Jumanne, 18 Julai 2017

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 14.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ninakukaribisha ndugu msomaji wangu katika safu  hii ya mafundisho ya Neno la Mungu kupitia makala zetu, leo tunamalizia kulitazama kabila la Yuda.
Mstari unaofwata una mantiki ya aina yake katika hii Nguvu ya Kiagano,
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
Wekundu wa macho unawakilisha Ghadhabu na Mvinyo kulevia, weupe wa meno ni umaridadi wa maneno yake ama hotuba zake. Tukimtazama Yesu alikuwa ni mwenye hekima kinywani mwake na aliyekubalika kwa maneno yake.
Kwa uapnde wa Mvinyo ama kulevia na Ghadhabu wasomaji wa maandiko wanafahamu fika ya kwamba ipo silaha ya ajabu sana ya kupigania vita kwenye ulimwengu wa roho itwayo kikombe cha ghadhabu, kikombe hiki hulevia kisha huaribu na kuangamiza. Mimi binafsi hukitumia sana kikombe hiki ninapokuwa nikipigana vita vya kimaagano na mizimu. Maana hutambua silaha hii ina nguvu ya ziada katika hivyo vita.

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 13.

Na Mwalimu Oscar Sama wa Ug Ministry.
Asante Yesu Kristo kwa majira haya mazuri uliyonikutanisha na msomaji wangu huyu, Leo mpendwa ni sehemu ya kumi na tatu ya makala hii na tunaendelea kuitanzama Nguvu ya Agano kwa kabila la Yuda.
Tutaanze na ule Mstari wa kumi,
10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Nisikilize, Baraka hizi zilinenwa miaka mingi ila zilibeba hatima nzima ya kiutawala na kifalume katika Iziraeli na Ulimwengu mzima.

Fimbo maana yake ni Mamlaka, tuna fahamu kuhusu habari za fimbo ya Haruni na Musa, kwa hiyo swala la Utawala katika Izireli lilikuwa chini ya kabila hili, ndio maana tunamuona Mfalume Daudi, Sulemani, na wengineo ambao walitoka katika hili kabila na kuwa watawala wenye historia kubwa.
Kisha anatajwa  Mwenye Miliki ambaye mataifa watamtii huyu sio mwingine bali ni YESU. Hii ni Nguvu ya Agano ya ajabu sana, ya kwamba usipo ifahamu unaweza ukaona mambo yanatokea kwenye maisha ukadhani yanakuja bahati mbaya ama kwa kubahatisha kumbe tayari mpangilio upo.
Jambo hili halikuishia hapo bali hata Nabii Isaya alilinena katika kulithibitisha kisha likaja jithiirisha katika Agano Jipya.
Ni Isaya 9: 6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 12.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Furaha ya leo iliyopo Moyoni Mwangu ni zaidi ya ile ya Jana, yamkini nimatokeo ya kuvushwa kwako kiroho kwa maudhui ya ujumbe wa jana. Leo ninakuletea matokeo ya baraka kwa makabila kumi na wawili ya Mzee Yakobo na uwenda nikapata kibali cha kudodosa machache ila ninaanza na kabila la Yuda. Tutaona siri ya Yesu kuitwa Simba wa kabila la Yuda ikiwa ni Jina la Kiagano huku wengine wakisalia bila kulijua hilo.

Katika kuwabariki wanaye ambao ndiyo makabila ya Iziraeli Mzee Yakobo aliwatamkia maneno ya baraka yaliyoambatana nao hadi kwenye hatima ya Maisha yao yote.
Tuone, Mwanzo 49: 1 Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.
2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.
 

YUDA: Mwanzo 49: 8 Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.
Jambo hili limekuwa halisi, kwani Mfalume Daudi, Yesu, Mfalume Sulemani, Ni miongoni Mwa watu waliosifiwa sana katika historia ya Bibilia kwani wao wote ni watu wa Yuda.

NGUVU YA AGANO.Sehemu ya 11.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry
Ni Siku nyingine yenye fanaka tele na uzima mwingi rohoni, ni yangu maombi kukutakia uzima huo kwa jina la Yesu kwa wewe ulioukosa, pia udumu ndani yako kwa wewe ulio nao. Ni sehemu ya kumi na moja ya makala yetu ya Nguvu ya Agano ikiwa ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA AGANO KIROHO. Ninacho kibali cha kukuletea kwa njia hii ya mtandao Agano hili moja na uwenda pia nikakudokezea lile la Yoshua lenye mizizi yake kwenye Kitabu cha Torati ya Musa ila maagano mengine kama lile la Sinai, La Chumvi,  Jipya, Daudi na hata lile la Nuhu; Huna budi kuwa na subira hadi kitabu kitoke kisha ukinunuwe.

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 10.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Laiti kungalikuwa na miwani inayoweza kukuonyesha tabasamu nililonalo dhidi yako leo kupitia haya maandishi, ningali kuazima ama kukununulia; Ni fika kila uchwao huwa na furaha kukupakulia chakula hiki cha kiroho ila ya leo ina mapana yake.
Jana nilikupa ahadi ya kukuletea huu ujumbe nami sinabudi kuitimiza hususani katika uzao wa Yusufu. Yusufu ni miongoni mwa wana wa Mzee Yakobo aliyepitia misukosuko mingi na alishinda huku mingi ikiwa na sura ya kiagano, tuliona alivyomiliki malango ya adui zao huko Misiri. Pia kabla ya nduguze  kuhamia ama kushuka Misiri alikuwa amepata watoto wa wili. Manase na Efraimu.

Manase ndiye aliyekuwa wa kwanza na kisha kufwatiwa na Efraimu; Mwanzo 41: 50 Kabla ya kuja miaka ya njaa, Yusufu akazaliwa wana wawili, ambao Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, alimzalia.
51 Yusufu akamwita jina lake yule aliyezaliwa kwanza, Manase, maana alisema, Mungu amenisahaulisha taabu zangu zote, na nyumba yote ya baba yangu.
52 Na wa pili akamwita jina lake Efraimu, maana alisema, Mungu amenipa uzazi katika nchi ya mateso yangu.

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 9.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Asante Yesu kwa juma pili hii njema yenye kuvutia na ya fanaka, na pili ninakuta kimaombi kukaa na msomaji wangu huyu kwa kumsaidia kuelewa somo hili na kulifanyia kazi. Kumbuka ndugu yangu katika Bwana wetu YESU KRISTO leo ni siku ama ni sehemu ya tisa ya makala yetu hii na hapo jana nilianza kukudokezea sehemu muhimu sana ya hili Agao la Ibrahimu na Mungu lililochanua matunda kwa wana wa Iziraeli tukiwemo mimi na wewe.

UG Tv, ASANTE YESU, TUMEFANIKIWA KUFUNGUA OnLine Tv Yetu.

Jumanne, 27 Juni 2017

NGUVU YA AGANO, Sehemu ya 8.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Nami sina shida kwani ni kweli waswahili husema kuwa ahadi ni deni, nami leo sina budi kulipa deni hili, Ndugu yangu katika Kristo kumbuka kuwa leo ni siku ya 8 ya makala yetu hii ya Nguvu ya Agano nami tokea siku kadhaa zilizopita nalikuaidia kukuonyesha kitu muhimu ambacho Ibrahimu alijuzwa na Mungu na hatimaye kuja kutokea kipindi cha Yakobo yaani Iziraeli ikiwa ni Jambo la Kiagano.

Ukisoma kutoka kitabu kile cha Mwanzo sura ile ya kumi na tano utamuona Mungu akimwambia Ibrahimu kuwa uzao wake utaenda kuishi Misiry ama utakuwa mgeni huko na kusudi kubwa la Mungu ni kuwazidisha ama kuwaongeza, na kuwatajirisha huko maana walitabiriwa kutoka na mali nyingi, huku muda wao ukiwa ni miaka 400, muda ulioamariwa na Mungu, ingawaje walikaa mika 430, na sababu za kuongezeka kwa hiyo miaka nimezielezea kwenye kitabu changu cha Namna ya Kuishi Wakati wa Majaribu au Mapito, na pia Mungu akinipa kibali nitaligusia kwenye kitabu kile cha Wito wa Kitumishi ili kukusaidia ujuwe umuhimu wa kumuombea Musa wako ili asichelewe kuitika ama asikimbiliye Midiani badala yakukukomboa kwa wakati.

Tusonge mbele na Agano, Sasa leo tunaona utimiajia wa jambo hilo ila awali ya yote ninawiwa kulidhibitisha jambo hilo ama kuliweka bayana mbele ya macho yako.

Kwa Furaha ya Moyo Fungua nami kitabu kile cha Mwanzo 15: 13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya

NGUVU YA AGANO, Sehemu ya 7.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ni mwingi wa furaha kwa Mungu kutuwezesha tena kukutana siku ya leo maana sio kwa uweza wetu wala fikra zetu bali ni kwa kudra zake Yeye liyemneemeshaji wa Neema na Baraka zote, Ameni.

Leo ni siku ya saba katika mfululizo wa hii makala yetu ya Agano na tunaendelea kumtazama Yakobo na Uzao wake, kwa sasa tumuone Yusufu Mwana wa Mzee Yakobo.
(k) Kupitia Yusufu walimiliki Malango ya Misiri, Natumai unakumbuka kuwa katika hili Agano pale Mwanzo 22 mara baada ya Ibrahimu kufaulu ule mtihani wa kumtoa Isaka sadaka Mungu alimuaidia kummilikisha Malango ya adui zake kupitia Uzao wake.
Tafadahali naomba tuhakiki jambo hilo ilituweze kwenda sawia ama sanjari. Ni Mwanzo 22: 17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

Alhamisi, 22 Juni 2017

NGUVU YA AGANO . Sehemu ya 6.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Sifa na Utukufu ni kwa Bwana wetu Yesu Kristo, nami kwa salamu hizo ninakukaribisha katika safu hii murwa na mubashara ya makala ambapo leo tupo kwenye mfululizo wa 6, wa  somo letu la NGUVU YA AGANO, Ikiwa ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA AGANO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
(i) Liliamua Mustakabali wa Maisha yao kindoa au kimahusiano, Tunafahamu Isaka alichaguliwa mke na babaye, huku naye akimchagulia Yakobo ama akimuelekeza mahali pakwenda kuoa, hii ikiwa na maana kwamba mwana wa Agano haulewi na kila mtu ama haowi kila mahali kiolela.
Alikadhalika jambo hili liliendelea hadi kwa watoto wa Yakobo yaani Iziraeli. Ukisoma katika Kitabu hiki cha Mwanzo sura ile ya 34, utamuona binti Lea aitwaye Dina alivyochukuliwa na mtu wa ile nchi aitwaye Shekemu mwana wa Hamori wa kabila la Hivi ama Muhivi.

NGUVU YA AGANO SEHEMU YA 5.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ninakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo ndugu msomaji wa makala hii ikiwa ni sehemu ya tano, na jana nilikuaidi kuendelea na kipengele kinachoonyesha jinsi Yakobo alivyobarikiwa katika Agano hili.
(h) Kubarikiwa kimali na kurudishwa katika nchi ya Nyumbani, Kumbuka kuwa Yakobo alikuwa akiishi katika nchi isiyo yake ama ya baba zake naye alikuwa kwa Labani ama kwa mjomba ake, ila majira haya Mungu anatumia Agano hili kumtoa huko pamoja na kumpa mali.
Tutayatazama hayo maandiko lakini nataka uyaone kwa sura ya kiagano. Yaana anza kwa Yakobo kuanza mipango ya kuondoka mara baada ya Mungu kumpa kibali na hapo anaongea na wake zake, katika hayo mazungumzo kunatajwa kitu kama mimi ni Mungu wa Betheli, katika mstari wa 13.( 13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.) 

Jumatatu, 19 Juni 2017

RATIBA YA MIKUTANO YETU KUANZIA MWEZI WA 7 MWAKA HUU 2017 NA KUENDELEA

 MWEZI WA 7, TUTAKWEPO ROMBO KWENYE VIWANJA VYA SOKO LA MAMSERA NA MANDA PALE SOKONI KILESI. MWEZI WA 8 AU WA 9 TUTAKWEPO TANGA. NA MWEZI 3 MWAKA 2018 TUTAKWEPO KWENYE VIWANJA VYA RELI HAPA MKOANI ARUSHA. BAADA YA HAPO TUTAELEKEA ZANZIBAR ENEO LA DARAJANI KWENYE KIWANJA KILICHOPO MKABALA NA DARAJANI HOTELI. KUMBUKA MIKUTANO YOTE HIYO NI YA SEMINA YA NENO LA MUNGU. ILA KATKA MWAKA HUU PIA TUTAELEKEA KARATU NA TUTAKUJUZA TAREHE.

Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA.

Na Mwandishi wetu, Ug Ministry.

Hakika kwetu Jehova Jire ni Ebeneza maana sio kwa uweza wetu bali ni kwa nguvu zake ndiposa tunayanena hayo. Jana tulifanikiwa kuhitimisha semina yetu huku nguvu za Mungu zikishuka mahali pale, watu wakifunguliwa na hakika semina ilikuwa ya Baraka maana licha ya watu kunufaika na mafundisho pia wapo waliookoka.

Kama ilivyo ada Mwalimu jana alianza kwa kuwaimiza wakristo kumtafuta Mungu kwanza na haki yake kisha hayo mengine yote wanayoyahitaji kutoka kwake Yeye atawajaza.

Siku ya jana Mwalimu alihitimisha kwa Mbinu ya 9, nayo ni ; Kufahamu athari za kuwa na Mali isiyo na Yesu. Katika hili alisisitiza mathara yanayoweza kujitokeza kwa mtu mwenye mali kisha akamkosa Yesu kwenye Uchumi wake.
Alinza na andiko lile la Ufunuo wa Yohana 3: 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Jumapili, 18 Juni 2017

PICHA ZA SEMINA YA NENO LA MUNGU SIKU YA 8, MOROMBO ARUSHA TANZANIA; Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry, Somo: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA.






Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA.

Mwalimu Oscar Samba
 Na Mwandishi wetu, wa Ug Ministry.

Ninakukaribisha sanjari na kukusalimu kwa jina lake Bwana wetu Yesu Kristo aliye pia Mwokozi wetu.Leo ni siku ya saba ya Semina Yetu na kumbuka somo hili ni la jana kwa hiyo kijografia jumapili ya leo ndiyo tunahitimisha semina hii ikiwa ni siku ya nane na ujumbe wa nane utaupata kesho.

Mwalimu jana alitilia tena msisitizo wa kukutaka kuutafuta kwanza Ufalume wake Yesu Kristo na Haki yake kisha hayo mengine utazidishiwa. Pia jana alifundisha mbinu moja kuu ambayo ilikuwa ni mbinu ya Akili, Hekima na Maarifa. Mwalimu alivifafanua vitu hivyo kwa mapana na kukuhitaji kuhakikisha ya kwamba una vifahamu ili uweze kunufaika na vitu hivyo.

Alitoa mfano wa Mfalume Sulemani aliyeomba hivyo vitu, 1 Wafalume 3:4-15, ila alisoma mstari wa12 na kukutaka mingine kujisomea.
12 basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.

Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Jumamosi, 17 Juni 2017

Picha za Semina ya Neno la Mungu Kutoka Morombo Arusha Tanzania na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry, Somo: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA, 7.

Mwalimu Oscar Samba


Mchungaji Denisi akifungua kwa Maombi.

Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA 6.

Na Mwandishi wetu wa Ug Ministry.
Ninakukaribsha katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yetu katika safu hii ya ujumbe wa Semina ya Neno la Mungu ikiwa ni siku ya sita kama ilivyofundishwa jana na Mwalimu.

Mwalimu alianza kwa msisitizo kwamba ili kufanikiwa Kiroho na kiuchumi ama kufikia mafanikiao ya kutajirika kiuchumi katika Kristo Yesu yatupasa kuutafuta kwanza Ufalume wa Mbinguni na Haki yake na kisha hayo tunayaoyahitaji tutayapata.

Jana alifundisha mbinu moja nayo ilikuwa ni KULIJUA KUSUDI LA MUNGU LA KUKUTAJIRISHA, katika mbinu hii Mwalimu aliwataka walio matajiri kufahamu jambo hili na kuliishi huku akiwafundisha wale wenye nia au kiu ya kutajirika kupitia mfumo wa kimbingu kuhakikisha wanalifahamu na kuliisha kusudi hili ili Mungu awatajirishe na akisha kuwatajirisha wahakikishe wanalitimiza hili kusudi ili mali ama fedha zisiwatowe kwake.

PICHA ZA SEMINA YA NENO LA MUNGU SIKU YA 6, MOROMBO ARUSHA TANZANIA NA MWALIMU OSCAR SAMBA KATIKA SOMO LA MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA 6.

Kushoto ni Mwinjilisti na Mwalimu SixMon akiwa na Mwalimu Oscar Samba katika Mkutano huo wa Semina


Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Ijumaa, 16 Juni 2017

Mwalimu Oscar Samba, MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA, 5.

Mwalimu Oscar Samba akifundisha katika semina
 jana hapa Morombo Arusha Tanzania
Na Mwandishi wetu, Ug Ministry.
Ninakukaribisha katika jina la Yesu Kristo Bwana wetu na Mwokozi wetu katika sehemu hii ya 5 ya ujumbe wetu kama alivyofundisha Mwalimu jana kwenye semina inayofanyika hapa mkoani Arusha kwenye viwanja ya Morombo nchini Tanzania.

Kama ilivyo ada alianza kwa kutoa msisitizo kwa watu kuutafuta kwanza ufalume wa mbinguni na haki yake na kisha hayo mengine ikiwemo ya uchumi ama utumishi watazidishiwa.

Mwalimu wetu alitoa utangulizi uliyolenga kuwakumbusha wanafunzi wake mahali aliponzia tangu siku ya kwanza na kusema ya kwamba alitamani kugusia somo la Agano la Chumvi ili kuwasaidia watumishi wa Mungu maana ni Agano la kitumishi ila kwa jana hakupata kibali ila siku ya mwisho ya semina huenda akakipata na ikumbukwe kuwa hasemi jambo kwa akili zake bali hunena lile ambalo Roho anataka alinene kwa wakati gani na sehemu gani.

Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Alhamisi, 15 Juni 2017

Picha Za SEMINA YA NENO LA MUNGU, MOROMBO ARUSHA TANZANIA SIKU YA 5, NA Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.



Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOOKOKA.

Mwalimu Oscar Samba
 Na Mwandishi wetu, Ug Ministry.

Ninayo furaha murwa kabisa nami bila iyana wala hofu ninakukaribisha katika sehemu ya nne ya ujumbe wa semina yetu mubashara inayoendelea hapa mkoani Arusha nchini Tanzania kwenye viwanja vya sokoni Morombo.

Jana Mwalimu alianza kwa ufafanuzi wa somo ambalo tunaendelea nalo wiki hii yote na katika hilo alichambua kiundani andiko la msingi ama la semina linalotutaka kuutafuta kwanza ufalume wa Mbinguni na haki yake na kisha hayo mengine yote tutazidishiwa. Alisema ni vyema kumtafuta Mungu kwanza kisha katika hapo ndipo tutapata Hekima, Akili na Moyo wa Maarifa; vitu ambavyo vitatusaidia kufanikiwa kiuchumi.

Alitanabaisha kuwa, hakuna mtu anayetaka kuwa dakitari kwa kuanza na kozi ya udakitari ama kushika sindano na kuvaa joho jeupe kisha kuanza kujiita ama kutaka kuitwa dakitari.

Jumatano, 14 Juni 2017

PICHA ZA SEMINA 4, SOMO LA MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA

Mwalimu Oscar Samba





Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA, 3.

Mwalimu Oscar Samba akifundisha  

NA Mwandishi Wetu, Ug Ministry.
Leo ni siku ya tatu ya ujumbe wetu huu Mubashara kama ulivyofundishwa na Mwalimu wetu kwenye Semina ya Mkutano wa Neno la Mungu inayoendelea ikiwa ni siku 8, hapa Mkoani Arusha nchini Tanzania kwenye viwanja vya Morombo.
Jana Mwalimu alianza kwa msisitizo kwenye andiko ambalo Mungu ametupa kutembea nalo kwenye semina hii nzima la kuutafuta kwanza Ufalume wa Mbinguni na Haki yake na kisha hayo mengine yote tutazidishiwa. Ni Mathayo 6:33.
Alisema kuwa inampasa kila mwana wa Nuru kuutafuta kwanza Ufalume wa Mbinguni na haki yake kisha Mungu atamzidishia akirudia mfano wa Mfalume Sulemani wa kumtafuta kwanza Mungu kwa kumuomba Moyo wa Hekima, Akili, Maarifa na kisha Mungu kumpatia hivyo vyote huku akimpa na Fedha. Kwa sababu alitafuta kanuni au mbinu teule ilizomuwezesha kutoka kwenye umasikini.

Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Jumanne, 13 Juni 2017

PICHA ZA SEMINA YA NENO LA MUNGU SIKU YA 3, MOROMBO ARUSHA TANZANIA, 13/6/207 NA Mwalimu Oscar Samba

Mwalimu Oscar Samba akifundisha kwenye Semina ya Neno la Mungu Hapa Mkoani Arusha leo jioni katika viwanja vya Soko la Morombo. Alifundisha ujumbe ulioitwa. MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA.











Mwalimu Oscar Samba, MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA. 2

Na Mwandishi wetu wa Ug Ministry
Nina Kusalimu katika jina la Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha Yetu, ni yangu taraja kuu ya kwamba huu mzima tena buheri wa afya. Ninakukaribisha katika makala hii fupi inayolenga kukujuza mafundisho ya Neno la Mungu yaliyofundishwa jana na Mwalimu Oscar Samba katika viwanja vya skolo la Morombo hapa mkoani Arusha.
Kama alivyoaidi kuanza na pwenti ya kuutafuta kwanza ufalume wa mbinguni na haki yake ndivyo ilivyokuwa jana. Mwalimu aliwataka watu waliokoka kuwekeza nguvu nyingi katika kumtafuta Mungu kwenye nyaja zote na kisha kumuomba maarifa, Moyo wa Akili na wa Hekima katika swala la uchumi na maisha kwa ujumla kama ilivyokuwa kwa Mfalume Sulemani na kisha Mungu kumpatia Utajiri.
Alisema kuwa wapendwa wengi hupenda kuomba fedha lakini hawaombi kufahamu kanuni za kupata fedha, alitoa mfano na kuwafananisha na mtu anayependa kupewa samaki badala ya kupenda kufundishwa namna ya kuvua samaki huku akibainisha kuwa Mungu akimfundisha kuvua basi ni lazima ampatiye na Ndoano.

Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Wtu W...

Picha za Semina ya Neno la Mungu Morombo Arusha Tanzania, Na Mwalimu Oscar Samba, Siku ya Pili

Kushoto ni Mwalimu Oscar Samba na Kulia ni Kulia ni Mchungaji Dani Sangale



Jumatatu, 12 Juni 2017

NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 3.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry
Ninakukaribisha katika sehemu ya 3 ya makala hii inayolenga kukujuza Nguvu iliyopo kwenye maagano ili usomapo maandiko uyasome kiagano ukijua kuwa ni sehemu ya maagano mbali mbali ambayo ni msaada mkubwa kwako kama utajua kuyatumia vyema kwa kunjenga hoja mbele za Mungu na kuzisimamia kimaombi vilivyo.
Jana nilikuaidi kuendelea na kipengele cha Isaka ikiwa ni muendelezo wa Agano ambalo Ibrahimu alifunga na Mungu, na ili kujua tulipoanzi yakupasa kusoma sehemu zilizotangulia yaani ya jana na juzi. Nilimalizia kwa kukufahamisha kuwa kwa Isaka Agano hili lilikuwa na Nguvu kubwa sana kwani wakati wengine wakioa kwa taabu kwake mambo yalikuwa ni MSWANO: Na hivi sasa ninakupa Nguvu ya hili Agano kwake kwa ulingo mpana zaidi.
(e) Lili Mpa Kuridhi Mali ya Babaye,Na kufanyika Lango la Uridhi kiahadi; Ni Agano pekee ndilo lililomuwezesha kuipata au kuupata Uridhi wa mali ya baba yake. Kwani maandiko yanamtaja kama mtu pekee aliyekabidhiwa mali ile huku wengine waliokuwa wana wa Masuria wakipewa zawadi tu.

Ni Mwano 25: 5 Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo.
6 Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu a

NGUVU YA AGANO . Sehemu ya 2.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Kwa furaha na tabasamu mwanana ninachukua muda huu kukukaribisha katika sehemu hii ya pili ya makala yetu ikiwa pia ni masomo yaliyopo kwenye kitabu changu cha NGUVU YA AGANO KIROHO.
Jana tuliishia katika kipengele cha pili cha Agano la Mungu na Ibrahimu lilolenga kumbariki kiuzao, Kiroho na hata kiuchumi. Kipengele cha kwanza tuligusia Baraka za uzao na kusema kuwa Mungu alimpa Isaka japo umri wake ulipita na sababu kubwa ikiwa ni Ahadi iliyokwepo kwenye lile Agano, Na ya Pili ilizungumzia Baraka za kiuchumi ambazo pia tutaziangazia hapo mbeleni zaidi. Sasa tuangaziye ya leo.
(c) Mungu alimjuza kuhusu maswala yajayo, Unapokuwa ni Mtu wa Agano, Mungu hawezi kukaa kimya bila kukujuza maswala muhimu katika hilo Agano. Fungua nami maandkyo yafawatayo:
Ni Mwanzo 15: 13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.

Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Wtu Wali...

Jumapili, 11 Juni 2017

Picha Za Semina ya 1, Kwa Morombo Arusha Tanzania, Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry. Somo:Mbinu Teule zitakazo kuwezesha watu waliokoka kutoka kwenye Umasikini 1

Leo hapa kwa Morombo Mwalimu Oscar Saba ameanza huduma rasimi katika huduma aliyoiasisi ya Ukombozi Gospel ama Ug Kwa Kifupi.

Na utajionea picha mbali mbali za matukio yaliyojiri mahali hapo.

Ujumbe wa leo ama wa Semina hii unatoka kwenye kitabu chake cha Tajirika kibibilia uitwao, "Mbinu Teule zitakazo wawezesha watu waliokoka kutoka kwenye Umasikini"

Mwalimu alianza kwa kusema kuwa watu wengi waliokoka leo wanaishi maisha ya umasikini ikiwa ni matokeo ya wao kutokutambua kuwa zipo kanuni zinazoweza kuwakwamua kutoka kwenye hali hiyo.

Ijumaa, 9 Juni 2017

NGUVU YA AGANO Sehemu ya 1.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Hakika ni jambo la kushangaza kwani siku chache zilizopita nilikuaidi kukuandikia kitabu hiki cha Nguvu ya Agano kama Mungu atanipa kibali na siku ile alinipa, leo amenitaka kuanza kukumegea baadhi ya vitu vilivyomo kwenye hicho kitabu na nilikuaidia kuwa katika kitabu hiki nitazungumzia kiundani aina yote ya maagano ikiwemo yale ya Mungu na yakipepo.

Atukuzuzwe Mungu juu mbinguni na duniani ilipo sehemu ya kuweka miguu yake, leo nitakujuza kiundani kuhusu maagano ama Nguvu iliyopo kwenye maagano ambayo tunaingia na Mungu. Pia jambo hili likupe kiu yakuingi agano ama maagano binafsi na Mungu ili kuwa katika uwakika mkubwa wakutembea na Mungu, kwani kama kuna kitu Mungu hukiheshimu ni Agano.

TUMAINI KWA ALIYEKATALIWA AU KUACHWA.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Haijalishi umeachwa ama kukataliwa kwenye Ndoa, Mwenzako amekuacha ama ni Mchumba amekusaliti, Umekataliwa kazini  na hatimaye kufukuzwa. Ama umekosa kibali mbele ya wapendwa kanisani kwako au viongozi wako wa kiroho wamekukataa na kukutelekeza na imefika hatua ya wewe kujiona kama mtu aliyeachwa.

NISIKILIZE, Leo nimekuletea TUMAINI na TUMAINI hili ni YESU KRISTO aliye Bingwa wakuwakumbatia waliokataliwa na kuachwa. Ni kweli jambo ama mambo hayo yanaumiza na mimi katika uzoefu wangu wa miaka isiyofika Theladhini hapa Duniani kwani umri wanguni ni miaka 28 na siku tatu, nimebaini kwamba kama kuna mambo ambayo huujerui moyo; Kukataliwa ni miongoni mwayo.
 Ukitaka kuamini, jaribu kumwambia mtoto mdogo asiyejua hata kunena ya kwamba unampenda atatabasamu na hata kuachia kicheko, ila punde umamwambiapo kwamba haumpendi, ama unamchukia tabasamu lile hugeuka kuwa simanzi. Ndio maana mtu anapokuwa kwenye tatizo ama uhitaji na kisha kuwaona watu hawaguswi na tatizo lake ni rahisi sana kuumia zaidi.

Ndiposa kwenye misiba wafiwa mara nyingi huzungukwa na watu, huku wakiwafariji na wengine huacha shuhuli zao na kuamua hata kulala kwao ama kujumuika nao kwa muda mrefu. Hiyo yote ni kuwaondolea upweke.
Jambo hili liliwai kumsumbua Mfalume Daudi, Zaburi  69: 20 Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.

MSAADA WA KIROHO KWA WANAOOTA NDOTO WANAKULA VYAKULA, NYAMA, DAMU ,IKIWA NI SEHEMU YA MAAGANO YA KIPEPO. Sehemu ya 2.

 Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Kwa furaha isiyopikama kwa Uzani wala Mizani ninakukaribisha tena katika sehemu hii ya pili na ya mwisho ya makala yetu, na ni rai yangu kama jana hukufanikiwa kusoma sehemu iliyotangulia basi yakupasa kuitafuta ili tuweze kweda sanjari.
NAMNA WATU WANAVYOINGI MAAGANO HAYA YA KIPEPO. Unapokwenda kwa mganga, na mganga kukupa mashariti, ya kufanya fahamu mashariti hayo ni sehemu ya agano la kipepo, kwa bahati mbaya wengine hulazimika kuingia ama kufanya kiapo cha uaminifu ama chakuto kuvunja au kukiuka mashariti hayo. Sio kwa waganga tu bali hata wa lewatu wa Fremason, Ilumineta na kadhalika.
Na agano hilo huwa na nguvu sana pale atakapokuhitaji kumwaga damu, mfano wapo wanaoambiwa walete kuku, mbuzi ama kondoo na hata ng’ombe. Na mganga humchinja. Pale anatafuta kulitia nguvu ama kulikamilisha lile agano. Kumbua Agano jipya maandiko husema kuwa lina nguvu kwa sababu ya mauti ya Yesu. Andiko tulilolisoma hapo juu la Luka tunamuona Yesu anasema  damu hiyo iliyo ndani ya kikombe ni Agano Jipya, ile imwagikayo. Maana yake damu ile ya kuku na mbuzi ama wengine hutoa kafara ndugu zao, kipepo ni agano pia.

MSAADA WA KIROHO KWA WANAOOTA NDOTO WANAKULA VYAKULA, NYAMA, DAMU ,IKIWA NI SEHEMU YA MAAGANO YA KIPEPO. Sehemu ya 1

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Kuna watu wamekuwa wakisumbuliwa na ndoto mbali mbali ikiwemo wanazoota wakiwa wanakula vyakula, baathi yavyo ikiwa ni nyama, na mbaya zaidi hula nyama za watu, wengine ni damu na nyingine ni damu za watu.

Na baada ya ndoto hizo hujikuta wakiwa na hali mbaya sana kiroho, huku nafsi zao zikigubikwa na huzuni, mafadhaiko yasiyo na uvumilivu, masononeko moyoni, na hata wapo wanaotamani kujiuwa ikiwa ni matokeo ya jambo hilo.

Wapo wanaoishilia kujikwamua katika hilo kwa kujikaza kwa aina ambayo waswahili huiita kujikaza kisabuni lakini adhari zake bado hazikwepeki kwani kama wameokoka hujikuta wakiwa wazito kwenda kanisani, kusoma Neno, kufanya Maombi, na kama walikuwa ni wahuduma kama waimbaji na kadhalika hujikuta wakiwa na uzito wa kuhudumu bila kuwa na sababu za msingi.

Jumatatu, 5 Juni 2017

ATHARI ZA KULA VYAKULA VYA FUTARI VYA DINI FULANI, VYA MAAGANO, SHEREHE ZA KIPEPO, MILA NA KISICHO SALAMA KIROHO.

 Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Kwa kifupi ujumbe huu hulenga kukupa mathara ya kula vyakula visivyosalama kiroho, kwani wapo wakristo ama watu waliookoka ambao hubugia ama hula kila kitu kilichopo mbele yao ama huwa na mazoea ya kula vyakula ambayo ni matokeo ya ibada fulani ama huambatana na ibada ya dini fulani. Na hufaya hivyo bila kujua athari zake. Leo Bwana amenituma kukupa mathara hayo.

Kwa dini za wenzetu vyakula ni ibada, kabla ya kupika na wakati wakupika huvunenea na pia muda wa kula. Hata kwetu ndivyo ilivyo, ndiposa Yesu alikuwa akifanya hivyo mara kwa mara, kumbuka ile mikate na samaki alishukuru na kuiombea.

Pia katika Luka 22 kabla ya kuumega ule mkate na kunywa maji ya mzabibu alishukuru na kisha kuwagaiwa wanafunzi wake. (Luka 22.19 Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.)

Jumapili, 4 Juni 2017

AGANO LA CHUMVI,

KINACHOKUFANYA UNIOGOPE NI NINI

Mungu ameweka mfumo maalumu ambao ninauita “System” ya Mungu ya namna atakavyo watunza watumishi wake, na jambo hili ameliweka kwa mfumo wa Agano, na mimi nitakuchambulia kama lilivyowekwa. Ikumbukwe pia miongoni mwa masomo ambayo Mungu amenipa kuyafundisha ni yale ya kiagano ndani ya Bibilia na endelea kunifwatilai kwani yamkini siku moja nikapata kibali cha kukujuza baadhi ya maagano hayo ikiwemo Agano Jipya na nguvu yake kwani limekamilishwa kwa Damu na Mwili wa Krsto na tafsiri ya maneno ya Yesu katika Luka 22 anaposema kikombe hiki ni Agano jipya, Sanjari na kauli ya Kitabu kile cha Waebrania kinaposema ya kwamba Nguvu ya hilo Agano ipo kwenye mauti na sababu ya maagano ya kipepo yanayolenga familia kuwa na nguvu pale muhusika anapokufa.

Jumamosi, 3 Juni 2017

Usikose Somo la Kesho, "AGANO LA CHUMVI" Ni Ujumbe unaolenga kuwasaidia Watumishi wa Mungu hususani wale wa Madhabauni kwani Agano hli ni lile ambao Mungu alifunga na Haruni na watoto wake na linashabaha ya kuwasaidia ama linatoa mfumo wa Mungu wakuwatunza watumishi wake kwani kumekuwa na kilio kikubwa cha Maisha Magumu kwa baathi ya watumishi wa Madhabauni huku sababu ikiwa ni Wao kutokujua Mfumo ambao Mungu amewawekea kwa kifupi ni wao kukaa nje ya System ya Mungu. Kumbuka ni Kesho

NAMNA YA KUJINASUA KWENYE VIFUNGO VYA PEPO MAHABA. Sehemu ya 5.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Hakika ni jambo la fanaka kukutana tena katika safu hii ya makala za kiroho na ikiwa ni sehemu yetu ya mwisho ya mfululizo wa makala hii, leo nimekuandalia mambo kadhaa kuhusu hadhari za huyu Pepo mahaba na ni ombi langu Mungu akupe kibali cha kukuletea ujumbe kama huu katika sura nyingine maana hakika Mungu amenipa hazina ya maarifa kuhusu roho hii hatarishi.
Moja kwa moja nianze kwa kukujuza ya kwamba hii ni miongoni mwamambo ama roho inayoitessa dunia mno. Ikumbukwe kuwa katika historia ya Bibilia Mungu aliwai kuiangamiza dunia kwa maji kipindi cha Nuhu na kwa moto mji ule wa Sodoma na Gomora na sababu kubwa ikiwa ni roho hii.
Utumishi wa Daudi na Samsoni uliingia doa na sababu kubwa ikiwa ni roho hii. Ilimtesa pia Musa na Joshua sanjari na Kalebu kule Jangwani. Kumbuka baada ya matokeo yale ya upelelezi ya nchi ile ya ahadi Mungu anasema ya kwamba wamefanya uzizi na aina inayotajwa pale sio ya kukutana kimwili bali ni taswira nyingine ya utendaji kwa upande waibada za miungu na imani inayotajwa kiroho na lipo somo litakalo gusia taswira hiyi nami nimekuonjesha mwishoni mwa makala hii. Tuone adhari moja wapo ya roho hii.
HUTIA JERAHA, KUKUVUNJIA HESHIMA, Kitabu kile cha Mithali kimebainisha jambo hili vyema. Mithali 6: 32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. 33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.
Kwa mantiki hiyo unapotenda dhambi hii ni fika kwamba unaijerui nafsi yako na kwenye nasi kuna vitu vikuu vifwatavyo, 1. Hisia, utajikuta uwezo wako wakumwambudu Mungu katika roho na kweli unatoweka huku ukipoteza upendo kwa Mungu na kwa mwanandoa wenzako ama mchumba maana Upendo ni matokeo ya hisia itokayo katika Nafsi. 2. Akili, hiki ni kitua muhimu sana na hakipatikani kwenye ubongo bali ni kwenye nafsi, na jambo hili linaudhibitisho kibibilia katika kitabu changu cha SAIKOLOJIA YA MTU WA NDANI, nitalidadavua zaidi. Kwa hiyo

NAMNA YA KUJINASUA KWENYE VIFUNGO VYA PEPO MAHABA. Sehemu ya 4.

 Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
 Kwa tabasamu Mubashara ninakukaribisha tena katika mfululizo wa makala yetu hii ikiwa leo ni sehemu ya 4 na kama hukusoma zilizotangulia ni vyema ukazisoma ili tuweze kwenda sanjari, pia kumbuka ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA NDOTO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
(8) Kusikiliza au kufwatilia Hadithi zenye elementi au chembe chembe za pepo mahaba.
Sikio ni malango wa rohoni tena hatarishi kama utatumiwa na adui. Elifazi aliota ndoto ambayo Shetani alitumia mlango wa sikio kupenyeza mathara kathaa ikiwemo hofu, kutetemeka mifupa na hata nywele kusisimka. Mstari ule wa 12 anasema kuwa alisikia na kusikia huko ndiko kulikoruhusu hayo mathara. Ona katika kitabu kile cha Ayubu 4:12-16. Na wewe kusikiliza hadithi zenye “elementi”/chembechembe za jini Mahaba kutakufanya kumfungulia mlango maana tayari masikio yameshamruhusu kupenya hali itakayompa uhalali wa kukutembelea ndotoni.

NAMNA YA KUJINASUA KWENYE VIFUNGO VYA PEPO MAHABA. Sehemu ya 3.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry  
Dalili/Ishara zitakazokujulisha uwepo wa Pepo Mahaba kwa njia ya Uridhi. (..Mpendwa Kesho ya jana ni leo, na ahadi ni deni kama waswahili wanenavo, nami sina budi kuendelea pale nilipo ishia jana. Kumbu hii ni sehemu ya 3 kwa hiyo kama uipitwa na zilizopita zitafute ili tuweze kwenda sanjari)
1. Wazazi au babu zako watakuwa na mafarakano kwenye ndoa, yaani migogoro au kutokuelewana na hali hiyo huwa kwa ndoa za ndugu zako pia.
2. Baathi ya ndugu wa kwenu kuwa na watoto wa nje ya ndoa. Ukiona mama au baba alikuwa na tabia hiyo na hatimaye watoto/mtoto kuiridhi jua roho hii ipo miongoni mwao.
3. Wanandoa kutengana, huyu kuishi huku na yule kule ni dalili kubwa sana ya Pepo Mahaba, na jambo hilo kuwa katika jamii husika.

Alhamisi, 1 Juni 2017

NAMNA YA KUJINASUA KWENYE VIFUNGO VYA PEPO MAHABA. Sehemu ya 2.

Karibu tena katika muendelezo wa makala hii ya kiroho na leo tunaendelea na dalili za mtu anayesumbuliwa na Mapepo Mahaba ikiwa ni somo lenye dhima ya kukunasuma na mateso hayo na nisehemu ya kitabu chang cha NGUVU YA NDOTO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.Pia kama hujasoma sehemu ya kwanza jitaidi uisome ili kujua tutokapo na tuendapo.
Kushindwa kujizuia, kutazama au kufwatilia kitu chenye kushawishi kufanya ngono. Aliyetawaliwa na Roho wa Mungu huwa mwepesi kufwatilia mambo ya Kiungu. Alikadhalika aliyevaliwa na roho ya mpira pia huwa mwepesi wa kufwatilia na hushindwa kujizuia kuacha kufwatilia maswala ya kimpira. Na hii ni matokeo ya roho hizo kukamata uwezo wa maamuzi yao, fahamu kuwa uwezo wa maamuzi upo kwenye nafsi, na nafsi ndiyo inayoratibu shuhuli na matendo ya mtu kwa kivuli cha moyo.

Jumanne, 30 Mei 2017

PAKUWA, DOWNLOAD BIBILIA TAKATIFU YA KISWAHILI, SWAHILI HOLY BIBLE

BONYEZA HAPA

Tumebadlisha anuani yetu ya blogu sio www.ukombozigosple.blogspot.com bali ni www.ukombozigospel.blogspot.com

NAMNA YA KUJINASUA KWENYE VIFUNGO VYA PEPO MAHABA. Sehemu ya 1.

 Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry 
 #SHARE  #SAMBAZA Ili kueneza injili hii Zaidi.
Kuna watu wanasumbuliwa kwa kuota ndoto wakiwa na Wanazini na mapepo Mahaba aidha kwa muonekano wa watu wanaowajua ama wasio wajua. Pia wapo wanaofanya ukahaba, Uzizi na hata vitendo vya kinyume na maumbile huku wakiwa hawapendezwi na hali hiyo na wamejaribu kutafuta msaada bila mafanikio.

Baya zaidi wapo wanandoa wenye kusumbuliwa na hali kama hiyo na tatizo hili linaiweka ndoa yao njia panda kwani hufanya ama huleta ugumu hata kwenye tendo la ndoa kwa mwenzi wake. Usiogope ama usiendele kulia tena kwani Mungu amesikia kilio chako na leo amenituma kukunasua hapao.

Jumatatu, 29 Mei 2017

WANAFUNZI MLIOKOKA NISIKILIZENI.

Na Mwalimu Oscar Samba #Ug Ministry
Nina wasalimu katika jina lenye Uweza na Furaha ya hali ya juu la Bwana wetu Yesu Kisto, Leo nimeandaa ujumbe mahususi kwa ajili ya wanafunzi waliokoka katika ngazi zote za Elimu hususani vyuoni ila wazazi walimu, walezi na watumishi pia ni wahusika wa ujumbe huu ili kutimiza adhima hii.

Kusudi kuu la ujumbe huu, Ni kuwataka wanafunzi kutokuacha utayari wao wakumtumikia Mungu pindi waendapo ama wamalizapo vyuo.

Kuna tatizo kubwa sana linawakumba wanafunzi hawa nalo ni hili, Kabla ya kwenda vyuoni katika makanisa walipotokea walikuwa ni watumishi wa zuri sana ila baada ya kwenda wanaacha kumtumikia MUNGU.

Wengine wanajitaidi pindi wa wapo chuoni ila wakimaliza na kupata kazi huacha kabisa kufanya utumishi na baya zaidi wengine wana WITO na kusudi la Mungu kuwapeleka vyuoni ni ili wamtumikiye.

Kama watafanya utumishi baada ya kuhitimu, wengi ni wakati wanasubiria majibu aidha ya chuo, vyeti ama yale ya Kazi.
Inamsikitisha sana Mungu kuona jambo hili linatokea, kwani Utumishi wake haukusudiwi kufanywa tu na watu ambao hawajafika kiwango hicho cha Elimu bali hata wasomi wana Nafasi kubwa kwake kwani Paulo Mtume alikuwa Msomi na aliifanya kazi yake kwa umakini na weledi mkubwa .

Kinachotokea ni hiki, Wanapokuwapo chuoni uwanapoteza utayari wakumtumikia MUNGU, ambao huwakilishwa na viatu kwenye ulimwengu wa roho.
Tuone kwenye kitabu kile cha Wefeso;  WAEFESO 6: 15 NA KUFUNGIWA MIGUU UTAYARI TUUPATAO KWA INJILI YA AMANI.
Na sababu inayopelekea hayo ni kuweka kando Fikra za kutumia elimu yao ili kuujenga ufalume wa mbinguni badala yake huzijaza nafsi zao na fikra za kufanikiwa kimwili kwa elimu yao.
Jambo hili maandiko yamelizungumzia kwenye mfano wa Mpanzi na yanalifananisha na mbegu iliyodondoka kwenye miiba na kusongwa nayo, ambapo tafsiri yake ni mtu aliyesongwa na shuhuli nyingi na udanganyifu wa mali. Kwenye shuhuli nyingi ni hizo fikra na udanganyifu wa mali ni huo udanganyifu wa mafanikio ya kielimu.

Ukiwahitaji kumtumikia MUNGU huwa na kisingizio cha “ubize” ama ratiba ni nyingi, kumbuka jibu la huo mfano wa Mpanzi linasadifu majibu yao. Tuhakiki hilo jambo.
Mathayo 13:22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shuhuli za dunia na udanganyifu wa mali hulisonga hilo neno, likawa halizai.

Rai yangu kwao ni kuwakumbusha jinsi MUNGU alivyowatoa mbali kipindi ambacho ada ilikuwa ikisumbua walivyomlilia kwa magoti, walipofukuzwa shule kwa kukosa karo za shule walivyoombolezana kuwaendea watumishi ila wakati huu imefika hatua ya kuwakwepa na wakipigiwa simu kuhusu changizo za huduma huzima hata simu ama huona wanasumbuliwa.
   Kumbuka ulipokosa msaada YESU alikupigania, kabla hujasoma ulivyokuwa na nia ya kuifanya kazi ya MUNGU tena kwa mzigo. Kumbuka siku ile ulipokuwa kwenye taabu kubwa kimaisha ulivyomuaidia Mungu kama atakutoa hapo kwa kumuwekea nadhiri ya jambo utakalolifanya kwenye utumishi wake.

Fanya hima sasa kumrejea yeye.
Ni kweli sio kila mtu ameitwa kuwa Mchungaji ama Mwalimu ila wapo walio waimbaji, wapiga vyombo, wanaodeki kanisani na cha ajabu wanaofanya usafi siku hizi sio wale wasomi wa chuo tena bali wasomi wameweka Elimu yao mpaka kwa MUNGU. Paulo alisoma ila alijishusha na Mungu kumuinua.

Mshahara wako utumiye kuifanya kazi yake, masomo ama kazi ikichukuwa muda mwingi ama kukupa ubize epeleke msalabani kwa maombi na sadaka maalumu ukimsihi MUNGU akupe hekima ya namna ya kumtumikia pia kukupa muda katika hiyo shuhuli.

Rudia enzi zile za maombi yako ya kufunga na kuomba, usiombe tu siku ukiwa na jaribu ama uliyokosa amani. Mungu akutiye nguvu pia #Share ujumbe huu na uweneze kwa wengine ikiwemo kwenye vikundi vya wanafunzi ili waliokoka wapone kiroho.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                       PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple                                              
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa                                                                       2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/home