Jumatano, 4 Septemba 2019

MADHARA YA KUTUMIKA KAMA NABII WA UONGO:

Tunaendelea na mfululizo wa jumbe za kinabii, katika kitabu chengu cha Wito na huduma ya Nabii, na leo tunatazama;
MADHARA YA KUTUMIKA KAMA NABII WA UONGO: Na Mwalimu Oscar Samba

1. Kutupwa pamoja na bwana zao katika hukumu ya Moto wa Milele: Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Nakutaka kuwa mkini sana mtu wa Mungu, hakuna faida yoyote ya kumtumikia  Ibilisi, tofautina kutupwa kwenye Jehanum ya moto au katika ziwa lile la moto, kwa hiyo ni yangu rai kukutaka kuachana na hiyo nia, au kuepuka na  kuwa makini naa jambo hili, wala usijihesabie haki kuwa mimi siwezi, wewe jiepushe na muombe Mungu akupe kuepuka jambo hili, wengi waliongea vivyo, lakini kwa kukosa udhabiti wa moyo, leo hii wanamtumikia Ibilisi, na hawajui kuwa ipo Ole kwa ajili yao;
Yuda 1:11 Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.
Petro anatuambia kuwa kama Mungu hakuwaacha malaika wale waliaoasi, hakika na hawa pia watapokea hukumu yao;
2 Petro 2:4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu.
12 Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao.
Hakika wataangamizwa: Yeremia 14: 15 Basi, kwa hiyo Bwana asema hivi, Kwa habari za manabii wanaotabiri kwa jina langu, wala mimi sikuwatuma, lakini husema, Upanga na njaa havitaingia katika nchi hii; Kwa upanga na njaa manabii hao wataangamizwa. Pia Yeremia 29:31-31, Ezekieli 13, na Zekaria 13.

Mathayo 7:22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
“Ukiweka masilahi yako binafsi katika huduma, hata kama kweli unalitumia jina la Yesu, na kubashiri waziwazi, na kufanya miujiza kwa jina la Yesu, na kupewa jumbe na mafunuo na huyu Roho Mtakatifu, maadamu ulitwa utukufu wake, ulipenda ujira wa aibu au kufanyia kazi mali, hakika, hatakutambua, na wewe ni miongoni mwa manabii wa uovu, narudia tena, ili ujuwe sijakosea, na sema hivi; ‘wewe ni miongoni mwa manabii wa uovu.’ Acha haraka.”
Lakini sio wao tu, bali hata na watu wao, yaani waumini wao, hao wanaopenda kusikiliza ngonjera zao, na huo uongo wao, au kwenda kutaka mashauri yao, nao pia ni wakosaji, twafahamu kibinadamu na kisheria mtoaji na mpokea rushwa wote ni wahalifu, na ndivyo ilivyo kwa hawa pia, yaani mtoa unabii wa uongo, na aliyemfuasi au msikilizaji au mpokeaji wake ama mshirika wake wote ni waalifu kiroho;
Yeremia 14: 16 Na watu hao, waliopewa unabii na wao, watatupwa nje katika njia kuu za Yerusalemu kwa sababu ya upanga na njaa; wala hawatakuwa na mtu wa kuwazika, wao na wake zao, na wana wao, na binti zao; maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.
(Wale waliogeuka mashabiki wao, ambao hupiga kele kwa kushangilia na kwamba ni viwanja vya mpira, au wapo kwenye kumbi za kutazama michezo ama sinema, kwao ibada zimegeuka, maeneo ya ushabiki, wao nao, watatendwa kama wao.)
2.Hana Furaha ya Wokovu, na ni mwenye Hofu, maana nafsi yake na dhamiri yake vinajua ukweli, kuwa baada ya kifo ni hukumu, naye anafahamu mshahara wa dhambi ni mauti, na maandiko niliyomsomea hapo juu anayajua, kuwa atahukumiwa katika ziwa ile liwakalo moto pamoja na bwana zake, kwa hiyo furaha ya wokovu ambayo huwa nao waliokoka, yeye hana, pili anafahamu atapokea ujira mkubwa wa adhabu maana yu afanya hayo kwa makusudi na hupotosha watu wengi.
Mathayo 23.14 [Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]
Yakobo 3 :
3:1 Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi.
3. Hana Heshima yoyote kutoka kwa Mungu, Mungu ananena kuwa anawaheshimu wale ambao wana mtumikia, kwa hiyo wasio mtumikia, ni chukizo kwake, Mungu huyachukia haya mafundisho na wafundishao katika misingi ya unabii wa uongo, (fahamu pi manabii hufundisha);
Ufunuo 2:6 Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia.
Utamsikia akisema nimefunuliwa kitu fulani,na hapo humsingizia Bwana, alafu anaanza kukifunza, tuwe makini, maana nyakati hizi ni za uovu.
Nataka kukupa andiko ambalo pia linadhibitisha kwamba ni kweli Mungu huwapuzia hawa manabii, na hapa anawafananisha na mkia, kumbuka mkia ni kitu cha nyumba, na ni kiungo chenye heshima duni, andiko hili wakati nalisoma, limenifuraisha na kujikuta binafsi najawa na kicheko;
Isaya 9:15 Mzee mwenye kuheshimiwa ndiye kichwa, na nabii afundishaye uongo ndiye mkia.
16 Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia.

Kwa Bwana ni kama Makapi na wa Kweli ni kama Ngano:
Yeremia 23: 28 Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana.
Ukipata muda pia jisomee sura nzima ya Yeremia 23.

4…………
NB: Yeremia 23: 32 Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema Bwana, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema Bwana.
Suluhu: Kama wewe umekuwa ni miongoni mwao, na unafahamu fika kabisa umeamua kuicha hiyo njia kwa kudhamiria, mimi ninakupa tiba, nayo ni toba ya kweli, kubali sasa kugeuka, na nyuma ya kitabu hiki ipo sala ya toba, ifuatishe hiyo, na baada ya hapo utakuwa umeokoka, kwa hiyo usitende ivyo tena na usifanye utumishi kwanza, bada yake tafuta Mchungaji wa kweli, ukatubu hapo alafu atakuelekeza huko mbeleni kuhusu jambo la kihuduma, ameni:
Ufunuo 2:15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.
16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.
FAHAMU: Kama umebishana nami, nataka tu, kukufahamisha kuwa Yesu tunayemuamini ni mkuu kuliko huyo bwana wako Ibilisi, kwa hiyo kwa ukuu wake, atamua huyo bwana wako, ni heri kulijua hili mapema, ili ujisalimishe kwake hutaki utakufa naye na kuteketea naye milele katika mateso ya moto, utalia na kuomboleza wala hatakuokoa maana naye atakuwa katika taabu kama yako.
2 Wathesalonike 2 :
2.8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo.
Nawataka pia watumishi wa Mungu aliye hai, kutangaza hukumu za Mungu wetu juu ya manabii kama hawa, bila woga, na wakishatangaza wazisindikize kwa maombi, kama nabii Elia alivyofanya alipoifunga mvua, Yakobo 5, anatuambia kuwa aliomba kwa bidii, nao pia wafanye hiyo, jambo hili la kishujaa alilifanya Yeremia, na ilikuwa hivyo kwa Hanania, aliyetafuta kibalia kwa wakuu wa taifa lile, na watu, angali Bwana hakumtuma, Nabii Yeremia alimtangazia kifo, na kweli alikufa;
Yeremia 28: 15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; Bwana hakukutuma; lakini unawatumainisha watu hawa maneno ya uongo.
16 Basi Bwana asema hivi, Tazama, nakutuma uende zako toka juu ya uso wa nchi; mwaka huu utakufa, kwa sababu umenena maneno ya uasi juu ya Bwana.
17 Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba.

Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fuatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com 
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel
 PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel
 Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA  https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA  (Ukombozi Gospel)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni