Jumamosi, 28 Septemba 2019

UWEKEZAJI WA ULIMWENGU WA ROHO KATIKA KIZAZI AU UZAO.

Yoshua 4:21 Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini?
22 Ndipo mtakapowaarifu watoto wenu mkisema, Israeli walivuka mto huu wa Yordani, kwa njia ya nchi kavu.
Mahali: Kanisa la TAG Mudio Masama, {Jerusalem Temple} Kilimanjaro, ndilo liiloasisiwa na Askofu Lazaro na kuwa kitovu cha Uamsho maeneo mengi Tanzania:
Tarehe: 27 na 28/9/2019. Na Mwalimu Oscar Samba.

Utangulizi:
Unapoona neno uwekezaji maana yake ni kunuia kupata faida, au kuna kitu kinapandwa, au kuwekwa, chenye nia ya kuzalisha ili kumpatia mwekezaji faida.
Katika uwekezaji kuna mwekezaji, eneo, kitu kinachowekezwa/bidhaa, na soko au walaji, na alikadhalika kiroho wawekezaji ambao ni aidha Mungu au adui Shetani, wote hawa eneo lao ni duniani wakinuia kumpata mwanadamu.


Huweza kutumia mtu mmoja kwa lengo la kuwapata wengi, kama adui alivyomnasa Adamu na mkewe na kuupata ulimwengu wote, kisha Mungu Baba kumtumia Yesu na kuuvuna ulimwengu !

Leo hii Shetani amekuwa akiwekeza kwenye vizazi au uzao akinuia kuipata jamii, na amekuwa akipingana sana na uwekezaji wa Mungu katika jamii kupitia watumishi wake, mfano katika kuzaliwa kwa Musa na Yesu alijaribu kuwaangamiza akijua kupitia mtu mmoja ni jamii kubwa kiasi gani itaokolewa !

Kwa hiyo ujumbe huu unanuia kukujengea kiu na shahuku ya kuhakikisha unawaombea watu waliowekwa na ufalme wa Mungu kuhakikisha awadhuriki na adui, maana hata Musa alimuhitaji mamaye aliyemjengea kisafina na dadaye aliyekuwa akimlinda !
Karibu tuanze ujumbe:

1. Imani huwa Inaridhisha, (adui huwa anajipanga kuuadhiri urithi huu,) 2 Timotheo 1:5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.

Wewe kama mzazi na Mtumishi ama mtu aliyeokoka akikisha watoto na wajukuu zako au washirika wanapata urithi huu wa kitu cha kiungu, adui naye amekuwa yupo kazini kuhakikisha watoto wa wateule wanaiacha imani au wanaikana ama hawakai katika mstari ama njia ya wazazi wao, Paulo anaina imani ya bibi yake na mama yake ndani ya Timotheo, sijui kwako kama tunaiona hiyo imani kwa wanao ? Au wajuku zako ! Fahamu kuna siku ya kutoa hesabu kwa Mungu kuwa nilikupa hawa na wale mbona hukutimiza wajibu wako kama ipasavyo !

2. Jifunze Kuombea Watumishi Waliowekwa katika Vizazi Vijavyo na Vya Sasa, (usiombee tu wanao bali ombea na watumishi walioandaliwa kwa ajili ya kuwavusha.)

(Adui amekuwa akihakikisha anawadhibiti au kuwazuilia.)
Mfano A. Musa; Kutoka 1:15 Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;

16 akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.
17 Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.

Kutoka 21-10, Inaeleza usalama au jinsi Mungu alivyomuifadhi:

NB: Kuchelewa kuitika kwa Musa ndiko kulikokuwa kuchelewa kutoka Misri kwa Wana wa Israeli, Mwanzo 15 inaonyesha jinsi ilivyopangwa miaka 400 ila walikaa miaka 430, maana Musa alikimbilia Midiani miaka 40. ( Ibrahimu angejua hili angemuombea na Musa, wazazi na jamaa yake pia na Musa.)

Mfano B: Uzao au Kizazi au Wana wa Yakobo walitegemea Utumishi wa Yusufu; Mwanzo 46:31 Yusufu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, Nitapanda mimi nimpashe Farao habari; nitamwambia, Ndugu zangu, na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa katika nchi ya Kanaani, wamenijia.

Mfano C: Uwepo wa Waamuzi kama Samsoni, Deora na Gideoni ilikuwa ni ishara ya ukombozi kwa kizazi husika !
Mfano D: Ukombozi wa Ulimwengu ulitegemea ujio na kusimama kwa nafasi vyema kwa Yesu, adui alijipanga kumuangamiza ili kuzuia uzao husika usipokee uponyaji:

Mathayo 2:12 Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.
13 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.

14 Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri; 15 akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwanangu.

16 Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi.

17 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, 18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.
19 Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, 20 akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.

21 Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli.
22 Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya, 23 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.

Natumai umeanza kupata picha ninayonuia uipate sasa ! Kwamba upo umuhimu wa kuhakikisha sio unamuombea tu mwanaoa, bali uwaombee na wakina Yesu, na Musa walioandaliwa kwa ajili ya kuwavusha watoto wako !

Maana adui amekuwa akihakikisha anawakwamisha ! Ndiposa kwa Musa aliweka vizingiti kama kile cha kuhakikisha wana wa kiume wanauawa, kwa Yesu ni vivyo, sasa ashukuriwe Mungu aliyehakikisha Yesu anatoroshwa na baba yake, sasa huwa ninauliza ingekuaje kama ndoa ya Yusufu na Mariamu ingalikuwa na migogoro ?

Ikupe kufikiri kwa kina kuwa adui anapoleta migogoro kwenye ndoa uwe na hakika kuna Yesu au Musa au Yusufu wa Yakabo anawindwa hapo, maana ndugu wa Yusufu na Daudi ndio waliofanyika kikwazo katika safari yao !

Wakati mwingine hana shida kwa baba na mama kuachana ila anashida na Yesu, kwa hiyo anajua babaye ndie anayetakiwa kumlinda na kumkimbizia Misri na anafahamu akifanikiwa kumfanya kuwa mlevi, kumfanya kuwa mpiga mama basi atatimiliza adhima yake !
Anajua Miriamu ndie mwenye jukumu la kumlinda mtoto, kwa hiyo akimfanya kuwa dada asiyetulia nyumbani wala asiyesikiliza wazazi ni amefanikiwa kumkwepesha jukumu la kumlinda !

Hii ikupe kuyatazama mambo ya kifamilia kwa jicho la kina !
Kuna mambo kama vile ya mimba kuharibika, wakina mama kutoa mimba, au wakina baba kukataa ujauzito, uwe na hakika ni Musa, na Yesu wanawindwa !

Kama vile Mungu alivyojisimamishia wakina Anna binti Fanueli, na Simeoni, ambao katika Luka wanaonekana dhairi walibebeshwa mzigo wa kumuombea Yesu, nawe simama katika hiyo zamu kumuombea aliyewekwa kwa ajili ya uzao wako, wasasa na ujao, aliyewekwa pia kwa ajili yako !

Msisitizo: Ukijua Mwanao au Mshirika wako, ama Mtoto wa mshirika wako amewekwa kwa ajili ya zamu ijayo yaani ni mbeba maono, basi hakikisha unasimama kwenye nafasi yako vyema kama Mariamu na mamaye Musa, kama Yusufu babaye na Yesu .

Na wewe kama ndie mbeba maono hakikisha unavuka vikwazo kama Yusufu, wazazi msifanye kosa la wazazi wa Daudi.
3. Kunapokwepo na Uzao Unaomjua Mungu Leo, Usiishi ukijua Uzao ujao Utakuwa vivyo, Bila Wewe Kuchukuwa Hatua.

Adui amekuwa akiwekeza kisiri kwa watoto ambao wameukuta wokovu, wamezaliwa kwenye neema na mara baada ya wazazi wao kuondoka hujikuta wakimuacha Mungu !
Mfano A: Mfalme Sulemani: 1 Wafalme 11:6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.

7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.

8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.
9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,
10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.

11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako.
Huyu babaye alimcha Mungu kwa viwango vikubwa sana, ila mwana alikuja kuanguka !

Mfano B: Uzao wa Kitabu cha Waamuzi; Waamuzi 2:10 Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
11 Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.

12 Wakamwacha Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.

13 Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.
Tazama Baba au Babu na Bibi Zao: Yoshua 24:16 Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache Bwana, ili kuitumikia miungu mingine;
17 kwa maana Bwana, Mungu wetu, yeye ndiye aliyetupandisha sisi na baba zetu kutoka nchi ya Misri; kutoka nyumba ya utumwa; naye ndiye aliyezifanya ishara zile kubwa mbele ya macho yetu, na kutulinda katika njia ile yote tuliyoiendea, na kati ya watu wa mataifa yote tuliopita katikati yao.

24 Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, Bwana, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii.
Huwa nikifika hapo siachi kusononeka, maana inaumiza kuona kinainuka kizazi ambacho hakimjuia Mungu kabisa kana kwamba hakuna aliyewahi kutembea naye huko nyuma ! Hakimjuia Mungu wa baba zao kabisa !

Huwa ninaitazama biblia kwa jicho la tofauti sana ! Kuna maeneo Paulo Mtume alihubiri injili huko, ikiwemo Rumi na Asia kama India na kadhalika, na watu waliipokea kwa kasi sana, ila leo hii kumejaa masanamu na upagani kama vile ni maeneo ambayo injili haikuwahi kuhubiriwa kabisa !

Yesu na wanafunzi wake waliiteka Yerusalemu na viunga vyake ! Samaria alipita na kukatokea mtikisiko mkubwa, naye Filipo akafanya vivyo ! Ila leo pita huko utazani ni kama vile injili haikuwahi kufika huko kabisa ?

Nilikuwa na msikiliza muhubiri mmoja akawa anauliza ipo wapi ile Marekani au U.S.A iliyoitikisa dunia kwa kutoa wahubiri wakubwa na kuwa kitovu cha umisheni ulimwenguni mwote ?
Siku za nyuma nchi ya Korea Kusini pia ilikuwa vivyo ! Lakini leo wanatoka wahubiri Afrika na Wamisheni kuelekea huko na nchi nyinginezo ?

Hili ni matokeo ya kizazi au vizazi kumuacha Yesu, ama ni matokeo ya kuibuka vizazi visivyomjua Mungu wa Bill Graham au Bonke, ama Maritini Lugha King !
Sasa nawe uwe makini leo hahakikishi kuwa uzao ujao hutamjua Mungu wako ! Adui hupambana ili kutuzuilia tuaimjue Mungu wa Askofu Lazaro, Askofu Mosesi Kolola, wakina Kuselya na kadhalika !
Wewe kaa katika zamu yako, uwaombee kwa mzigo na kadhalika !

4. Jifunze Kumkabidhi Mungu Uzao wako Kiagano: Mfano A; Yoshua 24:15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.

25 Basi Yoshua akafanya agano na wale watu siku ile, akawapa amri na agizo huko Shekemu.
26 Yoshua akayaandika maneno haya katika kitabu cha torati ya Mungu; kisha akatwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko, chini ya ule mwaloni uliokuwa karibu na patakatifu pa Bwana.

27 Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya Bwana aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu.
Mfano B: Zaburi 89:3 Nimefanya agano na mteule wangu, Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu. 4 Wazao wako nitawafanya imara milele, Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.

27 Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia. 29 Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.

30 Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu, 31 Wakizihalifu amri zangu, Wasiyashike maagizo yangu,
32 Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo. 33 Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye, Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo.
34 Mimi sitalihalifu agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu. 35 Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu, Hakika sitamwambia Daudi uongo,
36 Wazao wake watadumu milele, Na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu. 37 Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi aliye mbinguni mwaminifu.

Unapoingia na Mungu agano ni unawafunga wanao kamba, au mwenzi wako, ni unamuingiza katika nira, au kifungo, ambacho ni kifungo kitakatifu !

Ni kumpa Mungu uhalali wa kukaa katika jamii au familia yako, ni kumkabithi Mungu utawala wa hiyo jamii, maana hata kwa Daudi japo kulitokea ukengemfu Mungu hakuwaacha kabisa, bali alikiacha kiti hicho, na uzao wake aliurejesha ndipo Kristo akatokea hapo kama chipukizi !

Wanao hata wakija kuiacha neema Mungu atawarejesha, atakutana nao hata kwa fimbo kama wakiisukumia mbali rehema yake !

5. Jifunze Kuwaombea Wanao au Wana wa Washirika au Washirika na Kuwabariki,  na Kuwatolea Sadaka; Mfano A; Ayubu, Ayubu 1:4 Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao.

5 Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.

Waombee, lakini pia wekeza au jifunze kuwatolea sadaka madhabahuni, unapotoa mwambie Mungu ninawatolea wanangu, warehemu, pia sadaka hii nikupayo ni ishara ya kukupa hawa watoto, kaa mioyoni mwao, na andika sheria yako katika mioyo yao !

Sijui kama uliwahi kulisoma hili andiko;Zaburi 118:27 Bwana ndiye aliye Mungu, Naye ndiye aliyetupa nuru. Ifungeni dhabihu kwa kamba Pembeni mwa madhabahu.

Dhabihu ni sadaka, na tunaambiwa kuwa unaweza kuifungia madhabahuni unapoitoa kwa aina hii ya imani ! Na sadaka inabeba moyo wa mtu !

Maana imeandikwa kuwa hazina yako ilipo ndipo ulipo na moyo wako ! Kwa hiyo ukitaka moyo wa mwanao uwe madhabahuni pa Bwana jifunze kumshikilia hapo na sadaka ! Ile sadaka ya shukurani au ya kumuweka mtoto wakfu anapozaliwa mara nyingi Mungu hutamani iwe ya aina hii !
Mfano B; Ibrahimu kwa Isaka, na Isaka kwa Yakobo a Yakobo kwa wanae, Mwanzo 49.

Mfano C; Musa kwa Wana wa Israeli; Kumbukumbu la Torati 33:1 Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake.

7 Na baraka ya Yuda ni hii; akasema, Isikize, Ee Bwana, sauti ya Yuda, Umlete ndani kwa watu wake; Alijitetea kwa mikono yake; Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake.

11 Ee Bwana, ubariki mali zake, Utakabali kazi ya mikono yake; Uwapige viuno vyao waondokao juu yake, Na wenye kumchukia, wasiinuke tena.
12 Akamnena Benyamini, Mpenzi wa Bwana atakaa salama kwake; Yuamfunika mchana kutwa, Naye hukaa kati ya mabega yake.

Baraka huzuilia urithi mbaya, baraka ambazo Mungu yupo ndani yake huwa na hofu yake, na katika kubariki mambo yao ya mwilini changanya hapo na hali yao ya kiroho kwa kuachilia utawala wa Kiungu maishani mwao ! Ukisoma Mwanzo 49, utaona kitu kama fimbo ya enzi haitaondoshwa, kitu kama amemfunga mwanapunda, na wasomaji hujua maana yake, maana Yesu naye alikuja kumfungua mwana Punda na kupita naye Yerusalem !

Fimbo ya enzi iliwakilisha utawala wa kifalme ambao ndio huo wa Kristo Yesu, ambao wadumu enzi na enzi !

6. Jifunze Kuhusia na Kuwaasa wana Wako; 1 Mambo ya Nyakati 28:9 Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa Bwana hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.

Waambie maneno mazuri wape nasaha toshelevu, waonye, wakemee na wataadharishe ! Hakikisha unakuwa na muda na mwanao au mjukuu wako !

Kunena naye, sio jukumu la mchungaji au mwalimu wake wa watoto kanisani tu bali na lako pia ! Nasaha hizi ndizo zilizokuja kuugeuza moyonwa mfalme Sulemani baadae na kutuandikia kitabu cha  Muhubiri kilichojaa toba na majuto ya kukengeuka kwake !

Maana katika Mithali hutujuza jinsi alivyokuwa mwana wa pekee wa mamaye na mshika sheria za babaye ! Hii ikupe kupanda mbegu ya nasaha, maana haitakufa itamea tu, hata akija kuyumba haya maneno yatazidi kuimba na kupiga kelele ndani yake !

Kuliwahi kuwa na mwanamziki mmoja wa kidunia ambaye alikuzwa katika wokovu, na kulelewa vyema kabisa, ila baadae alikuja kuacha njia na kuhamia duniani, ila alipokuwa mzee na kuugua karibu na kufa alituma mtu na kuitiwa mtumishi ikiwa na maana ya kuikumbuka njia aliyolelewa nayo ! Na alikufa katika Bwana ! Sasa wewe wekeza katika kulipanda neneo au mbegu njema !

7.  Iruhusu Nafasi ya Mungu Mioyoni Mwao; Ikiwemo Kuwafundisha, wajengee pia fikra za kumtegemea Mungu; Isaya 54:13 Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.

Pia kumshauri; Zaburi 32:8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
Ni muhimu kujifunza kumfunua Yesu moyoni mwa mwanao, au mshirika wako, ikiwa na maana kwamba akuwe akimjua Mungu wako,asikuwe akiona kama hizo ni nasaha au mahusia ya kawaida tu, bali amuone Mungu ndani yake ! Akuwe katika hofu ya Mungu, yaani uchaji na sio hofu ya kukuoga wewe tu ! Bali amuohofu na Mungu pia !
Ujumbe huu pia limeurekodi kwa njia ya Sauti kwa hiyo waweza jaribu kuutafuta mtandaoni kama nitakuwa tayari nimeshauweka !

Ila nina neno moja kwako muhimu sana ! Maana ni jambo jema na la busara kujua hatima ya maisha yako kama ukifa leo, au Yesu akija sasa hivi utakuwa u mgeni wa nani wewe ! Ni muhimu roho yako na maisha ya wana wako kuwa salama kwa kumpokea huyu Yesu !
Kama hujaokoka na unataka kuokoka tafadhali fuatisha nami kwa imani sala hii ya toba, Sema: Mungu Baba, nisamehe, nimetambua ya kuwa ni mwenye dhambi, sasa ninatubu, ninakuamini na kukupokea moyoni mwangu kama Bwana na mwokozi wa maisha yangu, nakuomba ufute jina langu kwenye kitabu cha huku na uliandike sasa kwenye kitabu cha uzima wa milele, Ameni.

Hongera kwa kuokoka, na tafuta sasa kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, na ujitambulishe kuwa umeoka hivi karibuni ili wakulee zaidi kiroho, kwa mawasiliano au sadaka M-PESA, maombi na ushauri, ni +255759859287, E-Mail: ukombozigospel@gmail.com, Tupo Arusha Tanzania. Na Mwalimu Oscar Samba. Zaidi tembelea, www.ukombozigospel.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni