Jumanne, 12 Novemba 2019

USIFANYE HARAKA KUFUNGUA HUDUMA, KUHAMA KANISANI AMA KUACHA KAZI NA KUFUNGUA BIASHARA.

Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu ninachoendelea naho cha: NAFASI YA VIUNGO VYA MWILI WA MWANADAMU KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

Na Malimu Oscar Samba:
12. Uwe na Subira, Saburi ni kitu muhimu sana, kuna wakati unakuwa katika vita vya kumiliki na kutawala lakini unakuta eneo unalotaka kumiliki au kuweka maskani yako bado hakuna nafasi, usiwe na haraka, wala usifanye haraka, endelea kuwa na uvumilivu, jambo la kuwekwa kwa adui chini ya miguu yako ni swala la mchakato, sio la siku moja, na swala la kukuwekea mazingira ya kuishi katika miliki yako kiroho iwe ni kihuduma, kiuchumi ama kiutumishi na kindoa na kadhalika linahitaji muda !

Jumatano, 30 Oktoba 2019

NGUVU YA KUWA NA UTULIVU MOYONI UNAPOKUWA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu cha Mungu yu Pamoja Nawe, pwenti ya nne, karibu: Na Mwalimu Oscar Samba.
4. Uwe na Utulivu Nafsini Mwako, kukosa utulivu maana yake ni kuwa na mahangaiko moyoni, ni kuwa na wasiwasi au mashaka, ni hali ya kujisumbukia au kuhaha.

Hali hii ni mlango wa dhambi, maana ni adui wa imani, humuondolea mtu uwezo wa kumtegemea Bwana, maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari liwezalo kupelekwa huku na kule na upepo !

Kukosa utulivu ni kukosa raha, ni kupungukiwa kwa kiasi kikubwa na amani, ambayo hiyo amani ni njia ya Mungu kuongea, maana maandiko husema kuwa na amani ya Kristo iamuwe mioyoni mwenu, kwa hiyo hayo mazingira humzuilia Mungu kuamua ndani yako, lakini pia amani ni njia ya Mungu kukuongoza, sasa ikipotea maana yake hutaiona njia, ndio maana dalili kubwa ya mtu aliyekosa utulivu na matokeo yake ni kuwa kama mtu aliyeko njia panda asiyejua njia ya kuiendea !

Jumatatu, 14 Oktoba 2019

HISTORIA YA WOKOVU, AMA SIMULIZI ya Uamsho wa MASAMA MUDIO. Sehemu ya 6, Zamani Enzi za Askofu Imanueli Lazaro

Utapatapia Unabii wa Askofu kuhusu kufa kwa zao la Kawaha, na Pigo kwa Uchumi wa wanaume na kuhamia kwa Wanawake.
.
Kulia ni Mwandishi wa Makala hii Mwalimu Oscar Samba akiwa na Msimulizi wetu Mch. Theofilo
Inasimuliwa na Mzee na Mchungaji Mstaafu wa TAG huko Masama, THEOFILO BARTOMAYO KIMARO, huyu ni pacha au ndugu na Mchungaji Wilsoni Kimaro.
Tuanze simulizi yetu; Niliokoka mwaka wa 1962 January na Mungu kuniita mwaka huo huo, niliunganika na kanisa huko Mbuguni, ambako kanisa nililikuwa halijaanza huko, (la wokovu) nilipokoka tukaanza kushuhudia nyumba kwa nyumba kama vijana.

Nakumbuka kuna mama mmoja kipindi hicho alishikwa na kansa, huyu mama sikuwahi kumuona kanisani maana alikuwa mgonjwa na alikuwa amekonda sana,

Jumatano, 2 Oktoba 2019

UJUZO WA HISTORIA YA UAMSHO WA MASAMA KAMA INAVYOSIMULIWA NA Afuraeli Munisi, Sehemu ya 5.

Anasema kuwa sio kwamba kanisa la TAG lilianzia hapa, lilikuwa limeshaanza huko Mbea hapa lilifika huo mwaka 1959, walianza kuokoka huko ni Askofu Lazaro na Jakobo Ringo ni mpare kutoka Same, walikutana na Askofu huko Arusha na mmeshenari Paulo Brutoni. ( Kama tulivyojionea hapo awali !)

Sikumbuki tarehe wala mwezi ila ni mwaka huo baada ya wao kuanza kushuhudia huko Arusha kidogo,hapo awali alikuwa ni mshirika wa KKT, na mama yake na baba yake pia, baba alikuwa ni mzee wa kanisa mtunza hazina wa hiyo dini, anaendelea kusimulia Mzee Munisi ! ( Ambae kwa sasa ni mzee wa miaka 83 na mke wake ni 72, aitwae Anarabi Afuraeli Munisi, ambao kwa kweli wamezeeka na mzee hapa huongea kwa utulivu maana pia sio buheri sana wa afya.)
Tunaendelea !


Walipokuja ndo walikuja

Jumamosi, 28 Septemba 2019

UWEKEZAJI WA ULIMWENGU WA ROHO KATIKA KIZAZI AU UZAO.

Yoshua 4:21 Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini?
22 Ndipo mtakapowaarifu watoto wenu mkisema, Israeli walivuka mto huu wa Yordani, kwa njia ya nchi kavu.
Mahali: Kanisa la TAG Mudio Masama, {Jerusalem Temple} Kilimanjaro, ndilo liiloasisiwa na Askofu Lazaro na kuwa kitovu cha Uamsho maeneo mengi Tanzania:
Tarehe: 27 na 28/9/2019. Na Mwalimu Oscar Samba.

Utangulizi:
Unapoona neno uwekezaji maana yake ni kunuia kupata faida, au kuna kitu kinapandwa, au kuwekwa, chenye nia ya kuzalisha ili kumpatia mwekezaji faida.
Katika uwekezaji kuna mwekezaji, eneo, kitu kinachowekezwa/bidhaa, na soko au walaji, na alikadhalika kiroho wawekezaji ambao ni aidha Mungu au adui Shetani, wote hawa eneo lao ni duniani wakinuia kumpata mwanadamu.

Ijumaa, 27 Septemba 2019

HISTORIA YA UAMSHO WA MASAMA ENZI ZA ASKOFU LAZARO, Ikisimuliwa na Jereremia Balitomayo Kimaro, mdogo wake na mchungaji Wilson Kimaro, Sehemu ya 4.

Ni watatu kutoka kwake.
Kushoto ni mwandishi wa makala hizi Oscar Samba akiwa na msimulizi wa sehemu hii ya nne Jeremia B. Kimaro wakiwa nyumbani kwake Mudio au Modia kama inavyotamkwa na wenyeji eneo la Masama.

Anasimulia; Tulikuwa wadogo ila kumbukumbu tunayo, miaka ya 1959 na 60 ndo uwokovu ulianza, Lazaro Askofu aliupatia kutoka Arusha, na kuja na kumkuta baba yetu (Bartolome Kimaro) ambaye alikuwa ni mdhaifu au mlemavu kidogo, na baba aliukubali, Walutheri ndio waliotufanyia fujo sana.

Wengine walipigwa mfano Mzee Lazaro na Sikustaili, pamoja na Mch Robert ambae aliwahi kupigwa chuma ya kichwani kwenye paji la uso.

Fujo ilipozidi sana walikimbia, anaendelea kusimulia mzee Jeremia, anasema kuwa mmishenari aitwae Pauli Brutoni nae alikimbia na kwenda kuita polisi !
Walipokuja mimi nilimpowenti mmoja na kusema ni huyu, walimchukuwa na kumpeleka magereza, akakaa huko kama miaka miwili, na alipokuja alisema lazima atanifanyia kitu na kuja kuniua !

Alhamisi, 26 Septemba 2019

Wajuwe Mashujaa waliochochea Uamsho wa Injili au Wokovu Masama Mudio, yupo Askofu Emanueli Lazaro, pia Rev. Au Mchungaji Wilson Kimaro, Sehemu ya 3.

Hawa ndi ambao wametajwa au kuwekwa katika mnara maalumu kanisani hapo, na makala nyingine zijazo au dodoso zijazo zitaendelea kuwaibua wengineo ikiwemo Wamisheni !


Eneo hili la modio Masama kipondi hicho cha mwaka 1959 kuanzia mwezi wa 12 kuna maajabu makubwa ya kiroho yalitokea, (kama sehemu zijazo zinenevyo,) na hawa ndio washirika na watendaji wa mwazoni kabisa.



1. Askofu Imanueli Kundandumi Mwasha( Askofu Lazaro.)
2. Mrs. Evagrace Imanueli.
3. Rev. Wilson B. Kimaro.
4. Firyandian Kundandumi.
5. Nkira Aranya Bartolomayo

Jumanne, 24 Septemba 2019

TUNAENDELEA NA HISTORIA NA DODOSO LA WOKOVU KIPINDI CHA ASKOFU LAZARO HUKU MUDIO MASAMA. Sehemu ya 2.


Kumbuka kuwa hili ndilo eneo ambalo ni chimbuko la wokovu kwa makanisa megi kanda ya Kaskazini na chazo cha uzalishaji wa matumishi wengi kama sehemu yetu ya tatu ishuhudiavyo kwa nchi Nzima !

Jumatatu, 23 Septemba 2019

Udodoso wa Historia na Ueneaji wa Kanisa la Tag na Wokovu kipindi cha Askofu Imanueli Lazaro Mwasha. Sehemu ya 1

Hili Ndilo Kanisa la Kwanza Kabisa kujengwa na Askofu Emanueli Lazaro, hapa Masama Moshi Kilimanjaro, mzee nilie nae hapa Philipo Mwasha anasema kuwa hapa kulikiwa ni Nyumbani kwa Babu yake na Askofu aliyeitwa Lazaro.

NIPO MASAMA MOSHI KWA ASKOFU LAZARO NADODOSA HISTORIA YA KANISA LA TAG

Nipo na Mzee Philipo Mwasha, ndugu wa ukoo au jamaa ya Askofu Emanueli Lazaro Mwasha, ananipa historia ya mambo ya kale, nipo Masama Moshi alipozaliwa Askofu, mengi zaidi utayapata www.ukombozigospel.blogspot.com

Jumamosi, 21 Septemba 2019

MSAADA KWA WALIOWAI KUMWAGA DAMU YAANI KUUA:


Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha SABABU ZA DAMU YA YESU KUWA NA NGUVU ILIYO NAYO.

Kama uliwai kuua mtu, kwa kukusudia au bila kudhamiria, kwa njia ya ajli, au kutumia silaha, kutoa mimba, ukiwa kama mama wa mtoto, baba, dakitari, au kushiriki kiushauri ama kiuwezeshaji ama kwa njia yoyote ile.

Pia hata kama ulihusika katika mauaji ya mtu au watu, kwa njia yoyote, ikiwemo ya ushauri, kupanga mipango, au unafahamu fika na bayana kuwa damu ya mtu fulani ipo juu yenu, au juu yako, au katika eneo unaloishi njia hii itafanyika msaada kwako au kwenu Lakini pia hata kama wewe ni asikari, au mwanajeshi, na uliwai kumwaga damu, haijalisha uliona ina hatia au la,

Jumamosi, 14 Septemba 2019

BARAKA ZA KWENYE NDOA, FAMILIA AU UZAO

5 Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
6 Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.

Bwana Yesu Asifiwe Mpendwa, mimi kama kuhani wa Bwana ninawiwa kumimina baraka juu ya uzao wako, ndoa, au familia yako, na hata kama bado hujaoa na kuolewa maombi haya fahamu ni akiba, au baraka hizi ziwe akiba kwako.

Amani yake Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na familia yako, uwe na watoto wenye afya njema na weledi wa akili, uzao wako ukamjue Mungu wa kweli na kumtumikia kiukamilifu na kwa nia ya kumkubali !

Jumatano, 11 Septemba 2019

Msihi Mungu Akupe ama Akugundishe Akili na Maarifa

Andiko hili linatupa uhalali wa kumsihi Mungu akupe ama akufundishe akili, na maarifa !
Yamkini wewe ni mwanafunzi msihi akupe za darasani, ni mfanya biashara msihi akupe za kiuchumi, yamkini ni mtumishi Mtumishi muombe akupe za kihuduma alikadhalika kiongozi au mwanasiasa mtake akupe za kiuongozi kama ilivyokuwa kwa mfalme Sulmani, pia uongozi huo waweza kuwa ni wa kitumishi kama shemasi au kiongozi wa idara, uchungaji alikadhalika uaskofu !

Zaidi tunacho kitabu cha NAFASI YA AKILI KTK KUKUFANIKISHA AU KUKUUFAISHA KIMAISHA, au kile cha MOYO WA UFAHAMU. Pia tembelea, www.ukombozigospel.blogspot.com
#MwalimuOscarSamba
#mwalimu
#yaelewemaandiko
#tanzania

Jumamosi, 7 Septemba 2019

MWAMBA UTOWE MAJI KWA AJILI YAKO.

                     
Wana wa Israeli walipokuwa wakisafiri kule jangwani na kuelekea Kanani walipita katika hali ngumu sana kiasi cha kuishiwa au kukosa maji ya kunywa, ila Bwana aliwafanyia mujiza kwa kuwatokezea maji huko jangwani !
Aliupasua mwamba napo maji yakawabubujikia; Zaburi 105:41 Akaufunua mwamba, kukabubujika maji, Yakapita pakavuni kama mto.

Nawe najua unapitia mahali pagumu, wala sio haba, ila huyu Mungu aliyetenda kwa Wana wa Israeli ni ombi langu atende na kwako siku hii ya leo, akufanyia mujiza kutokana na haja ya moyo wako, akufanyie maji, akupe mana yaani chakula cha mbinguni, wewe amini tu na umwamini Bwana maana Yeye ni mwaminifu wala hasemi uongo, atakutokelezea tu !

Ni ombi langu kwa Bwana maji yakutiririkie siku hii ya leo !


Alhamisi, 5 Septemba 2019

YESU KAMA MTULIZA MAWIMBI AU DHORUBA.

                                                  Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry  #SHARE  #SAMBAZA Ili kueneza injili hii.
Siku moja wanafunzi wa Yesu walikuwa wakisafiri majini ama ziwani na walilenga kufika nga’ambo ya ziwa ili kufanya jambo fulani, lakini walipokuwa katika safari yao, Punde si Punde bahari ili kumbwa na Mawimbi makubwa yaliyoambatana na Upepo mkali.

Hali hiyo iliwapa hofu kubwa mno, Lakini katika mazingira yote hayo hawakukubali kukwama safarini bali walimwamsha Yesu aliyekuwa akipiga usingizi, Hii ina maana kubwa sana na hapo mbeleni nitaifafanua.

Tuyadodose maandiko ili kujionea jambo hili kiunaga ubaga, Soma Marko 4:35-41.  Marko 4:35 Siku ile kulikuwa jioni, akawaambia, “Na tuvuke mpaka ng’ambo.” 37Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi ya kakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye mwenyewe alikuwapo katika Shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu sii kitu kwako kuwa tunaangamia?” 39 Akaamka, akaukeme upepo, akaiambia bahari, “Nyamaza utuliye!” Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
Hapo ninapata funzo kubwa naamini nawe unapata jambo la kushangaza sana; ya kwamba mtu huyu tuliye naye sio wakufananishwa kwani anaweza kutuliza mambo yaliyoonekana kuwa ni magumu maishani mwetu na wewe sasa jenga imani hiyo na usisite kumuamsha ili atulize yanayokusonga. Ili na kwako kuwe, “SHWARI KUU”

Maandiko hayo yanatuonyeshe dhairi shairi kwamba YESU alikuwa na malaka juu ya mawimbi, na upepo, na ukitazama kiumakini utagundua kuwa mamlaka hii tulishapewa tangu enzi za umbaji wa ulimwengu Mungu alipowaambia Adamu na Hawa kuwa amewapa uwezo wa kutawala ndege wa angani, (Mamlaka dhidi ya Anga), Samaki wa Baharaini, (Ni Mamlaka juu ya bahari), Na Wanyama wote wa Nchi kavu, (Ikiwa ni mamlaka juu ya Aridhi) pamoja na hayo mamlaka hiyo inaambatana na vitu vilivyopo sehemu husika.

Kwa hiyo adui mkubwa aliyewafanya wasiweze kuitumia hiyo mamlaka ni kwanza ni Uelewa wao, hawakulijua hili, maana walikuwa na Yesu, ni kweli ila hawakujua kama anauwezo wa kutuliza hadi mawimbi na upepo, ndio maaana baada ya mujiza huo wanashangaa,
“.. Wakaambiana, ‘Ni nani huyu, hata upepo na bahari humtii? ” Mariko 4:41. Fikiri kwa kina kwamba wapo na Yesu miaka ya kutosha ila bado hawakufahamu mamlaka/uwezo aliyo nao, kuhusu tatizo walilokuwa nalo.

Na wewe yamkini umeokoka ila hujafahamu uwezo wa Yesu kuhusu dhoruba zinazokukumba, usimwamshe Yesu katika mtazamo wa wale wanafunzi walio mwamsha ili wateseke wote na Yesu katika kupamba na ile hali kwani hawakutarajia YESU kutenda lile, ndio maana walimwambia hivi,
“..Sii, kitu kwako kuwa tunaangamia,” Mariko 4:38.  Katika Luka walitumia maneno; Bwana mkubwa huku wakiita zaidi ya mara moja. Usipotazama andiko hilo kwa jicho la uchunguzi hutaiona hii fikra ya wanafunzi, ila iinajidhirisha pale wanaposhangaa uweza wake mara baada ya mujiza kutendeka hali inayobainisha bayana ya kwamba kumuasha kwao hakukuwa na taraja ya mujiza ule bali kulikwa na mtazamo wa “tupambane sote.”
Nataka kukujengea Imanii ili utambue ya kwamba hilo unalolipitia Yesu analiweza kwa shabaha ya kukataka kuacha kuwatazama wanadamu ambao hawatakusaidia badala yake wengine wataishia kukusema ama kukusengenya hali itakayokukwamisha kiroho kwani maneno hayo yanatakumiza bure badala yake unapaswa kumtaza YESU huku ukitambua ya kwamba ndani yake ipo Mamlaka na itumiye kama alivyokupa ili utulize hayo mawimbi na upepo kwani Yesu aliukemea na wewe kemia hiyo misukosuko kwenye ndoa yako, uchumi familia au huduma sasa.

Jambo la pili lilikuwa ni WOGA, ukiogopa ni dhairi kwamba Imani yako itayumba hali itakayokufanya kushindwa kuitambua ama kuitumia mamlaka uliyopewa na Yesu Kristo juu ya hayo matatizo.
Tuone mafundisho haya ya Uoga kwenye ujumbe huu kama nilivyokudokezea kwenye kitabu changu cha Namna ya Kuishi Wakati wa Majaribu au Mapito katika Ukurasa ule wa 31 na kuendelea.

“….Natumai sasa utakubaliana nami vyema pale Yesu alipokuwa na wanafunzi wake katika boti na mawimbi ya kaja wakaogopa Yesu aliwauliza “Imani yenu iko wapi” Luka 8:25. Akiwa anamaanisha kuwa wameogopa na hofu ilimdhirishia Yesu kuwa tatizo ni Imani, katika swala hili;Tutazame tena Mathayo 8:26 Akawaambia “mbona mmekuwa waoga, enyi wa Imani haba” Waoga alafu wa Imani Haba , haba maana yake chache,Kwenye luka anataka kujua walipo iweka imani yao, hapa anawaambia kuwa Imani mliyo nayo ni chache, Joshu anawaambia “wala msiwaogope”

Twende kwenye Marko tuone Mfano ama stori hiyo hiyo ya dhoruba ziwani. Marko 4:40 Akawambia , “mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado ?”. Hapa Yesu anauliza Uwoga pili hamna Imani bado jumlisha na hoja ya luka na Mathayo changanya na hiyo ya Marko (“Imani yenu iko wapi” + “mbona mmekuwa waoga, enyi wa Imani haba” na “mbona mmekuwa waoga? +Hamna imani bado ?”)
Kuna kitu nilikuaidia kukudokezea hapa mbeleni nacho ni hiki, Yesu alipokuwa amelala sio kwamba hakujua kitakachotokea, La! Asha!! Alijua fika, ila alikuwa akihitaji kuona au kupima ama kufahamu kiwango cha wanafunzi wake kumjua, pili Uwezo wao wakukabilina na matatizo na tatu kiwango cha Imani yao. Ndiposa alipoamka aling’aka hali iliyoonyesha kuwa amekasirshwa na matokeo ya mtihani uliowakumba.

Nakudhibitisha hilo tazama kwa kina maneno yake katika vitabu vyote vitatu, 1. Imani yenu iko wapi 2. enyi wa Imani haba 3. Hamna imani bado ?”).
Kwa anayetazama mambo kwa jicho la tatu kama mimi, kuna kitu anajifunza hapo, na miongoni mwacho ni hiki cha kiwango cha Imani na Sehemu ilipowekwa, hali inayomaanisha kuwa ukimya wa Yesu ulikiwa ukiashiria usimamamizi wa Mtihani.

Walioenda shule walao hadi chekechea wanafahamu kuwa sura ya Mwalimu wakati anafundisha ni tofauti na ile wakati akiwa anasimamia mtihani, na ujio wa sura ya wakati wa kutoa matokeo unategemea na ujibuji au ufaulu wako wa mtihani. Ukifeli utaona mikunjo ya ndita na hamaki ila ukifaulu utaona furaha na tabasamu mwanana, linaloambata na jicho angavu .

Jumatano, 4 Septemba 2019

MADHARA YA KUTUMIKA KAMA NABII WA UONGO:

Tunaendelea na mfululizo wa jumbe za kinabii, katika kitabu chengu cha Wito na huduma ya Nabii, na leo tunatazama;
MADHARA YA KUTUMIKA KAMA NABII WA UONGO: Na Mwalimu Oscar Samba

1. Kutupwa pamoja na bwana zao katika hukumu ya Moto wa Milele: Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Nakutaka kuwa mkini sana mtu wa Mungu, hakuna faida yoyote ya kumtumikia  Ibilisi, tofautina kutupwa kwenye Jehanum ya moto au katika ziwa lile la moto, kwa hiyo ni yangu rai kukutaka kuachana na hiyo nia, au kuepuka na  kuwa makini naa jambo hili, wala usijihesabie haki kuwa mimi siwezi, wewe jiepushe na muombe Mungu akupe kuepuka jambo hili, wengi waliongea vivyo, lakini kwa kukosa udhabiti wa moyo, leo hii wanamtumikia Ibilisi, na hawajui kuwa ipo Ole kwa ajili yao;
Yuda 1:11 Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.
Petro anatuambia kuwa kama Mungu hakuwaacha malaika wale waliaoasi, hakika na hawa pia watapokea hukumu yao;
2 Petro 2:4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu.
12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao.
Hakika wataangamizwa: Yeremia 14: 15 Basi, kwa hiyo Bwana asema hivi, Kwa habari za manabii wanaotabiri kwa jina langu, wala mimi sikuwatuma, lakini husema, Upanga na njaa havitaingia katika nchi hii; Kwa upanga na njaa manabii hao wataangamizwa. Pia Yeremia 29:31-31, Ezekieli 13, na Zekaria 13.

Jumatano, 28 Agosti 2019

MSAADA WA KUTOKA KWENYE KIFUNGO CHA MADENI.

Kunamtu ameniandiki hivi, "Mtumishi Bwana Yesu asifiwe mnaendeleaje ss wazima mtumishi nina Hitaji tuombe niwezekupata hela ya kulipa madeni kwani ni nadaiwa sijui napata wapi pesa."
Nami kumjibu hivi:

Hatua ya kwanza ni kuvunja roho ya utumwa kupitia madeni,Mithali 22:7 Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.
Pili, lipa hayo madeni rohoni kwa Damu ya Yesu, tatu ndo kuomba milango ya fedha ifunguke ili uyalipe mwilini, 4, omba nidhamu ya Mungu ili fedha hiyo ikija uwe mwaminifu kulipa nasio kufanyia mambo mengine ! 5. Tumia hekima y

Jumamosi, 24 Agosti 2019

MAMBO MUHIMU KATIKA UINJILISTI:

Bwana Yesu aifiwe Mpendwa, leo tunageukia kitabu changu cha Wito na Huduma ya Uinjilisti, na tunaangazia kipengele kimoja;
 MAMBO MUHIMU KATIKA UINJILISTI:
Na Mwalimu Oscar Samba, wa Ug Ministry.
Kumbuka mada hii inahusiana na utendaji, maana yake namna ya kufanya unapokuwa shambani, au namna ya kujindaa kwa ajili ya kuingia katika eneo la mavuno, wala hapa sineni habari za mfumo, au tabia za Mwinjilisti kama huko awali.

Mambo haya yatake sana kuyajua ili uwekeze nguvu kubwa hapo katika maandalizi, maombi na hata wakati unahubiri:
1. Watu Kumuamini Yesu, 2. Kumkiri, na 3. Kumpokea kama Bwana.
Warumi 10.9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

Jumatatu, 19 Agosti 2019

#JE_WAJUA_KUWA_UKIFA_HUJAOKOKA_UTAENDA_MOTONI?


Awali ya yote pokea salamu zangu, leo ninataka kukufikirisha tu walau kwa kiduchu, kuwa maisha unayoishi leo ndio yenye hatima ya maisha yako ya baadae.
Kulikuwa na tajiri mmoja na masikini mmoja jina lake Lazaro, tajiri huyu hakumjua wala kumcha Mungu, ila Lazaro alikuwa ni mtu mwema.

Ikatokea siku wote wakafa, njia ambayo mimi na wewe ni shariti tuipitie, Lazaro alienda Mbinguni, na tajiri motoni;
Luka 16:22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

Alhamisi, 1 Agosti 2019

NAMNA YA KUMJUA NABII WA KWELI NA WA UONGO.   Mwalimu Oscar Samba wa Ug Minisry.
Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha Wito na huduma ya Nabii,
(a) WA UONGO:
1. Tazama Misingi yao ya Kihuduma, Hawana msingi wa neno, Hofu ya Mungu haipo pamoja nao, mambo muhimu ya kiroho kama Ubatizo, Toba ya dhambi, Ujazo wa Roho Mtakatifu, Msisitizo wa kudumu katika imani ya kweli, msisitizo katika maombi ya kufunga na kuomba katika Roho na Kweli, au matumizi ya jina la Yesu hayatakuwa yakitumika kama ilivyo amriwa, na kamwe hawezi kuitumia Damu ya Yesu.
Kumbuka hata akijifanya kujitahidi kubatiza, hataweza kutumia utatu mtakatifu au maji mengi, na kuwafunza watu wake katika Roho kuhusu huo ubatizo.
Mambo hayo yatazame sana katika huduma ambayo unaitilia shaka.
2. Chunguza Matunda yao, Yesu alituhusia na kutufahamisha kuwa tutawatambua kwa matunda yao, akibainisha kuwa mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, alikadhalika mti mbaya huzaa yaliyo mabaya.
Mathayo 7:15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?