Jumamosi, 21 Septemba 2019
MSAADA KWA WALIOWAI KUMWAGA DAMU YAANI KUUA:
Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha SABABU ZA DAMU YA YESU KUWA NA NGUVU ILIYO NAYO.
Kama uliwai kuua mtu, kwa kukusudia au bila kudhamiria, kwa njia ya ajli, au kutumia silaha, kutoa mimba, ukiwa kama mama wa mtoto, baba, dakitari, au kushiriki kiushauri ama kiuwezeshaji ama kwa njia yoyote ile.
Pia hata kama ulihusika katika mauaji ya mtu au watu, kwa njia yoyote, ikiwemo ya ushauri, kupanga mipango, au unafahamu fika na bayana kuwa damu ya mtu fulani ipo juu yenu, au juu yako, au katika eneo unaloishi njia hii itafanyika msaada kwako au kwenu Lakini pia hata kama wewe ni asikari, au mwanajeshi, na uliwai kumwaga damu, haijalisha uliona ina hatia au la,
ila ujue ukweli wa hatia hiyo na uhalali wa mauaji hayo anayefahamu ni Mungu mwenyewe, Shetani na damu husika , kwa hiyo nawe yafanye haya maombi, ukijaribu kujihesabia haki kuwa ulikuwa ukitimiza wajibu wako sawa, au uliwajibika kufanya hivyo na haoni kosa lako, “it’s ok,” ila kwa ushauri wangu na waimizo la Roho Mtakatifu ndani yangu, huna budi kufanya hivyo:
Hakikisha unainyamazisha hiyo damu, ili isiendelee kunena mabaya au kulia kisasi au malipizi kwenye ulimwengu wa roho. Lakini kanuni ya kwanza;
1. Omba Rehema, tubia tukio hilo, muombe Mungu akusamehe, wala usijihesesabie haki, kwa namna yoyote ile. Tumia Damu ya Yesu katika kutubia hilo kosa, ombea rehema kutokana na umwajikaji wa Damu ya Yesu kwa ajili ya ondole la dhambi, Mathayo 26:28. Omba hadi upate mani ya kiungu moyoni mwako.
2. Inyamazishe hiyo damu. Katika maandiko tunaambiwa kuwa damu ya Habili ilinena, ukienda katika Mwanzo 4: 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Tunaona hapo kuwa hii damu ililia, ukiendelea mbele yake, unaona Mungu akiachilia adhabu, ikiwa na mantiki kuwa kilio kile kilihitaji ulipizaji wa kisasi, kwani baada ya kisasi hatuinoni ikilia tena.
Kwa kuwa wewe umeshaomba Rehema, ni fika kuwa Mungu amesha kusamehe, au kufuta hilo tukio kiroho, kwa hiyo unao uhalali wa kutumia Damu ya Yesu ili kunyamazisha hiyo damu iliyomwagwa.
Tamka kuinyamazisha kwa kumwaga Damu ya Yesu juu yake na kuitaka inene mema, tumia andiko la Waebrania 12:24 linalosema kuwa Damu ya Yesu inanena mema kuliko ile ya Habili.
Omba hivi, kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth, natumia Damu ya Yesu kuinyamazisha hiyo damu iliyomwagika, “kama unamjua mtaje jina,” namwaga Damu ya Yesu kwenye hiyo aridhi, kwa Damu ya Yesu Kristo, ewe damu nyamaza kimya, milele, ninakuamrisha nyamza kimya, namwaga Damu ya Yesu ile ya Agano jipya, sawasawa na Luka 20:22, na Matayo 26:28, ninakunyazamazisha ewe damu ya fulani, pia ninaitaka Damu ya Yesu kunena mema ili kubatilisha sauti za kisasi na maneno ya malipizi kutoka kwenye hiyo damu ya fulani.
Fanya hayo maombi kwa imani, huku ukimnyima Shetani kukuhukumu moyoni kuwa uliua, fahamu toba uliyoifanya tayari Mungu alishakusamehe, kwa hiyo hatia yako haipo tena mbele za Mungu na Mungu akishasamehe huwa anasahau kabisa. Kwa hiyo hukumu ya kipepo ipinge kwani inalenga kukuondolea ujasiri mbele za Mungu, na fahamu kwa mujibu wa Waebrania, tunaambiwa tukisogele kiti cha Neema kwa Ujasiri ili tupate Rehema, kwa hiyo hakikisha unapingana na Ibilisi katika hili jambo pili nafsi yako pia isi-kuhukumu, na muombe Mungu ama Roho Mtakatifu aiwezeshe kujisamehe.
3. Futa Madhara Yote yaliyopenya na yaliyokusudiwa, kunapotokea mauaji au umwajikaji wa damu isiyo na hatia, kwenye ulimwengu wa roho Shetani hutumia jambo hilo kama lango la kupenyeza madhara, au matatizo fulani, lakini pia, hata Mungu huachilia adhabu, ukitaka kuamini vyema, nenda kwa Kaini nawe hapo utajionea haya mambo vyema.
Kwa hiyo nyunyiza Damu ya Yesu huku ukitamka kufuta hayo madhara, na kuyachomoa, yaweza kuwa ni magonjwa, roho ya kukataliwa, mauti kwenye uchumi, mauti kwenye ndoa na kadhalika.
Chimbuko la ujumbe huu, ni pale mwanamke mmoja aliyenifuata siku chache zilizopita, akiniambia kuwa uchumi wa mume wake upo mahali pa gumu, na kubainisha kuwa kazini kwao, kuna mfanya kazi mwenzao, alisababisha ajali, na aliyegongwa alifariki.
Mara baada ya ajali hiyo uchumi wa kiwanda umekuwa mahali pa gumu hadi kufikia hatua ya mishahara ya wafanya kazi kusumbua.
Mimi nilielewa kwa haraka kuwa damu ya mauti iliyomwagika ilisababisha hayo madhara, na iliachilia mauti kwenye uchumi wa kiwanda.
Kwa hiyo ilinibidi kuomba rehema kisha kuinyamazisha ile damu kwa Damu ya Yesu, na kuitaka Damu ya Yesu inene, mema, nikiwa na maana kuwa ile ya aliyegongwa ilinena au kulia au kuhitaji mauti kwenye uchumi wa kiwanda sasa hii ya Yesu itafuta yale maneno, na kunena Baraka, na mafanikio katika kiwanda.
Kama upo makini, umeshaelewa umuhimu wakutubia hata matukio yaliyofanywa na wengine, kwani yana matokeo makubwa kwako, kieneo, kihuduma, na hata kikazi kama yapo mafungamano, pia hata kindugu kama upo uhusiano, kwani mtoto wa Kaini, na mke wake, wanashiriki matokeo ya adhabu ya baba yao, au mumewe.
Kwa hiyo, tamka kuondoa hayo madhara kwenye ulimwengu wa roho, hata kama huja yajua, Roho Mtakatifu atakusaidia kuomba vyema au kukufahamisha pia zuia yaliyokusudiwa yasitokee.
4. Itisha Urejesho, Upatanisho na Matengenezo, Jambo hili liliharibu kasa maisha ya Kaini, na kwa kiwango fulani maisha ya Mfalme Daudi pale alipomua yule mume wa mke aliye mtwaa, yaani Uria.
Kwa hiyo, maadamu Mungu ameshakusamehe, au kumsamehe muhusika, au rehema yake ipo juu yenu au juu ya eneo husika taasisi na hata kampuni, ni fika unaweza sasa kumuomba Mungu afanye urejesho kama kuna vitu vilivyo haribika, au kupotea, au kufa kabisa, kama uchumi, afya kusumbua na hata migogoro, unaweza fanya urejesho kupitia damu ya Yesu.
Fanya pia matengenezo, kweye vitu vivyo haribiwa, maana mauti hufanya mauti na uharibifu mwingi kwenye mengi, kwa Daudi kulitokea mauaji kwa wanae, Amnoni kuuawa na Absalom, wake au masuri wake, kutezwa na mwanaye, ufalme wake kutaka kupinduliwa, hata yeye kuvunjiwa heshima, “ingawaje kulikuwa na makosa mawili, yaani la kulala na mke wa mtu, lakini pia la mauji ya mume wa mtu, lilichangia mno.”
Pia itisha upatanisho, kama ulikuwa nami vyema katika kitabu hiki utafahamu kuwa Damu ya Yesu inafanya upatanisho nami nimekujuza toka hapo awali kuwa kupitia shuhuli za kikuhani, hapo zamani za Agano la Kale, kuwa ipo dhima ya Upatanisho.
Tatizo hili la mauaji, lina tabia ya kuleta mafarakano kwenye ulimwengu wa roho, na hata kujidhiirisha mwilini, kama ni kwenye kampuni, imetokea ajali au mauaji fulani, au kwenye taifa, kabila na kabila wanapouana, kinachofuata ni watu hao kuwa na uhasama, au kuchukiana, kitu ambacho ni hatari na kinazuia upatikana wa amani sana, maana hali hii huenda kizazi hadi kizazi.
Kwa hiyo jipatanishe na patanisha jamii husika, kupitia Damu ya Yesu, kwa mujibu wa maandiko tuliyoyaona hapo awali kwenye pwenti zilizotangulia humu kitabuni, Damu hii ina uwezo mkuwa, na ukizingatia ni Damu ya kuhani mkuu, na kama tunavyo fahamu kuhani ana dhima ya kufanya upatanisho, wa Agano la Kale walitumia damu za wanyma na hata za ndege, ila huyu Yesu alijidhamini kwa Damu yale mwenyewe, kwa mantikii hiyo nguvu yake ni kubwa mno.
5.Futa Alama ya damu ya Mauti na Adhabu, damu inapomwagika bila hatia, huwa inaacha alama mahali husika kwenye ulimwengu wa roho, kwa hiyo ifute kwa Damu ya Yesu, sio katika aridhi tu, bali hata katika taasisi, kampuni, serikali, na hata, familia au kazi fulani, au mtu binafsi, kanisa na kadhalika.
Lakini pia, kuna kuwa na Alama, ya Adhabu, jambo hili utaliona vyema kwa Kaini;
Mwanzo 4: 15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Unaweza usilielewe jambo hilo kama utachambua hilo andiko kimwili, maana utaona tu, kuwa alama hiyo ni matokeo ya maombi ya Kaini ya kwa Mungu au kama kinga ili asidhuriwe.
Lakini licha ya jambo hilo ambalo kweli lipo, na lipo dhairi, ila ukweli ni kwamba, umwagaji damu, huachilia alama fulani ya kiadhabu, ambayo pia hufanyika kama lango la haribifu.
Ukisoma hapo katika hilo andiko, utafahamu kuwa hiyo alama inanenewa, kuwa kila atakayemua, Kaini, atalipizwa mara 7, kwa hiyo alama yake, ilibeba au ilikuwa na mukutadha wa mauti, uliyotoka na mauti, ambapo tena, una maudhui ya kimauti kwa atakayesababisha mauti.
6. Funga hilo Lango la Uharibifu, Fanya maombi ya Malango, kama huyafahamu tafuta kitabu changu cha MALANGO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
Kwa kifupi, damu isiyo na hatia ya mauti ni lango la Uharibifu, lilisababisha uharibifu kwa Kaini, kwa Daudi, kwa Yoabu, na wenzake, (1 Wafalme 2: 5 Na zaidi ya hayo, umejua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kuimwaga damu ya vita wakati wa amani, akautia damu ya vita mshipi uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake.)
Kwa hiyo nyunyiza Damu ya Yesu kwenye hilo lango, na tamka kulifunga wakati unanyunyiza, fanya maombi haya mfumo wa maombi ya vita.
Pia kama ni mauti au maujia ya kikabla, jamii na jamii, au vuta vya wenyewe kwa wenyewe, huna budi kuhakikisha unayafanya kwa mzigo zaidi, na ukisha maliza achilia amani ya Bwana kwenye eneo, jamii, kampuni, mtu au sehemu husika.
Mwisho, Mshukuru Mungu kwa uponyaji wake, na msamaha, lakini pia nyunyiza, Damu ya YESU, kama ulinzi, juu yako, au katika eneo ulilokuwa ukiliombea, na ifunge kabisha hiyo roho ya mauti isirejee tena, au kuendelea kukaa hilo eneo.
Na kama uliyemuombea, yupo mahabusu, futa kesi kwa Damu ya Yesu, kwani rehema imesamuondolea hatia rohoni, na kama mmekata rufa, tengua hukumu husika kimaombi.
Pia kama yupo gerezani yaani amehukumiwa tayari, na haijalishi amehukumiwa kunyongwa au la! Na hataka kama ni kifungo cha maisha au miaka mingi gerezani, wewe tamka kufunguliwa kwake, maana hii Damu ya Yesu, ina huo uwezo, na jambo hili lipo wazi kimaandiko;
Zekaria 9: 11 Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo na maji.
Cha msingi ni wewe kuwa na imani ya kutosha, kuhusu matumizi ya hii Damu ya Yesu.
Tumia pia Andiko la Isaya 61:1, ili kutangaza uhuru wake, au kujitangazia uhuru wako, kama ni wewe unajiombea;
Isaya 61: 1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
#Dalili au ishara zitakazokujulisha kuwa damu iliomwagika ingali juu yako:
Na Suluhu la kuepukana na mambo haya ni kufuata hatua za kanuni iliyotangulia hapo juu, kama umeshaifutua, rudia tena kufanya hayo maombi, na ukimaliza, fanya maombi ya vita dhidi za hizo roho za mauti la lango lake, na lango la ndoto za mauti ulifunge.
1. Hofu ya Mauti, Ukiona kila ukikaa mwenyewe, au ikifika usiku, au ukilala, ukitembea, ama ukikumbuka hilo tukio, unaingiwa na hofu kubwa, fahamu fika roho ya mauti inakufuatilia, na inatumia lango la hiyo damu.
Ukisoma katika 1 Wafalme 2, utajione mwenyewe kuwa Yoabu, aliingiwa na hofu kama hii, na kukimbilia madhabahuni, ila aliuawa hapo hapo.
Ikiwa na maana hofu inayokuja, inalenga kudai ulipizwaji wa kisasi, kwa hiyo ni vyema kushuhulikia jambo hilo, maana njia kuu ya mauti ni hofu, na dalili kuu pia ni mtu kuwa na hofu, woga, ukiona mtu anyeumwa, nakwambia anasikia kufakufa au ana hofu kubwa sana, jua Mauti imekaribia, kama ni muombaji msaidie.
2. Kuota Ndoto za Mauti, Hali ya kuota upo msibani, makaburini, eneo lenye maiti, ni dalili ya kwamba lipo lango la mauti linalokufuatilia, na ndoto hizo huweza kuua, uchumi, ndoa, kazi, na hata kuleta mauti ya kimwili.
Lakini pia wengine hutokewa katika ndoto na marehemu, na wapo ambao sio katika ndoto bali wazi wazi, huweza kuwa mchana, au usiku, wapo ambao pia huona kivuli chake, kumbuka sio yeye, bali ni mizimu, au mapepo ya mauti yanatumia lango la mauti yake.
Lakini, wengine hufika mahali pa kupiga kelele, hali ambayo inaweza kuwafanya kuonekana kama vile wamerukwa na akili au kuchanganyikiwa, mfano utamsikia akisema, “hao, wanakuja kunichukuwa, hao, hao, nisaidieni, wanakuja,” anaweza kuwataja na majina yao, au kujikuta kitaja aliowahi kuwaua, wachawi wanateseka sana na kifungo kama hiki.
Wasio jua huenda kwa waganga ili kupa msaada, ambapo hatapata suluhu, ila watazituliza, au kupunga hayo mapepo yaliyokaa kwenye hilo lango la mauti ya damu isiyo na hati, lakini madhara yako palepale, na udhibitisho ni kwamba baada ya muda hali hiyo hujirudia tena.
Lakini baya zaidi mashariti ya mganga huweza kudai agano au kafara ya damu, halia ambayo italifanya tatozo kupanuka, na kuwa kubwa zaidi kwani umwagaji wa damu nyingi utaliimarisha tatizo, na kuongeza ukubwa wake, na kuikaza hiyo nira, na kuongeza idadi ya mapepo.
Ila wanao jua, wataitumia njia nilizo zitaja humu kitabuni ili kujiepusha na hili tatizo, wala hawataangaika kutumia sindano za usingizi au kuamini muhusika amerukwa na akili au kalewa kwa pombe na hata kulogwa ama kutupia majini, bali ni mapepo ya mauti, katika lango la mauti la damu isiyo na hatia.
Bali wakati madakitari wanadunga sindano za usingizi, yeye anapabana na tatizo kiroho.
3. Kujiwa na Kumbukumbu za hilo Tukio, kwa wengine wanapo pita eneo husika, au kila inapofika muda fulani, kumbukumbu hizo humjilia, na wengine husikia maumivu kama ya moyo kuuma, ila ni katika eneo la kulia la mwili wake, ukiona hivyo fahamu ni ishara ya roho ya mauti kutumia hilo lango.
4. Uchungu wa Mauti, wapo wanaoua, na wao kujiua, au kutamani kufa, au kuwa na uchungu iliopitiza au huzuni ya mauti.
Yuda Iskariote alipomsaliti Yesu alitamka bayana kuwa ameisaliti damu isiyo na hatia, matokeo yake, ni yeye kumbilia kitanzi;
Mathayo 27:3 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.
Kilichofuata ni yeye kujinyonga, kwa nini? Uchungu wa mauti na huzuni yake;
I Wakorintho 15:56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
2 Wakorntho 7:10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.
(Kama wewe ndie uliyeua, ninakutaka kuomba rehema na sio kujidhuru)
Pia kama tatizo hili lipo kwenye eneo, au nyumba unayoishi au kufanyia kazi, basi kila ukiishi hapo, au kufika hapo, utasikia uchungu huu wa mauti, na dawa yake ni kumwaga Damu ya Yesu kwenye hilo eneo, ukiomba Rehema, kuinyamazisha na kufuta uhalali wake, na kuitaka ile ye Yesu inene mema.
Kama kuna mtu aliwi kuua, au kuuawa, na anawatokea mara kwa mara, bila kujali, ni ndugu yenu alihusika au la, wewe tumia Damu ya Yesu ya Agano Jipya kumwaga juu ya kaburi lake, au mauti yake, na ukifanya hiyo kwa imani, hatawatokea tena milele, nimelifanya hili na nimeona matokeao yake, kwa hiyo sikufundishi nadharia bali ni jambo ambalo ni bayana na hakika.
5. Kuota Ndota ukiwa unakula nae chakula, au kula na watu waliokufa, hii ni ishara kwamba, unaishi chini ya agano la mauti, yaani kuna mtu amekuingiza, au kuliingiza eneo unaloishi chini ya hilo agano au lipo agano ulilowai kuingia lenye mauti ndani yake, yaani lilosababisha damu ya mtu asiye na hatia kumwagika.
Kumbuka unapoenda au mtu anapoenda kwa mganga, na kuhitaji utajiri, kisha kupewa mashariti ya kumchukuwa mtu msukule au kafara ya damu, ni bayana jambo hilo huwa ni agano la mauti au la damu.
Sasa kama umeajiriwa, au kufanya kazi kwenye kampuni kama hiyo, ninakutaka kujitenga na hilo agano, kwa maombi ya Damu ya Yesu, lakini kama umerithishwa au kuinunua hiyo kampuni, ni fika hilo agano unapaswa kulifuta, kwa maombi ya rehema, na yakulifuta kwa Damu ya Yesu, tubia ufanyikaji wake kiundani katika kuomba rehema, na yafanye hayo maombi kwa kuugua.
Kumbuka kama unafanya kazi kwenye hiyo kampuni, au biashara au ni muajiriwa hapo, na kufahamu lipo agano la damu, sija kwambia, ulivunje, ni elewe, wala usijifanye wa kiroho kuko mimi au Roho Mtakatifu, nimekwambia jitenge, ila kama kampuni umeinunua wewe, au kuirithi, hapo unapaswa kulivunja.
Na ukimuona mtu kama huyu, kama ni muajiriwa, mtenge na hili agano kimaombi, kama ni nyumba uliyo panga kitenge chumba chako au eneo unaloishi kwa Damu ya Yesu.
Udhibitisho wa kuwa ndoto kama hizo, za kuota unakula chakula ni ishara ya uwepo wa agano la mauti, upo katika kitabu kile cha Mathayo 26, na Luka 22, katika karamu ya Yesu, Yesu alimega mkate, kumpa kila mwanfunzi wake na mzao wa mzabibu, akisema jambo hilo ni ushirika wa kiagabo, na yale maji ya mzabibu, katika Luka 22:20, na Matahyo 26:28 tunaambiwa ni Agano jipya, lakini ukitazamwilini ni chakula na shurubati au “juice” kwa kingereza.
Lakini pia yawezekana ni agano lilofungwa na babu zako, au baba zako, au jamii ya kwenu, cha muhimu ni wakina nani unaowaota, na mahali gani au moyoni mwako unashudiwa kuwa ni wakina nani.
Usijaribu kupuzi mambo haya, maana yasiposababisha mauti ya kimwili, huweza kuwa ile ya kiuchumi, na hata kiroho, au kiafya ama kihuduma.
Kuna watu wakisha ota hivyo, gafla hali ya kuhudumu au utayari wa kufanya huduma unapotea, au kufifia na hata kufa, au anapoteza ile ladha ya kusoma biblia, kufanya maombi au utumishi fulani, na Roho Mtakatifu ananiambia hata ushirika na wapendwa wenzake huadhirika pia, akiwaona atwakwepa, atakwua mziato kuchangamana nao, na huweza hata kuondoka nyumbani akijua atakuja, cha ajabu hana hata sababu ya msingi uzito tu unakuja moyoni na nafsi mwake na ni hatari zaidi ukiingia hadi rohoni.
Ukisoma vyema hayo maandiko ya karamu ya Yesu utabaini kwamba, jambo lile lililenga kuwa na ushirika pamoja na Kristo, ndio maana hata leoa, tunatakiwa kufanya hivyo, yaani kushiriki meza ya Bwana.
Licha ya hivyo, katika Yohana 6. Tunataarifiwa, ili tuweze kuurithi uzima wa mielele, ni lazima tuule mwili,wake , na kunywa Damu yake.
Kama kwa Yesu lililenga kutupa ushirika pamoja naye, ni bayana hata kwa Shetani linanuia kumfanya huyu mtu kuwa na ushirika na mizimu, au roho za kuua huduma, kiroho ukisha ingizwa kwenye ushirika na nguvu za giza ni dhairi kuwa hali yako ya ushirika na Kristo Yesu, itafifia.
Ndio maana kulitoa pepo lililoingia ndani ya mtu kwa njia ya chakula, au akiota ndoto anakula au kunywa na watu, huwa linasumbua sana, na ukitaka hauweni ya haraka, mnyeweshe huyo mtu Damu ya Yesu ile ya Agano Jipya.
(Lakini pia fahamu sio kila ndoto ya kuota unakula, ni ya kipepo, nyingine huwa na ujumbe wa Mungu, zaidi tafuta kitabu changu cha NGUVU YA NDOTO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.)
NB: Ukigundua eneo au aridhi uliyonunua, kuwa ina Damu ya Mauti juu yake, yaani iliyomwagika bila hatia, ama kitu ulichonunua, au biashara uliyo nayo, gari ulilorithi na hata nyumba, huna budi kuhakikisha kuwa, utafuata hizo kanuni za kujinasua na hilo dhara, kwani hata kwa kiwanja au eneo lilonunulia kwa fedha za usaliti wa Yesu alizopewa Yuda, lilitwa konde la damu;
Matendo ya Mitume 1:18 Basi mtu huyu alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka matumbo yake yote yakatoka.
1.19 Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemu; hata konde lile likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu.
Unaonaje kama wewe ukija kununu kiwanja cha konde la damu na kuishi hapo bila kushulikia hilo tatizo?
Utashanga roho za mauti haziachi kubisha hodi kwenu, nyumba nyingi zenye matatizo, ambazo hazikaliki au zenye mauza-uza, au majini, zina hili tatizo.
Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry #SHARE #SAMBAZA Ili kueneza injili hii Zaidi.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fuatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel
Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA (Ukombozi Gospel)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni