Jumamosi, 14 Septemba 2019

BARAKA ZA KWENYE NDOA, FAMILIA AU UZAO

5 Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
6 Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.

Bwana Yesu Asifiwe Mpendwa, mimi kama kuhani wa Bwana ninawiwa kumimina baraka juu ya uzao wako, ndoa, au familia yako, na hata kama bado hujaoa na kuolewa maombi haya fahamu ni akiba, au baraka hizi ziwe akiba kwako.

Amani yake Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na familia yako, uwe na watoto wenye afya njema na weledi wa akili, uzao wako ukamjue Mungu wa kweli na kumtumikia kiukamilifu na kwa nia ya kumkubali !



Kwenu ama kwako kusiwe na tasa wala mgumba, ubarikiwe katika kazi za mikono yako na mawazo yako yakapate kibali mbele za Bwana sawasawa na mapenzi yake na akupe kuyajua hayo mawazo anayokuwazia !

Kapu lako na pipa lako la mafuta na unga visiishiwe ! Mifugo yako ikuzalie mapacha, na uzao wako na mwenza mwenzako uwe wa mapacha !

Magongwa na matatizo ya kurithi kama migogoro ya ndoa, tabia hatarishi na kila roho hatarishi visipate kibali kwako, ninavifungia mlango na kuviwekea mipaka kwa jina la Yesu Kristo !

Damu yake Bwana wetu Yesu Kristo ikufunike wewe na mwenzi mwenzako ! Muwe na maisha ya amani, na furaha tele !

Misiba ya kipepo isipate upenyo kwenu !

Kwa mamlaka niliyopewa ya kufunga na kufungua, sawasawa na Mathayo 16:19, ninafunga sasa kila roho za migogoro na mafarakano kwenye ndoa, na ninafungulia baraka za Ibrahimu za uzao na ndoa, ninafungulia zile za kiroho, kiuchumi, na kiafya, Mungu akukumbuke daima, wala asikusahau wewe na uzao wako !

Wewe na nyumba yako ukamtumikie Bwana !

Sasa, ili baraka hizi ziwe halisi kwako, zifungamanishe na sadaka maalumu, kama Ibrahimu alivyofanya !

Waweza itoa kanisani kwako, (kama ni mahali walipookoka,) au kwa yatima au mjane kadri Bwana atakavyokuongoza !

Pia, kama hujaoka hakikisha uonaokoka, maana wokovu hukupa nafasi kubwa zaidi ya kuzirithi baraka hizi za kiagano, asante na kwa heri ! Lakini pia mshukuru Mungu kwa upako huu alionimiminia kwa ajili yako, maana sio maombi na mambo ambayo huyafanya mara kwa mara !

Kama hujaokoka na unataka kuokoka tafadhali fuatisha nami kwa imani sala hii ya toba, Sema: Mungu Baba, nisamehe, nimetambua ya kuwa ni mwenye dhambi, sasa ninatubu, ninakuamini na kukupokea moyoni mwangu kama Bwana na mwokozi wa maisha yangu, nakuomba ufute jina langu kwenye kitabu cha huku na uliandike sasa kwenye kitabu cha uzima wa milele, Ameni.

Hongera kwa kuokoka, na tafuta sasa kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, na ujitambulishe kuwa umeoka hivi karibuni ili wakulee zaidi kiroho, kwa mawasiliano au sadaka M-PESA, maombi na ushauri, ni +255759859287, E-Mail: ukombozigospel@gmail.com, Tupo Arusha Tanzania. Na Mwalimu Oscar Samba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni