na ukiokolewa kwenye huo moto kama hao mashujaa hapo pia
ni Mungu.
Kutokujibiwa kwako, au kuchelewa kujibiwa; ama kupokea majibu
ambayo hujayatarajia, hakumbadilishi Mungu. Yesu hakuokolewa
msalabani; wala hakujiokoa, na hiyo haikumbadilisha MUNGU AMA
KUATHIRI Ungu wao. Uungu na uweza wake ulisalia pale plale,
maana hivyo ndivyo ilivyoupendeza Uungu.
Epuka kuona kwamba Mungu anakuonea. Au kuzikubalia akili
na fahamu zako, kukosa sababu za kuelewa ni kwa nini
anakupitisha hapo. Madhara yake ni kuzaliwa na kukua kwa hali
ya kutokumuelewa Mungu!
Usipomuelewa Mungu! Hutaona thamani ya kuendelea kuvumilia
kuwepo hapo! Thamani ya kupitia hapo ikitoweka au
kupungua, uwe na uhakika sababu za wewe kuvumilia
zitakosekana. Hali itakayokufanya kuona kuendea
kuvumilia hakuna faida yoyote. Ni sawa na kujiumiza na
kupoteza muda bure. Linda sana sababu yoyote inayonuia
kukufanya kutokumuelewa Mungu isikukaribie.
Waliokwama jangwani ni matokeo ya kutokumuelewa Mungu!
Walifikia hatua ya kuona ni kama vile aliwatoa Misri ili aje awaulie
jangwani!
Sasa nawiwa kukujuza jambo hili, katika ile mistari ambayo
tuliitazama pale, kuna mstari huu muhimu sana, “kuwa Yesu alijitenga
na wanafunzi wake..kisha akasogea mbele kidogo akaomba..”
Luka 22.41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe,
akapiga magoti akaomba,
42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki;
walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
Ukitazama kwa makini na kwa jicho nililo nalo. Ndipo utakapokuja
kugundua kuwa; aina ya ajenda aliyokuwa nayo Yesu ingeweza kupata
upinzani mkubwa: kutoka kwa wana timu wenzake!
Na kabla sijafika huko, ngoja ni kwambie kuwa; hitajio kubwa kwa
Yesu kutoka kwa wanafunzi wake ni wamuombee. Hali aliyokuwa
nayo kwenye nafsi yake, hakunuia sana mapenzi ya Mungu kutoka
kwao, bali ile hali ya kusumbuka ndani. hali iliyompelekea kuwa na
huzuni iliyopitiliza.
Sasa ngoja nikujuze, aina ya ajenda ya Yesu ilimfanya kujitenga kidogo
na wanafunzi wake. Yesu moyoni mwake alikuwa na nia kabisa ya
kupita msalabani! Ila mwili ulikuwa ukimpigia kelele au kumzuia. Na
alifahamu fika kuwa akiwaeleza wanafunzi wake moja kwa moja, kuwa
anataka kupita hapo, upinzani lazima ungekwepo. Maana hawakuwa
wameuelewa mslaba, kwa namna ambavyo Yesu alikwa amefahamu.
Ukija kule awali kwenye kitabu cha Mtahato ile 16, utafahamu kuwa
Petro alikuwa amemgomea kwa kupinga kufa kwake. Ukija hata baada
ya hayo maombi; kipindi hicho cha kukamatwa kwa Yesu, Petro alitwa upanga na kumkata mtumwa wa kuhani mkuu sikio (akipinga kufa kwa
Yesu)!
Yesu alifahamu kuwa, wakimsikia moja kwa moja, ya kuwa anaomba
apite hapo; kuna hatari ya kukabiliana na upinzani mwingine. Najua
walijua kuna kitu mbele, ndio maana na wao walipaswa kumuombea.
Ila sio kwa namna ambavyo Yesu pia angeomba, maana hata baada na
hata wakati wa kufa kwake, namna walivyokabiliana na matokeo yale
pale awali inasadifu jambo hili sana.
Nataka kukujuza au kukufunza nini hapa? Kuna aina ya maombi ya
mapenzi ya Mungu, unaweza omba mbele ya watu na wao wasikuelewe
kabisa. Hata kama una timu ya maombi, uwe na hakika kuwa kuna
majira ya kujitenga na kuzama kwenye kunena kwa lugha ili kuepuka
aina ya upinzani. Wanaweza wasikwambie, ila na wao kujikuta
wanaomba kinyume na wewe. Hali itakayokuletea vita vipya kwenye
ulimwengu wa roho. Maana kuna muda inakuwa ni mwenye nguvu
mpishe. Nikimanisha maombi megine yasiyo sahihi yanaweza
kufanyika zuio.
Ndio maana Mungu alimuonya Balaamu na kumkamata kinywa maana
kungekuwa na athari kama angeachiwa kufanya hivyo. Unajua kama
kungekuwa na uwezekano wa kutokuwa na madhara; basi kusingekuwa
na umuhimu kwa Mungu kutumia nguvu kubwa kwa kiasi hicho
kumdhibiti!
Na wewe ukabili ushirikina wa kimaombi wenye kutumia jina la
Yesu; kwa kutumia hekima! Maana maombi hata yakiombwa kinyume
huwa yanaweza kukudhuru. Maana hapa inawezekana nia yao ni njema,
ila katika hili la mapenzi ya Mungu; ambayo yapo mbele yako; wao
hawaja yafahamu wala kuyaelewa. Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi
wa Yesu. Japo ujuzo huu haupaswi kukupa moyo wa kugomea
mashauri yao; au kujisemea kuwa hawatakuelewa. Au hatanielewa
maana hata Mwalimu Oscar alishawazungumzia watu kama hawa!
Hapa usinisingizie, huko ni kukosa maarifa, Roho wa Bwana
anapaswa kukuongoza. Na fahamu kuwa kuna muda hutumia watu
kukujulisha aina ya mapenzi yake. Ni kazi kwako kuwa na uwezo wa
kujua hapa ni wapi. Na huyu ni adui ama ni Roho Mtakatifu ndani
yake!
Na Wiwa Kukuongea na Pointi ya 6:
6. Washirikishe ama Omba Msaada kwa Wapendwa; Ni muhimu kujifunza kuunganisha nguvu, Esta alipokuwa katika hali ya
njia panda; maana Modekai alimuleza wazi mara baada ya kujaribu
kulikwepa shauri la Bwana: ilimbidi aombe msaada wa maombi ya
kufunga na kuomba kwa muda wa siku tatu.
Yesu mwenyewe aliyekuwa ni Mungu, aliomba msaada; Akawajia wale
wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza
kukesha pamoja nami hata saa moja? Mathayo 26:40
Ni kweli maombi haya yalikuwa na umuhimu kwa wanafunzi pia, ili
wasije kuingia majaribuni, ila kiukweli na kihalisia Yesu alihitaji
waombaji pamoja naye! Na wewe usiendelee kukomaa wewe
mwenyewe. Vita nyingine inahitaji msaada. Hata kama ukiona huwezi
kujielezea mbell yao moja kwa moja, wewe waambie tu niombeni.
Maana kuna mahali napitia, kwa kweli pananiweka njia panda ya
kiroho, ninasueni kwa kuniombea nipata nguvu za kiroho. Na naniweze
kuyafuata mapenzi ya Mungu maana kwa kweli inatishia kiroho
changu.
Usipitwe na Mfululizo wa 9, wenye pointi ya 7. Kama Hujui Chakufanya Usifanye Chochote.....
Km Bado Hujaokoka, Nikutie Moyo Kufanya Hivyo Sasa...
Sema; BWANA YESU, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUOMBA UNISAMEHE SASA: Amen.
Tafuta Kanisa la Watu Waliokoka Ukasali Hapo
Usiache Kufolo Channel Hii ya Wasapu
Tumeunda Channel ya WhatApp, Tufolo; https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Ni Maalumu kwa Ajili ya Mafundisho ya Neno la Mungu.
Kwa Maombi: +255759859287
http://www.ukombozigospel.blogspot.com
Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD
Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk
Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv
Kwa Maombi +255759859287
Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook: https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL
UWE NA AMANI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni