Alhamisi, 5 Septemba 2019

YESU KAMA MTULIZA MAWIMBI AU DHORUBA.

                                                  Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry  #SHARE  #SAMBAZA Ili kueneza injili hii.
Siku moja wanafunzi wa Yesu walikuwa wakisafiri majini ama ziwani na walilenga kufika nga’ambo ya ziwa ili kufanya jambo fulani, lakini walipokuwa katika safari yao, Punde si Punde bahari ili kumbwa na Mawimbi makubwa yaliyoambatana na Upepo mkali.

Hali hiyo iliwapa hofu kubwa mno, Lakini katika mazingira yote hayo hawakukubali kukwama safarini bali walimwamsha Yesu aliyekuwa akipiga usingizi, Hii ina maana kubwa sana na hapo mbeleni nitaifafanua.

Tuyadodose maandiko ili kujionea jambo hili kiunaga ubaga, Soma Marko 4:35-41.  Marko 4:35 Siku ile kulikuwa jioni, akawaambia, “Na tuvuke mpaka ng’ambo.” 37Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi ya kakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye mwenyewe alikuwapo katika Shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu sii kitu kwako kuwa tunaangamia?” 39 Akaamka, akaukeme upepo, akaiambia bahari, “Nyamaza utuliye!” Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
Hapo ninapata funzo kubwa naamini nawe unapata jambo la kushangaza sana; ya kwamba mtu huyu tuliye naye sio wakufananishwa kwani anaweza kutuliza mambo yaliyoonekana kuwa ni magumu maishani mwetu na wewe sasa jenga imani hiyo na usisite kumuamsha ili atulize yanayokusonga. Ili na kwako kuwe, “SHWARI KUU”

Maandiko hayo yanatuonyeshe dhairi shairi kwamba YESU alikuwa na malaka juu ya mawimbi, na upepo, na ukitazama kiumakini utagundua kuwa mamlaka hii tulishapewa tangu enzi za umbaji wa ulimwengu Mungu alipowaambia Adamu na Hawa kuwa amewapa uwezo wa kutawala ndege wa angani, (Mamlaka dhidi ya Anga), Samaki wa Baharaini, (Ni Mamlaka juu ya bahari), Na Wanyama wote wa Nchi kavu, (Ikiwa ni mamlaka juu ya Aridhi) pamoja na hayo mamlaka hiyo inaambatana na vitu vilivyopo sehemu husika.

Kwa hiyo adui mkubwa aliyewafanya wasiweze kuitumia hiyo mamlaka ni kwanza ni Uelewa wao, hawakulijua hili, maana walikuwa na Yesu, ni kweli ila hawakujua kama anauwezo wa kutuliza hadi mawimbi na upepo, ndio maaana baada ya mujiza huo wanashangaa,
“.. Wakaambiana, ‘Ni nani huyu, hata upepo na bahari humtii? ” Mariko 4:41. Fikiri kwa kina kwamba wapo na Yesu miaka ya kutosha ila bado hawakufahamu mamlaka/uwezo aliyo nao, kuhusu tatizo walilokuwa nalo.

Na wewe yamkini umeokoka ila hujafahamu uwezo wa Yesu kuhusu dhoruba zinazokukumba, usimwamshe Yesu katika mtazamo wa wale wanafunzi walio mwamsha ili wateseke wote na Yesu katika kupamba na ile hali kwani hawakutarajia YESU kutenda lile, ndio maana walimwambia hivi,
“..Sii, kitu kwako kuwa tunaangamia,” Mariko 4:38.  Katika Luka walitumia maneno; Bwana mkubwa huku wakiita zaidi ya mara moja. Usipotazama andiko hilo kwa jicho la uchunguzi hutaiona hii fikra ya wanafunzi, ila iinajidhirisha pale wanaposhangaa uweza wake mara baada ya mujiza kutendeka hali inayobainisha bayana ya kwamba kumuasha kwao hakukuwa na taraja ya mujiza ule bali kulikwa na mtazamo wa “tupambane sote.”
Nataka kukujengea Imanii ili utambue ya kwamba hilo unalolipitia Yesu analiweza kwa shabaha ya kukataka kuacha kuwatazama wanadamu ambao hawatakusaidia badala yake wengine wataishia kukusema ama kukusengenya hali itakayokukwamisha kiroho kwani maneno hayo yanatakumiza bure badala yake unapaswa kumtaza YESU huku ukitambua ya kwamba ndani yake ipo Mamlaka na itumiye kama alivyokupa ili utulize hayo mawimbi na upepo kwani Yesu aliukemea na wewe kemia hiyo misukosuko kwenye ndoa yako, uchumi familia au huduma sasa.

Jambo la pili lilikuwa ni WOGA, ukiogopa ni dhairi kwamba Imani yako itayumba hali itakayokufanya kushindwa kuitambua ama kuitumia mamlaka uliyopewa na Yesu Kristo juu ya hayo matatizo.
Tuone mafundisho haya ya Uoga kwenye ujumbe huu kama nilivyokudokezea kwenye kitabu changu cha Namna ya Kuishi Wakati wa Majaribu au Mapito katika Ukurasa ule wa 31 na kuendelea.

“….Natumai sasa utakubaliana nami vyema pale Yesu alipokuwa na wanafunzi wake katika boti na mawimbi ya kaja wakaogopa Yesu aliwauliza “Imani yenu iko wapi” Luka 8:25. Akiwa anamaanisha kuwa wameogopa na hofu ilimdhirishia Yesu kuwa tatizo ni Imani, katika swala hili;Tutazame tena Mathayo 8:26 Akawaambia “mbona mmekuwa waoga, enyi wa Imani haba” Waoga alafu wa Imani Haba , haba maana yake chache,Kwenye luka anataka kujua walipo iweka imani yao, hapa anawaambia kuwa Imani mliyo nayo ni chache, Joshu anawaambia “wala msiwaogope”

Twende kwenye Marko tuone Mfano ama stori hiyo hiyo ya dhoruba ziwani. Marko 4:40 Akawambia , “mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado ?”. Hapa Yesu anauliza Uwoga pili hamna Imani bado jumlisha na hoja ya luka na Mathayo changanya na hiyo ya Marko (“Imani yenu iko wapi” + “mbona mmekuwa waoga, enyi wa Imani haba” na “mbona mmekuwa waoga? +Hamna imani bado ?”)
Kuna kitu nilikuaidia kukudokezea hapa mbeleni nacho ni hiki, Yesu alipokuwa amelala sio kwamba hakujua kitakachotokea, La! Asha!! Alijua fika, ila alikuwa akihitaji kuona au kupima ama kufahamu kiwango cha wanafunzi wake kumjua, pili Uwezo wao wakukabilina na matatizo na tatu kiwango cha Imani yao. Ndiposa alipoamka aling’aka hali iliyoonyesha kuwa amekasirshwa na matokeo ya mtihani uliowakumba.

Nakudhibitisha hilo tazama kwa kina maneno yake katika vitabu vyote vitatu, 1. Imani yenu iko wapi 2. enyi wa Imani haba 3. Hamna imani bado ?”).
Kwa anayetazama mambo kwa jicho la tatu kama mimi, kuna kitu anajifunza hapo, na miongoni mwacho ni hiki cha kiwango cha Imani na Sehemu ilipowekwa, hali inayomaanisha kuwa ukimya wa Yesu ulikiwa ukiashiria usimamamizi wa Mtihani.

Walioenda shule walao hadi chekechea wanafahamu kuwa sura ya Mwalimu wakati anafundisha ni tofauti na ile wakati akiwa anasimamia mtihani, na ujio wa sura ya wakati wa kutoa matokeo unategemea na ujibuji au ufaulu wako wa mtihani. Ukifeli utaona mikunjo ya ndita na hamaki ila ukifaulu utaona furaha na tabasamu mwanana, linaloambata na jicho angavu .


Na yamkini umekuwa katika wakati kama huo, wa Yesu kulala kwenye Shetri, Madamu umembeba mzima mzima kama alivyo, yakupasa sasa kuhakikisha unamuasha kwani kwa kuukemea upepo na mawimbi kwa jina lake na sio kwa kupiga yowe za kuogopa kuzama huku ukimwambia kuwa mbona unateseka na mapito na Yeye yupo kimiya, akiamka katika hali hiyo atanga’aka juu yako na kukuuliza ulipoiweka imani yako ila ukiukemea upepo na mawimbi ataamka na kukupiga tafu huku akikupongeza na hakika hatakuita wa IMANIA HABA, MUOGA ama HUNA IMANI bali atakupongeza kwa kukupa “BIG FIVE” ikiwa ni ishara ya kufaulu mtihani kwani ukimya wake ulikuwa ni sura ya kusimamia mtihani.

Natumai umependezwa na ujume huu uliokujia wakati muafaka na tayari moyoni mwako umeshaazimia kuchukua hatua ambazo miongoni mwazo ni maombi ya kufunga na kuomba yatakayokuwa na taswira ya maombi ya vita na yenye mamlaka ilengayo kuukemea upepo na dhoruba. Tumia pia maandiko ya mamlaka ikiwemo lile la Petro alivyokabidhiwa mamlaka pale kwenye Mathayo 16:19, Mathayo 10:1, Luka 10:19 pia Marko  16:16-18, huku ukijua kuwa Yesu amekabidhiwa vyote na kama ndivyo ukiviitaji atakupa tena na zaidi; Mathayo 28:18. Usiyasahau na yale ya umbaji kwenye mwanzo.
Niombe kwa Mungu ili nifundishe mapema somo langu liitwalo, “NAMNA YA KUTUMIA MALAKA KIBIBILIA.” Sio kwamba Mungu wa leo hatendi Ishara na miujiza kama enzi za uandishi wa Bibilia, anatenda tena yamkini na kuzidi sema shida ingalipo kwetu sisi ambao hatujui namna ya kuzitumia hizi malaka maana hata wakina Petro walikuwa nazo ila hawakujua nammna ya kuzituamia na baadaye Petro na Yohana walipojua ndipo yule kiwete waliyekwepo kwenye mlango mzuri wa kanisa ama hekalu alipopona.  Tuonane kesho Swaiba.

Usikose makala nyingine ya NYUMA YA MLIMA.
Kama hujaokoka na unataka kuokoa tafadhali fwatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KAUMINI KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com  Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com   #UkomboziGosple  #MwalimuOscarSamba
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundila Fb, ili kuupta habari hizi kwa haraka, zaidi. Ug Ukombozi Gosple,                                                                                       PAGE: https://www.facebook.com/Ug-Ukombozi-Gosple                                             
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Endelea kusoma makala nyingine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni