Jumamosi, 23 Mei 2026
. Chuki Ina Nguvu Kama Mauti. Kati ya jambo la ajabu sana nililojifunza na ningependa ulifahamu; ni hili la nguvu ya chuki. Ni hakika chuki ina nguvu sawa na roho ya mauti. Lakini pia chuki hutenda kazi kama ilivyo roho ya mauti. Sio jambo jepesi kulielewa kama halijawahi kukuta ama kama hujawahi kujifunza somo hili kwa sura ya namna hii. Na Mwl Oscar Samba Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu Chetu cha IMANI INAPOJARIBIWA; Karibu... Walipomchukia Yusufu na kumuuza; ni wazi alishakufa ndani ya mioyo yao. Katika kujifunza hili somo nilijikuta nawaza hivi ilikuaje wakati Yakobo analia na kuomboleza wale ndugu wakawa kimya sana, na wakamuacha baba yao akiwa analia siku zote na kukaa hali ya ukiwa? Liliwezekanaje jambo hili! Yaani katika maombolezo makuu namna hii hawa ndugu bado wapo kimya tu! Tazama; Mwanzo 37:34 Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi. 35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia. Maneno kama haya, waliyashuhudia: "Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia." Katika kumtuliza baba yao nao hao waliomuuza walikwepo. Huo mstari anaposema binti na wana, uwe na hakika Biblia ya Kingereza imetumia neno "sons" ikiwakisha wana wa kiume. Nao wanahusika katika kumtuliza, angali ndio waliomuuza; Mwanzo 37:35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia. And all his sons and all his daughters rose up to comfort him; but he refused to be comforted; and he said, For I will go down into the grave unto my son mourning. Thus his father wept for him. (Neno wote limetumika.) Nalijiuliza sana huu ujasiri ulitoka wapi; Mwanzo 37:32 Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. 33 Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa. Baada ya kufikiri sana mahali huo ujasiri ulipotoka, ndipo nilipokuja kutambua ya kwamba, chuki ina nguvu kama mauti. Kwa maana kwamba, waliposema tumue, alikuwa ameshakufa kwanza kwenye mioyo yao. Wanasaikolojia wanasema hivi; kabla mtu hajamua mtu, anaanza kuiuwa dhamiri yake kwanza, ndipo auwe mtu. (Kifo cha kukusudia.) Yusufu ni kweli alishakufa kwenye mioyo yao. Hapa ilikuwa ni madhiirisho tu! Tazama; Mwanzo 37:20 Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake. Ndio maana waliweza kumuuza na wakamsahau kabisa. Haya ni majibu ya swali nililokuwa najiuliza, ya kwamba ilikuaje wakamuuza sawa; ila wakaweza kumsahau kabisa kwa muda wa miaka 27? Na "actually" walishamsahau kabisa, kabisa. Maana kama asingalisimama mbele yao wakati wamekimbilia Misri, bado kumbukumbu lake lisingali kwepo. Kumuuza ni sawa, labla ni matokeo ya kughafilika tu; lakini kumsahau kabisa, kabisa! Hili sii jambo dogo hata kidogo. Tena ndugu wa damu! Nilikuwa nawaza mimi binafsi ya kwamba hawa watu ni kweli wamenifukuza kazi, tena bila kunisikiliza au kupewa nafasi ya kujibu mashitaka yao...lakini wanawezaje kunisahau namna hii! Sizioni hata fadhili za kanisa, ni kama vile sikuwahi kusimama mbele yao kabisa kabisa. Ndipo Roho Mtakatifu akanisemesha kwa ndani; chuki ina nguvu kama mauti. Kwenye moyo wao ulishakufa. Haiwezekani kumsahau Yusufu kana kwamba kweli kafa, kumbe angali hai. Ukiona hivyo, ndani yao ni kweli amekufa. Nilijifunza pia chuki ina tabia ya kukua na kuambukizwa. Sasa eneo la kuambukizwa sitalisemea, maana kuna wengine wanashiriki kukuchukia angali hukuwahi kuwakosea lolote. Nataka kukugusia eneo la kukua. Hapo awali walikuwa wanamchukia kwa kiwango fulani, lakini hapa; chuki ilizidi kukua. Maana chuki inayolandana na mauti, ni chuki yenye kiwango kikubwa kabisa. Na kwangu tukio la kuoa, lilikuza chuki kwa kiwango kikubwa sana. Usiniulize kwa nini? Kwa Yusufu ni hili hapa; Mwanzo 37:5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia. Hiyo ndoto ilileta chuki, hapana shaka kabisa ilikwepo ikaongezeka. Lakini mstari ujao linaongezeka neno na maneno yake. Ina maana wazi kabisa Yusufu kwa kuwa alikuwa na ujuzi wa kutafsiri ndoto, aliwapa na tafsiri yake. Kitu kilichokuza chuki zaidi, na zaidi. Mwanzo 37:8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Ndoto ya pili iliongeza au ilikuza tena kiwango cha chuki; Mwanzo 37:11 Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili. Watu wengi hawajui ya kuwa azimio na kikao rasmi cha kumua Yesu kilizaliwa au kuja mara baada ya muujiza wa kufufuka kwa Lazaro. Ni kweli awali walikuwa wakimuwinda, ila hapa ndipo chuki ilipokuwa na kufikia ukomo. Hatua isiyovumilika kabisa kabisa. Sifa ya chuki iliyofikia hatua hii, ni mtu kuwa radhi kufanya lolote ili tu akuangamize. Hatajali hatima yako, maana mauti ina tabia za namna hiyo. Tazama; Yohana 11:45 Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini. 46 Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu. 48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu. 49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; 50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. Chuki kwa Daudi ilikwepo, lakini ilikua zaidi kutoka kwa Sauli mfalme, kwa sababu ya tukio hili; 1 Samweli 18:6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. 7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. 8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? 9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. 10 Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake. 11 Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili. Shetani ana tabia ya kupanda chuki ndani ya moyo wa mtu pole-pole, anajua anachokifanya. Kuna siku anafahamu itakuwa, na kisha kubeba mimba, itazaa mwana tu. Kiufupi ni kwamba, chuki ina tabia ya kupasuka kama nyongo. Nimepita mikononi mwa wachunguji na viongozi kadhaa. Mkuu wangu akinichukia huwa na mpa muda tu. Najua asipotumbua hilo jipu na kukamua mapema; litakuja kupasuka tu. Ndio maana nimekuwa nikiishi kama mgeni katika mazingira ya namna hii. Hili ni jambo nililojifunza tangu awali. Kuwa makini sana na mtu anayekuchukia. Huwa nasema hivi, kuna watu wakikosa uchafu chumbani kwako; wanaenda kwenye "dustbin" au chombo cha takataka cha hapo ndani ama nje na kupekua. Wakikosa na hapo huwa wanaenda jalalani, kisha wanachukua uchafu na kuja kuumwaga sebleni kwako. Wanapiga picha na kusema ushahidi huu hapa tunao kumuhusu huyu mtu. Epuka sana watu wanaokaa kikao cha kuuwa, kisha ndipo wanatafuta makosa yako. Sio kosa linawasukuma kukuuwa, bali ni chuki. Kisha hiyo chuki inahalalishwa kwa makosa waliojiokotea. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu. Yaani, unahukumiwa kabla hata ya kukutwa na kosa. Na ndivyo viongozi wetu wengi wa kidini walivyo. Lakini ashukuriwe Mungu ambaye hatuachi tuwe mateka wa adui zetu. Wanandaa mauti, lakini Bwana anaigeuza na kuwa ushindi. Ingawaje ni kweli majira haya yanaumiza sana. Ila ndio njia ambayo mashujaa wengi hupita. Nimejikuta nikimuomba Mungu awaondoe moyoni mwangu kama walivyoniondoa wao. Anipe kuwasahau kama walivyo nisahau. Wafe kwenye nafsi yangu, kama nilivyotangulia kufa ndani yao. Maana nikifikiria jinsi nilivyojitoa, moyo unaumia kama ule wa Daudi katika Zaburi. Maana sio jambo la kawaida hata wazee wa kanisa kwa umoja wao waseme tumjuliye hali mchungaji, jamani hata mashemasi nao! Mshirika mmoja akaniambia baba, nimeambiwa eti hapa ndio utamaduni wetu ya kwamba mchungaji akishaondoka ndo ameondoka, hairuhusiwi hata kumpigia simu! Ninachojua ni kwamba chuki imewaambukiza lakini kila penye chuki kuna sheria. Ukishangaa sheria kwenye chuki nenda katika Danieli, mashujaa watatu na Danieli wenyewe ilibidi ipitishwe sheria ili kuwatia hatiani. Lakini sheria ya kulinda chuki utaikuta kwa Mafarisayo, walishatangaza kuwatenga watu na sinagogi kama watamkiri Yesu kama Masihi na kadhalika. Na kweli hata sasa watu huwa katika kundi fulani kama wataambana na mtu ambaye mkuu kwa hila zake mwenyewe kaamua kumchukia. Sauli alipomchukia Daudi, alisababisha ufa mkubwa. Kukawa na kundi la Daudi na la Sauli. Watu walilazimika kujipendekeza kwa mfalme ili kulinda ugali wao. Kuna sheria za "wananzengo" (kwa kanda ya ziwa ni wana jamii wa mtaa mmoja,) ya kwamba mtu akitengwa na "nzengo" alafu wewe ukashirikiana naye, au ukaenda kwake; na wewe unatengwa. Hii ni tabia ya roho ya chuki. Ikusaidie kukujibu mbona hadi fulani na fulani nao wamenichukia! Nimemuomba Mungu pia ya kwamba, nafsi yangu iweze kutambua ya kuwa Bwana ameshanitenga nao. Hii itanisaidia kuniondolea maumivu na kutokuwatazama tena moyoni mwangu. Hakiki hapa kuhusu nguvu ya chuki kimauti: nikuonye tena; kuwa makini na mtu anayekuchukia; 1 Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake
Kati ya jambo la ajabu sana nililojifunza na ningependa ulifahamu; ni hili la nguvu ya chuki. Ni hakika chuki ina nguvu sawa na roho ya mauti. Lakini pia chuki hutenda kazi kama ilivyo roho ya mauti. Sio jambo jepesi kulielewa kama halijawahi kukuta ama kama hujawahi kujifunza somo hili kwa sura ya namna hii.
Na Mwl Oscar Samba
Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu Chetu cha IMANI INAPOJARIBIWA; Karibu...
Walipomchukia Yusufu na kumuuza; ni wazi alishakufa ndani ya mioyo yao. Katika kujifunza hili somo nilijikuta nawaza hivi ilikuaje wakati Yakobo analia na kuomboleza wale ndugu wakawa kimya sana, na wakamuacha baba yao akiwa analia siku zote na kukaa hali ya ukiwa? Liliwezekanaje jambo hili! Yaani katika maombolezo makuu namna hii hawa ndugu bado wapo kimya tu!
Tazama; Mwanzo 37:34 Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi.
35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.
Maneno kama haya, waliyashuhudia: "Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia." Katika kumtuliza baba yao nao hao waliomuuza walikwepo. Huo mstari anaposema binti na wana, uwe na hakika Biblia ya Kingereza imetumia neno "sons" ikiwakisha wana wa kiume. Nao wanahusika katika kumtuliza, angali ndio waliomuuza; Mwanzo 37:35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia. And all his sons and all his daughters rose up to comfort him; but he refused to be comforted; and he said, For I will go down into the grave unto my son mourning. Thus his father wept for him. (Neno wote limetumika.)
Nalijiuliza sana huu ujasiri ulitoka wapi; Mwanzo 37:32 Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo.
33 Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa.
Baada ya kufikiri sana mahali huo ujasiri ulipotoka, ndipo nilipokuja kutambua ya kwamba, chuki ina nguvu kama mauti. Kwa maana kwamba, waliposema tumue, alikuwa ameshakufa kwanza kwenye mioyo yao. Wanasaikolojia wanasema hivi; kabla mtu hajamua mtu, anaanza kuiuwa dhamiri yake kwanza, ndipo auwe mtu. (Kifo cha kukusudia.) Yusufu ni kweli alishakufa kwenye mioyo yao. Hapa ilikuwa ni madhiirisho tu!
Tazama; Mwanzo 37:20 Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.
Ndio maana waliweza kumuuza na wakamsahau kabisa. Haya ni majibu ya swali nililokuwa najiuliza, ya kwamba ilikuaje wakamuuza sawa; ila wakaweza kumsahau kabisa kwa muda wa miaka 27? Na "actually" walishamsahau kabisa, kabisa. Maana kama asingalisimama mbele yao wakati wamekimbilia Misri, bado kumbukumbu lake lisingali kwepo.
Kumuuza ni sawa, labla ni matokeo ya kughafilika tu; lakini kumsahau kabisa, kabisa! Hili sii jambo dogo hata kidogo. Tena ndugu wa damu! Nilikuwa nawaza mimi binafsi ya kwamba hawa watu ni kweli wamenifukuza kazi, tena bila kunisikiliza au kupewa nafasi ya kujibu mashitaka yao...lakini wanawezaje kunisahau namna hii! Sizioni hata fadhili za kanisa, ni kama vile sikuwahi kusimama mbele yao kabisa kabisa. Ndipo Roho Mtakatifu akanisemesha kwa ndani; chuki ina nguvu kama mauti. Kwenye moyo wao ulishakufa.
Haiwezekani kumsahau Yusufu kana kwamba kweli kafa, kumbe angali hai. Ukiona hivyo, ndani yao ni kweli amekufa.
Nilijifunza pia chuki ina tabia ya kukua na kuambukizwa. Sasa eneo la kuambukizwa sitalisemea, maana kuna wengine wanashiriki kukuchukia angali hukuwahi kuwakosea lolote. Nataka kukugusia eneo la kukua.
Hapo awali walikuwa wanamchukia kwa kiwango fulani, lakini hapa; chuki ilizidi kukua. Maana chuki inayolandana na mauti, ni chuki yenye kiwango kikubwa kabisa. Na kwangu tukio la kuoa, lilikuza chuki kwa kiwango kikubwa sana. Usiniulize kwa nini?
Kwa Yusufu ni hili hapa; Mwanzo 37:5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia.
Hiyo ndoto ilileta chuki, hapana shaka kabisa ilikwepo ikaongezeka. Lakini mstari ujao linaongezeka neno na maneno yake. Ina maana wazi kabisa Yusufu kwa kuwa alikuwa na ujuzi wa kutafsiri ndoto, aliwapa na tafsiri yake. Kitu kilichokuza chuki zaidi, na zaidi.
Mwanzo 37:8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.
Ndoto ya pili iliongeza au ilikuza tena kiwango cha chuki; Mwanzo 37:11 Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.
Watu wengi hawajui ya kuwa azimio na kikao rasmi cha kumua Yesu kilizaliwa au kuja mara baada ya muujiza wa kufufuka kwa Lazaro. Ni kweli awali walikuwa wakimuwinda, ila hapa ndipo chuki ilipokuwa na kufikia ukomo. Hatua isiyovumilika kabisa kabisa. Sifa ya chuki iliyofikia hatua hii, ni mtu kuwa radhi kufanya lolote ili tu akuangamize. Hatajali hatima yako, maana mauti ina tabia za namna hiyo.
Tazama; Yohana 11:45 Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini. 46 Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu.
48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu.
49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; 50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima.
Chuki kwa Daudi ilikwepo, lakini ilikua zaidi kutoka kwa Sauli mfalme, kwa sababu ya tukio hili; 1 Samweli 18:6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda.
7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.
8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme?
9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.
10 Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri ndani ya nyumba. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake.
11 Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili.
Shetani ana tabia ya kupanda chuki ndani ya moyo wa mtu pole-pole, anajua anachokifanya. Kuna siku anafahamu itakuwa, na kisha kubeba mimba, itazaa mwana tu. Kiufupi ni kwamba, chuki ina tabia ya kupasuka kama nyongo.
Nimepita mikononi mwa wachunguji na viongozi kadhaa. Mkuu wangu akinichukia huwa na mpa muda tu. Najua asipotumbua hilo jipu na kukamua mapema; litakuja kupasuka tu. Ndio maana nimekuwa nikiishi kama mgeni katika mazingira ya namna hii. Hili ni jambo nililojifunza tangu awali.
Kuwa makini sana na mtu anayekuchukia. Huwa nasema hivi, kuna watu wakikosa uchafu chumbani kwako; wanaenda kwenye "dustbin" au chombo cha takataka cha hapo ndani ama nje na kupekua. Wakikosa na hapo huwa wanaenda jalalani, kisha wanachukua uchafu na kuja kuumwaga sebleni kwako. Wanapiga picha na kusema ushahidi huu hapa tunao kumuhusu huyu mtu.
Epuka sana watu wanaokaa kikao cha kuuwa, kisha ndipo wanatafuta makosa yako. Sio kosa linawasukuma kukuuwa, bali ni chuki. Kisha hiyo chuki inahalalishwa kwa makosa waliojiokotea. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu. Yaani, unahukumiwa kabla hata ya kukutwa na kosa. Na ndivyo viongozi wetu wengi wa kidini walivyo. Lakini ashukuriwe Mungu ambaye hatuachi tuwe mateka wa adui zetu.
Wanandaa mauti, lakini Bwana anaigeuza na kuwa ushindi. Ingawaje ni kweli majira haya yanaumiza sana. Ila ndio njia ambayo mashujaa wengi hupita. Nimejikuta nikimuomba Mungu awaondoe moyoni mwangu kama walivyoniondoa wao. Anipe kuwasahau kama walivyo nisahau. Wafe kwenye nafsi yangu, kama nilivyotangulia kufa ndani yao. Maana nikifikiria jinsi nilivyojitoa, moyo unaumia kama ule wa Daudi katika Zaburi. Maana sio jambo la kawaida hata wazee wa kanisa kwa umoja wao waseme tumjuliye hali mchungaji, jamani hata mashemasi nao! Mshirika mmoja akaniambia baba, nimeambiwa eti hapa ndio utamaduni wetu ya kwamba mchungaji akishaondoka ndo ameondoka, hairuhusiwi hata kumpigia simu! Ninachojua ni kwamba chuki imewaambukiza lakini kila penye chuki kuna sheria.
Ukishangaa sheria kwenye chuki nenda katika Danieli, mashujaa watatu na Danieli wenyewe ilibidi ipitishwe sheria ili kuwatia hatiani. Lakini sheria ya kulinda chuki utaikuta kwa Mafarisayo, walishatangaza kuwatenga watu na sinagogi kama watamkiri Yesu kama Masihi na kadhalika. Na kweli hata sasa watu huwa katika kundi fulani kama wataambana na mtu ambaye mkuu kwa hila zake mwenyewe kaamua kumchukia.
Sauli alipomchukia Daudi, alisababisha ufa mkubwa. Kukawa na kundi la Daudi na la Sauli. Watu walilazimika kujipendekeza kwa mfalme ili kulinda ugali wao.
Kuna sheria za "wananzengo" (kwa kanda ya ziwa ni wana jamii wa mtaa mmoja,) ya kwamba mtu akitengwa na "nzengo" alafu wewe ukashirikiana naye, au ukaenda kwake; na wewe unatengwa. Hii ni tabia ya roho ya chuki. Ikusaidie kukujibu mbona hadi fulani na fulani nao wamenichukia! Nimemuomba Mungu pia ya kwamba, nafsi yangu iweze kutambua ya kuwa Bwana ameshanitenga nao. Hii itanisaidia kuniondolea maumivu na kutokuwatazama tena moyoni mwangu.
Hakiki hapa kuhusu nguvu ya chuki kimauti: nikuonye tena; kuwa makini na mtu anayekuchukia; 1 Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni