Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Nami sina shida kwani ni kweli waswahili husema kuwa
ahadi ni deni, nami leo sina budi kulipa deni hili, Ndugu yangu katika Kristo
kumbuka kuwa leo ni siku ya 8 ya makala yetu hii ya Nguvu ya Agano nami tokea
siku kadhaa zilizopita nalikuaidia kukuonyesha kitu muhimu ambacho Ibrahimu
alijuzwa na Mungu na hatimaye kuja kutokea kipindi cha Yakobo yaani Iziraeli
ikiwa ni Jambo la Kiagano.
Ukisoma kutoka kitabu kile cha Mwanzo sura ile ya kumi na
tano utamuona Mungu akimwambia Ibrahimu kuwa uzao wake utaenda kuishi Misiry
ama utakuwa mgeni huko na kusudi kubwa la Mungu ni kuwazidisha ama kuwaongeza,
na kuwatajirisha huko maana walitabiriwa kutoka na mali nyingi, huku muda wao
ukiwa ni miaka 400, muda ulioamariwa na Mungu, ingawaje walikaa mika 430, na
sababu za kuongezeka kwa hiyo miaka nimezielezea kwenye kitabu changu cha Namna ya Kuishi Wakati wa Majaribu au
Mapito, na pia Mungu akinipa kibali nitaligusia kwenye kitabu kile cha Wito
wa Kitumishi ili kukusaidia ujuwe umuhimu wa kumuombea Musa wako ili asichelewe
kuitika ama asikimbiliye Midiani badala yakukukomboa kwa wakati.
Tusonge mbele na Agano, Sasa leo tunaona utimiajia wa
jambo hilo ila awali ya yote ninawiwa kulidhibitisha jambo hilo ama kuliweka
bayana mbele ya macho yako.
Kwa Furaha ya Moyo Fungua nami kitabu kile cha Mwanzo
15: 13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya