Jumatano, 2 Oktoba 2019

UJUZO WA HISTORIA YA UAMSHO WA MASAMA KAMA INAVYOSIMULIWA NA Afuraeli Munisi, Sehemu ya 5.

Anasema kuwa sio kwamba kanisa la TAG lilianzia hapa, lilikuwa limeshaanza huko Mbea hapa lilifika huo mwaka 1959, walianza kuokoka huko ni Askofu Lazaro na Jakobo Ringo ni mpare kutoka Same, walikutana na Askofu huko Arusha na mmeshenari Paulo Brutoni. ( Kama tulivyojionea hapo awali !)

Sikumbuki tarehe wala mwezi ila ni mwaka huo baada ya wao kuanza kushuhudia huko Arusha kidogo,hapo awali alikuwa ni mshirika wa KKT, na mama yake na baba yake pia, baba alikuwa ni mzee wa kanisa mtunza hazina wa hiyo dini, anaendelea kusimulia Mzee Munisi ! ( Ambae kwa sasa ni mzee wa miaka 83 na mke wake ni 72, aitwae Anarabi Afuraeli Munisi, ambao kwa kweli wamezeeka na mzee hapa huongea kwa utulivu maana pia sio buheri sana wa afya.)
Tunaendelea !


Walipokuja ndo walikuja
na huyo mmishenari, huyu ndie mjenzi wa kanisa la TAG Calivary Temple, wakashuhudia, na watu wa Lutheri wakaona ni jambo la ajabu maana walimuona ni mtoto wa hapa hapa, imekuaje, alipoanza maombi na kushuhudia wakamwambia hilo sio dhehebu letu umekuja na lingine ! Ndipo akaanza kujitenga, ilikuwa ni vurumai anakazia mzee Munisi, na kuendelea kutanabaisha kuwa.

Ikabidi utawala wa kimangi uingilie kati, utawala uliokwepo kwa wakati huo ! Sasa wale Walutheri wakaenda kwa Mangi kulalamika ni kwa nini huyu kijana anatuvurugia dini yetu ikawa ni mashitaka kabisa sasa !
Sasa kwa kuwa walipokuwa wakishuhudia kwa wakati uke wakristo walikuwa wakiongezeka sana, hasa vijana, wakifanya maombi, nguvu za Mungu zilishuka na walikuwa wakiwafanyia fujo ila wakashindwa !
Na watu walikuwa wakisema huyu ndie Mungu wa kweli, na watu wa dini hiyo kuingilia na kusema wewe sasa Imanueli umetoka hapa juzi juzi unataka kuwa mchungaji zaidi ya wachungaji wetu !
Ikawa vurumai, na hata wakienda mahakamani walikuwa wakienda kwa kuimba !

Kitu ninachokumbuka siku moja waliingia kanisani na kumkuta Yakobo na kumpiga sana, wakimkanyaga na mateke, lakini hakufa !
Na Yakobo alisema nipigeni tu maana hata Stefano aliuawa nami nitaifanya kazi ya Mungu sitaacha !
Sasa mkristo mmoja alikuwa akitwa Peneli Shenesario, ambae amekuwa mzee wa kanisa karibu miaka 50 kwenye kanisa hili, amezeeka amekufa akiwa mzee kwenye hili kanisa !

Sasa huyu ndie aliyejitolea akitoa eneo ambalo alikuwa amepewa na baba mkwe wake, alisema mimi natoa tujenge kanisa hapa, ( wakati huo tulikuwa tunaabudu kwenye majumba ya watu tu, tukifukuzwa tunaabudu kwa watu tu,) ndipo waliposema tujenge hapo, ndipo fujo ikatoke,wakafukia msingi, wakataka kumpiga na kuvunja vunja gari lake, akakimbia yaani mmishenari !

Ndipo mkubwa wa kanisa la KKT Alifanyo Salema akiwa ni mchungaji mkubwa ama kiongozi wa wachungaji au mwangalizi wa hili eneo, japo kulikuwa na Askofu Stefano Rafaeli Moshi, wa kanda hii, ndiposa mchungaji Salema akaitisha kikao cha kanisa na wakiristo wote wakaitwa, na alisema neno moja tu alisema !
" Ninyi mnaowapiga hawa watu ni watoto wenu, maana imeandikwa kipindi cha mwisho Roho atawashukia watu, imeandikwa kuwa Roho atawashukia watu hamsomi maandiko ninyi ! "

Na kuendelea kusema, " kama hii ni kazi ya Mungu na kama wokovu huu umetoka kwa Mungu, na kama wameokoka kikweli kweli hamuwezi kuzima hii kazi hata muuwe mtu, hata muuwe watu kumi."
Akasisitiza na kudokeza kuwa, " Kule Yerusalemu walimpiga Stefano na kumpiga na kumua kwa mawe na ndipo injili ilipopamba moto."
Aliongeza, kuwa, " kama ni kitu cha Mungu hamuwezi kukizima ninyi, kama sio cha Mungu kitakufa chenyewe."

Mzee Munisi anasema kuwa Mchungaji Salema, aliongeza vivi, " Kila siku napata mashitaka mmepiga mtu, mmepiga acheni."
Anasema Wakristo walikasirika kweli kweli, na kusema unatuzuilia kupiga watu ama kuua unataka kuungana nao ! Anadokeza kuwa wengi walikufa moyo.

 Ila vijana waliokwepo hapo waliokoka walifurahi na kusema huyu ndie mchungaji aliyeokoka ! (Baada ya hapo Mchungaji Salema ambae ameingia katika historia njema ya wokovu wa Uamsho wa Masama alifanikiwa kuzima fujo zile kabisa.)
Baadae Mwaka wa 1960 ndipo mchungaji Wilson Kimaro aliokoka, ambae ndie binamu yake na Askofu, na kujitolea eneo lake na kujengwa hapo kanisa !

Alipookoka, akapata mke na harusi kufungwa hapo hapo kanisani alipotoa toa pajengwe kanisa na alioa mke ambae alikuwa ameokoka aitwae Nalindwa kutoka upareni.
Tulianza katika nyumba yake,sio kwamba kelele na mafuriko yameisha la ! Bali yaliendelea tulipokuwa tunataka kupanua kanisa !
Siku moja alipigwa mmishenari Brutoni na kijana mmoja alie mdogo wangu alipigwa ringi la kichwani, na kuvuja damu nyingi.

Walitaka kulipindua gari la mmishenari lakini aliliendesha kwa kasi, saa hiyo Askofu Lazaro wakamkimbiza ili wa muuwe, wakamkimbiza mpaka akafika Polisi, na polisi kipindi hicho ilikuwa mbali sana ni ile ya Sanya, alienda na Jakobo !

Polisi wakaja kesho yake na kutafuta na wachache walikamatwa, na wengine walijificha na kukimbia, anasema tukio hili ni la mwaka wa 60.
Nakumbuka aliwahi kukamatwa Bwana mmoja aitwae Maikoledy, alikuwa akiitwa pia Michaeli, na waliendelea kutishia !
Walipoenda Polisi, na shauri hilo lilitupwa kwa mkuu wa kanisa lao nae kuuliza ni kwa nini mnapiga watu, kama hawa wamekuwa Wapentekoste waacheni, na baadae likarudi mahakamani.
Na mahakama ikatoa kibali, na kusema nchi inaruhusu kuabudu, kama ni kanisa la TAG limeenea maeneo mengine Tanzania ninyi mnazuiaje, na mahakama kuwataka kama wakijenga watoe tu taarifa serekalini wapatapo eneo.

Ila hata baada ya hapo bado vita haikukoma kiwepesi.
Baadae mmishenari aitwae Patrasiky alikuja na kutoa misaada ya ujenzi wa hili kanisa, na kutoa fedha na wakristo wakachangia baathi ya vifaa, anasema wakati huo sasa ni uhuru bila kelele, "tunaabudu kwa uhuru kabisa", nasisitiza mzee Munisi.
Sasa baada ya kelele kile kutulia sasa kile cha fujo, ndipo Askofu akawa anashuhudia akiwa ndie kiongozi wa hili kanisa, akashuhudia kule kijiji cha Lemira, na kupata wakristo huko, na anasema akifungua huko na vita ilikuwa ni hivyo hivyo, kama ilivyokuwa huku awali, walikuwa wanatoka watu huko na kuja hapa, mpaka walipokuwa wengi.
Walipoongezeka wakafungua kanisa la pili huko Lemira ! Huko ni Masama Magharibi.

Akaenda tena akashuhudia sehemu moja inatwa Sonu, napo watu waliokoka wakaanza vita, kanisa la Kilutheri wakaanza kupiga watu, wakaja kuabudu hapa sijui miaka mingapi, wakaongezeka na kufungua kanisa lingine tena huko ! Anaongea kwa masikitiko na kusema kuwa, " kazi ya Mungu ikawa vurumai kweli kweli !" Huku akiwa na hisia kali.
Anasema Askofu alipokuwa akisha fungua alikuwa akiwapeleka wachungaji katika chuo cha Bibilia kule Arusha ! Soni ni Masama Kaskazini !

Hakuishia hapo, akaenda kijiji kingine kiitwacho Roo, kijiji ambacho kipo Mashariki, likafunguliwa kanisa lingine, na kupeleka huko mchungaji mwingine ambae yupo hai hadi leo,(leo ya mwandishi wa makala hii,) anaitwa Abeli Shoo; huyo Mchungaji wa Roo.

Ananidokezea kuwa, wakati huo sasa baada ya kufungua kanisa katika vijiji hivyo vyote, alimkaribisha Mosesi Kolola, na wakati huo hakukuwa na kupigwa tena, na Askofu alikuwa akienda kuomba kibali serekali, na mkutano wa kwanza ulianzia hapa kanisani kwetu, ( Mudio Masama) na watu walikuwa wakifurika wakitokea, mbali, maana kulikuwa hakuna kupigwa tena.

Hiyo ndio mikutana yake ya kwanza hapa Kilimanjaro, na watu wengi waliokoka kweli kweli, anasisitiza mzee Munisi.
Anasema baada ya kufunguliwa kanisa la Roo lilifunguliwa lingine la Kware, ni Kusini ya Masama kuelekea Boma ya Ngombe !

MGAWANYIKO:
Sasa kutoka hapo sasa, ndiposa sasa alikuja machafuko ya vikundi vingi, kuna kikundi cha Lutheri kiitwacho Jitenge, kilianza kufungua makanisa.
Likaja Makanisa la Askofu Isanja, la PCT ikiwa ni matokeo ya mgawanyiko wa kanisa la TAG.  Ikiwa ni mwangaza wa makanisa mengi kushamiri.

Anasema TAG na, kitu cha ajabu wale waliokuwa wakitupiga vita huko huko ndani yake kumeinuka watu waliokoka ! Leo hii imani ipo kabisa hakuna tena vitisho.

Anasema pia kanisa la Kinondoni Rogate Swai ametokea hapa, Mchungaji Wison Kimaro, wa Calivary Temple Arusha, yupo Philipo Munisi, pia Philipo wa Mchungaji Kimaro, anasisitiza kuwa hili ni kanisa mama !
Mke wake na Munisi, Anarabi anaongea kwa sauti ya kilugha ya kichagga cha kimachame na kusema kuwa, " ni kanisa mamaah" ikiwa ni lafyuzi ya kilugha !

Mumewe anaendelea, na kusema kuwa lipo kanisa pia la mchungaji wa nyumba ya Mungu, wengine wapo  kidia moshi vijijini, wengine Tpc pia nyumba ya Mungu, na Askofu mwenyewe yupo pale Moshi mjini, sehemu nyingi sana na vijana wengi wametoka hapa, hapa ambapo ni kanisa mama.

Huyu Rogaty Swai nae amepanuka na amefungua makanisa mengi sana, ( hii inadhibitisha utendaji wa Uamsho huu.)

Mzee anasema kuwa walipojaribu kumtumia Mangi Charlesi Shangali na Mangi Muitori, ambae ndie aliyekuwa mkuu wao, waliwahi kufika hata hapa kanisani, na siku tunafungua kqnisa Mangi Charlesi. Ambapo ilikuwa ni 1970 ambapo ndipo alikuwa wakihamia hili jengo ninaloliona kwa leo, ( Nifika kuwa hawakufanikiwa kuuzima huu moto,) anendelea;
Huyu Charles mzee anasema aliwaambia kuwa, "watu wameamua kuabudu Mungu wao mnawazuiaje ! Mnapiga watu bure, na nchi yetu ina uhuru wa kuabudu."

Wao walimjibu na kumwambia kuwa wanaiba watoto wetu, naye kusema kuwa, " mtu anaamini mwenyewe sio kwamba wanamuiba."
Ndugu yangu shuhuda hizi zinadhiirisha jinsi kazi ya Mungu isivyoweza kushindwa japo vita huwa haviachi kuja, lakini kama wateule wakisimama ushindi ni lazima.

Nikiendelea na mzee Munisi ananiambia kuwa kitu kingene ambacho ninakikumbuka ni kwamba makanisa sasa au kanisa letu kwa sasa limeenea maeneo mengi hata sijui idadi yake !
Ninakukumbusha tu kuwa Uamsho hauhitaji watu wengi, bali mmoja au wachache ambao ndio huwa chachu ya Uamsho husika, ( mimi  mwandishi wa makala hii nipo tayari sijui wewe ? )

Mzee namalizia kuwa; Anasema kinachomshangaza wale wote waliokuwa wakiwapiga wakristo kwa hasira walikwishakufa wote !
Anasema kuwa yupo mzee mmoja tu ambae hakuwapiga na yupo hai hadi leo ! Anaitwa Enenery Abrahamu, na mke wake yupo hai, Makidalena, na watoto wake wapo hai, na mtoto wake anaitwa AnnaNdumi ! ( Fahamu kuwa Ndumi ni Mungu, kwa mujibu wa kimachame, na Annandumi maana yake anamfuata Mungu. Na mwaka wa uandishi wa makala hii ni 2019 mwezi wa 9 siku ya 29.)

Anashuhudia kuwa ameokoka ila bado naye anaabudu Lutheri, wakati huo naye ndie kijana wa mwaka wa 62, mimi nimeoa, mwaka huo, ila yeye hakumpiga mtu wala kumburuta ! Na wana wake pia wapo waliokoka !

Nikamuliza Mungu na kumwambia wewe umejua moyo wake mbona amekuja kuokoa juzi juzi, amekaa na uzee wake salama, na kanisani kwetu huwa anakuja kutoa shukurani zetu, na kwa upande wangu ni mjombaa angu !

Ndiposa ninakwambia kuwa kazi ya Mungu ni ya Mungu peke yake, haina mashindano na mtu, bali ina mashindano na Mungu na Shetani peke yake wewe ukijiingiza hapo shauri yako !
Nani alikuwa kama Paulo Mtume, ambaye aliangukiwa kwa ghafula na giza neno na kuulizwa na Yesu mbona unaniudhi na kushangaa,  kwa hiyo Mungu ni Mungu tu !

Tumfanyie Mungu kazi yake naye atatulipa tukiwa waaminifu, ana wosia wa kuwataka vijana kutokukata tamaa !

Kuna mfanyakazi wao wa nyumbani anamuliza babu wewe hukupigwa !
Anasema yeye hakuwa mshuhudiaji ama bado hakuwa amemjua Mungu mapema, ila mdogo wake alikuwa ni mshuhudiaji mkubwa, Ndenimfoo Kundaeli, kwa hiyo sikuweza kufanya lolote maana mdogo wangu alikwemo huko !
Na mimi nilikuja kuokoka mwaka wa sabini !

Anatudokezea kuwa Askofu alipokea naye Ubarikio na Sakrameti alikuna naye, kwa kimila tunasema ndie mwenzangu, (rika) ilikuwa kwenye mwaka wa 1956.
Anashuhudia wakati yeye anaokoka aliponishauri mimi niliogopa sikumfuata kwa haraka, maana nilisema ndugu yangu mdogo wangu ameokoka, tukiuawa wote itakuaje, nilikuja kumfuata baadae na kanisa limetulia, ila mimi sikumpiga mtu !

Kulikuwa na Wanyaturu walikuwa wakifanya kazi kwa mama yangu, ambao walikuwa wameokoka, siku moja walifukuzwa usiku wakitaka kuwaua !

Anasema mke wake alitangulia kuokoka, yeye aliokoka tangu mwaka 1959, anasema wokovu uliingia huko huko kanisani Lutheri wakiwa ni wakata shauri, anasema kufika nyumbani ndo anajua ameokoka, unamuoa mtu huko huko hujui akija ndani anakataa matendo ya kiovu maana ameokoka.
Anashuhudia siku ya kuokoka alipasua masufuria ya pombe, na kata za pombe, na kumuomba msamaha mke wake maana kabla ya wokovu alikuwa akimpiga, maana alikuwa akiacha ulezi wa pombe unaliwa na kuku na kwenda kanisani.
Anasema aliokokea katika mkutano wa Mosesi Kolola, (mzee huyu ni jarani kabisa na kanisa, wametengenishwa tu na barabara, hapa nilipo nipo kwake na nikigeuka naliona kanisa, hata kuna picha nimeipiga ya kanisa nikiwa eneo lake, kwa heri na ubarikiwe !)

Usiikose Sehemu ya sita ambapo inasimuliwa na Mzee wa miaka 87 aitwae Theofili Bartolomayo Kimaro, huyu ni ndugu na Wilson Kimaro ambapo ni mapacha, mke wake na huyu mzee aliokoka kwa kutokewa na Yesu ! Akiwa katika familia ya kiisilamu, alipigwa ila hakuacha wokovu, aliniambia kuwa hakushuhudiwa na mtu wokovu, bali aliupokea toka juu moja kwa moja ! Sehemu ijayo usiikose, na huu ndio Uamsho wa Masama ! Ukiandikwa kwa kina na Mwandishi wako Oscar Samba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni