Jumatano, 6 Mei 2026
KUUJENGA UKUTA KUNA GHARAMA na Shujaa Hushinda Vita
Nehemia alighamua nia ya yule nabii mke na mwovu na alichonuia kukifanya. Alitaka kumjengea hofu kwa kupitia aina fulani ya maneno ili aweze kumuondoa katika kusudi.
Adui Shetani alipoona wakina Tobia na Sanbalati wameshindwa kuzuia ukuta kwa njia mbalimbali, aliamua moja kwa moja kutumia njia hii. Lazima ujifunze hatari ya maneno unapokuwa unavikabili vita. Yawe yanatoka kwa adui au mtu mwingine. Na yakitoka kwako huwa mabaya zaidi. Maana Shetani atakufanya kama kiwanda cha kuzalisha hofu itokayo ndani mwako. Mawazo ya kushindwa yatakutawala nawe utazungukwa na kushindwa muda wote.
Tazama; Nehemia 6:11 Nami nikasema, Je! Mtu kama mimi nikimbie? Naye ni nani, akiwa kama nilivyo mimi, atakayeingia hekaluni ili kuponya maisha yake? Sitaingia.
12 Nikatambua, na tazama, siye Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; nao Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri.
:13 Kwa sababu hii aliajiriwa, ili mimi niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo habari mbaya, ili wanishutumie.
14 Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, Tobia na Sanbalati sawasawa na hayo matendo yao, na yule nabii mke Noadia, na hao manabii waliosalia, waliotaka kuniogofya.
15 Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili.
16 Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo makafiri wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu.
Alitumwa mjumbe, mwenye ujumbe! Sii kila maneno unapaswa kukubaliana nayo. Shujaa huwa makini sana anapokuwa vitani. Sii kila mwanajeshi aliyevaa nguo na zenye nembo kama yako unapaswa kumuamini! Wengine wameajiriwa na wakina Sanbalati ili wakuogofye. Nia yao ni kukutia hofu. Wanajifanya wana mpango mzuri wa kukusaidia, kumbe ni baada ya wao (kama Sanbalati) kukwama katika kukuzuilia kuujenga ukuta.
Watakupa maneno mengi ya kwamba huyu ana misimamo mingi sana; ni mtu wa misimamo mikali...wewe usijali. Mimi huwa nasema ya kwamba asiye na misimamo ni maiti pekee. Lakini baadae nafikiria nakusema hata maiti ina misimamo maana imeshachagua upande wa kufa. Na uzima sio sehemu yake tena. Ukiumaliza ukuta ndipo watakapokuja kukuelewa. Usilazimishe kueleweka mapema na kila mtu.
Unajua, anayeona unakoelekea ni wewe mwenyewe; kwa hiyo epuka kuwalazimisha wasiona waone kama wewe. Kama kila mtu atafanikiwa kuona kama unavyoona wewe basi hayo sio maono tena. Maono sifa yake moja wapo ni aidha mtu mmoja ama watu wachache kuona kwa niaba ya wengine.
Na usikubali wasiona wakalie nafasi ya maamuzi yako. Wengine ni kweli uko nao ila ni wakina Tobia na Sanbalati, hili lazima ulielewe daima. Ukiona mtu unakataa ushauri wake na anakukasirikia au anakuwa mkali kama pilipili; uwe na hakika haukuwa ushauri bali yalikuwa ni maamuzi au maelekezo aliyokuwa anakupatia. Na inapendeza sana kama ukifanikiwa kujua roho iliyo ndani yake kama Nehemia dhidi ya Noadia nabii mke. Maana kama ingelikuwa ni ushauri kusingekuwa na haja ya yeye kukasirika. (Kuna watu fulani waliwahi kunifanyia fitina, moyoni mwangu nikajisemea wanafikiri mimi ni dhaifu kiasi hicho. Ningekuwa dhaifu nisingefika hapa). Nehemia asingekaza katika kusudi ukuta usingejengwa.
Utakutana na Ujumbe Huu Katika Kitabu Chetu Kipya cha KUJARIBIWA KWA IMANI
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni