Jumamosi, 7 Septemba 2019
MWAMBA UTOWE MAJI KWA AJILI YAKO.
Wana wa Israeli walipokuwa wakisafiri kule jangwani na kuelekea Kanani walipita katika hali ngumu sana kiasi cha kuishiwa au kukosa maji ya kunywa, ila Bwana aliwafanyia mujiza kwa kuwatokezea maji huko jangwani !
Aliupasua mwamba napo maji yakawabubujikia; Zaburi 105:41 Akaufunua mwamba, kukabubujika maji, Yakapita pakavuni kama mto.
Nawe najua unapitia mahali pagumu, wala sio haba, ila huyu Mungu aliyetenda kwa Wana wa Israeli ni ombi langu atende na kwako siku hii ya leo, akufanyia mujiza kutokana na haja ya moyo wako, akufanyie maji, akupe mana yaani chakula cha mbinguni, wewe amini tu na umwamini Bwana maana Yeye ni mwaminifu wala hasemi uongo, atakutokelezea tu !
Ni ombi langu kwa Bwana maji yakutiririkie siku hii ya leo !
Naam, wakati ukipokea mujiza wako huo muhimu naomba unipe nafasi ya kuuliza swali hili muhimu moyoni mwako ! Je, umeokoka; Na ukifa leo au Yesu akija sasa utaenda wapi; Ama ni ipi hatima ya maisha yako ?
Kama hujaokoka na unataka kuokoka tafadhali fuatisha nami kwa imani sala hii ya toba, Sema: Mungu Baba, nisamehe, nimetambua ya kuwa ni mwenye dhambi, sasa ninatubu, ninakuamini na kukupokea moyoni mwangu kama Bwana na mwokozi wa maisha yangu, nakuomba ufute jina langu kwenye kitabu cha huku na uliandike sasa kwenye kitabu cha uzima wa milele, Ameni.
Hongera kwa kuokoka, na tafuta sasa kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, na ujitambulishe kuwa umeoka hivi karibuni ili wakulee zaidi kiroho, kwa mawasiliano au sadaka M-PESA, maombi na ushauri, ni +255759859287, E-Mail: ukombozigospel@gmail.com, Tupo Arusha Tanzania. Na Mwalimu Oscar Samba
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni