Jumanne, 30 Mei 2017
NAMNA YA KUJINASUA KWENYE VIFUNGO VYA PEPO MAHABA. Sehemu ya 1.
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
#SHARE
#SAMBAZA Ili kueneza injili hii Zaidi.
Kuna watu
wanasumbuliwa kwa kuota ndoto wakiwa na Wanazini na mapepo Mahaba aidha kwa
muonekano wa watu wanaowajua ama wasio wajua. Pia wapo wanaofanya ukahaba,
Uzizi na hata vitendo vya kinyume na maumbile huku wakiwa hawapendezwi na hali
hiyo na wamejaribu kutafuta msaada bila mafanikio.
Baya zaidi
wapo wanandoa wenye kusumbuliwa na hali kama hiyo na tatizo hili linaiweka ndoa
yao njia panda kwani hufanya ama huleta ugumu hata kwenye tendo la ndoa kwa
mwenzi wake. Usiogope ama usiendele kulia tena kwani Mungu amesikia kilio chako
na leo amenituma kukunasua hapao.
Jumatatu, 29 Mei 2017
WANAFUNZI MLIOKOKA NISIKILIZENI.
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Nina
wasalimu katika jina lenye Uweza na Furaha ya hali ya juu la Bwana wetu Yesu
Kisto, Leo nimeandaa ujumbe mahususi kwa ajili ya wanafunzi waliokoka katika
ngazi zote za Elimu hususani vyuoni ila wazazi walimu, walezi na watumishi pia
ni wahusika wa ujumbe huu ili kutimiza adhima hii.
Kusudi kuu
la ujumbe huu, Ni kuwataka wanafunzi kutokuacha utayari wao wakumtumikia Mungu
pindi waendapo ama wamalizapo vyuo.
Kuna tatizo
kubwa sana linawakumba wanafunzi hawa nalo ni hili, Kabla ya kwenda vyuoni
katika makanisa walipotokea walikuwa ni watumishi wa zuri sana ila baada ya
kwenda wanaacha kumtumikia MUNGU.
Wengine
wanajitaidi pindi wa wapo chuoni ila wakimaliza na kupata kazi huacha kabisa
kufanya utumishi na baya zaidi wengine wana WITO na kusudi la Mungu kuwapeleka
vyuoni ni ili wamtumikiye.
Kama
watafanya utumishi baada ya kuhitimu, wengi ni wakati wanasubiria majibu aidha
ya chuo, vyeti ama yale ya Kazi.
Inamsikitisha
sana Mungu kuona jambo hili linatokea, kwani Utumishi wake haukusudiwi kufanywa
tu na watu ambao hawajafika kiwango hicho cha Elimu bali hata wasomi wana Nafasi
kubwa kwake kwani Paulo Mtume alikuwa Msomi na aliifanya kazi yake kwa umakini na
weledi mkubwa .
Kinachotokea
ni hiki, Wanapokuwapo chuoni uwanapoteza utayari wakumtumikia MUNGU, ambao
huwakilishwa na viatu kwenye ulimwengu wa roho.
Tuone kwenye
kitabu kile cha Wefeso; WAEFESO 6: 15 NA KUFUNGIWA MIGUU UTAYARI TUUPATAO KWA INJILI YA
AMANI.
Na sababu inayopelekea hayo ni kuweka kando Fikra za kutumia elimu yao
ili kuujenga ufalume wa mbinguni badala yake huzijaza nafsi zao na fikra za kufanikiwa
kimwili kwa elimu yao.
Jambo hili maandiko yamelizungumzia kwenye mfano wa Mpanzi na
yanalifananisha na mbegu iliyodondoka kwenye miiba na kusongwa nayo, ambapo
tafsiri yake ni mtu aliyesongwa na shuhuli nyingi na udanganyifu wa mali. Kwenye
shuhuli nyingi ni hizo fikra na udanganyifu wa mali ni huo udanganyifu wa
mafanikio ya kielimu.
Ukiwahitaji kumtumikia MUNGU huwa na kisingizio cha “ubize” ama ratiba
ni nyingi, kumbuka jibu la huo mfano wa Mpanzi linasadifu majibu yao. Tuhakiki
hilo jambo.
Mathayo 13:22 Naye aliyepandwa penye
miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shuhuli za dunia na udanganyifu wa
mali hulisonga hilo neno, likawa halizai.
Rai yangu kwao ni kuwakumbusha jinsi MUNGU alivyowatoa mbali kipindi
ambacho ada ilikuwa ikisumbua walivyomlilia kwa magoti, walipofukuzwa shule kwa
kukosa karo za shule walivyoombolezana kuwaendea watumishi ila wakati huu
imefika hatua ya kuwakwepa na wakipigiwa simu kuhusu changizo za huduma huzima
hata simu ama huona wanasumbuliwa.
Kumbuka ulipokosa msaada YESU
alikupigania, kabla hujasoma ulivyokuwa na nia ya kuifanya kazi ya MUNGU tena
kwa mzigo. Kumbuka siku ile ulipokuwa kwenye taabu kubwa kimaisha ulivyomuaidia
Mungu kama atakutoa hapo kwa kumuwekea nadhiri ya jambo utakalolifanya kwenye
utumishi wake.
Fanya hima sasa kumrejea yeye.
Ni kweli sio kila mtu ameitwa kuwa Mchungaji ama Mwalimu ila wapo walio
waimbaji, wapiga vyombo, wanaodeki kanisani na cha ajabu wanaofanya usafi siku
hizi sio wale wasomi wa chuo tena bali wasomi wameweka Elimu yao mpaka kwa
MUNGU. Paulo alisoma ila alijishusha na Mungu kumuinua.
Mshahara wako utumiye kuifanya kazi yake, masomo ama kazi ikichukuwa
muda mwingi ama kukupa ubize epeleke msalabani kwa maombi na sadaka maalumu
ukimsihi MUNGU akupe hekima ya namna ya kumtumikia pia kukupa muda katika hiyo
shuhuli.
Rudia enzi zile za maombi yako ya kufunga na kuomba, usiombe tu siku
ukiwa na jaribu ama uliyokosa amani. Mungu akutiye nguvu pia #Share ujumbe huu
na uweneze kwa wengine ikiwemo kwenye vikundi vya wanafunzi ili waliokoka
wapone kiroho.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple,
PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Jumapili, 28 Mei 2017
MAJIRA YA FARAO ASIYEMJUA YUSUFU.
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Yapo majira
ya Kuingia, kuishi na hatimaye kutoka Misiri huku ukiyakabili majira mapya ya
Jangwani ama nyika isiyopandwa kitu kwani haina umande, pia yapo majira ya kuingia
ama kuishi Kanani.
Na majira
hayo yote yamegawanyika katika majira kadhaa, na leo ninakujuza kuhusu Majira
ya Farao Asiyemjua Yusufu. Ni kweli wana wa Iziraeli waliingia Misiri na Mungu
alihaidi kuwabariki ama kuwazidisha huko kupitia ahadi ya Ibrahimu; Mwanzo
15:13. Andiko hilo pia lilitaja muda wa kuishi huko ikiwa ni miaka 400.
Na kipindi
cha Mzee Yakobo jambo hili lilitimia pale Mungu alipomtaka kushuka huko Misiri
na ajenda iliyowasukuma ilikuwa ni njaa; Mwanzo
46. Baada ya hapo maisha yalikuwa mazuri mno kwani Kijana wake Yusufu
alipata kibali na kibali hicho kikawa juu ya Iziraeli yote.
Lakini ili
ahadi ya Mungu ya kuwatoa Misiri itimiye ni lazima wapitiye Jangwani, na maisha
ya jangwa ni magumu mno, na Mungu alilazimika kuhakikisha ya kwamba anatengeneza
mazingira yakuwafanya wayaone walau maisha ya jangwani ni bora kuliko ya
utumwani. Kwani lazima wapitiye shule iitwayo jangwa ili kuweza kuishi vyema
katika jiji la raha liitwalo Kanani.
Ndiposa
Mungu akaruhusu majira mazuri mno kiroho ila magumu sana kimwili ya itwayo; “MAJIRA
YA FARAO ASIYEMJUA YUSUFU.” Kwani Mungu alitazama jinsi walivyoyafuraia yale
maisha ya masufuria ya nyama na matango na matikiti ukizingatia walikimbia njaa
kule Kanani.
Tuyadodose
hayo majira kwa mapana zaidi: Kutoka 1:8 Basi akainuka mfalume mpya
kutawala Misiri, asiyemjua Yusufu.
Huyu ndiye
Huyo Farao, Tutizame atakayotenda.
9 Akawaambia watu wake,
“Angalieni watu wa wana wa Iziraeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. 10
Haya! na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, kukitokea vita wao
nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi
hii.” 11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao
wakamjengea Farao miji yakuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.
Mstari wa kumi na mbili unadhibitisha faida
yangu moja wapo ya majira haya kwani unasema ya kwamba; “Lakini kwa kadri ya walivyowatesa
ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa
Iziraeli.” Na wewe kadri
wanavyokutesa ndivyo unavyozidi kuongezeka kiroho na upako unajaa huku mafuta
ya Mungu yakikutiririkia mara dufu huku ukaribu wako na Mungu ukipanuka kila
Uchwao.
Natumai
umeanza kujionea kuhusu ugumu au majira haya, ila sio huo tuu bali tujionee
zaidi.
13 Wamisiri
wakawatumikisha wana wa Iziraeli kwa ukali; 14 wakafanya maisha yao kuwa uchungu
kwa kazi ngumu; kazi za chokaa na
matofali, na kila namna ya kazi za mashamba; kwa kazi zao zote
walizowatumikisha kwa ukali.
Mateso
hayakuishia hapo bali yalizidishwa makali kama ule moto wa mfalume Nebkadreza
kwa wakina Azaria ulivyochochewa mara 7 zaidi, tumulike mstari wa 15.
15 Kisha mfalume wa
Misiri akasema na wazalishaji wa waebrania, … 16 akasema, “Wakati mwazalishapo
wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume,
basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamuke basi na aishi.”
Hakika
hayakuwa majira mepesi kwao lakini Mungu aliyaachia kwa makusudi na hili ndilo
kusudi lake: Alitaka kuwatengenezea msuli wa kuweza kuimili mikikimiki ya
jangwani, pili alilenga kuwafanya watambuwe kuwa hiyo sio nchi yao kwani
hatuwaoni mahali wakiwa na kiu yakurejea kama ilivyokuwa kwa Yusufu ambaye
alitamani kurejea kiasi chakuwataka kutokuacha hata mifupa yake huko.
Tatu,
alilenga kutengeneza hoja itakayowafanya wana wa Iziraeli kuishikilia na
kuisimamia ili kuwa na umoja wakutoka katika nchi hiyo na itamfanya Farao na
taifa lake kutamani ama kutaka kuwaachiilia huku ikikumbwa kwamba wamisiri
walishaonyesha chuki juu yao. Na fahamu kuwa mtu unayempenda kumuachuilia ni
ngumu hata kama ni hatari kwako ila ukisha mchukia waweza muachilia ingawaje
bado unamuitaji.
Nne,
alitafuta namna yakuwatoa ambayo itamfanya akumbuke Agano lake na awatowe
kiagano maana aliwapeleka kiagano.
Katika njia
hii Mungu alifanikiwa mno, Wana wa Iziraeli walilia kwa sauti iliyo kuu katika
majira haya, na kumlilia Mungu. Maombi yaliyomfanya Mungu kutokutulia na
hatimaye kumtuma Musa huku akilikumbuka Agano. Kwa moyo mkunjufu ninakufunulia
maandiko hayo.
Kutoka 6:2-8, 4 Tena nimelidhibitisha agano langu nao,
la kuwapa nchi ya Kanani, nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni. 5 Na zaidi ya hayo
nimesikia kuugua kwao wana wa Iziraeli, ambao wa misiri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.
Musa anatumwa kwa ajili ya ukombozi, Na fahamu
anatumwa katika majira ya FARAO ASIYEMJUA YUSUFU, kwa hiyo Mpendwa mwenzangu
yamkini unapita katika mazingira magumu sana kimaisha na hali hiyo inakupa
kusononeka sana ila fahamu ya kwamba hayo ni majira ya Frao asiyemjua Yusufu na
Mungu amesikia kilio chako ndiposa mimi nikatumwa kama Musa ili kukutangazia
ukombozi wako hivi leo.
Yamkini hapo awali ulikuwa na kibali sana kwa
Mchungaji wako, Shemasi ama kiongozi fulani kanisani na uwenda ikawa ni kwenye
kwaya ila hivi sasa kimetoweka. Ulipendwa na kukubalika mno kazini ila kwa sasa
ni kama umepoteza mvuto.
Mume ama mke alikupenda na kukudhamini, wazazi
na hata wakwe walikuona ni mwenye dhamani ila muda huu wamekunyanyapaa.
Nisikilize, hayo ni majira mapya kwako kwani
ilikuwa hivyo hata kwa wana wa Waebrania kwani kiti ama cheo au nafasi ile ile
ya Farao iliyompa kibali ama kumpongeza Yusufu kipindi kile ndiyo iliyokuja
kugeuka na kuwa adui ama sehemu ya utumwa kwa wanae na nduguze.
Tazama Farao aliyemjua namna alivyomkubali na kumpa
Heshima hii sanjari na sifa kemukemu ama kedekede;
Mwanzo 41:38 Farao akawaambia watumwa wake, “Tupate
wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?” 41 Farao akamwambia
Yusufu, “Tazama, nimekuweka juu ya nchi
yote ya Misiri.” 42 Farao akavua pete
yake ya mhuri mkononi
mwake, akaitiya mikononi mwa
Yusufu; akamvika mavazi ya
kitani kizuri, na kumtia mkufu wa dhahabu
shingoni mwake.
Yamkini na
wewe hapo awali walikuona hivyo, kwani walisema; “Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake”
Ila kibao kwa sasa kimegeuka na kuwa hivi:
“Haya!
na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka” ama “Wamisiri wakawatumikisha wana wa
Iziraeli kwa ukali.” Walikuona mtumishi mzuri tena mwenye heshima,
muimbaji bora, kijana mcha Mungu. Walikushirikisha kila jambo kipindi cha
majira ya Farao aliyekujua ila majira yamebadilika.
Wewe mtazame
Yesu kwani kubadilika kwa majira hayo ni kwa ajili ya kukutoa katika nchi ya
utumwa, na ninakuhakikishia ya kwamba muda wa ukombozi wako umekaribia. Wewe
mliliye Mungu na punde mambo yako yatakaa sawa kwani ninakwambia hili kama Musa
aliyekwisha kukutana na Mungu pale
kijiti kilipokuwa kikiwaka moto na ujumbe wangu ni huu.
“Kwa sasa
lia mbele za Mungu ili alikumbuke agano lake ulilofunga na Ibrahimu kwani wewe
ni sehemu ya hilo agano tangu pale ulipoamua kuokoka. (Mwanzo 15:16 Siku ile Bwana akafanya agano na Abrahamu, akasema, “Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misiri mpaka huo mto mkubwa,
mto Frati.”)
Pili
hakikisha haupambani na huyo Farao bali wewe muachiliye kwa Bwana naye
atashuhulika naye kwa maana yapo mapigo kumi kwa ajili yake na wewe bahari ya
Shamu itafunguka kwa ajili yako.”
Hongera kwa
kuwa pamoja na mimi na ni yangu imani ya kwamba wakati wako wakutoka hapo
utumwani umefika na hautatoka kwa kutoroka bali mpaka umempata Musa wako maana
ukifika Masa yeye ndiye atakayeupiga mwamba wa Horebu ili ukupatiye maji na pale
Shamu fimbo yake ndiyo itakayo ugawa mwamba. Ukimpata Musa basi na Yoshua unaye
maana ndiye atakayekurithisa Kanani yako.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com #UkomboziGosple #MwalimuOscarSamba
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka,
zaidi. Ug Ukombozi Gosple, PAGE:
https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple
Jumamosi, 27 Mei 2017
BONDE LA KUKATA MANENO.
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Kwa furaha
isiyo na kifani wala uzani ninakukaribisha ndugu yangu katika Bwana wetu Kristo
kwenye safu hii ya makala za kiroho zenye dhima ya kukuinua kiroho, langu jina
ni Mwalimu Oscar mwana wa Flora Samba kipenzi cha Mzee Prospa.
Katika
makala hii sehemu ya kwanza nitakujuza athari ya maneno huku sehemu ya pili
nikikupa mbinu za kupambambana na silaha hii ya maneno yenye nguvu kuliko
bunduki ama mabomu yatengenezwayo na wanadamu.
Awali ya
kukuletea uhodo huo natamani nikujuze maana ya bonde la kukata maneno. Huu ni
ufunuo nilioupata na unamaanisha ya kwamba mtu yupo kwenye mazingira magumu ya
kiroho kivita huku hali hiyo ikiwa ni matokeo ya maneno mabaya anayosemwanayo
kutoka kwa watesi wake na nguvu ya vita hivyo ni ukaribu wa watu hao aidha
kimwili au kiroho.
Ijumaa, 26 Mei 2017
NYAMAZENI NI VUKE.
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Ayubu 13:13a Nyamazeni, niacheni, ili nipate kunena.) Hayo ni maneno ya
Shujaa Ayubu aliyoyanena mbele ya adui zake. Na wewe leo ujumbe huu ni wa kwako
kwani ninakutaka kutokutishwa ama kubabaishwa na maneno au mtazamo mbovu wa
adui dhidi yako bali wewe mtazame Yesu aliyebingwa wakuwafunga vinywa kwa
Utukufu atakao kutendea.
Adui zako walinena
kila lilobaya vinywani mwao, huku wakimtuhumu ya kwamba ametenda dhambi.Ndio
maana mabaya yanampata, tutizame sehemu ya maneno ya Elifazi.
Ayubu 4: 7 “Kumbuka, tafadhali:
ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali
wapi? 8Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, na kupanda mathara, huvuna yayo
hayo. 9 Kwa pumzi ya Mungu huangamia, na kwa kuvuma kwa hasira yake humalizika.
”
Ona tena kebei hii
katika mstari wa 11; “Simba mzee
huangamia kwa kukosa mawindo, nao watoto wa simba mke wametawanyika
mbalimbali.”
NYAMAZA KIMYA MUNGU AKUTETEE.
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Ayubu
akawaambia adui zake; “Laiti mnge nyamaza kabisa, hilo
lingekuwa hekima kwenu.” Ayubu 13:5.
Kumbe Ukimya ni Hekima? Na wewe fanya hima kuipata Hekima hii. Yaamkini
adui zako wamekusonga na maneno kila kona, ukigeuka kulia unasikia, Eti
Umefilisika, Kushoto wanasema; Huna tena Upako, Ukitaka kusonga mbele masikio
yako husikia haya, “Alijiona kapata kumbe kapatikana.” Unafika mahali unataka
kukata tamaa kwa kurudi nyuma, Looh! Kumbe Nyuma nako hakurudiki kwani yapo
manongono haya; “Mwaka huu lazima atembee na viraka.”
Basi unajilazimisha kubaki hapo ulipo, napo hapakaliki kwani kila uchwao
wanakuwinda kwa ndimi zao ili wakumalize, tena cha ajabu ni watu wako wa karibu
na yamkini ni viongozi wako kanisani.
SHINDA VIKWAZO TUKUTANE NG’AMBO YA YORIDANI.
Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry |
Maziwa na
Asali, hayapatikani Misiri wala jangwani hakuna malisho yawezeshayo ng’ombe
kutoa Maziwa ama maua ya mimea ili nyuki wazalishe Asali. Bali ukiyataka
yakupasa Kufika Kanani kwani ndiko kwenye mizabibu na tini na zaituni zenye
maua mazuri ya wezeshayo nyuki kutanda hapo na kisha kufwonza na hatimaye kuunda
Asali.
Maziwa ama
majani yatoayo maziwa hustawi kando ya mito na karibu na chemichemi za maji, na
vitu hivyo hupatika kanani ambapo ndipo paitwapo; “NG’AMBO YA YORIDANI.”
Huku
hawaingi, Waoga, Wasioamini ahadi za Mungu, yaani wasiochanganya ahadi za Mungu
na imani, Wanung’unikaji, kwani hao hufa kwa nyama za kware kuwatokea puani;
Hesabu 11. Ama kwa nyoka wa Moto; Hesabu 21.
Jumanne, 23 Mei 2017
HAYUPO KABURINI AMEFUFUKA.
Mwalimu Oscar Samba |
Tatizo lako
halipo tena kaburini bali limefufuka na Bwana YESU, Wakati watu wakikuona
wanakuona kama mtu aliyepoteza matumaini ama wengine wakikumbuka jinsi
ulivyokuwa mfanikiwa ila kwa sasa maisha ni kama yamekupiga wewe tambua ya
kwamba matatizo hayo ni kweli yalikwepo
ila kwa sasa yamekwisha kufufuka na YESU WALA HAYUPO TENA KABURINI.
Mtazamo wa
wengine usikutishe kwani hadi leo huko Uyaudi zipo dini zinazongonja masiya
wakiamini kuwa hajaja na wapo wachache wanaoamini ya kwamba YESU hakufufuka
kama viongozi wa mafarisayo na wakuu wa makuhani walivyowahonga wale walinzi na
kuwataka kusema ya kwamba watangaze eti wanafunzi wamemuiba na haja fufuka. Hakiki hilo jambo hapa, Matahyo 28:11-15.
Naguswa
kukudokezea walau kidogo, 13 wakisema, “Semeni, ya kwamba wanafunzi
wake walikuja usiku, wakamuiba, sisi tulipokuwa tumelala.” 15….Na neno hilo
likaenea kati ya Wayahudi hadi leo.
USILIYE.
Mwalimu Oscar Samba wa huduma ya Ukombozi Gosple |
Najua
umekuwa na wakati mgumu sana maishani mwako, na umelia vyakutosha, ila sasa
ninakwambia usiliye tena maana Yesu amekusikia na kukuhurumia.
Kitabu kile
cha Luka 7:11-17, Kinaeleza kisa cha
mwanamke mjane aliyefiwa na kijana wake wa pekee, na Yesu alipoukaribia huo mji
wa Naini alimuona na kisha kumuhurumia na hakuishia kumuhurumia tu, bali
alimwambia; “USILIYE.”
Mara baada
ya maneno hayo alitenda mujiza wa kumfufua mwanaye. Bila iyana nakufunulia
maandiko hayo ili ujidhibitishiye mwenyewe.
13 Bwana alipomuona
alimuonea huruma, akamwambia, “Usiliye.” 14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale
waliokuwa wakilichukuwa wakasimama. Akasema, “Kijana nakuamuru: Inuka.” 15 Yule
maiti akainuka, akaketi, akaana kusema. Akampa mama yake.
BELIVE ON YOUR DREAMS, AMINI KATIKA NDOTO ZAKO.
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Ni nani unataka
kuwa, Dakitari, Mwanasiasa, Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Muhubiri fulani
mwenye Upako wa hali ya Juu? Whom one you what to be, a Doctor, A Singer,
Politician or a Preacher. God Never lie. Mungu kamwe hasemi uongo.
AMINI KATIKA
NDOTO ZAKO, Usiruhusu Mtu mwingine yeyote akwambiye kuwa hauwezi, wala mazingira
yasikuaminishe hiyvo. Wewe amini tu ya kwamba inawezekana kuwa unayehitaji kuwa
kesho bila kutazama wewe wa leo. Belive on You are Dreams.
Tumtizame
Yusufu kijana wa Mzee Yakobo, aliamini kuwa ipo siku anachokiona kitageuka uhalisia.
Mwanzo 37:7 Tazama sisi tulikuwa
tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama,
miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.
Hiyo ndiyo iliyokuwa ndoto yake, ambayo ilibeba ukuu katika maisha
yake, na wewe tazama ndoto yako kisha, amini katika hiyo wala sio katika kitu
kinginecho.
YATOSHA.
Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry |
Ila yapo
majira ya mambo hayo kukoma, na ndiposa Yesu pale msalabani akasema IMEKWISHA,
na Mungu akawaambia wana wa Iziraeli wakati wanazunguka ile milima ya Seiri
yakwamba YATOSHA. “Mlivyouzunguka
mlima huu yatosha; geukeni
upande wa kasikazini.” Ni Torati
1:2.
Na wewe
imetosha sasa kuteseka kulala njaa, Nasema imetosha kulialia kwani majira ya
furaha yako yamekwisha kutimia. Kwa waliyokosa watoto kwa muda mrefu ninaachilia
Neno la kinabii kwao ya kwamba majira kama haya mwakani watapakata wana na kama
ilivyokuwa mwisho wa machozi ya Hana kwa kumpata Samweli na kwao itoshe hivyo.
NYUMA YA MLIMA.
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Baraka zako
ama majibu ya maombi yapo nyuma ya mlima
mpendwa kwa hiyo usichoke kuupanda huo mlima kwani ukiumaliza utakutana na majibu yako.
Ninakuhakikishia
ya kwamba PITO hilo ulilonalo ni kama mlima maishani mwako na uhakikisho ni
huu; Ukilimaliza salama utakumbana na majibu ya maombi yako.
Wana wa
Izirali waliizunguka milima ya Seiri siku za kutosha ila mara baada ya kumaliza
kuizunguka nyuma yake walikutana na majibu yao yaliyolenga kuwapitisha salama
na Mungu kufungua ukurasa wa kanuni za kuishi nchi ya ahadi sanjari na
kuwawezesha kuifikia Kanani yao kwa wepesi zaidi.
kumbukumbu la Torati
2:1 “Ndiposa tukageuka, tukashika safari yetu kwenda jangwani kwa njia
ya Bahari ya Shamu, kama alivyoniambia Bwana; tukawa tukiizunguka milima ya Seiri siku nyingi. 2Bwana
akanena akaniambia 3 Mlivyouzunguka mlima huu yatosha;
geukeni upande wa kasikazini.
YESU KAMA MTULIZA MAWIMBI AU DHORUBA.
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Siku moja
wanafunzi wa Yesu walikuwa wakisafiri majini ama ziwani na walilenga kufika
nga’ambo ya ziwa ili kufanya jambo fulani, lakini walipokuwa katika safari yao,
Punde si Punde bahari ili kumbwa na Mawimbi makubwa yaliyoambatana na Upepo
mkali.
Hali hiyo
iliwapa hofu kubwa mno, Lakini katika mazingira yote hayo hawakukubali kukwama
safarini bali walimwamsha Yesu aliyekuwa akipiga usingizi, Hii ina maana kubwa
sana na hapo mbeleni nitaifafanua.
NGAMBO YA YORIDANI, Sehemu 2.
Na Mwalimu Oscar Samba Ug Ministry |
Yesu
akawambia wanafunzi wake, “Natuvuke mapaka ng’ambo ya ziwa”
Luka 8:22. Kisha mbele yake kukatoke dhoruba kali iliyolenga kuwazuia wateule
hawa wa Mungu kulifikia kusudi la Mungu lilopo ng’ambo ya Ziwa.
Mariko 4:37Ikatokea dhoruba
kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye
mwenyewe alikuwapo katika Shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia,
Mwalimu sii kitu kwako kuwa tunaangamia?” 39 Akaamka, akaukeme upepo, akaiambia
bahari, “Nyamaza utuliye!” Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
NGAMBO YA YORIDANI Sehemu ya 1
Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry |
Ni kweli
Maziwa na Asali ni Ahadi ya Mungu maishani mwako, lakini kabla ya kuuvuka mto
Yoridani, nilazima ukutane na bahari ya Shamu, Kisha ugumu wa jangwa.
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake na tuvupe mpaka ng’ambo, lakini kabla ay kuvuka
walikumbana na dhoruba kali baharini, Upepo ambao uliwapa hofu kuu. Petro
alitamani kutembea juu ya maji ili
amfike alipo Yesu. Ila kabla ya kumkaribia wimbi lilifanyika kikwazo
kwake.
Jumatano, 17 Mei 2017
MAREHEMU WALIOGEUKA JESHI KUBWA, (MIFUPA MIKAVU).
Na Mwalimu Oscar Samba Ug Ministry |
Nabii
Ezekieli alionyeshwa bonge lilojaa mifupa ya wafu na aliitabiria mara mifupa
ikageuka na kuwa maremu, kisha marehemu wakapata uhai kwa kufufuka. Na wewe leo
hicho kilichokufa maishani mwako na kusaulika, kitafufuka kwa JINA LA YESU na
kisha kuwa hai tena.
Kama ile
maiti ilivyogusana na mifupa ya Nabii Elisha ndivyo itakavyokuwa kwako leo, kwa
hicho kilicho kufa kugusana na YESU KRISTO MTENDA MIUJIZA. Aliyemfufua Lazaro,
Binti wa mama yule mjane wa mji wa Naini, Kijana aliyekuwa amekufa na Yesu
kusema amelala, kisha watu kumcheka. Ila punde si punde, maiti alifufuka.
Yamkini na wewe unapowambia nitaolewa, wanakucheka sana, kwani umri umesonga,
ama unapowaambia ya kwamba, utasoma, utajenga, utamiliki magari na hata
majumba, hucheka sana. Wewe endelea kumuamini Yesu aliyemfufua huyu mfu sanjari
na mifupa ile mikavu, ikawa mibichi, marehemu na kisha WALIO HAI.
Jumanne, 16 Mei 2017
Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry aandaa Mkutano Mkuwa wa Semina ya Neno la Mungu kwa Morombo Arusha Tanzania.
Mwalimu wa Neno la Mungu Oscar Samba,wa Huduma ya Ug Ministry, anakuletea Semina kubwa ya Mkutano wa Neno la Mungu. Itakayofanyika hapa kwa Morombo Mkoani Arusha kuanzia tare 11-19/6/2017. Walete viwete, vipofu na viziwi pamoja na wagonjwa wote ikiwemo wa UKIMWI na Wakoma. Yesu Mtenda miujiza atakwepo katika Mkutano huo. Watu wote mnakaribishwa.
LAZARO HAJAFA, AMELAA NA WEWE AMINI TU.
Na Mwalimu Oscar Samba Ug Ministry |
Wakati Dada
yake Lazaro anasema, Lazaro amekufa na
ni siku ya nne sasa, na kunuka ananuka, Jemedari YESU anasema, “Lazaro ajafa
bali amelala.” Na kumtaka dada huyu amini tu, ili mujiza utendeke.
Na kwako
wakati wanasema kuwa, ndoa yako, imekufa,Uchumi wako umedidimia, Eti ndoto zako
za kuwa mbunge, kiongozi, msomi ama dakitari na hata zile za kuwa na huduma
kubwa zimekufa, mimi ninakwambia kwa jina la Yesu aliye hai hazijafa bali
zimelala tu, na siku ya leo zitaamka kama Lazaro na kijana walivyo fufuliwa.
Jumatatu, 15 Mei 2017
USITISHWE NA MAZINGIRA, MUNGU AKISEMA AMINI TU.
Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry |
Kuna wakati
ukitazama mazingira uliyonayo na kulinganisha na ahadi ya Mungu maishani mwako,
unapata vitu tofauti ama visivyowezekana. Mungu alimuaidia Ibrahimu na Mkewe
Sara kuwafanya taifa kubwa, cha ajabu aliwapa mtoto mmoja. Kimazingira ilikuwa ngumu kwani
tungalitarajia kupewa watoto wengi.
Isaya 51:2 Mwangaliye Ibrahimu, baba yenu, na Sara aliyewazaa; kwa maana alipokuwa
mmoja tu nalimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.
Mazingira
haya yalikuwa hayasadifu ahadi hii ya Mungu ila Ibrahimu na mkewe waliishika
kwa Imani iliyo kuu kwani licha ya kupewa mtoto mmoja pia walikuwa hawajapata
mtoto huyo hadi kufikia uzeeni ambapo Ibrahimu alimpata Isaka akiwa ni mtu wa
miaka mia na ushee, jambo hili halikuwa dogo kwake maana yeye na mkewe
walicheka wakati ahadi hii inatokea kwa kudhibitishwa.
KWA NINI UJINYONGE, KWA NINI UJIUWE, KWA NINI UKATE TAMAA? WAKATI YESU ANAWEZA.
Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry |
Ipo nguvu ya
ajabu ipatikanayo katika msalaba wa Yesu Kristo iwezayo kukupa majibu ya masumbuko
unayoyahitaji. Na kama msaada upo basi haipaswi kukata tamaa ama kuendelea
kufadhaika bali wewe uhitaji huu msaada ili uwe salama.
Kuna kisa
kimoja kwenye Bibilia nacho ni cha Petro ambaye alitembea juu ya maji, ila
punde mara baada ya kuanza tendo hili la Imani alianza kuzama. Petro hakunyamza,
wala hakufikiria kuzijizamisha kama wengine hivi leo wanavyofikiria kujiua, kwa
kujinyonga ama kunywa sumu. Bali rafiki yangu huyu alimuita Yesu. Na Yesu
alimsaidia.
EPUKA KUYAFANYA HAYA PUNDE UMUONAPO MUNGU YUPO KIMYA.
Kijana mmoja
akasema, “Sitowi tena sadaka maana kila nikitoa ndo kama matatizo yanaongezeka”
Wengine
wameanguka kwenye uzizi na uasherati huku sababu ikiwa ni kumuona Mungu kama
awasikii ama amechelewa kuwaletea majibu yao, aidha ya kuolewa ama mtoto.
Sarai akamwambia Abrahamu/Ibrahimu, “Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae,
umwingiliye mjakazi wangu, labla nitapata uzao kwa yeye.” Abrahamu akaisikiliza
Sauti ya Sarai. Mwanzo 16:2.
Baada ya
hapo kilichofwata ni Ibrahimu kuzaa na kijakazi huyo wa bibi Sarai na hatimaye
kumpata Ishmaeli ambaye
MUNGU ANAPOKUWA KIMYA FANYA YA FWATAYO. Sehe. 2.
Inaumiza
kuwa katika pito gumu na unamtumaini Mungu kisha kumuona Yupo kimya, Ingawaje
wakati mwingine huongea ila hatuelewi ila kiukweli upo wakati anakuwa kimya
kama wakati ule wa Yesu pale msalabani.
Wengine
hujifariji kuwa alinyamza kwa sababu Yesu alikuwa amebeba dhambi na Mungu
hachangamani na wenye dhambi. Hoja hii kwangu ni dhaifu kwani kama aliweza
kuzungumza na Petro katikati ya dhambi yake ya kumkana Yesu kwa ishara ya jogoo
kuwika huku Yesu akimgeuki na kumkumbusha moyoni maneno yale ya kwamba kabla ya
jimbi kuwika atamkana, alishindwaje kunena na mwanaye aliyemtuma kwa kusui
hilo?
Ila katika
yote hayo haipaswi kukata tamaa ama kutafuta njia za mkato kama wengine
wafanyavyo baada ya hali kama hii.
MUNGU ANAPOKUWA KIMYA FANYA YA FWATAYO. Seh. 1
Ila kumbuka
hali hii ilimkuta hata Yesu, “Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?”,
Mathayo 27:46. Kiukweli Mungu
alikuwa Kimya. Hatumuoni akiongea naye wala kumjibu lolote baada ya kukamatwa
kwa Yesu.
Kuna taswra
kuu mbili za Mungu kunyamaza kimya, ya kwanza ni ile ya mtu kutenda dhambi na
Mungu kumuacha, na ya pili ni ile ya mtu kuwa katika hali ya pito huku Mungu
akipima subira yake iliyondani ya Saburi ya Kimungu ama Mungu akimsubiria
achukuwe hatua fulani ndipo amjibu.
YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU KWA MUNGU YANAWEZEKANA.
Mwalimu Oscar Samba |
Uhali gani
mpenwa mwenzangu katika Bwana? Natumai u buheri wa afya.
Leo
nimekuandalia ujumbe mahususi kwa ajili ya kukujuza ukubwa na Uweza wa Yesu
Kristo katika mambo yaliyoonekana ni magumu kama mlima ama bahari katika maisha
yako.
Ni kweli
hitaji ama jambo lilopo mbele yako ni kubwa kuliko wewe na hata mimi mwenyewe
ni kweli siliwezi, ila Yesu tunayemuamini analiweza. Amini tuu kama alivyomwambia
dada yake na Lazaro rafiki yake kuwa anapaswa kuamini tu.
MTAZAME NYOKA WA SHABA.
Ndugu yangu,
wasalamu katika Bwana Yesu Kristo, Ewe unayepita katika mapito magumu
usifadhaike wala kukata tamaa badala yake mtazame Yesu kama Nyoka wa Shaba.
“Kama Musa alivyomuinua yule nyoka wa shaba
jangwani ndivyo Mwana wa Adamu hanabudi kuinuliwa.”
Katika
maandiko matakatifu yaliyopo kwenye kitabu kile cha Hesabu yanaitaja nyoka ya
shaba kama ishara ya ushindi katika nyakati zilizo ngumu kimaisha. Kwani
kipindi hiki wana wa Iziraeli walikuwa wakiumwa na nyoka wa moto ama wenye sumu
kali na walipoteza maisha punde.
Ila Musa
alipata maelekezo kutoka kwa Mungu ya kwamba ainuwe nyoka ya shaba kwa
kuitundika juu ya mti na kila aliyeng’ata na nyoka ya moto alipomtazama nyoka
huyu alipokea uponyaji.
“Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka
juu ya mti: hata ikiwa nyoka amemuuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya sahaba, akaishi”.Hesabu 21:9.
Nami leo hii
ninakuta kutokukata tamaa ama kuacha WOKOVU kwa sababu ya ugumu wa maisha ama
mateso kwenye ndoa, uchumi ama biashara kuwa ngumu, magonjwa, kukataliwa au
vita kwenye ulimwengu wa roho.
Bali inua
macho yako ya Imani na kwa Imani; umtazame Yesu aliyeinuliwa kwenye ulimwengu
wa roho kama yule nyoka wa shaba jwangwani na hakika hapo utapata majibu yako.
Kumbuka
walioshindwa kumtizama yule nyoka wa shaba walipoteza maisha yaani walikufa
hali iliyowafanya washindwe kufika Kanani. Na wewe ukilitazama tatizo lako
utakwama maana ni kubwa kuliko wewe bali mtazame Yesu aliye dawa ya tatizo lako
nawe utashinda, tena na zaidi ya kushinda.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana
nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza
itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com
Jumanne, 9 Mei 2017
Jumatatu, 8 Mei 2017
Jumapili, 7 Mei 2017
Wanafunzi wa Vyuo na Shule, Usimwache Yesu mfikapo vyuoni/Shuleni
Mwalimu Oscar Samba |
Jambo hili ni hatarishi kwao kwani mazingira ya masomo hufananishwa na eneo la kivita kwenye ulimwengu wa roho. Katika maeneo kama haya ndipo hujitokeza wanafunzi waliozoezwa kutumia ushirikina au wenye ujuzi katika mambo hayo. Na wewe ukiyumba kiroho maana yake ni kwamba utashindwa na mambo hayo na kujikuta ukididimia kiroho na kimwili huku maono au ndoto zako zikikwamia njiani.
Pia wachawi na waganga wa kienyeji ama washirikina hupenda kudhuru maeneo hayo kwenye ulimwengu wa roho ili kuiba nyota za wanafunzi, kuwachezea ama kuwatumikisha kichawi na hata kujipatia wajumbe wao hapo.
Ndio maana katika maeneo ya mashule ama yvuo hakuishi vituko vya kishirikina hususani kwenye vyoo na hata mabweni. Ukiwa na Yesu utayashinda haya kirahisi na wewe hawatakuweza.
Na sababu zifwatazo ndizo huwafanya wanafunzi wengi kumuacha Yesu punde wafikapo katika mazingira kama haya;
1. Kufwata mkumbo, wanafunzi wengi hujikuta wakifwata mkumbo kwa kuiga mambo yasiyofaa, ikiwemo vitendo vya ulevi na hata ukahaba. Pamoja na mavazi.
2. Kukosa ujasiri wa kumtaja Yesu ama kuona wokovu kama ni aibu, Nisikilize kwa bidii ili upone, Yesu sio mzigo wala sio aibu kuwa naye bali ni sehemu ya Ushindi. Kumbuka msalaba kwao wapoteao ni upuzi bali kwetu siye ni ushindi, uzima, na nguvu tele maishani mwetu. Usikubali kuona haya kumtangaza Yesu maana anasema atakayemkana mbele ya watu naye atamkana mbele ya Baba.
3. Kuwa na marafiki waovu, siku zote rafiki wa mtu ni mtu, na unapojifanyia marafiki wasiofaa ni kwa uaribifu wa nafsi yako na maisha, na maono yako kwa ujumla. Mithali 18:24a Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa uaribifu wa nafsi yake..
Mithali 22: 24 Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi, wala usiende na mtu wa gadhabu nyingi.
Bibilia inatupa muongoza sahihi wa namna ya kuwa na marafiki kwani ukiwa na rafiki mwizi na wewe utakuwa kama yeye, aliye kahaba ama mwenye tabia ya kuchuna wanaume "Mabuzi" ama mwenye macho ya kutamani mabinti, "Mademu" hakika na wewe utafanana naye.
Katika hili ninakuta kuwa makini sana na marafiki, ingawaje dhumuni langu sio kukunyima kushirikia nao kimasoma, ila shabaha yangu ni kukuondolea ukaribu nao.
4. Kuwa na gelifrend au Boyfrendi, Kitendo hiki cha mwananfunzi kuamua kuwa na mpenzi kabla ya wakati wa kibibilia ama nje ya mpango wa kimungu ni dhambi na jambo hili hufungua mlango kwa Shetani unaomuwezesha kunyonya hali yako ya kiroho polepole na kujikuta ukianza kuwa na Wokovu wa mazoea ama wa kidini na hatimaye kuwa debe tupu litoalo upatu.
Usidanganywe eti huo ni uchumba, hii ni hila ya Shetani kwani uchumba wakibibilia haufanyiki hivyo, na huwa na utaratibu ufwatao , Mchungaji wako ajue, Wazzzi wafahamishwe, kisha mchakato wa mahari ufanyike na utangazwe kanisani.
Kama hayo hayajafanyika ama hakuna rathi hiyo fahamu kuwa mpo mtegoni.
Na huku ni kumkosea Mungu Mpendwa, Wimbo uliobora 3:5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini: msiyachoche mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vyema yenyewe.
Ndugu yangu kiimani ninakutaka kumshika Yesu kwa bidii unapokuwa katika masomo yako na endelea na misingi ya kiroho ili kufanikiwa vyema. Usikubali kuwa mlokole ukienda likizo ila kibaka ama mwizi au mtukanaji ukiwa shueni. Achana na utamaduni wa kumwa mwema mbele ya wazazi ila muovu mbali ya upeo wa macho yako.
Swala la kiroho ni lako wewe na Mungu wako. Wakina Meshaki, Shedraki na Aberinego na Danieli walipofika uamishoni kule Babaeli na kuingizwa katika iamaya ya kifalume huku wakipelekwa darasani ili kuijua lugaha ya wazawa na maarifa ya kifalume kwa shabaha ya utumika kwa mfalume Nebukadreaza hawakumwacha Yesu; Badala yake waliongeza bidii na hatimaye Mungu wao kutukuzwa hapo.
Na wewe hapo ulipo inahitajika Mungu wako atukuzwe na kila mtu amptambuwe huyo uliye naye kama wakina Meshaki na Aberinego, Shedraki na Danieli kipindi kile.
Pia kama hujaokoka fanya hima umpokee huyu Yesu kwani ndiye atakayekuwezesha kuishi maisha mazuri chuoni maana bila Yeye wachawi, walozi na wasoma nyota wanaweza kukuibia mafanikio yako na kujikuta unafukuzwa shule bila sababu za msingi ama kuishilia kwenye vitendo vya ulevi na ukahaba na hatimaye kuvurugikiwa maishani.
Kumbuka kuwa sio kila anayetenda mambo ya ajabu ama maovu vyuoni ama mashuleni amependa bali wengine wamelogwa au kuchezewa kwenye ulimwengu wa roho na watu wenye husuda, wivu na hata wenye nia mbaya. Wapo walioibiwa nyota, na waibao hutupa tabia za ulevi, ukahaba ama mwenendo mbaya pia magonjwa ili mshuhulike na hayo badala ya kugundua wizi huo wa nyota ama huwa kama bumbuzi kwa kutokuja kuwa ameibiwa.
Yesu pekee ndiye awezaye kumuweka huyu mtu salama,
Kama huja Okoka na unataka kuokoa ama ulikuwa umeokoka na ukalega kiroho ama wakati huu upotayari kurejea tafadhali fanya sala hii ya toba.
Sema, Mungu Baba, nipo mbele zako, Nimetambua yakuwa mimi ni mwenye dhambi, Na nipotayari kukufwata, Na ninakuamini na kukupokea kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu, ninakupenda Yesu, nilinde kiroho na kimwili. Ameni .
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la kihoho mahali ulipo ukaabudu, Ameni.
Na Huduma ya Ukombozi Gosple, kwa maombezi ama ushauri na sadaka Ya M-pesa tumia +255 759 859 287.
USIFIYE JANGWANI MPENDWA
Na Mwalimu Oscar Samba |
Ndugu yangu mpendwa katika Bwana ninakutaka kutokukata tamaa
na maisha ya wokovu, kwani haijalishi ni jambo gani unalolipitia, mbele upo
ushindi.
Wana wa Iziraeli walisafiri kutoka nchi ya utumwa ya mateso ya Misiri ili kuelekea nchi ya Maziwa na Asali kama Bwana alivyo waaidia, ila iliwalazimu kupita jangwani. Haikuwa safari nyepesi kutokana na ugumu na manthari ya Jangwa.
Ila wale walioshinda walifanikiwa kuingia Kanani na hatimaye kuyaishi maisha yale ambayo Mungu aliwaaidia. Na wewe yakupasa kushinda.
Wana wa Iziraeli walisafiri kutoka nchi ya utumwa ya mateso ya Misiri ili kuelekea nchi ya Maziwa na Asali kama Bwana alivyo waaidia, ila iliwalazimu kupita jangwani. Haikuwa safari nyepesi kutokana na ugumu na manthari ya Jangwa.
Ila wale walioshinda walifanikiwa kuingia Kanani na hatimaye kuyaishi maisha yale ambayo Mungu aliwaaidia. Na wewe yakupasa kushinda.
Ijumaa, 5 Mei 2017
Wasifu, Mjuwe Mwalimu Oscar Samba.
Mwalimu Oscar Samba |
Pia ni mwandishi wa vitabu vya Neno la Mungu, na kitaaluma ni mwandishi wa habari mwenye elimu ya ngazi ya Diploma/Stashahada na ngazi ya Cheti cha Juu. Amesomea kwenye chuo cha AJTC kilichopo mkoani Arusha.
Ana elimu ya Thielojia ngazi ya cheti aliyoipata kwenye chuo cha kupanda makanisa Makuyuni mkoani Arusha kikiwa ni tawi la chuo cha TAG cha BIBILIA ARUSHA, kwa hivi sasa ni Chuo cha Bibilia Kanda ya Kasikazini.
Pia amehitimu shule ya Msingi Maharo na ya sekondari ngareni zilizopo mkoni Kilimanjaro. Kabila lake ni mchaga wa maeneno ya Rombo. Na Dini yake ni Mlokole.
Baba yake ni Prospa, Mama yake ni Flora. Na Ukoo wake ni Samba. Ni mtoto wa pili katika familia ya Mzee Prospa.
Kuzaliwa ni 6/6/1989,
Anaishi mkoani Arusha na kiasili ni mtu wa mkoani Kilimnjaro.
Pia Kabla ya kuingia kwenye wito wa kitumishi aliwai kufanya Siasa na alikuwa mwanachama wa vyama viwili ambapo chama cha kwanza alikitumikia kwa muda mrefu zaidi na hatimaye kuhamia kingine kutoka na masilai ya kisiasa.
KUTOA MIMBA NI DHAMBI
Na Mwalimu Oscar Samba |
Ninataka kukufahamisha bayana ya kwamba utoaji wa mimba ni mauaji, na kibibilia hakuna muuaji mwenye uzito zaidi ila ukubwa ama kipimo cha kosa hilo la umwagaji damu ni sawa.
Yaani aliyeua mtoto aliyetumboni na aliyeumuua mtu wa miaka kumi ama zaidi wote hukumu yao inalingana.
Kwa kifupi aliyetoa mimba na aliyeshiriki wote ni kundi la wakina kaini.
Ikumbukwe kuwa kibibilia mtoto ama mtu hutambulika toka tumboni, Na hapo Mungu umuhesabu sawa na aliyezaliwa.
Ndio maana akamwambia Yeremia kuwa "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa..." Yeremia 1:5
Yohana mbatizaji alicheza akiwa tumboni mara baada ya mama yake kukutana na mama yake na Yesu. Hii ni ishara kwamba kusudi la Mungu lilidhirishwa ndani yake angali tumboni mwa mamaye, sanjari na hapo kwaYeremia.
Kwa hiyo epuka kushiriki dhambi hii kwa namna ya aina yoyote ile na kama ulishashiriki tubu haraka.
USIKATE TAMAA YESU ANAWEZA
Mwalimu Oscar Samba |
Hivyo ndugu yangu ninakutaka kutokukata tamaa na maisha kwa namna ya aina yoyote ile kwani Yesu anayaweza yote.
Yeye aliyefanya njia kwenye bahari ya Shamu atafanya njia pia katika mapito yako.
Yeye aliyemfufua Lazaro, aweza fufua leo Uchumi wako, Ndoa yako na hata kukurejeshea afya yako.
MAOMBI YANGU KWAKO:
Mungu wangu na akuponye na magonjwa yako yote na kukuondelea mateso yako leo. Amen.
Alhamisi, 4 Mei 2017
Jumatano, 3 Mei 2017
Nukuu iliyopo kwenye Kitabu cha Sadaka Kama Mbegu cha Mwalimu Oscar Samba
"Ni jambo la hatari sana kufikia hatua ya kula Sadaka ambayo Mungu amekupa kama Mbegu na umejua fika kabisa alikupa kuitoa ila kwa sababu una hitaji fulani ukalazimika kuitumia. Nisikilize kwa ukaribu na utulivu: Maana hitaji na uhiitaji wa mwadamu hauishi, na Mungu anapotaka umtolee Sadaka kama Mbegu haimaanishi kuwa haioni shida yako, laa! Asha! Anaiona na amepanga kuitatua kwa kukupa njia ya upandaji.
Hivi kama una uhitaji wa mahindi kilogramu 30 na una mbegu ya mahindi kilo mbili. Itakufaidia nini kula mbegu hizo leo na kubakiwa na uhitaji wa kilogramu 28? Ni ya heri kuzifukia mbegu mchangani kama Yesu alivyosema kwenye Mariko 4:26-29. Na hatimaye kukupatia mavuno yatakayokidhi mahitaji yako.
Masikini wegi ni masikini kwa sababu walikwepa garama za kutoka katika umasikini. Na matajiri wengi ni matajiri kwa sababu walikuwa majasiri wa kuzikabili gharama za kutoka katika umasikini huku wakiwa wanajua faida za kuwa tajiri.
"
Hivi kama una uhitaji wa mahindi kilogramu 30 na una mbegu ya mahindi kilo mbili. Itakufaidia nini kula mbegu hizo leo na kubakiwa na uhitaji wa kilogramu 28? Ni ya heri kuzifukia mbegu mchangani kama Yesu alivyosema kwenye Mariko 4:26-29. Na hatimaye kukupatia mavuno yatakayokidhi mahitaji yako.
Masikini wegi ni masikini kwa sababu walikwepa garama za kutoka katika umasikini. Na matajiri wengi ni matajiri kwa sababu walikuwa majasiri wa kuzikabili gharama za kutoka katika umasikini huku wakiwa wanajua faida za kuwa tajiri.
"
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)