Ijumaa, 27 Septemba 2019

HISTORIA YA UAMSHO WA MASAMA ENZI ZA ASKOFU LAZARO, Ikisimuliwa na Jereremia Balitomayo Kimaro, mdogo wake na mchungaji Wilson Kimaro, Sehemu ya 4.

Ni watatu kutoka kwake.
Kushoto ni mwandishi wa makala hizi Oscar Samba akiwa na msimulizi wa sehemu hii ya nne Jeremia B. Kimaro wakiwa nyumbani kwake Mudio au Modia kama inavyotamkwa na wenyeji eneo la Masama.

Anasimulia; Tulikuwa wadogo ila kumbukumbu tunayo, miaka ya 1959 na 60 ndo uwokovu ulianza, Lazaro Askofu aliupatia kutoka Arusha, na kuja na kumkuta baba yetu (Bartolome Kimaro) ambaye alikuwa ni mdhaifu au mlemavu kidogo, na baba aliukubali, Walutheri ndio waliotufanyia fujo sana.

Wengine walipigwa mfano Mzee Lazaro na Sikustaili, pamoja na Mch Robert ambae aliwahi kupigwa chuma ya kichwani kwenye paji la uso.

Fujo ilipozidi sana walikimbia, anaendelea kusimulia mzee Jeremia, anasema kuwa mmishenari aitwae Pauli Brutoni nae alikimbia na kwenda kuita polisi !
Walipokuja mimi nilimpowenti mmoja na kusema ni huyu, walimchukuwa na kumpeleka magereza, akakaa huko kama miaka miwili, na alipokuja alisema lazima atanifanyia kitu na kuja kuniua !


Ila Mungu alivyomkubwa hakuna aliyekuja kunifanyia fujo, anasema wote waliowafanyia fujo hawakuwa na maisha marefu wote walikuja kufa.

Kulikuwa na Mchungaji mmoja aliyeitwa Alifanyo, huyo mchungaji fujo zilipozidi, aliwakataza na kusema " jamani waacheni watu wa Mungu wakae, maana kama ni neno la Mungu litakaa, na kama sio watasambaratika"  basi wale waleta fujo wakatulia, Huyu ni Mchungaji wa Lutherani aliyewatuliza waamini wake.
Baada ya hapo walichanga fedha na kumtuma Mangi, ( Mangi ni mkuu wa kikabila kama chifu huku uchagani, yaani kiongozi,) ili awanyamzishe wakisema wanawapigia kelele, anasema ilikuwa siku ya ijumaa, hakudhubutu kuwafikilia, (maana kila ijumaa tulikuwa na maombi,) yule Mangi alipokuja na kuona jinsi watu au Roho wa Mungu alivyokuwa ana miminika aliduwaa, na hakudhubutu kufanya lolote !
Anaendelea kutanabaisha kuwa; Akanyamaza kimya hakudhubutu kusema chochote, na akasema, nisameheni naomba tu mnionyeshe njia inayopandisha hivi inayoenda Mbwera, ( wakiwa Mudio) nao walimuelekeza .
Alipoenda aliwaambia waliomtuma yaani hilo kanisa, kuwa wale watu mimi sikuweza kufanya chochote, anasema toka hapo hawakusumbuliwa tena. Huyu ni Mangi Charlesi Shangali. ( Ndie Mangi wa mwisho Machame.)
KUBOMOLEWA KWA KANISA:
Mmishenari Brutoni alikuwa ameshapima kanisa pale kwa Penueli, na walikuja watu wa hiyo dini baada ya kugonga kengele na kujikusanya kisha na kuanza kupiga watu, na kuufukia huo msingi.

Hapa ndipo mahali pa kanisa la kwanza ambapo walikuwa wameanza kuabudu hapo, ndipo kaka yangu, yaani ( Mchungaji Kimaro) akajitolea, palikuwa na nyumba ya makuti ndogo, ndipo watu wakaanza kujaa na kupanua kanisa na kujenga jengo la miti. ( Hapa ndipo unapoona picha zake katika makala hizi ama ndipo palipojengwa jengo ambalo linatumika hadi leo.)
Na Askofu Lazaro ndie mchungaji wa kwanza. Na Yakobo Ringo akiwa ndie msaidizi wake, huyu ndie yule aliyetoka nae Arusha.
Anaendelea na kusema kuwa Mchungaji Wilsoni Kimaro yaani kaka yangu alielekea Moshi na kuwa Mchungaji wa hapo, yaani la Moshi mjini, ambapo wachungaji watatu walikuwa wameshakaa hapo, na baadae kuhamishiwa Arusha.
Anasema walikuwa wakiondoka wachungaji sana kutokana na ugumu wa hapo, maana wengi walikuwa sio watu wa kudumu yaani wafanyakazi wa kuhama hama, ndiposa kanisa likashindwa kusimama.
Baada ya Wilsoni alikaa hapo Mchungaji Saimoni Malia, Mchungaji wa Temeke, ( Ni mtu wa Machame.)
Anasema wale waliokuwa wakijaribu kushirikiana na sisi walikuwa wakishikwa na kupigwa au kuadhibiwa.
NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU:
Anasema walipokuwa kwenye ibada mara kwa mara Roho Mtakatifu alikuwa akishuka hadi wanasikia mtikisiko wa nyuma yaani tetemeko la nchi au aridhi.
HISTORIA AU ODODOSO KATIKA KANISA LA SWIDISHI FREE MISHENI, kwa sasa KLP.
Tulikuwa na mmishenari Brink Back maeneo ya Rombo na Marangu, tulianzia Marangu, Marangu tulikuwa na Mchungaji Erasto Mshomi, Elihuruma na ....
Tulijenga Kanisa la Marangu nao, baadae tukaenda Keni Rombo, tukaanza kazi hapo na kuingia Mkuu, baadae mwaka wa 1979 kwa 1980 ndo tulifanya hivyo. Baada ya hapo nikarudi nyumbani.
Kwenye mwaka wa 1980, tukiwa kama wanafunzi tukipelekwa na Mshomi tulienda Mamsera na kuacha kanisa pale limeanza, ila kwa sasa sijui kama limeendelea au la ! ( Ni wanafunzi wa chuo cha Biblia Marangu.) Zaidi tembelea, www.ukombozigospel.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni