Tunaanza na Utangulizi (kinapatikana Google Bure)
Na Mwl. Oscar Samba
Utangulizi
Kitabu hiki kimenuia kumsaidia mtu ambaye yupo katika mazingira
magumu ya kimaamuzi, na mbele yake kuna aina zaidi ya moja ya
maamuzi ambayo anahatarishwa kuyachukuwa au yanayomkabili,
inawezekana lililo hatari ni moja, au salama ni moja ila kuna zaidi ya
aina mbili au moja na kadhalika.
Kitabu hiki ni matokeo ya sehemu ninayopitia sasa kuhusu ndoa yangu.
Ikumbukwe sasa ni mwaka unaokaribia wa nane toka mwenzangu
tuoane na kujikuta ananiacha kwa talaka mahakamani hali inayonipa au
kunipelekea kuwa njia panda. Njia panda yangu inaweza isiwe na tija
sana kwako ila la muhimu ni wewe kufahamu mazingira ya kitabu
hiki ili kikusaidia. (Wakati nakitoa, imetimia miaka 10/11, “2015-
2015”.)
Unaweza usione umuhimu wake kwa leo ila nikuhakikishie kuwa
chakula hiki ni kama akiba, kuna muda tunakula leo lakini chakula
hicho kinatusaidia kesho; sio kwamba tuliingia kwenye mfungo la! Bali
homa ya ghafula imetukuta na kutunyima hamu au uwezo wa kula. Ila
kwa akiba ya jana ambayo hatukuwa hata na wazo la kula tumevuka leo
salama!
….Nikikuongezea ni kwamba, mara baada ya kuandika
utangulizi huu, na nikiwa tayari nimeshaanza kukiandika hiki
kitabu, njia panda nyingine ilijitokeza kama sio moja basi ni
zaidi, licha ya swala la ndoa, lakini pia limeibuka swala la
kusimamishwa masomo chuoni. Kumbuka nipo katika chuo cha
Biblia Dodoma cha CBC; mara baada ya kutofautiana na
kiongozi wangu mmoja wapo katika swala fulani, nilijikuta
nikipewa adhabu ya kusimamishwa masomo mwaka mmoja.
Nikiwa tu nimetoka kuchukuwa barua zangu, (ikiwa moja yangu na ya
mchungaji wangu kingozi,) ndipo nilipokutana na mchungaji mmoja wa
dhehebu jingine akiniambia kuwa nihamie kwake. Maana huku
kumekuwa kugumu kwangu na katoa sababu kadhaa: zingeweza
kuonekana ni zenye mashiko maana nyuma ya pazia jambo langu
limeonekana ni matokeo ya mimi kuwa na tabia ya kutetea na kudai haki. Pamoja na kusema ukweli pale ambapo ninapoona mambo
hayajaka sawa.
Wazo hili halikwepo kabisa kichwani mwangu, maana nilishapitia
mahali kama hapa mara baada ya uongozi wangu wa sehemu huko
Arusha kutofautina nami na kunichukulia mamuzi ambayo sikuyapenda
maana sikusikilizwa kimapana!
Japo mara baada ya taarifa za kusimamishwa kwangu, wenzangu
niliokuwa nao chumba kimoja miongoni mwa ushauri wao wa kwanza,
ni ule wa kunitaka nisihame dhehebu, sikuwa nimewaelewa maana
wazo hili halikwepo. Sasa baada ya ushauri wa kuhama niliokuja
kuupata baadae, na hususani nikiwa kwenye gari wakati narudi
nyumbani; ndipo wazo hili la ile mbegu ya yule mtumishi likataka
kumea au kukua ndani yangu. Niliing’oa kwa haraka kwenye mawazo
yangu! Maana nilijua kitu adui anachokitafuta.
Japo kulizaliwa nyingine ya je, nikimaliza adhabu nirudi tena hapo
chuoni au nihame! Maana mazingira yaliyonipelekea hapo ninafahamu
fika bado yangalipo! Nafika nyumbani nako nakuta mradi wa kuku
niliouanzisha kuku wamekufa kama asilimia 75 hivi!
Njia panda nyingine inazaliwa ya kukata tamaa; kuuendeleza au
kuupatia nguvu tena! Ila baada ya imizo kubwa moyoni mwangu
nikajisema kuwa; ukiniuliza swali kwamba kwa nini Oscar nafanikiwa
nitakujibu kuwa, nilifeli somo la kukata tamaa!
Mimi sijui njia panda yako ni ipi! Ila unatakiwa kuwa makini na aina ya
maamuzi unayofanya hususani ukiwa katika nyakati ngumu! Utulivu ni
muhimu sana. Utanielewa katika kipengele cha utulivu.
Ngoja nikuongezee jambo jingine!
Niongeza hii inakuja mara baada ya kukikamilisha kitabu hiki kabisa,
na ninaiongezea mwaka huu wa 3/2025, maana nilikianza na
kukikamilisha mwaka huo wa 2022 kwenye mwezi wa 3.
Kwanza mara baada ya mkasa huo wa kusimamishwa masomo,
nilijikita katika maombi ya siku 21, ghafula nikagundua dozi haitoshi.
Nikaendeleza megine ya siku 40, jumla yakawa siku kama 61 hivi.
Katika maombi hayo ndipo nilipopokea agizo na imizo moyoni
mwangu la kuanza mikutano ya injili. Na nilimwambia Shetani wazi ya
kuwa umenipiga chuoni, mimi ninakupiga mtaani.
Nilifanikiwa kufanya mikutano ya injili kama 24 ndani ya miezi 7.
Ukifanya idadi ya wiki kwa kufanya 7x4=28 ukitoa hiyo mikutano 24
utapata ni wiki 4 tu ambazo siku hubiri.
Idadi hiyo ya mikutano iliwapa hofu sana wachungaji wenzangu wa
dhehebu langu. Kukainuka vita vikubwa sana. ikaenea propaganda ya
kuwa nina mpango wa kufungua kanisa huko Rombo, kwa hiyo
nikifungua nitachukuwa washirika wao wote. Maana pia nilikuwa
nafanya na mikesha ya maombi nyumbani kwangu, na kwenye baadhi
ya makanisa yaliyotupa kibali. Sanjari na hayo tulikuwa tukifanya
mikesha kama hiyo kwenye nyumba za watu wenye mahitaji
mbalimbali, kundi lilikuwa ni kubwa.
Mikesha hiyo ilikuwa ikiudhuriwa na baadhi ya wachungaji, wake zao,
na familia zao. Lakini pia na wazee wa kanisa kutoka makanisa
mbalimbali ya dhehebu langu huko Rombo.
Nilipofikia mkutano wa 14, nilikutana na upinzani mkali uliotishia
kuendelea kwangu na mikutano hiyo; ulitoka kwa mlezi wangu kiroho
ya kuwa niache kuendelea na mikutano hiyo. Japo, toka mwanzoni
kabisa mara baada ya mikutano kadhaa, niliona hali ya kunyimwa
ushirikiano. Upinzani huo ulipanuka hadi ngazi ya sehemu na kiongozi
mmoja wapo wa jimboni kuwa sehemu ya swala hilo.
Wachungaji kadhaa ambao nilipaswa kuhitaji ushirikiano nao,
walijikuta wakipewa taarifa mbaya kuhusu mimi; hali iliyotishia
ufanyikaji wa mikutano yangu. Kwa hiyo, dehebu langu la nyumbani
likanisusa kabisa. Watu wengine wakajitokeza na kunipa ushirikiano.
Wakati nikipambana katika kipindi hicho hicho, sasa nikiwa ninaelekea
mkutano wa 15; ndipo nilipopokea ujumbe wa simu ya mkononi kutoka
kwa mlezi wangu kiroho wa kunifukuza kanisani. Sababu ni kwamba
ninafanya mikutano kwa kiburi. Nilipokonywa na spika. Nikasalia na
spika zile za juu “horn speaker” na baadhi ya vyombo.
Sikuacha, nikahubiria kuzipitia hizo hizo. Ila Mungu akanipatia “midi
speaker” kipindi cha muda mchache mbeleni. Watu wa madhebu
mengine wakaibuka, wakitaka nijiunge nao. Kiukweli walinipa
ushirikiano mkubwa sana, japo nia ya kunivutia kwao ilikuwa ni kubwa
pia.
Kama hilo halitoshi, ngazi ya sehemu bila kunisikiliza, au kujitetea,
nayo ikatangaza kunifukuza. Na wakasema nimefukuzwa katika kanisa
la nchi nzima. Kumbuka hapo nimesimamishwa masomo, na huku
ninafukuzwa.
Nilikuwa, katika hati-hati ya kuendelea na mikutano au la! Nilijisemea
moyoni ya kuwa, sitarudi nyuma. Nitaendelea na mikutano hadi
mwisho, kisha nitaona atakalolitenda Bwana. Mara baada ya juhudi za
kuhitaji suluhu, nilijibiwa ya kwamba labla niache kuhubiri; ndipo
tutakaa na kuzungumza. Niliwajibu, kama kuhubiri ni kiburi basi
amueni wenyewe. Japo jibu hilo nililitoa moyoni; sio mbele zao moja
kwa moja. Nikajisemea tena, kama kuhubiri ni kiburi, basi hiki ni kiburi
kizuri Zaidi.
Niliijua hofu yao, walisema ya kuwa hii ni “movement.” Na
wanamashaka itachukuwa washirika wao wote, wakidai nina kibali sana
kwao. Kwa hiyo, makakati wao ulikuwa ni kunizima! Matunda ya watu
kuokoka, ilikuwa ni nguvu yangu.
Wakati huu, hali ilikuwa ngumu kidogo. Maana tangazo la sehemu
lilipiga marufuku hata washirika wa kawaida kuwa pamoja nami,
wakionekana tu na mimi wao nao watafukuzwa. Kwa hiyo,
wakalazimika kutuma tu watoto wao kuja kunisaidia kuimba pamoja
nami kwenye mikutano. Wao wakaishilia kunichangia na kuniombea.
Wachache sana walidiriki kuja na kunisaidia majukumu moja kwa
moja.
Nilikabiliwa na njia panda nzito ya kuendelea kusalia na dhehebu langu
au la. Tofauti na kipindi nilichofukuzwa Arusha, kipindi hiki sikuwa na
shida sana kuhusu kutaka kuhama mwamvuli wa dhehebu. Ila washirika
baadhi yao walinishindikiza, wakisema muulize Mungu uwenda wakati
huu anataka uhame, tofauti na ule wa Arusha aliokuzuilia.
Mchungaji mmoja rafiki yangu akaniambia, labbla niache kwanza
kuhubiri niingie maombi ya siku 40. Nikamuuliza ya nini? Akanijibu ni
ili nimulize Mungu ni kwa nini ninapigwa vita? Nikamjibu, maombi
nilishaomba. Maana ule ulikuwa ni muda wa kazi. Nikamwambia Roho
alishanijibu. Akaniuliza, amenijibuje? Nikamwabia ameniambia;
“kanyaga twende; kanyaga twende.” Tukaishilia kucheka, ila huo ndio
uhalisia.
Nilipokaribia na mwisho, nikapokea ufunuo kutoka kwenye Zaburi, ya
kwamba nimetengwa na mpenzi wangu, waliopaswa kunisaidia
nimetengwa nao. Nikajikita katika maombi ya siku 4. Bwana
kanipatanisha na adui zangu, nikaandikiwa barua mbili. Moja ya
kunirudisha katika ushirika, na pili ilikuwa ni ya kunirudisha chuoni.
Na kipindi hicho cha kufukuzwa, ashukuriwe Mungu aliniinulia
mhazini wa Jimbo, ambaye alinipokea kwa nguvu. Kinyume na taratibu
maana nilipofukuzwa sikupewa mahali pa kusali; nikawa chini yake
nikaabudu kwake.
Leo ninavyoongea yaani 2025 hii ni miongoni mwa watumishi muhimu
katika dhehebu hili hili. Kwa hiyo, adui aliijua kesho yangu, na akataka
kunizuilia. Jiulize, ni wangapi wanaopitia katika nyakati kama hizo na
kujikuta wanafanya maamuzi ya kuhama katika makanisa, au madehenu
yao? Hapana shaka ni wengi, kwa hiyo adui ameua kesho za watu
wengi kwa kupitia njia panda kadha, wa kadha alizozileta mbele yao!
Ukiamua vyema leo, utaifikilia ndoto yao. Usibadili urai wa uzao wa
Yakobo, kisa ndugu zako wamekuchukia na kukuuza. Salia nyumbani.
Maana wewe ndiwe msaada wao miaka kadhaa ijayo.
Tafadhali Usikose Sehemu Ijayo (2)
Km Hujaokoka Okoka Sasa...Sema: *BWANA YESU, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAKUOMBA UNISAMEHE; Ameni*
...Tafuta Kanisa la Watu Waliokoka Ukaabudu Hapo...Nimekuombea
Karibu Sana Katika Channel Yetu Hii
Tafadhali Tembelea na Hufuma Zetu Nyingine
Ni Maalumu kwa Ajili ya Mafundisho ya Neno la Mungu.
Kwa Maombi: +255759859287
http://www.ukombozigospel.blogspot.com
Tumeunda Channel ya WhatApp, Tufolo; https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h
Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD
Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk
Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv
Kwa Maombi +255759859287
Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook: https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL
*UWE NA AMANI*
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni