Jumanne, 23 Desemba 2025

Mfululizo wa 6 Katika Kitabu Chetu cha CHAKUFANYA UKIWA NJIA PANDA.

Mada ya 2 ya Mambo Mengine ya Kufanya au Kuepuka Ukiwa Njia Panda.

Na _Mwl. Oscar_ Samba 

Pointi  ya 3. Ingia kwenye Maombi ya Muda Mrefu. Yanaweza pia yasiwe 

ya muda mrefu, ila yakawa ya kina na mazito au yenye mzigo mzito. 

Lakini imizo la maombi ya muda mrefu sio la kupuuza, ni muhimu sana 

kulizingatia. Yanaweza kuwa ya siku tatu kavu, masaa 24, au ya wiki 

moja. Huweza kuwa katika mfumo wa masaa 12 au 24 kwa 24 ama 

masaa 36 na kadhalika. Ni kadri Roho wa Bwana atakavyo kuongoza.

Kuna baba mmoja alikuwa akipitia mahali pa gumu sana, aliingia ubia 

wa kibiashara na mtu ambapo ilimbidi aweke dhamana mali zake 

muhimu. Na Yule mtu baadae akajakukimbia na ile fedha; alifikia hatua 

ya kutaka kujiua. Maana ilikuwa ni fedha nyingi, mkewe alimshauri 

asijidhuru badala yake wa mgeukiye Bwana.

Aliamua kuingia kwenye maombi ya siku tatu, alipokuwa kwenye hayo 

maombi alisikia sauti ya Roho Mtakatifu ikimwmabia sio siku 3 bali ni 

siku 90. Lilikuwa jambo gumu sana kwake, alimueleza wazi kuwa 

kwake hata maombi ya siku 21 yale yanayotangazwaga kanisani 

kufunga kwa ufanisi ni tatizo. Kwa ujumla alikuwa; ni mdhaifu kwenye 

hilo eneo, alimuomba amtie nguvu lakini pia amuinulie watu. Ghafula 

akaanza kusikia kutoka kwa watu asiyowajua kwamba wamepewa 

mzigo wa kuomba naye, huyu wiki na yule muda kadhaa.

Wakiwa na baada ya maombi alipokea majibu makubwa sana kutoka 

kwa Mungu. Biashara zake zilifunguka na mipango mingine ya 

kibiashara ilifana sana. Akajikuta anapata fedha za kulipa ule mkopo, 

jambo lililonusuru kuuzwa kwa mali zake muhimu alizoziweka kama 

dhamana.

Alikuwa katika njia panda ambayo sio kwamba ilitishia tu uhai wake 

wa kiroho ama mahusiano yake na Mungu; bali alitaka kujidhuru hata 

mwilini! Bahati nzuri alimgeukia ama alimtafuta Bwana.


Yesu alipokuwa katika njia panda ya kuamua aende msalabani au 

akwepe! Aliamua kuingia kwenye maombi mazito. Maombi haya ni 

aina au ni moja ya maombi ambayo mbingu na nchi haziwezi 

kuyasahau kabisa. Maana yalibeba hatima ya ukombozi wetu! 


Kumbuka njia panda yoyote ile imewekwa ili kukupa kuamua maamuzi 

yatakayo beba hatima yako ya baadaye. Ndio maana ni hatari kuamua 

kuolewa kiholela kwa sababu tu ya kungoja mchumba kwa muda bila mafanikio! Matokeo au madhara yake ni makubwa sana, jaribu kufikiri 

nini kingetokea kama Yesu angekwama kwenye njia panda ile! Ni 

hakika tusingalikuwa na ukombozi hivi leo!

Mathayo 26:39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka 

kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, 

kikombe hiki kiniepuke;..


Kitu kimoja wapo maombi haya hufanya ni kukutia nguvu, kuna watu 

wamefikia hapa sio kwamba mioyo yao imeharibika au imegeuka ila ni 

matokeo ya wao kuishiwa nguvu kabisa. Mioyo imezimia na haipo tayari 

kusonga mbele; lisikie Neno la Bwana ndugu yangu! Wazimiao watapokea 

nguvu mpya, nao watapanda juu kama tai, wala hutachoka tena! Hiyo ni 

Isaya 40, maana ndivyo Mungu anavyotuambia. Hali inayoashiria kuwa swala 

la kuchoka na kuzimia au kufa moyo; kupo ila yupo mtoa nguvu, na mombi ya 

mzigo ndiyo yatakayokupa uweza huo!

Kwa Yesu hili lilitokea; 22: Malaika kutoka mbinguni akamtokea 

akamtia nguvu. 

44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari 

yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.] 

Luka 22:43-44.


Kutiwa nguvu kupo, ila tatizo linakuja katika nia ya mtu, ukichoka na 

kufikia hatua ya kugoma kuhitaji msaada wa kutiwa nguvu; hilo ni 

tatizo tena kubwa! Ni sawa na mgonjwa nayekataa dawa. Na baya zaidi 

akataa na kula chakula na kunywa maji! 

Maana kuna muda mwili unapambana au unajipambania maana 

kibaolojia umepewa kutengeneza kinga yakujihami na kushambuliana 

na magonjwa! Sasa kama haupewi chakula na maji ni hatari sana! Kama 

huwezi hicho ni kitu kingine, tatizo ni nia, ndio maana hospitalini kuna 

kutundikiwa maji ya dawa, au yenye nguvu ama maji kama maji. 

Kuongezewa damu na kwa wengine hata kulishwa kwa njia ya mpira! 


Lakini kama hutaki, uwe na hakika ukipata nguvu kido tu

utaishimamisha hiyo “dripu” au utaichomoa! Maana hutaki kuishi tena! 

Hapa sio swala la mwili kuwa dhaifu tu; bali ni mtu kuwa na nia ya 

kutokutaka tena msaada kwa kiwango kikubwa.

Nampenda sana Elia, maana alipokuwa amechoka katika ile 1 Wafalme 

19 alikimbilia chini ya Mretemu. Huu ni mti wenye kivuli kizuri. Na ukizingatia ilikuwa ni jangwani, jua ni kali, hakukubali kujiweka penye 

jua. Na alipoletewa chakula au ku ndaliwa na malaika. Alikubali kula, 

akalala bado alipoamshwa au kuimizwa tena alikula. Na baada ya hapo 

alikubali sasa kuuendea au kuendelea na mpango wa Mungu juu yake.

Ukiona umechoka kiroho, na hutaki msaada, ukiwaona wapendwa 

unawakwepa., hutaki kupokea hata ya simu ya mchungaji wako. 


Ukimuona mama mchungaji unajifanya kama vile hujamuona! Uwe na 

hakika u sawa na mgongwa anayeikwepa hospitali! Mgonjwa anaye 

mkimbia “nesi” badala ya kumkimbilia.

Ukiedelea utagundua kuwa baada ya haya maombi, Yesu anawaambia 

wanafunzi wake laleni sasa! Ikiwa na maana kuwa vita amefanikiwa 

kuvimaliza.


Tutajionea kwa mfalme Hezekia, na Yehoshefathi, walipokuwa kwenye 

kipindi kigumu cha kivita, adui zao waliwatishia. Maana walikuwa na 

uwezo mkubwa kuliko wao; ila waliamua kumkimbilia Mungu. kwani 

adui waliwatengenezea mazingira magumu ya kujisalimisha; walikuwa 

na njia kuu mbili mbele yao. Kusisalimisha kwa adui au kumtazama 

Mungu! Na kwa hila adui alijitutumua mbele yao kana kwamba ana 

guvu kuliko wao na Mungu wao. Ndio maana walitaja ukuu wa miungu 

yao. Hususani huyu aliyekuwa akipamba na Hezekia, alijigamba sana.

Na kueleza jinsi miungu yake ilivyompigania; akiwataka Wayahudi 

wasimuamini mfalme wao akiwa na nia ya kuwafanya wabadilike 

kimtazamo. Bali walikaza katika kumtazama Bwana kimaombi na 

kiimani na hatimaye Bwana aliwapigania.


Kama Hujaokoka, Nikutie Moyo Kufanya hivyo Sasa, Sema  BWANA YESU MIMI NI MWENYE DHAMBI NAKUOMBA UNISAMEHE SASA; Amen.


Tafadhali Tafuta Kanisa la Watu Waliokoka Ukasali Hapo... Àsante...Tuandikie pia katika namba hapo chini ili tukutumie Kitabu cha Kuukulia Wokovu... Asante..


Usikose Mfululizo Ujao wa 7 katika pointi isemayo Tafuta Ushauri Sahihi..kwa mfuluzo huo na mingine tangulizi usiache kuifuatilia Channeli yetu hii: ..


Karibu Sana Katika Channel Yetu Hii

 

 *Ni Maalumu kwa Ajili ya Mafundisho ya Neno la Mungu.* 

Tufolo; https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h 


Tafadhali Tembelea na Hufuma Zetu Nyingine


BIBLIA TAKATIFU 


https://whatsapp.com/channel/0029Vb6yb822f3EB3Zfbep3z 


BARAKA ZA MUNGU 

https://whatsapp.com/channel/0029VbBZGFZ1CYoaefQvAa12 


Kwa Maombi: +255759859287 

http://www.ukombozigospel.blogspot.com


Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD

Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv

Kwa Maombi +255759859287 

Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook: https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL


UWE NA AMANI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni