#AINA ZA #UPAKO
1. Upako Unaotokana na Mahali Unapopitia
2. Upako Unaotokana na Maombi
3. Upako Unaotokana na Neema au Karama. Au Unao ambatana na Wito ama Mafuta. (Ingawa kuna ambaye ana Mafuta ya Wito 'kila aliyeitwa hupewa.' Na kuna yule mwenye mafua hayo pamoja na neema ya ziada ambapo huitwa Karama.
4. Upako Unaotokana na Utii wako kwa Mungu katika Maelekezo aliyokupatia. Mfano aina ya ujumbe, kibali cha kuhudumu eneo au mahali husika na kadhalika. (Mapenzi Makamilifu ya Mungu.)
5. Upako Unaotokana na Kuombewa, au Kubandikwa Mikono na Muhubiri au mtumishi fulani. Paulo anamueleza Timotheo ya kwamba kuna aina ya mafuta aliyapata kwa kuwekewa mikono na wazee. (Uwe makini sio kila mzee amebeba roho sahihi.)
Aina Nyingine
6.Tukio Maalumu la Kutembelewa na Nguvu za Mungu Katika Ibada.
7. Uwezo wa Kufuata Maelekezo Maalumu Yanayokuja Saa hiyo hiyo Unapokuwa Madhabahuni.
Huambatana na matumizi ya karama nyingine kama za neno la maarifa, unabii, kupambanua roho na kadhalika.8. Upako Unaotokana na Neno la Mungu Lenye Uzima. (Waliokuwa wanashangaa mafundisho ya Yesu ya kuwa alikuwa akifundisha tofauti na waandishi wao; kuna kitu cha namna hii walikutana nacho. (Kitabu chetu cha UTUMISHI WENYE MATUNDA MBELE ZA MUNGU; kitakusaidia kulielewa hili zaidi.
9. Upako Unaotokana au Uliopo Ndani ya Mafunuo. Waefeso huutaja kama roho ya mafunuo na hekima. Ni watumishi wachache wanaoijua hii siri.
10. Upako Unaotokana na Imani ya Anayeombewa. Matendo ya Mitume 14:9 Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa.
Utamuelewa Yesu sasa ni kwa nini alikuwa akimjengea mtu imani kwanza ya uponyaji kabla ya kumuombea. Ni ili akutanishe imani yake na ya Yesu. Katika Yohana 11 anahakikisha Matha amejaa imani ya ufufuo ili amfufue kwanza Lazaro.
Hapa watumishi wengi wa ukanda wa Afrika Mashariki tunakwama. Tunaona ni kushuka kiroho kumjengea muhusika imani kwanza. Ndio maana eneo la matendo ya miujiza hatuna matokeo makubwa sana kama wenzetu wa ukanda wa Kati na Afrika ya Magharibi.
Yule mtu aliyemwambia Yesu nisaidie kwa kutokuamini kwangu ni mfano mzuri sana. (Usilazimishe imani yako kama muhubiri au mtumishi pekee ifanye maajabu.
Hatukuumbiwa hili kila wakati. Jifunze kanuni hii na itakusaidia. Mungu aliiweka ili kuhakikisha muhusika naye anakuwa sehemu ya muujiza huo ili kumuondolea kukuabudu. Badala yake awe na msingi wa kuweka imani kwa Yesu.
Wahubiri wengi wa imani potofu hili hawalifanyi. Na wa imani sahihi hili nalo hawalijui. Lakini tazama miujiza mingi ya Yesu utakutana na imani shirikishi. Yaani imani ya Baltomayo kipofu na Yesu. Kitendo cha Yesu kumuuliza wataka nikufanyie nini? Kinatosha kutupa kutambua ya kuwa kuna namna Yesu alihitaji kukutanisha zile imani mbili.
Kwa mujibu wa Waebrania 11:1, imani imebeba dhima ya kuwa na tarajio. Baltomayo kipofu alitarajia kuona. Ndio sababu ya Yesu kumuuliza nikutendee nini? Wengine aliwauliza je, wataka kuwa mzima?
Mama aliyetokwa na damu miaka 12 yule wa Marko 5, Yesu anamwambia ya kuwa, mama imani yako imekuponya na usiwe na msiba wako tena!
Umeona kitu hapo! Sio imani yangu Yesu imekuponya, bali ni imani ya yule mama!
Sasa, mimi na wewe tunataka imani zetu kama waombeaji zitende kazi tu! Hii huwa mara chache-chache sana.
11. Upako Unaotokana na Uwepo wa Mungu Juu/ Katika Kusanyiko la Mahali Pamoja, Dini yaani Dhehebu au Taasisi. Yaweza kuwa pia familia kama kusanyiko la kiibada, kikundi cha maombi, kwaya au timu ya kusifu wa na kuabudu.
Musa akamwambia Mungu, uwepo wako usipoenda pamoja nasi usituchukue mahali hapa. (Kutoka 33:15 Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. And he said unto him, If thy #presence go not with me, carry us not up hence.)
Namna ya Kuutunza....
Sababu Zinazoweza Kuupoteza...
Namna ya Kuurejesha.
Dalili Zitakazokujulisha kuwa Upo au Haupo.
1. Umwagiko wa Nguvu za Roho Mtakatifu katika Kusanyiko Husika. (Zaidi ni Kwenye Kitabu Chake..)
12. Upako Unakaa au Uliopo Katika Eneo, Aridhi, Anga, Nyumba, Chombo cha Usafiri, ama Madhabahu (kama eneo maalumu la kiibada.) Hata ule upako unakaa kwenye vitu kama vitabu, maandiko ama machapisho fulani fulani ya kiroho, mtandaoni: kama kwenye blogu au tovuti na kurasa mbalimbali; huingia katika hili kundi.
Mfano kwa Musa, alipoambiwa avue viatu aridhi ile ni takatifu, kuna namna ilimanisha katika eneo lile, kuna uwepo wa nguvu za Mungu kipekee. (Katika aridhi.)
Unapomsikia mtu anasema anga la mahali hapa ni gumu, kuna namna uwepo wa nguvu za Mungu ni mchache ukilinganisha na ule wa adui. Ama kuna namna adui anamiliki hilo anga, (uwepo wake angani.)
Mfano wa Yakobo, katika Mwanzo 28, analipoona ngazi ikiwa na urefu kutoka aridhini hadi mbinguni, akasema mahali pale Mungu yupo.
Namna ya Kutengeneza Mazingira ya Upako Huu Kukaa Katika Eneo Lako. Iwe la Kiibada au kibiashara na hata Kimakazi.
(Utaikuta Kwenye Kitabu Chake..)
Written by Mwalimu Oscar Samba
+255759859287 Mwanza Tanzania.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni