Hili Ndilo Kanisa la Kwanza Kabisa kujengwa na Askofu Emanueli Lazaro, hapa Masama Moshi Kilimanjaro, mzee nilie nae hapa Philipo Mwasha anasema kuwa hapa kulikiwa ni Nyumbani kwa Babu yake na Askofu aliyeitwa Lazaro.
Ambapo hapa ndipo walipoanza kama kanisa la nyumbani ! Ambapo Askofu alipotoka Arusha alikuwa akiwakusanya hapa na kuwashirikisha neno la Mungu, ilikuwa kama kikundi kisha baadae kanisa, Mzee Philipo ambae ni ndugu na Askofu anasema Askofu alimaliza shule ya msingi Kware alielekea Arusha kutafuta kazi na ndipo alipokutana na mzungu Brutoni na kumuhubiria kisha kumfunza neno la Mungu ambapo ndipo aliporudi kijijini na kuwakusaya na kuwafunza neno la Mungu.
Na hapa pakiwa ndipo kituo chao cha makutano, na ananijuza zaidi jina Lazaro sio la baba yake la babu yake, je wajua baba yake anaitwaje ?
Anaitwa Kundandumi Mwasha .
Kanisa hili linaitwa Jerusalem Temple Mudio, lilianza mwaka 1959
Endelea kuyembelea soma www.ukombozigospel.blogspot.com dondoo zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni