Jumatatu, 14 Oktoba 2019

HISTORIA YA WOKOVU, AMA SIMULIZI ya Uamsho wa MASAMA MUDIO. Sehemu ya 6, Zamani Enzi za Askofu Imanueli Lazaro

Utapatapia Unabii wa Askofu kuhusu kufa kwa zao la Kawaha, na Pigo kwa Uchumi wa wanaume na kuhamia kwa Wanawake.
.
Kulia ni Mwandishi wa Makala hii Mwalimu Oscar Samba akiwa na Msimulizi wetu Mch. Theofilo
Inasimuliwa na Mzee na Mchungaji Mstaafu wa TAG huko Masama, THEOFILO BARTOMAYO KIMARO, huyu ni pacha au ndugu na Mchungaji Wilsoni Kimaro.
Tuanze simulizi yetu; Niliokoka mwaka wa 1962 January na Mungu kuniita mwaka huo huo, niliunganika na kanisa huko Mbuguni, ambako kanisa nililikuwa halijaanza huko, (la wokovu) nilipokoka tukaanza kushuhudia nyumba kwa nyumba kama vijana.

Nakumbuka kuna mama mmoja kipindi hicho alishikwa na kansa, huyu mama sikuwahi kumuona kanisani maana alikuwa mgonjwa na alikuwa amekonda sana,
tukamshuhudia habari za Yesu kisha tukamuombea na Mungu kumponya siku hiyo hiyo ikiwa ni baada ya kuokoka.
Alienda kanisani, na kilichoshangaza alikuwa hajawahi kwenda kanisani, na alisema kimaro alikuwa amekuja hapa akaniombea na vijana wenzake nikapona, ( Waliokokea Lutherani,) na baada ya hapo ikawa kero, tukaitwa !
Hili ndilo eneo tajwa kuwa kanisa lilianzia kama kusanyiko la nyumbani kwa Penueli.
Tukaambiwa embu elezeni jinsi mulivyomuombea yule mama ! Tulivyoelezea tu mmoja wetu akapigwa, na mzee mmoja, akasema ndio hata Yesu alipigwa hekaluni ! ( Japo kiuhalisia Yesu hakupigwa hekaluni.)

Tukaamua kwenda porini, na kuabudu kwetu ilikuwa ni porini, ikawa siku moja katika kuomba Yesu akatushukia porini, unajua ilikuaje ! Anasema mzee Kimaro .
Mimi niliamua kujitenga, nilikuwa nasongwa na mambo yangu binafsi ya kimaisha, nilijitenga na kukaa hapo kutwa nzima, nikisoma na kuomba pole pole, niliguswa sana kusoma kitabu cha Isaya.
Nikaja nyumbani na kuwasimulia wenzangu jinsi ilivyotokea, nao wakasema na sisi tutaenda, kesho yake wakanitoroka wakaenda, maana walikuwa na hamu, anasema "kila mtu alikuwa na hamu."

Nilipoenda nikasikia wanaomba kama wanaombea angani, niliposogea nikasikia Roho Mtakatifu ananena kama yule wa Matendo ya Mitume !
Nikamwambia Mungu, Roho umemleta huku duniani kama siku ya Pentekoste ! Nikafurahi na kuimba haleluya kama vile ninapaa !
Nikaenda au tukaenda nyumbani, Siku hiyo alikuamekuja mchungahi Wilsoni Kimaro, ile kumsalimia tu, hatukuweza kusalimia kwa kawaida, bali tulijikuta tukinena kwa lugha !
Akanigusa kichwani na kusema Roho wa manabiii huwatii manabii, ile lugha ikakoma kabisa !

Ilinichukuwa siku nne ndipo ninakasena tena baada ya kuanza kuomba tena . Tuliendelea kujitenga maana tulitengwa.

Baadae alikuja kumuita Askofu Lazaro, huyu Mchungaji Wilson Kimaro, walipogundua tumeokoka walienda kumuita na Mmishenar Fody, ndipo walipotubatiza tukiwa Moshi mjini, na mchungaji aliyetubatiza alikuwa anaitwa Saoni Malia, mwaka 1963 ndipo niliporudi nyumbani Masama maana ndugu yangu yaani pacha wangu Wilsoni alikuwa anaoa.
Kwa hiyo ile dhiki mimi sikuikuta, maana ile dhiki ilitiwa nguvu na ukoloni, maana ilikuja 1959 maana ukoloni ulikwepo katika dini, yaani Lutherani, Katoliki, na Angilikana, sasa dini mpya ilikuwa ngumu sana.

Mtu mmoja aliniambia hivi, alikuwa ni mzee wa kilutheri maana tuliitwa dini ya usiku, dini ya kulia au dini ya haleluya, sasa baba huyo akaniambia kwamba tulikusanyika wazee wa kilutheri kwa ajili ya kuja kuwangamiza maana kwa serikali hamna shida ndio wao.
Anasema baraza lilipokaa, kitu cha ajabu kwao ni kwamba mchungaji alifungua andiko la Matendo ya Mitume kuhusu lile la Gamalieli, maana hoja zao zilikuwa nzito maana tunavurugu kanisa la Mungu, na maandiko husema anayehubiri injili nyingine na alaaniwe !

Basi baba yule alipewa hekima ya ajabu sana, na Mch huyu alikuwa akiitwa Alifanyo Salema, na alipofungua hilo andiko nafikiri ni la Matendo 5 akasema hawa watu tujiadhari nao, kama ni wa Mungu, sawa, akisema kama sio watapotea, akitoa mfano jinsi ya watu walivyoinuka kipindi kile na walipotea na kutawanyika, waacheni isije ikawa mna pingana na Mungu kama sio cha Mungu kitatawanyika.
Anaendelea kusema kuwa hiyo ilitupa changamoto, tuende wapi ili tupate ulinzi, maana bado hatukuwa na usajili, maana kwetu ni Roho alishuka na kuanza kujiongoza.
Anasema siku za kwanza huko udoro katika Kanisa la Lutheri kuna vijana kama 40 walikuwa wanaomba na kujazwa Roho walitengwa, na wengine kuogopa,sasa ilitusumbua tujisajili wapi !

Ndio maana pale kwamze Penieli Munisi kulikuwa kujengwe kanisa, yaani watu waliinuka usiku mmoja tu, kulikuwa na mawe na punde mawe yote yaliamishwa !
Kengele zilipigwa Masama kote ! Nikimnukuu anasema, "ngengee nge'ngee." Anasema wakapiga kengele na watu walijikusanya, mimi sikuona nilihadithiwa hili sikwepo ila Mungu alimponya, (Askofu Lazaro) maana Polisi walishindwa, maana alipanda gari la Polisi na ikabidi ashushwe !

Anasema kuna kanisa la Pentekoste Swidishi Misheni, ndilo kanisa lao la kwanza huku, lipo kule Marangu na Tabora ambako kulikuwa na chuo cha Biblia, ambacho nilisoma huko mwaka 1964, nikisomea uchungaji, maana baada ya kuokoka nilipata wito na kutamani sana kutumika, nilisoma hapo tu kipindi kimoja na sikuweza kuendelea sana .
Niliporudi nyumbani wakataka niunganike nao ila sikuweza, nikachukuwa masomo kutoka Nairobi ya kanisa moja ya PEFA, kwa njia ya Posta nilifaulu vizuri sana ila sikuweza pia kuunganika nao maana ni kama hao wa awali maana walitaka nihame nyumbani.

Nikarudi nyumbani na kuungana na wakina Askofu Lazaro na Wilsono Kimaro, alitokea mtu mmoja aitwae Yakobo Ringo, akiwa ni mpare huyu, bahati mbaya alikuja kuondoka TAG akiwa na Sikustaili na walitenganeza katiba yao na niliwahi kuisoma.

Hii ya kufanya mikutano na ushuhudiaji masokoni na nyumba kwa nyumba ilisaidia kukua kwa kanisa.
Na baada ya hapo ndipo Askofu Lazaro akaenda kumtafuta Mmishenari wa kanisa la Asemblies of God Misheni, maneno hayo yalikuwa na nguvu akimaanisha vipeperushi walivyopewa, anasema maneno hayo ni;  ninakuletea kanisa la Asemblies of God Misheni, anasema huyu ndie aliyejenga kanisa la Calivary Arusha na chuo cha Ngaramtoni. Mimi na mzee Penueli tulishauri pia kuhusu ujenzi wa jengo la kanisa hapa Mudio.

Anasema kuwa Askofu aliwaambia kuwa tulikataa makanisa mengine ya kiroho kwa sababu ya misingi yao, aliwambia kuwa tunataka tujiunge na kanisa lilosajiliwa, tuliandikisha majina yetu wote na mmishenati alikubali, na Askofu alikuwa mwangalizi wetu, na alikuwa mwangalizi hadi Dodoma, maana Kilimanjaro lilikwepo la Masama tu, na la pili ilikuwa ni nyumba tu na hakuna washirika,mwaka wa 1960 la Moshi lilijengwa ila hapakuwa na washirika.
Anasema aliyelijenga la Moshi ni baba mkwe na mmishenari aitwae Klini Fody, ambae ni mzungu mwenzake !
Na wa Dodoma alikuwa akiitwa Manyihila, huyu ni mgogo,kingine hii dini ilikuwa ni ya kuhubiri na Askofu alikuwa ni muhubiri,walimpa pia pikipiki ya Honda 50 19 cc50, aliiendesha toka Dodoma hadi hapa Masama, ilishangaza !

Baada ya kujiunga na yule Mmishenari tukawa chini yake sasa, na mwaka wa 1968 chuo cha Biblia Arusha, kikafunguliwa, maana kilisimamishwa kwa muda japo kilifunguliwa mwaka 1960 ambapo ndipo Askofu Lazaro na Wilsoni Kimaro walisoma na wanafunzi wengine, na kilipofunguliwa tena mimi nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wa kwanza hapo.

Nilishindwa kumaliza, nikasoma kwa muda mfupi, walinichukuwa na kunipeleka Dar es Salam katika kanisa ambalo lilileta matatizo, lilianzishwa na Mch Saimoni Malia,sasa mshirika wa Twmeke alifungua kanisa Kinondoni, mtu mmoja aliitwa Nabii Elia akawa amesema Yesu atakuja, aliwachukuwa kutoka Dar es na hata huku Masama na kuwapeleka kwake Upareni, na kwamba Yesu amewaambia wakusanyike katika mlima huo, na kuwafanya watumwa wake. ( Mama moja aitwae mama Stephano anasema hata alipokufa alikuwa amewambia wasimzike hadi aje achukuliwe, na walipokaa nae ilipofika siku ya nne na kuona anaoza walimzika.)

Nikakaa Dar es Salam mwaka mmoja, na mwaka wa pili yaani 1971 kulikuwa na wimbi kubwa la Askofu Lazsaro na Mosesi Kulola na kuzuka sana 72 waziwazi.

Anaendelea na kusema kuwa, baada ya hapo niliambiwa niende chuo cha  Biblia 1972, ilikuwa ni Arusha,  baadae tulikaa kama wajumbe, au wachungaji, kutoka Arusha, Dodoma, Kilimanjaro na Mbea, ndipo tulipoondoa Misheni na kuwa na Tanzania Asembllies of God badala ya kuwa na vikundi vikundi na kulisajili serekalini.
Mch Mosesi Kulola hapo awali alikuwa mtu wa kanisa la, AIc, alipotoka huko aliiungana na Daud Kuselya, na walipomuona Kulola walimkubali na kuungana nae, na hapo walifanya kazi ya ajabu sana na kufanya kazi ya kuhubiri injili nchi nzima !

Nikiwa TPC mwaka 1977 tulikuwa tukiliombea sana hili jambo maana lilitesa sana watu, sasa mimi nikiwa katika maombi Mungu alisema nami, kuwa kila mmoja alikuwa na kundi lake, nilipanda gari hadi Moshi mmjini nikampa maneno hayo, Askofu Lazaro, japo sikumbuki ni Yeremia ngapi, maana ndivyo Mungu alivyoniangazia, aliniambia ni kweli, japo sikuwezakuongea nae sana maana alikuwa ni mkubwa kiroho !

Mzee anasema walipokuwa wakiabudu kuhusu nguvu za Roho Mtakatifu kuwa ilikuwa ni kwa njia za ajabu sana, na tulikuwa kama watoto wadogo, na zile changamoto zilitufanya kumtafuta Mungu kwa bidii, siku hizi hakuna changamoto kama za zamani za kupigwa na wazazi na ndugu, kwa mfano mke wangu aliokoka mwaka wa 1953 ambapo hapakuwa na neno la kuokoka, alipokutana na mtu wa mbinguni hapakuwa na mtu aliyemshuhudia, na alipoenda kanisani alikutana na fundisho la mimi ndimi niliyekuumba, na maana ndilo andiko alilopewa ! Hapo ilikuwa ni kanisa la Kilutneri.
Mwaka1965 alikuja kanisani kwetu yaani la kilokole na 67 tukaanza urafiki, na 68 tukaona.

Anasema zamani hiyo watu walitupinga, na kwa kuwa hakukuwa na waalimu, maana tulijifunza wenyewe, na tulikutana na changamoto kubwa ya kupingwa lakini Bwana alitusimamia na kututia nguvu, na mpaka walipokuja wamishenari hasaa kutoka Mbea maana ndiko kanisa liipoanzia la Tag mwaka 1939 japo kule Mbea kulikwepo na kanisa la Elimu Pentekoste na hilo la Swidishi.
Hili la Elimu Pentekoste lilianza mwaka 1920 maana nilikutana na mchungaji mmoja aliyeokoka mwaka wa 1926, mtu mmoja wa la Swidishi aliyeokoka aliniambia aliokoka mwaka 1929 kwa hiyo lilianza nalo muda mrefu.

Anasema makanisa mengi yalianzia Mbea kwa sababu wapo karibu na Malawi, maana walipitia nchi hiyo. Na walipoyapokea hayakuwa na kasi sana ya kuenea, hadi mika ya 60.

Sitasahau, sikumbuki ni mwaka wa stini na ngapi, Askofu Lazaro alikuja akitokea Nairobi kwenye mkutano wa viongozi kuwa Mungu amesema naye kuwa zao la kahawa linaenda kufa kwa sababu wanaume wamepiga wake zao na kwenda kunywa pombe, na baya zaidi wamama ndio wanaenda kuuza na wanawake hurudi na maguni wababa wakienda kunywa pombe.

Kwa hiyo Mungu alisema nae kuwa amesikia kilio ha wanawake na hilo zao linaenda kufa, anasema mwaka 1968 kahawa zilizaa sana, na mwaka wa 69-71 kuliingia ugonjwa wa sidi-d ambapo kahawa ikawa inaungua, hakukuwa na dawa na zilizokwepo hazikusaidia, pia kahawa shina lake likawa linapasuka vipande viwili kwenye shina lake, anasema nilijitahidi kutunza kawa mwanangu, lakini haikuwezekana.

Mwaka 1980 nilingoa kawaha zote, na huo ndio unabii aliousema Askofu Lazaro ! Na jambo la pili alisema pesa Mungu amesema atazirudisha mikononi mwa wanawake ! Huo ndio unabii ninaukumbuka !

 ( Mambo haya yamekuwa halisi kweli nami kama mwandishi nimelishuhudia leo,ila nimeazimia kuchukua hatu ya toba, huku ni kulijenga boma mahali palipobomoka !) Sijui wewe ?

Tutaendela na historia hii katika kipengele cha, ..  ananiambia leo muda hauta ruhusu. ( Kwa hiyo Mungu akitujalia siku nyingine tutakudodosea kwa kina hiki cha mambo yake binafsi..)

MAMBO YAKE BINAFSI
Ananidokezea kuwa kwa mara ya kwanza Mungu aliposema nae, kupitia andiko la Petro kuwa mateso ni kama dhahabu ipitishwavyo kwenye moto, yaani mateso hutungarisha, pia mambo yangu binafsi, watoto wangu, habari ya viongozi na kufa kwa wachungaji ni mambo yaliyonitesa sana.
Na nilifundishwa na Mungu kuwa watakatifu wanapokufa hakuna anayekufa kwa hasara, maana nilipata taabu baada ya kufa kwa wachungaji wengi, na aliniambia kuwa mwanangu niliwaepusha wasije wakapata hasara pamoja na dunia.
Kwa uchungu ananiambia kuwa, "nimetamani mimi kuondoka, nimetamani sana mwanangu wewe acha tu !"
Ndio maana nasema mbambo mengi yanahitaji tuwe na mama, nasema mke wangu Mungu amasema naye juzi maana naye anatamani kuondoka na Mungu kumwambia kuwa kufa ni kwa faida yako, na kuishi ni kwa faida yangu.
Sasa sisi sio watu ambao tunahuduma lakini Mungu anataka tukae kwa nini ?
Nilitamani kukuletea kwa kina ushuhuda wa mkewe jinsi alivyookoka, ambapo alipokuwa mwislamu  alifahamika kama Myasa Safarani Omari, ila muda haukuniruhusu, kwani kiza kiliingia, ila siku yaja nitakudodosea nikirejea tena Masama panapo majaliwa ya Mola Maulana !
Lakini mkewe alinijuza hivi hapo awali, kuwa kuna siku moja alikuwa nje kidogo na nyumbani, na kutokewa na mtu mmoja mweupe, ana ngaa, na mtu huyu kumwambia kuwa mimi ni mtu kutoka mbinguni, ndie niliyekuumba !

Alimshuhudia habari za wokovu, na alipofika nyumbani alikuwa na hofu sana na mamaye kumuuliza kilichomsibu ni kipi, alipomueleza aliamua kumpeleka kwa baba yake, ambapo alipiga kitu kama ramli au kuuliza kwa majini yake !
Nayo kumwambia kuwa mwanao amekutana na kiumbe cha ajabu ambacho hatukuwahi kukiona, ni kama moto, au waliona moto tu !

Ndipo alipoaswa kuachana na hiyo imani na kupigwa sana ila hakukubali, walimpiga mara kwa mara bila mafanikio na kuanza kuabudu Lutheri ambapo baadae alikuja kuokoka kama nilivyokujuza hapo awali.

( Picha inayoonekana kama nyumba ya watu ambayo ni yenye uzio wa maua, ndipo kwa Penueli ambapo kanisa la kwanza lilianzia na kushindikana kujengwa, na hiyo nyingine ni mimi na mzee Theofili Mchungaji huyu Mstaafu tukiwa nyumbani kwake ambapo ndipo aliponipa hii simulizi !)
Zaidi soma: www.ukombozigospel.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni