Jumatano, 28 Agosti 2019

MSAADA WA KUTOKA KWENYE KIFUNGO CHA MADENI.

Kunamtu ameniandiki hivi, "Mtumishi Bwana Yesu asifiwe mnaendeleaje ss wazima mtumishi nina Hitaji tuombe niwezekupata hela ya kulipa madeni kwani ni nadaiwa sijui napata wapi pesa."
Nami kumjibu hivi:

Hatua ya kwanza ni kuvunja roho ya utumwa kupitia madeni,Mithali 22:7 Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.
Pili, lipa hayo madeni rohoni kwa Damu ya Yesu, tatu ndo kuomba milango ya fedha ifunguke ili uyalipe mwilini, 4, omba nidhamu ya Mungu ili fedha hiyo ikija uwe mwaminifu kulipa nasio kufanyia mambo mengine ! 5. Tumia hekima y
a kuwa na bahasha au mfuko maalumu kwa ajili ya kuweka fedha za kulipa madeni, waweza tenga kila asilimia tano ya pato lako. (Kila hatua ni muhimu.)

Nami nakuongezea kuwa au nakitaka ukumbuke kuwa; Zaburi 37:21 Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.

Kwa hiyo kushindwa kulipa madeni ni kupoteza haki au ni kuwa mdhalimu ama mdhambi !
Ukiweza anza kwanza na maombi ya Rehema, maana roho nyingine huwa na uhalali, kuhusu kipengele cha kulipa kwa Damu ya Yesu ni kwamba hii Damu kama ilitununua maana yake inaweza kutulipia, na madeni huwa rohoni na mwilini, rohoni tunalipa kwa Damu yake Yesu na mwilini kwa fedha, kulipa kwanza rohoni kutakupa wepesi wa kulishuhulikia mwilini na kumzuilia adui kulitumia kama lango la mashitaka na upinzani katka maisha yako !





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni